![]() | |
| Bendera ya Tanganyika |
Imeandikwa na Mdau VM
Ni lini tuta sherehekea Uhuru wa Tanganyika?
Kila mwaka utasikia sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara!!!!!
Ni lini sasa tutasherehekea Uhuru wa Tanganyika? Hivi kweli huu ni umbumbumbu wa Historia kwa miongoni mwetu watanganyika au ni unyanyapaa wa Tanganyika, na ustaarabu kwa Z'bar? Mimi Sipendi!
Mapinduzi ya Z'bar yapo kila Januari 12 tena kwa mbwembwe zote, sherehe za kumbukumbu ya Muungano zipo kila Aprili 26 kwa kwa kila hamasa, lakini Uhuru wa Tanganyika ni lini??? Mimi sipendi!!!
Tunaambiwa eti Uhuru wa Tanzania Bara! Sipendi!!!
Ok. Potelea mbali. Sasa hivi Tanzania Bara imefikisha umri gani? Miaka 47 au 50? Hivi Tanzania Bara haikuzaliwa Aprili 26, 1964. Sasa hiyo ni miaka mingapi, 50 au 47? Mi sipendi kabisa kuvuruga na kuchanganya historia.
Sipendi watoto wetu, wadogo zetu, kupotoshwa kwa makusudi kuhusu Uhuru wa Tanganyika! Tunawadanganya ili iweje? Sipendi kabisa!!!.
Siendi kwenye sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara wala siangalii televisheni kuhusu uhuru huo, hadi ntakapo sikia tunaazimisha miaka kadhaa ya Uhuru wa Tanganyika! Labda mnisaidie kuelewa, vinginevyo hakuna. Asante.
Vins



