Showing posts with label Mlimani City. Show all posts
Showing posts with label Mlimani City. Show all posts

Tuesday, August 26, 2014

Jamaa Aibiwa Baada ya Kutoka Benki Mlimani City

Hali inatisha.Allah atusalim salama! 


JAMANI HALI INATISHA SANA,NIPO HAPA NILIKUWA NA MTU NAFANYA NAE KAZI ANANIHADITHIA JINSI ALIVYOIBIWA PESA IJUMAA ILIYOPITA NIMEOGOPA,SIJUI TUFANYEJE TUWAPO NA PESA UUWIIIIIII.

NAHISI KABISA WAHUDUMU WA BANK AU MAMENEJA WA BANK WANASHIRIKI HUU MCHEZO,ANASEMA ALICHUKUA MKOPO NMB SH MILIONI 30!!KWA NIA YA KUMALIZIA UJENZI,SIKU YA IJUMAA KUNA KAZI ALITAKA KUFANYA NA FUNDI KUNA VIFAA WALITAKIWA WANUNUE PAMOJA NA GHARAMA ZA UFUNDI INGEFIKA KM MILION 10 HIVI,AKAENDA BANK MLIMANI CITY KUCHUKUA HIZO PESA,

AKIWA TAYARI AMESHAZICHUKUA FUNDI AKAMPIGIA SIMU KUWA AMEFIWA KWA HIYO KAZI HAITAFANYIKA KWA SIKU 3,YULE KAKA AKAONA ASIKAE NA PESA NYINGI HIVYO AKAAMUA AZIWEKE TENA MILION 7 ABAKI NA 3,NAHISI ALIVYOCHUKUA ZILE PESA AKAWA AMESHALENGESHWA,ALIPOTOKA TU BANK AKAPIGIWA SIMU NA MTU MWINGINE WALIONGEA DILI LA TILES KUWA AMRUSHIE M 1 KWENYE M PESA MAANA DILI LIKO TAYARI,AKAINGIA PALE VODA AKAWEKA PESA AKAMTUMIA AKABAKI NA M 2 AKAWEKA NA NYARAKA ZAKE FULANI MLE KWENYE BAHASHA YA FEDHA,AKATOKA,ANASEMA MUDA WOTE KUNA KIJANA ALIKUWA ANAMFATA NYUMA AKIINGIA SEHEMU YULE KIJANA ANASIMNAMA NJE KUZUGA LKN HAKUMTILIA MAANANI,AKAINGIA KWENYE GARI AKAONDOKA KUPITIA GETI LA UPANDE WA SURVEY,ILE ANAKATA KONA PALE ZINAPOPAKI BAJAJ KUNA PIKIPIKI IKAM BLOCK,AKAJA KIJANA MMOJA DIRISHANI ANA BASTOLA AKAMWAMBIA TUPE HIZO MILION 10 ZETU,USIPIGE KELELE KISHA ONDOA GARI FASTA,KWA KUKUHURUMIA HATUKUUI,TUPE HELA NA HUO MKOPO TUTAUTUMIA WOTE!!!.

YULE KAKA ANASEMA ALIBAKI MDOMO WAZI,HAWA WATU WAMEJUAJE KM NIMEKOPA??BASI ALICHOFANYA AKAWAPA ILE BAHASHA FASTA IKIWA NA MILION 2 LKN IMETUNA NA YALE MANYARAKA MENGINE WAKAJUA MILION 10 IKO MLE KUMBE MWENZAO ALIZIRUDISHA NYINGINE,AKAONDOA GARI MBIO,ANASEMA ILE TU KUNUSURIKA KUFA ALICHANGANYIKIWA AKATOKA MBIO MOJA KWA MOJA HADI MSIKITINI MWENGE,AKASWALI KUMSHUKURU MUNGU,AKARUDI NYUMBANI,ANASEMA ANAOGOPA KBS KWENDA TENA BANK NDO ALIKUWA ANAOMBA NIMUELEKEZE JINSI YA KUHAMISHA FEDHA TOKA KWENYE ACOUNT KWENDA M PESA ILI AWE ANATOLEA KWA WAKALA,TUWE MAKINI JAMANI PESA ZETU WENYEWE ZITATUUA!!!

