Showing posts with label Msiba. Show all posts
Showing posts with label Msiba. Show all posts

Monday, May 15, 2023

Tanzia - William Malecela aka. LeMutuz

 

Hayati William Malecela aka Le Mutuz
1961-2023

Yaani, kweli hujui siku utaaga dunia hii. Nimeshutuka sana kusikia habari ya kifo cha kaka yangu wa ubatizo, William Malecela 'aka' LeMutuz.  Baba yake  Mh. John Malecela, na marehemu mke wake walisimamia ubatizo wangu.

Nilikuwa namwona William Dar wakati nasoma Zanaki Girls Secondary School. William kipindi kile alikuwa na afro, kijana fit. Nilisikia alienda kuwa baharia, halafu nilikutana naye tena New York City.  Baada ya muda aliamua kurudi kimoja Tanzania. Tulikuwa tunawasiliana kwa muda lakini...ndo hivyo alivyokuwa King wa Social Media Tanzania, alikata mawasialiano maana skikubaliana naye kuhusu mambo kadhaa.  Nikawa namwona  kwenye mtandao tu...mara kanda za majungu..mara fashion show. 


Mara la mwisho kumwona William ilikuwa hivi na shati hiyo hiyo...tuliongea kidogo..Aliniaga na mikono hivyo hivyo  kama pichanai..kumbe ananiaga. Siku hiyo nilimwona Mlimani City, Dar es Salaam. Sikujua itakuwa mara la mwisho kumwona ana kwa ana.

Kaka William ametangulia.  Mungu ailaze roho yake mahal pema mbinguni. Amen

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

Saturday, December 31, 2022

Papa Mstaafu Benedict wa XVI (16) Afariki Dunia



                                                      Hayati Papa Benedict XVI

 Papa Mstaafu Benedict XVI amefariki dunia leo asubuhi huko Vatican, Italia.  Ilitanganzwa mapema wiki hii kuwa afya ya Papa Benedict XVI ilikuwa imezorota.  Amefariki kwenye Monestari ya Vatican.  Alikuwa na miaka 95. Jina aliyozaliwa nayo ilikuwa Joseph Ratzinger. Alizaliwa Ujerumani mwaka 1927.

Atazikwa Alhamisi Ijayo huko Vatican baada ya Misa itakayosimamiwa na Papa Francis.  Papa Benedict XVI hakutaka mazishi enye makuu. 

Papa Benedict XVI  alistaafu ghafla mwaka 2013.   Alikuwa Papa wa kwanza kustaafu katika miaka 600 iliyopita ya Vatican. Kwa kawaida mtu anaachia upapa akifa.  Papa (Pope) ni mkuu wa kanisa Katoliki duniani.

Mungu Ailaze Roho ya Papa Benedict XVI mahala pema peponi.  Amen



Saturday, March 20, 2021

Mh. Samia Suluhu Hassan Aapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania

Kutoka BBC SWAHILI

Samia Suluhu Hassan aapishwa kuwa Rais wa Tanzania na Jaji Ibrahim Juma katika Ikulu ya Jijini Dar es Salaam.

Mama Samia ameapishwa katika hafla ndogo iliyofanyika katika Ikulu ya Magogoni na kuhudhuriwa na marais wastaafu wa Tanzania na Zanzibar.

Mara baada ya kuapishwa alipigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride maalumu kwa mara ya kwanza akiwa kama amiri jeshi mkuu wa majeshi ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

Mama Samia mwenye miaka 61, ndio mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huu nchini Tanzania na wa pili Afrika Mashariki.




Wednesday, March 17, 2021

Rais John Pombe Magufuli Afariki Dunia!



KUTOKA GAZETI LA MWANANCHI 

 Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amefariki dunia Machi 17, 2021 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa za kifo cha Rais Magufuli, zilitangazwa jana na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan ametangaza kifo akisema Magufuli alifariki dunia saa 12 jioni kwa maradhi ya moyo baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Machi 6.

Amesema awali, Rais Magufuli alifikishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Machi 6 akisumbuliwa na tatizo la moyo la mfumo wa umeme ambalo alikuwa nalo kwa zaidi ya miaka 10.

“Machi 14 mwaka huu, alijisikia vibaya akakimbizwa hospitali ya Mzena ambako aliendelea na matibabu chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete hadi umauti ulipomkuta,” amesema Mama Samia.

Amesema Tanzania itakuwa katika kipindi cha maombolezo ya siku 14 na bendera zitapepea nusu mlingoti. Alisema wananchi watajulishwa juu ya taratibu za mazishi za kiongozi huyo mkuu wa nchi.

Tuesday, February 26, 2019

Saturday, January 13, 2018

Tanzia - Yona Fares Maro

The Late Yona Fares Maro  1988-2018

Rest in Peace

Inasemekana Kaka Yona Alijiua kwa Kunywa sumu baada ya ugomvi na mke wake.  Lakini pia huenda alikua na frustrations za tangu afungwe jela mwaka jana. Alikaa huko siku 60.
\



Huu ndo ujumbe wa Yona aliouacha nyuma ya kifo chake.....

