Showing posts with label Lukwangule Entertainment. Show all posts
Showing posts with label Lukwangule Entertainment. Show all posts

Friday, November 21, 2008

Walimu Wachachamaa Tena!

Walimu wakitafuta majina yao


OFISI za maDC na Maded wa Temeke na Kinondoni leo zilipata matatizo kidogo wakati walimu walipovamia kutaka kujua kulikoni baada ya majina yao kutokuonekana katika karatasi za malipo kwenye mbao.Pichani ni walimu wakiangalia majina yao.Imeelezwa kuwa wilaya ya Kinondoni zaidi ya walimu 200 walijiandikisha kuuliza kulikoni kwingine wakafanya maandamano.

OniSomething is wrong somewhere kwanini taarifa sahihi zisitolewe kuhusu nini kinafanyika mbona watu wanafanya vitu vionekane kama matusi? Na nilipowatafuta jamaa kujazia stori kila mtu akawa anaruka kimanga. Kuna shida kwelikweli na ofisi hizi za umma, utafiti vile wanalinda magunia ya bangi. - Lukwangule
********************************************************
Nami nauliza hivi Tanzania walimu wetu wanadhauruliwa kiasi hicho? Hao walimu wanakazi nzito ya kuelimisha watoto wetu. Kazi wataweza kufanya vizuri kweli kama wanakuwa na wasiwasi wa kulipwa mshahara, tena ambao wamekwishaifanyia kazi? Hii ni aibu sana. Zamani shule za serikali zilikuwa za hakika lakini siku hizi mmmmh!- Chemi

Thursday, August 21, 2008

Kulikuwa hakuna Makuu!

Rais Kikwete akihutubia Bunge leo

Imeandikwa na Beda Msimbe

Gumzo la lukwangule:Nilichovuna saa 4 za kumsikiliza rais

JANA nilisema kwamba kutakuwa na makubwa leo. Naamini saa nne za kumsikiliza JK hazikuzaa hasara kama mtuma habari. Lakini kama mchambuzi wa masuala ya kisiasa na kiuchumi yapo makubwa yaliyoainishwa na kutolewa ufumbuzi ambao unaweza usiwe bora leo lakini miaka kadhaa ijayo.

Jambo la msingi ambalo mimi nimeliona ni kuwa masulaa niliyodhani atayagusa aliyagusa, sikutarajia mengi makubwa katika EPA kwa kuzingatia mfumo wa sheria wa nchi yetu, lakini kwa sasa wabunge waliokuwa hawaelewi nini EPA sasa watakuwa wameelewa.

Nilichotoa hai katika EPA ni kufilisiwa kwa watu, kunyimwa nafasi ya kusafiri na fedha hizo zinazorejeshwa kusaidia wakulima kwa kuanzisha ruzuku katika mbolea na pia katika kusaidia TIB yaani Tanzania Investment Bank kuwa na uwezo wa kukopesha wakulima kwa muda nrefu na riba nafuu.

Swali linalobaki je hawa wahuni waliotwaa fedha ambazo si za serikali lakini serikali inaweza kudaiwa watafanywa nini? Matajiri azimio la Arusha walishughulikiwa kwa kurejesha mali zao kwa umma je hawa hawastahili kweli kushtakiwa, wanasheria wanajua lakini la maana zaidi utawala wa sheria hauna maana ya kuachia wakwivi kutokomea hivi hivi tu lakini pia si kwa kuwafanya waingie mahakamani bila kigezo, hawa ni wevi au wajanja hilo ni swali kwanza kisha... waswahili wanasema habari ndio hiyo... lakini amesema kwamba Novemba Mosi kitaeleweka mahakamani.

Nilisema shauri la Zanzibar lakini kidiplomasia kabisa kasema watu wasikoroge mambo na kwamba ukiwa nje ni tanzania ukirejea hapa unazungumza zanzibar, alitumia akili sana kuhusu hili hasa aliposema wimbi hili nalo litapita walio watu wazima wasiwe wapuuzi, nadhani kimeeleweka.

