Jamani haya mambo ya kujikrimu/kujichubua hawayafai kabisa! Hebu mpende ngozi mwenyezi mungu aliyokupa!
Showing posts with label Kujichubua. Show all posts
Showing posts with label Kujichubua. Show all posts
Monday, June 09, 2014
Saturday, March 27, 2010
Kumbe Kweli Michael Jackson Alikuwa Anajichubua!
Ukweli umefichuka. Kumbe ni kweli Michael Jackson alikuwa anajichibua na makrimu, ndo maana rangi yake iligeuka kuwa kama mzungu. Jackson alikuwa anaumwa ugonjwa wa Vitiligo ambao muathirika anakuwa na mabaka mwilini. Ni mweusi lakini nakuwa na vipande vikubwa kama ngozi ya kizungu. Mimi niliona vigumu kuamini habari ya vitiligo. Kwanza nafahamu watu wengi hapa Marekani ambao ni waathrika na hata wakipaka make-up kuficha mabaka utawajua tu. Kumbe Jackson aliaamua awe mzungu kimoja na afute hayo mabaka meusi!
Leo kuna habari kuna tube kibao za krimu za kujichubua zilikutwa nyumbani kwa Jackson alivyofariki. Wanasema kuwa watu walijaribu kuzificha. Miaka ya 80 mwanzoni kulikuwa na madai kuwa Michael Jackson alikuwa anaoga katika madawa ya kujichubua na usikua alikuwa anajipaka makrimu kibao za kujichua na kusudi ziwe kali zaidi alikuwa anafunika mwili waka na plastiki (cling wrap) wakati analala. Kulikuwa na habari kuwa Jackson alisema kuwa anachukia weusi wake. Huenda ni kweli maana alichonga pua yake kuwa kama ya mzungu.
Kwa habari zaidi someni:
Labels:
Cream,
Kujichubua,
Michael Jackson,
Skin Bleaching
Subscribe to:
Comments (Atom)





