Showing posts with label Burlington. Show all posts
Showing posts with label Burlington. Show all posts

Tuesday, April 29, 2008

Sinema - Paul Blart:Mall Cop

Mimi na Mcheza sinema, Jamal Mixon kwenye set ya Mall Cop
Mimi na Mcheza sinema, Jerod Mixon


Mcheza sinema, Kevin James
Mcheza sinema, Jayma Mays
Segway

Wadau, jana nilikuwa extra kwenye sinema, Paul Blart:Mall Cop ambayo itakuwa sinema ya vichekesho (Comedy). Nilishinda kwenye seti huko Burlington Mall siku nzima. Kuanzia saa 2:30 asubuhi hadi saa nne usiku (8:30am -10:00PM). Tulifanya kwanza scene ya arusi. Bwana arusi ni Kevin James na Bibi Arusi ni Jayma Mays. Kevin ndo mhusika mkuu wa hi sinema, yeye ndiye Paul Blart:Mall Cop.

Kwanza tulipiga scene tumekaa kwenye meza kama wageni waalikwa. Food Court ulikuwa umepambwa kama ukumbi wa arusi. Halafu walipiga scene kadhaa, wanafungishwa ndoa, busu, Bibi harusi kutupa bouquet, wahusika wakuu wengine wa sinema waki-react kwenye arusi. Halalfu walipiga scene za Bibi na Bwana arusi kuondoka wakiwa kwenye segways. Halafu tuliambiwa tucheze densi. Wimbo ulikuwa, 'Ain't No Mountain High Enough' ulikuwa unaimbwa na kaka yake Kevin James.

Mwisho walicheza densi wakiwa kwenye segways ndani ya gazebo. Hapo tuliambiwa tuzunguke gazebo. Ilitokea kichekesho wakati titi la Jayma ilitoka nje ya gauni la arusi. Watu walichecka walisema kumbe ana matiti feki. Yaani unaona kabisa ni mpira wa kupachikwa.
Basi, kuna kipindi tulikuwa tunapumzika. Akatokea mcheza sinema, Shirley Knight, ambaye anacheza kama mama yake Jayma Mays. Alikuja mezani kwetu alichukua kisu na kasema, "Naomba mtu anichome kisu!" Heh! Tulipigwa butwaa na kubakia midomo wazi. Alichukua kisu na kuanza kujichoma maeneo ya tumbo. Tukadhania huyo mama ni mwendazimu. Basi aliishia kucheka na kusema kavaa mapedi kusudi aonekana ni mnene maana siyo mnene hivyo. Hapo na sisi tulianza kucheka. Lakini kwa kweli tulishikwa na woga.

Kwenye scene ya mwisho ya arusi, mimi na mama mwingine mweusi tuliambiwa tusimame na Jamal Mixon. Nilifurahi kweli maana hapo chensi ya kuonekana vizuri kwenye sinema inakuwa kubwa kama uko na moja na wahusika wakuu wa sinema. Jamal utamkumbuka kwenye sinema kama, The Nutty Professor na Gridiron Gang.

Baada ya kumaliza scene ya arusi, tuliambiwa tubadilishe nguo. Halafu tulipiga scene ambayo tunakimbia. Jamaa anafoka, "Kuna mtu mwenye bastola!" Basi ndo tunakimbia kutoka nje ya mall. Karibu tukanyagane utadhani mtu alikuwa na bastola kweli.

Wakati tunasubiri kupiga hizo scene niliongea na Jamal na kaka yake Jerod Mixon. Kwa kweli ni vijana poa sana. Tuliongea kuhusu sinema za Hollywood na jinsi roles kwa ajili ya weusi ambazo ni za maana ni chache. Jamal alisema kuwa anatunga screenplays sasa akiwa hayuko kwenye sinema.

Kuona scene kutoka The Nutty Professor Bofya linki chini ni sinema ya kwanza ambayo Jamal alifanya wakati huyo ana miaka 14:

Monday, April 07, 2008

Sinema - The Proposal

Kuelekea kwenye set ya filamu huko Burlington, Massachusetts. Hayo mabango ya njano ya kuelekeza pa kwenda.
Baadhi ya Extras wakisubiri kuitwa kwenye set. Huyo dada alicheza kama karani kwenye ofisi ya Uhamiaji

Hao akina dada nilikaa nao meza moja. Hao wawili weusi ni mamodo (models).

Baada ya kusibiri muda mrefu watu wanaanza kuwa Bored.
Lunch time. Kwenye set ya sinema za Hollywood huwa watu wanalishwa vizuri sana. Huyu bibi mwenye nywele nyeupe ndiye anacheza kwenye ile commericial ya Joe Kennedy ya watu maskiniwanaohitaji misaada ya mafuta kwa ajili ya kupasha joto nyumba zao.

Hivi huyo caterer kakosea njia maana Burlington siyo Hollywood na huyo ni caterer wa Hollywood. Ni hivi kwa sasa sinema nyingi zinapigwa Boston hivyo wanaita watu kutoka majimbo mengine kusaidia.
Huyo ni mcheza sinema na mwimbaji Doug Weeks, aliwahi kucheza kama Pilato (Pontius Pilate) kwenye Jesus Christ Superstar ilivyokluwa Broadway.
**************************************
Wadau, leo nilibahatika kucheza kama mhamiaji wa kiafrika katika sinema, The Proposal. Stelingi wake ni Sandra Bullock. Bahati mbaya sikumwona kwenye set. Scene ilikuwa kwenye ofisi ya uhamiaji. Nilibahatika kuambiwa niongee kiswahili. Sasa huyo mama ambaye nilikuwa naongea naye alikuwa hajui hata neno moja la kiswahili ilikuwa kichekesho.