Rais Jakaya Kikwete akilihutubia Bunge hilo kwa mara ya pili tangu ashike madaraka mwishoni mwa mwaka 2005 nilichoona kama alivyowahi kusema katika hotuba yake ya kwanza alitumai tena fursa hiyo kuelezea mwelekeo wa uchumi wa taifa na masuala mbalimbali ambayo serikali yake imekuwa ikiyapa kipaumbele.

Na shida zote alisema tusigombee fito, tunajenga nyumba moja na hili siwezi kulikataa, lakini inakuwaje unapokuwa na watu ambao hawaelewi hasa nini wanatakiwa kukifanya, na watu hao wakiwa viongozi? Lipo tatizo la ufinyu wa sheria na utawala pengine Sitta yuko sahihi sheria zetu zinaruhusu mambo kuenenda kigoigoi zaidi.

Huu muungano nao aliuzungumzia vyema, alisema wazi ubaya wa uropokaji, alisema matamshi ambayo yamekuwa yakitolewa na baadhi ya viongozi yanaweza kuchangia kuwavuruga kama siyo kuwachochea wananchi.

Ilivyo ni kwamba kama ni kujadili suala la Muungano basi hapana budi mjadala ufanyike kwa hekima na busara na siyo jazba kama ambavyo imejitokeza katika siku za karibuni, hili siliendelezi sana.Na huu mpasuko wa Zenj kumbe ulishafikia hatua nzuri lakini jamaa hawa wa Unguja kama wanavyosema katika suala la U nchi na Usio nchi amesema wanashindwa kuaminiana.

Kitu ambacho nilikiona kuwa kidogo cha mgomo, kumbe sivyo, rais alizungumzia haki ya watu kugoma, lakini ndani ya sheria, ndani ya uelekezi wa kawaida uliokubalika, kama kweli ni mgomo unaostahiki. Hapa alifafanua vyema kuhusu mgomo unaokuja, hakuugusia wa walimu lakini huu wa TUCTA alisema mpaka kwa Kiingereza haukubaliki. Alikuwa na vigezo vyake.Alisema kwamba mfuko wa hazina baada ya makubaliano sio ATM ni lazima kuweka sawa baada ya bajeti na walizungumzia Agosti sasa watu watazame kama serikali haitalipa.

Kweli kabisa serikali kwa mgao wa kota si ATM lakini nini maana ya maneno yote hayo ambayo serikali inazungumza. Inamaananisha kwamba haipo tayari kuyumbishwa, makubaliano ni muhimu watu wa TUCTA wanajua wamevumilia kiasi gani lakini wachambuzi wa mambo wa naweza pia kuelewa kwa kina nini maana ya kauli ya serikali kuhusiana na njia zilizotumika kutangaza mgomo.

Shauri la mwisho ambalo mimi nilisema ni la kawaida ni matumizi mabaya ya uhuru wa kunadika na kusema, maandamano,kupiga domo, kupinga serikali,kushughulikia hasira na kutuliza munkari.kwa haraka haraka unaona kwamba alikuwa anachimba mkwara, lakini kama yeye aliwezesha upana wa mambo katika kucheua sumu mwilini alitaka watu wawe wastaarabu wasitapike bila mpangilio wakawavushia matapishi wenzao wakabaki wananuka bila sababu.

Hili halina ubishi kucheua sumu muhimu lakini utapike kwa mipangilio na uwe na sababu sio uachie tu mradi mdomo wa kutapikia unaoKimsingi mimi nasema rais saa zake nne hazikuwa mbaya sana ingawa haya mengine ni elekezi za kawaida za nini amefanikisha katika miaka miwili na miezi saba ya utawala wake, kilichobaki ni kuangalia ushauri wa spika kwamba kunahitajika kasi zaidi kushughulikia wanaohujumu uchumi kwa mtindo wa EPA.

