(kutoka kushoto - Anika Noni Rose, Jill Scott, Lucian Msamati)Wadau, mkipata nafasi hebu tazama TV show, The No. 1 Ladies Detective Agency. Kama mnakumbuka niliwadokeza mwaka jana kuwa walikuwa wanapiga sinema huko Bostwana. Hiyo sinema imekuwa 'pilot' (Show ya kwanza) na sasa HBO wameagiza iwe series. Hivyo kila wiki tutafaidi show kutoka Botswana. Kwa sasa inaonyeshwa kwenye stesheni za HBO na BBC.
Stelingi wa The No. 1 Ladies Detective Agency ni mwimbaji Jill Scott ambaye ni MMarekani. Anayoigiza utadhani ni MBotswana. Stelingi mwingine ni Anika Noni Rose ambaye utamkumbuka alikuwa kwenye sinema Dreamgirls.
Stelingi mwingine ni Lucian Msamati, ambaye ana asili ya Tanzania ingawa ni MZimbabwe. Wazazi wake ni waTanzania. Alizaliwa Uingereza na alipelekwa Zimbabwe akiwa mdogo.
Nimefurahi kuona jinsi watu wanavyofurahi The No. Ladies Dectective Agency. Wazungu wanaipenda kweli na sasa tayari wameanza kusema kuwa huenda Jill Scott atapata Emmy Award! Hayo ni makubwa!
Botswana wanasema kuwa utalii kwenda Botswana unaongezeka na wanaishukuru hiyo show maana inaonyesha Botswana ilivyo ukweli. Serikali ya Botswana iliwaunga mkono hao watengeneza show na imekuwa na mafanikio makubwa. Kuna aerial shots (scenes zilizopigwa kutoka kwenye ndege) safi sana. Watu wanapata ajira kama wafanyakazi wa filamu, na pesa zinaingia kwenye kukodi mahoteli, chakula, usafiri na megineo.
Je, Tanzania tuko tayari kuwa na show ambayo inapigwa huko? Je, serikali itawaunga mkono watengeneza TV show wakiomba kupiga nchini Tanzania?
Na kwa wasiojua miaka ya 60, kulikuwa na TV show, 'Daktari' ambayo ilikuwa inapigwa Kenya.
Ilihusu daktari wa wanyama ambaye alikuwa mzungu. Stelingi wake alikuwa marehemu Marshall Thompson.