Nimekuwa kwenye matatizo ya ndoa kwa miaka 4, kila wiki nikipambana na mke mlevi na mzinzi. Tukio la jana usiku na leo asubuhi limenisononesha na kunitia simanzi kubwa. Nimekata tamaa ya kila kitu na kila jambo nangoja mapenzi ya Mungu tu. Nalazimika kutumia dawa za usingizi lakini wapi. Sasa nipumzike nimwache mke wangu Eng Mloelya na mchepuko wake Eng Lossy wa Idara ya Maji Mbeya waendee!



Tuesday, February 07, 2017

Rais Mstaafu George H.W. Bush ni Mzima!

Wadau, siku Rais Donald Trump anaapishwa tulidhani kuwa Rais Mstaafu George H. W. Bush, yuko mahututi atakufa dakika yoyote. Mke wa Barbara naye alikuwa hoi hospitalini. Ajabu juzi tuliwaona kwenye mchezo wa Super Bowl, wakitabasamu,kupungia watu na hata kufanya coin toss, kujua nani atarusha mpira kwanza. Wataishi maisha mrefu hao. Sasa watu wanafanya matani !😂😂😂
j

Tuesday, September 13, 2016

Msiba Boston - Mrs. Aisha.Rupia

                                            Aisha Rupia, mume wake Paul Rupia na watoto wao.


Tunasikitika kuwajulisha kuwa Paul Rupia amefiwa na mke wake Aisha Rupia ambaye ametutoka leo alfajiri 9/13/2016.  Mungu amlaze mahali pema peponi, Amin.
Msiba utakuwa nyumbani kwa Paul, 16 Feener Circle, Randolph, MA.
Mipango ya mazishi inaendelea, tutawajulisha zaidi hapo baadaye.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na...
Paul Rupia 781-913-9363
John Rupia 857-251-4408
Stella Rupia 617-792-8815
Abela Haley 781-913-2107


It is with great sadness that we announce Aisha Rupia, wife of Paul Rupia has passed away today 9/13/2016. May God Rest her soul in Peace, Amen.  The bereavement will be at their house, 16 Feener Circle, Randolph, MA. Further information will follow after funeral arrangements have been finalized.
For more information, contact...
Paul Rupia 781-913-9363
John Rupia 857-251-4408
Stella Rupia 617-792-8815
Abela Haley 781-913-2107

Wednesday, September 07, 2016

Mama Bishanga na Wadogo Zake Wafiwa na Mama Yao

MAMA BISHANGA NA WADOGO ZAKE WAFIWA NA MAMA YAO

         MWALIMU AGNES NDEMBO HATIA
Watoto wa marehemu mzee Isaya Innocent Hatia tumempoteza mpendwa mama
yetu mpendwa Mwalimu Agnes Ndembo Hatia kilichotokea hospitali ya Regency
 jana jumamamosi mchana. Mama yetu alikuwa nguzo pekee iliobakia nasi baada
ya kufariki baba yetu Mzee Isaya Innocent Hatia mwaka 2011. Tunamshukuru
Mungu sana kwa upendo wake kwa mama yetu aliempa nguvu ya kuishi miaka
tisini na sasa amempenda zaid mama yetu, bibi yetu na amempumzisha usingizi
wa milele na milele Ameni
Mwalimu Agnes Ndembo Hatia amefundisha watu wengi sana darasa la kwanza
tangia miaka ya hamsini hadi alipostaafu Tabora, Uhuru shule yamsingi.
Mama, ametuacha watoto wake Christina wa USA, Geofrey wa Namibia, Mwl
Mark Hatia wa Tambaza shule ya secondary, Bernadetta wa Dar, Isaya wa Finland,
Costancia wa Kibaha, na Oscar mdogo wetu wa mwisho. Ameacha wajukuu, na
vitukuu wengi ambao ni watoto na wajukuu zetu sisi watoto wake pamoja na dada
zetu marehemu Joyce Hatia na Mwalimu Cecilia Hatia. Picha zinaonyesha
mama Hatia mwaka 1966 akiwa na Constacia ambae picha yake pembeni ni Costancia
alivyo sasa, na zingine ni mama na wanae wajukuu na vitukuu
Kwa taarifa za maandalizi na ratiba piga simu zifuatazo. 0653 763 201 Kilian Kamota,
0755 333 948 Dick Hatia, 0788 627 430 Ibra Yunus, na 0763 833 893 Solmon.
 BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA. TUMSIFU YESU KRISTO: AMEN
 

Sunday, August 14, 2016

Tanzia - Mh. Mzee Aboud Jumbe

Rest in peace Mh. Mzee Aboud Jumbe. (1920 - 2016)

Saturday, June 04, 2016

Muhammad Ali Alipotembelea Tanzania 1980

Wadau, Nina kumbuka vizuri marehemu Bondia Muhammad Ali, alipokuja Tanzania kutembea mwaka 1980. Watu walikuwa na  kiwewe kumwona shujaa wao Vijana walivamia fensi na  kukimbiza ndege yake pale airport  Dar!   Watu walisema bora Ali angemtwanga Mzee Nchimbi (picha ya pili). Sijui kwa nini walikuwa wanamchukia.