 

Monday, July 21, 2014

Tapeli Lililojidai Kishoka wa TANESCO Adakwa Live Mlimani City

10500539_819006161445574_7780628803053090260_n

Pichani juu na chini ni Kishoka wa Tanesco aliyekamatwa Mlimani City.

Na Mwandishi wetu

TAPELI lililokubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka washirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.

Kwa mujibu wa Bi. Usia akieleza tukio hilo, alidai kuwa tapeli huyo alifika asubuhi akiwa na wenzake sita, nyumbani kwake wakasema wanatoka Tanesco wamekuja kucheki mita ya Luku. Hata hivyo wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung'oa mita, eti waliona kwenye GPS yao kuwaUmeme hauendi vema.

“wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa kinafyatuka halafu Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.

Na kuongeza kuwa vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange. tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuitePolisi, basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme, nikawaambia naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi chuo nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani, tukawakuta wameondoka.

Mzee akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City, tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo, tukaandikisha maelezo. tunasubiri hatua itakayofuata.

10417599_819006198112237_2101442257557265538_n  

Hapa likiwa chini ya ulinzi na pingu mkononi.

--

Tuesday, November 25, 2008

Yaliyompata Mdau Mlimani City

Nimeletewa hii na mdau huko Dar:

******************************************************

TAHADHALI WATANZANIA WENZANGU

Jumamosi ya juma lililopita tarehe 22 majira ya jioni,

Nilipata nafasi ya kutembelea duka la nguo lijilikanalo Mr.Price hapo mlimani city,

Katika kujichagulia nikapenda na top moja nyeupe,mi nikaenda kuijaribisha ile top,pamoja na nguo zingine nilizozipenda,wakati naangia na ile nguo,yule dada amabye yuko mlangoni kwenye chumba cha kubadilisha akaniambia angalia nguo yangu nyeupe usije ukaichafua,ah mi nikamwambia kwa mfano ikitokea ikachafuka itakuwaje akasema ah aha mi nakuambia tu,basi mie nikajaribu kwa umakini sana tena sana lakini haikunitosha so ikawa sio chaguo langu tena,ile nguo ilivyotoka nje baada ya dakika 10 wakati najaribu nguo nyingine na kunitosha ndo nikawa naelekea kaunta kulipa zile zilizonitosha yule dada akaniitia walinzi wao kuwa nimechafua shati lao jeupe kwa wanja(make up ya machoni),na sheria yao ni kwamba mtu akichafua nguo lazima alipe.basi wakaning’an’gania nilipe ile top ya thamani ya Tsh22,000/= .kwa kweli nilighadhilika na kuwaambia kuwa mimi sitaweza kulipa maana sikuona kuwa nimechafua na kama nimeichafua ni bahati mbaya na wala hamkuniambia kuwa kuna malipo iwapo mteja akitokea kudamage nguo,basi nikawaambia hapa kwenye kapu nina nguo ya thamani ya 150,000 na hii top moja mnayotaka kuninunulisha ni 22,000 tu sasa nilipie hizi zilizonisha nah ii niache au niziache hizi za laki na nusu,wakasema utajua mwenyewe,na hapo uku mie mteja napewa lugha za kashfa na dharau mtindo mmoja kutoka kwa hawa wafanyakazi wa humo MR PRICE..Basi mie nikaawaambia mie narejesha hizi za laki na nusu na kulipia moja ya 22,000/= wakasema kwa jeuri sawa.sasa sijui hapa nani kaumia ni mimi ambaye iyo Top nilimpa mdogo wangu hapo hapo maana ilikuwa inamtosha au wao kuleta sifa mbaya na kutokuwa na customer care na kupoteza laki na nusu na kuku bali 22,000 pia kupoteza wateja?

Maana sikatai kuwa kuna watu wananunua hadi laki5 but mteja ni mteja tu hata kama akiwa mweusi mwenzio na wewe uko unafanya kazi kwenye duka la mzungu sasa unajiona na wewe mzungu,na kudharau wabongo wenzio.

Hii ni tahadhari kwa WaTanzania wenzangu watembeleapo maduka ya MR Price pale mlimani city dar es salaam,unaweza ukapata kiherehere cha kujaribu nguo labda kwa lengo la kuja kuifata kesho then ukawa hauna pesa,utajikuta umegadishwa kwa muda mrefu na kupoteza muda wako kwa wabaguzi na wasiojua biashara ya nguo kama hawa.

Ni hayo tuu.

MDAU