Hii ilitokea Mei 5, 2013 Mjini Dar es Salaam
Kutoka Zeddylicious Blog
Majambazi yamempora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi na kutokomea kusikojulikana....
Tukio hilo limetokea leo saa 5:16 jioni na inavyosemekana ni kuwa mwanamke huyo alikuwa akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikuwa yakimfuatilia..
Alipotoka ,majambazi hayo
yalimfuata na kuligonga gari lake makusudi na ndipo dada huyo
aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja
alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha
pesa. ..