Muhammad Ali amefariki dunia leo katika hospitali huko Arizona.  Alikuwa na miaka 74.  Alkuwa na ugonjwa wa pneumonia.  Lakini pia alipambana na ugonjwa wa Parkinson's disease (mwili ktetetmeka) muda mrefu.  

Rest in peace Muhammad Ali (1942-2016). 

Kusoma historia ya Muhammad Ali BOFYA HAPA:



Sunday, May 15, 2016

Shukurani Kutoka Kwa Familia ya Michuzi - Msiba wa Maggid Muhidin

Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi inapenda kutoa shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa, majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika Kusini Jumapili ya wiki iliyopita na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.
Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu. Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko wengi mno.
Pamoja na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na familia yao yote, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Ombeni Sefue pamoja na wafanyakazi wenzie wote wa baba mfiwa kwa kuwa karibu naye katika wakati wote, na kuhakikisha kuwa kila kitu katika msiba huu kinaenda sawasawa. TUNAWAOMBEA KWA MOLA AWAPE BARAKA ZAKE ZOTE...

Salamu zingine za kipekee ziwaendee watumishi wote wa Ubalozi wetu Afrika kusini mjini Pretoria ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na Afisa wa Ubalozi kaka Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha mwili kutoka Durban kuja Dar es salaam. MOLA AWAONGEZEE PALE MTAPOPUNGUKIWA...

Vile vile shukrani za kipeke ziwaendee Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania waishio Durban pamoja na Muslim Burial Society ya hapo hapo Durban ambao walihakikisha mwili wa marehemu unahifadhiwa, unakafiniwa na unasafirishwa kwa heshima zote. ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO...

Kwa Uongozi wa msikiti wa Maamur uliopo Upanga Dar es salaam pia familia inatoa shukurani za kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni pamoja na mwongozo wa kidini katika wakati wote wa msiba na mazishi.
Tutakuwa watovu wa fadhila endapo kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa magrupu ya WhatsApp yote ambayo baba mfiwa Ankal ni mwanachama. Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group (KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari, Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas, RUBY 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani. TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA KWA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA...
Mwisho, lakini sio kwa umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani za kipekee kwa shirikia la ndege la Emirates kwa kufanikisha usafiri wa mwili wa marehemu, hali kadhalika kampuni mahiri ya SWISSPORT kwa kusaidia logostics zote katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.

HATUNA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUTOA SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA WENU AWABARIKI KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE...

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un

AMIN!




Saturday, May 14, 2016

Mazishi ya Maggid Muhidin Leo

CODES:
Mwili wa marehemu ukiingizwa katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es salaam leo tayari kwa kuswaliwa kabla ya mazishi.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kushoto) akimfariji baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi.
Mama wa marehemu (aliyevaa nguo nyeupe) akiwa na ndugu wa karibu wakiomboleza.
Baba wa marehemu akiwa na viongozi wa dini wakiombea mwili wa marehemu dua.
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na ndugu wa marehemu.
Baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi akipata chakula.
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwasili msibani Wazo hill akiwa na baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi.
Baba wa marehemu akiwa na Balozi Cisco Mtiro na baadhi ya waombolezaji.
Baba wa marehemu (mwenye kofia), Ankal Issa Michuzi akipewa pole na baadhi ya waombolezaji mara baada ya maziko ya mtoto wake Maggid Muhidin Michuzi (18)yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akimpa pole Issa Michuzi.
Rais Mstaa mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akimfariji Ankal Issa Michuzi.
Issa Michuzi (mwenye kofia) akifuatiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe Ombeni Sefue. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo wakati maziko.
Waumini wakiomba dua.
Baba wa marehemu Issa Michuzi (katikati) akiwa na huzuni akiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde
Baba mkubwa wa marehemu, Ismail Issa Michuzi akitoa shukrani kwa walioshiriki mazishi ya mtoto wao.
Mroki Mroki ambaye aliyekuwa MC akitoa ya muongozo wakati wa mazishi.
Waombolezaji wakiweka udongo kwenye kaburi la marehemu.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi akiweka udongo.
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akiweka udongo kaburini.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiweka udongo kaburini.
Baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi akiweka udongo kaburini.
Mwili wa marehemu ukiwekwa kaburini.
Mwili ukiwasili makaburini.

Rais mstaafu Jakaya Kikwete akimpa pole baba wa marehemu, Ankal Issa Michuzi. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi. Picha zote na Francis Dande