Naam, kweli tunahitaji mabadiliko kwani hii ni salamu, kazi yenyewe bado iko kwa wananchi wenyewe, ni hotuba inayotakiwa kuchambuliwa, kuna mengi sana ambayo sikuyatia hapa kwani huenda yakasaidia miaka mitatu ijayo wakati wa uchaguzi: ni ukweli kuwa wanaobungua nchi hii ni viongozi wafanyabiashara kwa hiyo tunahitaji waamue ama kuwa na biashara au kuwa wanasiasa na viongozi, hata ughaibuni linajulikana.

Wednesday, July 23, 2008

Wabongo wachemsha tamasha la filamu la ZIFF?

Maoni ya Kaka Beda Msimbe Lukwangule Entertainment Blog:

Wabongo wachemsha tamasha la filamu la ZIFF?

There is something very seriously wrong with Tanzania artist and this can been seen katika tamasha la filamu la kimataifa linaloishi ndani ya nchi hii ZIFF ambalo hufanyika Zanzibar kila mwaka. What is wrong jamani!!!!!

Nikiandika katika busati la filamu Habari leo Jumapili nilishawahi kusema jamani tutumbukize filamu huku kwani ipo nafasi ya kwenda maeneo mengine, kukosolewa na pia kuna sababu... lakini Roma haikujengwa kwa siku moja, lazima tusonge mbele.. kwa kujionyesha hadharani.. lakini wapi kw amara nyingine tena tamasha la 11 lina upungufu mkubwa wa local component.

Watu wanatoka all the way from Europe,America and Far East to look for nafasi just to shoo his or her film but Watanzania wanaozalisha filamu kwa fujo kwa sasa wamepeleka filamu hizi zifuatazo na moja nadhani ni ya Da Chemi huko Marekani, Bongoland II ambayo katika entry imeelezwa director wake ni Josiah Kibisa.

ZIFF hufanyika Zanzibar kila mwaka na ni tamasha kubwa kama hutaki filamu yako iingie katika mashindano lakini angalau uonyeshe basi kwa watu:Nini majidai kama hatuwezi hata kufanya kweli kwenye tamasha lenye heshima Afrika Mashariki na Kati?

CEO wa ZIFF mtanzania mwenzetu, manake nasikia wakati ule (zamani) watani zetu wakiingiza filamu kama nyuki tulikuwa tunasema ohh Foreigners hawatutakii mema, sasa huyu mswahili wa Tanga mwenye utaalamu wa filamu ambaye ameishi ughaibuni na anafundisha ughaibuni ametoa wito sana toka mwaka jana akililia filamu za nyumbani lakini mwe wamesema waluguru chilanga komo, yaani unayashangilia maji halafu unakuwa kama huna akili nzuri jamaa wanakucheka, tuache hayo kwani tulikuwa tunazungumzia filamu zilizoingia ZIFF kutoka hapa nyumbani nazo ni hizi zifuatazo:Bongoland ll,Mwanahiti l (oloibon na Layoni)na ll Zawadi ya Fisadi;The Trip ya James Gayo; Sasa na Jando.

Can you imagine?

Watu sijui niwasemeje, labda sijui woga? Haya hatukupeleka hizo sineema zetu je tutaenda kuhudhuria kujifunza manake nasikia kuna manguli wa filamu kutoka Amerika ya Kusini, Amerika kaskazini, Nigeria na Asia ya mbali wanakuja kutufunza mambo ya ABC za utengenezaji sinema, tutakwenda?

Mimi yangu macho.CEO wa ZIFF Dr Martiun mhando amesema kwamba hakuwa na chaguo la kutosha kwani hata zile zilizoletwa hizo zitakazoonyeshwa ni nafuu zaidi na yeye anasema I wonder, kweli hata mimi namuunga mkono I wonder.Hatuwezi kukua kisanii kama tusipokubali kuwa tunamapungufu na lazima tuwasikilize watu watusaidie.