Showing posts with label Lena Horne. Show all posts
Showing posts with label Lena Horne. Show all posts

Monday, May 10, 2010

Lena Horne Afariki Dunia Akiwa na Miaka 92.

Lena Horne 1917-2010
(pichani Lena Horne akiwa na Bill Robinson aka. Bojangles na Cab Calloway mwaka 1943)

Wadau, leo tunamka kusikia habari ya kifo cha Lena Horne. Lena alifariki jana huko New York akiwa na miaka 92. Aliishi maisha marefu.

Lena alipambana sana na ubaguzi Hollywood. Alikuwa mweupe mno, na mara nyingi ilikuwa akiigiza katika sinema na wazungu ilibidi wampake make-up kusudi aonekane mweusi zaidi na wazungu wasidhani ni mzungu. Wakati huo sinema zilikuwa zinapigwa katika black & white.

Safari yake kwenda Hollywood ilianza mwaka 1933 alipokuwa katika stage show ya Cotton Club huko, New York. Lena aliigiza katika sinema, Cabin in the Sky. Katika hiyo ni kimada wa Little Joe. Walipiga scene ambayo Lena alikuwa anaoga katika bathtub huko akiimba akijiandaa kwenda kwa Little Joe. Scene ilikatwa eti kwa vile wazungu hawataamini kuwa weusi wanaoga!

Lena alikuwa mwimbaji maarufu pia. Aliimba katika klabu nyingi, na pia katika bendi za Noble Sissle, Duke Ellington na Cab Calloway. Alikuwa katika sinema The Wiz pia na Michael Jackson na Diana Ross.

Mwaka 2004 ilikuwa watengeneze sinema kuhusu maisha yake. Janet Jackson ndo alikuwa stelingi wake. Lakini baada ya Janet Jackson kuonyesha titi lake kwa umati akiwa kwenye Superbowl, Lena Horne alisema hataki "mtu mwenye fikra za kimalaya" aigize kama yeye. Alisha Keyes atakuwa stelingi wa hiyo sinema.

Rest in Peace Lena Horne.


Tuesday, January 08, 2008

Alicia Keys atakuwa Lena Horne!


Habari kutoka Hollywood zinasema kuwa Oprah, amemchagua mwimbaji maarufu, Alicia Keys, kuigiza kama mcheza sinema na mwimbaji maarufu wa Marekani, Lena Horne. Sinema hiyo itaitwa The Lena Horne Story.

Watu wamengojea miaka mingi hii sinema. Production bado haijaanza.

Lena Horne alikuwa maarufu miaka ya 1940' na 1950's. Alikuwa pia ni moja wa masex symbol wa wakati huo. Ana miaka 90 sasa.

Kwa wasiojua, Lena Horne, alikuwa mmarekani mweusi wa kwanza kupata studio contract Hollywood, 1940. Alicheza katika sinema kadhaa kama Cabin in the Sky (1943), Stormy Weather na Panama Hattie. Alikuwa mwimbaji maarufu mpaka miaka ya 80 alivyostaafu. Weusi wametoka mbali katika Hollywood na ubaguzi bado upo. Enzi hizo kama ni mweusi unaingia mlango wa nyuma, hakuna ushirikiano na wazungu, mnatumia choo duni, unakula chakula nje, hakuna kulala hotelini na mengine mabaya.

Bi Horne alimtaka Janet Jackson, amwigize. Baada ya ile kasheshe ya Superbowl mwaka 2004, (Janet Jackson kuonyesha umati chuchu), Horne alisema hana habari na Janet Jackson tena wala hataki kusikia habari zake.

Oprah ameanza kutengeneza sinema za weusi tena. Alikuwa amepumzika kwa sababu ile sinema ya Beloved , ilikuwa bomu. Watu wengi wanasema Beloved isingekuwa bomu, kama mtu mwingine angeigiza kama mhusika mkuu, Sethe. Oprah aliigiza kama Sethe na alikuwa na Scenes za mapenzi pamoja na scene ambayo ananyanyua gauni na kukojoa. Pia watu wanasema kama wangesema ni sinema ya matishio (horror) ingefika mbali zaidi. Sinema nyingine ambayo Oprah ame produce hivi karibuni ni The Great Debaters starring Denzel Washington.