Showing posts with label Lake Tanganyika. Show all posts
Showing posts with label Lake Tanganyika. Show all posts

Monday, September 28, 2009

Ramani ya Enzi za Mjerumani

BOFYA PICHA KUONA PICHA KUBWA ZAIDI:

Kwa wadua wasiojua, hapo zamani za kale, Rwanda na Burundi zilikuwa sehemu ya Tanganyika. Hii picha ni ya enzi za Mjerumani wakati ni German East Africa. Bibi yangu marehemu alikuwa mtoto mdogo Mjeruman alipotua pale Manda, Ludewa Ziwa Nyasa. Anasema walikuwa wanacheza halafu wakatokea wazungu kwenye maboti.

Monday, April 14, 2008

Twende tukaogelee!


Vijana wakienda kuogelea huko Ziwa Tanganyika mwaka 1930. Picha kutoka 'Phtography and Image' Blog
Nakumbuka kuona vijana wakienda kuogelea hivyo uchi, huko kwetu Ziwa Nyasa.

Tuesday, October 16, 2007

Sinema kuhusu M.V. Liemba



Kuna sinema aina ya Documentary, itatoka hivi karibuni kuhusu ile meli maarufu ya ziwa Tanganyika, M.V. Liemba. Hiyo meli bado ni imara na inaendelea kufanya kazi japo ina miaka karibu 100!
Kwa habari zaidi na kuona clip nenda: http://www.liemba.org/