Showing posts with label Jamie Lynn Spears. Show all posts
Showing posts with label Jamie Lynn Spears. Show all posts

Friday, December 21, 2007

Jamie Lynn Spears ana mimba! Ana miaka 16!


Bila shaka mmesikia habari za huyo binti Jamie Lynn Spears, ambaye ni mdogo wake Britney Spears. Ana mimba na ana miaka 16 tu. Baba wa mtoto Casey Aldridge, ana miaka 19. Anatoka Mississipi. Sehemu zingine hapa USA hiyo ni kosa la jinai kumtia mtoto mimba, na angeitwa sex offender.

Jamie Lyyn sasa anaitwa, kila jina chafu ya kiingereza ambayo unaweza kufahamu ya neno malaya. Kaitwa tramp, whore, ho, slut, skank. Wanasema ni nyege mwasho kama dada yake Britney.

Familia yake wametukanwa kuwa ni wazungu wasio na thamani. Wameitwa Cracker, white trash, trailer trash, bayou swamp trash, washamba, inbred (kuzaana wenyewe kwa wenyewe katika ukoo) doh! Wanasema "The apple doesn't fall far from the tree" ( Yaani tuna la apple haianguki mbali na mti wake). Yaani sikujua kuwa wazungu wanaweza kutukanana hivyo!

Wamekasirika kwa sababu Jamie Lynn Spears ni mdogo wake Britney Spears. Jamie Lynn ana TV show kwenye Nickolodeon inaitwa Zoey 101. Wasichana wanaipenda kweli na wazazi wengi walimwona kama mtu wa kumwiga. KUMBE!

Halafu alikuwa anajifanya ni Mkristo mwema. Mtakatifu hawezi kuvunja amri za Mungu. Yaani awe bikira mpaka siku ya kuolewa. Sasa hiyo mimba inaonyesha watu alikuwa anafanya nini. Inatoboa siri, hakuna cha ubikira hapo.

Na jambo la kuongeza chumvi hapa. Mwezi wa saba gazeti la National Enquirer walitoa stori kuwa huyo binti ana mimba. Nickolodeon walitafuta mawakili na kuandika barua kali kuwa watawa-sue kwa ajili ya kuchafua jina la binti mwema, Mkristo safi kama Jamie Lynn. Sasa inaelekea huenda hiyo habari ya mimba ilikuwa ya kweli na aliitoa.
Sasa watu wanasema kuwa Nickolodeon ni wanafiki maana angekuwa ni msichana mweusi show yake ingesimamishwa mara moja. Lakini wameruhusu iendelee kuonyeshwa.

Mama yao alikuwa anaandika kitabu kuhusu malezi bora. Publishers wa hicho kitabu wamesimamisha mkataba waliokuwa naye maana inaelekea hawezi kumlea mtu.

Karibuni mtoe maoni hapo.

Kwa habari zaidi someni: