Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, mafundi na wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO wameanza kufuatilia kujua chanzo chake hasa ni nini na taarifa Zaidi zitatolewa kila baada ya muda ili kuufahamisha umma na watuamiaji wa umeme.
Saturday, December 02, 2017
TANESCO: HITILAFU KWENYE GRIDI YA TAIFA IJUMAA
Kwa mujibu wa Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, mafundi na wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO wameanza kufuatilia kujua chanzo chake hasa ni nini na taarifa Zaidi zitatolewa kila baada ya muda ili kuufahamisha umma na watuamiaji wa umeme.
Saturday, September 13, 2014
Tanzanian Appointed Head of Rusumo Power Project
Monday, July 21, 2014
Tapeli Lililojidai Kishoka wa TANESCO Adakwa Live Mlimani City
Pichani juu na chini ni Kishoka wa Tanesco aliyekamatwa Mlimani City.
Na Mwandishi wetu
TAPELI lililokubuhu kwa masuala ya kulaghai watu kwa njia ya kujifanya kishoka washirika la Umeme Nchini, Tanesco, jana asubuhi limedakwa baada ya kuwekewa mtego walipokuwa wakitaka kutapeli kwa mmoja wa Afisa wa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma- Ledama.
Kwa mujibu wa Bi. Usia akieleza tukio hilo, alidai kuwa tapeli huyo alifika asubuhi akiwa na wenzake sita, nyumbani kwake wakasema wanatoka Tanesco wamekuja kucheki mita ya Luku. Hata hivyo wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata Umeme na kung'oa mita, eti waliona kwenye GPS yao kuwaUmeme hauendi vema.
“wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia. nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi? si ingepaswa tulipe kidogo? wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba Umeme) huwa kinafyatuka halafu Umeme unakwenda zaidi! “ alielezea Bi. Usia.
Na kuongeza kuwa vishoka hao wakakata Umeme wakaondoka, tujipange. tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halafu wanalazimisha mambo, wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki. tukapiga simu Tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuitePolisi, basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie Umeme, mengine Jumatatu. wakaja fasta wakarudisha Umeme, nikawaambia naenda aTM wasubiri nikawaacha na mzee nikatoka mbio mpaka Polisi chuo nikawahadithia wakanipa Polisi 3 nikaja nao nyumbani, tukawakuta wameondoka.
Mzee akawapigia simu waje hela imepatikana wakasema tukutane Mlimani City, tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia. tumemuacha selo, tukaandikisha maelezo. tunasubiri hatua itakayofuata.
Hapa likiwa chini ya ulinzi na pingu mkononi.
--Tuesday, November 27, 2012
Shilingi Bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatarini
PRESS RELEASE: Shilingi Bilioni 86 zaibwa Wizara ya Nishati/TANESCO, Gridi ya Taifa hatariniby zittokabwe |
Saturday, February 04, 2012
Bei ya Bidhaa Yapanda Ghafla Dar!
******************************************************
Kwa masikitiko makubwa, ninalazimika kuandika ujumbe huu kufuatia ninayoyaona sokoni leo.
Kwa bahati mbaya, anaeathiriwa na mabadiliko yote haya ni mlaji wa mwisho ambae ni mwananchi.. Kupanda kwa gharama ya umeme, kumeongeza bei za vitu kwa takribani asilimia 25 hadi 40.
Mfano, maji ya Azam (1 lt) yalokuwa yanauzwa kwa Tzs 500 sasa ni Tzs 600. Yale ya (1/2 Lt) yanauzwa Tzs 400 na yale ya (1/4 Lt) yanauzwa Tzs 250. Bei hizi ni kuanzia leo. Maji hayo kwa bei ya jumla yamepanda kwa takriban Tzs 700 kwa kila carton.
Kwa bahati mbaya, makampuni mengine ya ya maji ya kunywa kama Kilimanjaro, Sayona na Maisha nayo yako mbioni kupandisha bei. Bei ya cement na nondo nayo imepanda na viwanda hivyo navyo vinajipanga kupandisha bei ili kufidia gharama ya umeme.
Viwanda vya bia navyo vimepandisha bei jana kwa Tzs 6000 kwa crate kwa bei ya jumla. Bia ya Serengeti haijapanda lakini nayo iko njiani kupanda. Kwa ufupi, mfumko wa bei (Inflation) itafikia 23% hadi 25% mwezi huu kama serekali haitachukua hatua za ziada kupunguza machungu hayo ya umeme.
Kwa ufupi, tunahitaji mabadiliko makubwa sana ya safu yote ya uongozi wa nchi hii, tangu serekalini hadi kwenye mashirika ya umma, ili kuleta tija na kuwa na maamuzi yasiyo ya kisiasa.
TUFANYE NINI kubadili hali yetu ya maisha kwenye mfumko wa bei unaosababishwa na kupanda kwa bei za mafuta na umeme?
Mdau EK
Thursday, December 01, 2011
TANESCO Kupanda Bei ya Umeme 155%!!! Nchi Imehribika! Mkutano Kesho!
Kesho tarehe 2 Disemba 2011 katika Ukumbi wa Makumbusho Dar es salaam (mkabala na IFM) kuanzia saa 4 asubuhi EWURA imeitisha Mkutano wa Wadau kujadili ombi la TANESCO la kupandisha bei ya umeme kwa wastani wa 155% (zaidi ya mara tatu ya bei ya sasa).
Nawaomba wanamtandao wote tuhamasishe umma kwa kutumia TEHAMA (sms, facebook, twitter, email na njia nyingine) ili wananchi waweze kuhudhuria mkutano husika kwa wingi na kutoa maoni.
Mtakumbuka kwamba tarehe 23 Novemba 2011 nilitoa taarifa kwa umma kwamba Serikali inapaswa kusitisha ombi la dharura la kupandisha bei ya umeme kwa kiwango kikubwa ili kuepusha athari katika usalama na uchumi kutokana na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha. Aidha, serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka kulinusuru Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) dhidi ya mzigo mkubwa wa gharama unaotokana na ufisadi wa muda mrefu katika mikataba ya gesi asilia na gharama za mitambo ya kufua umeme wa dharura badala ya kuweka mkazo katika kuongeza bei ya umeme kwa wananchi wa kawaida.
Izingatiwe kuwa tarehe 9 Novemba 2011 Mamlamka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea ombi la dharura toka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kuidhinisha ongezeko la bei za huduma ya umeme kwa wastani wa asilimia 155 ya bei ya sasa (zaidi ya mara tatu).
Naomba umma wa watanzania uzingatie athari za maombi hayo katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla hivyo mjadala wa kitaifa unahitajika na natoa mwito kwa wananchi kuweza kutoa maoni yao kuanzia sasa. Aidha ni muhimu kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika mkutano wa kukusanya maoni ya wadau ulioitishwa na EWURA tarehe 2 Disemba 2011.
Umma wa watanzania ufahamu kwamba ongezeko hili sio ombi la TANESCO pekee bali ni agizo kutoka kwa serikali kwa kurejea maelezo ya Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja bungeni katika mkutano wa nne wa bunge na kusisitizwa na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda mwezi Septemba 2011 akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Mara.
Namshangaa Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake kwa taifa tarehe 18 Novemba 2011 alipozungumzia utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme hakuwaeleza watanzania kwamba uwasilishaji wa ombi hilo ni sehemu ya mpango huo wa dharura ambao utawaongezea wananchi bei ya umeme na gharama na maisha na hivyo kuathiri utekelezaji wa ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania.
Wananchi wakumbuke kwamba hii ni mara ya pili katika kipindi cha takribani mwaka mmoja kwa TANESCO kupandisha bei ya umeme; mara ya kwanza ikiwa mwezi Januari 2011 ambapo umeme ulipanda kwa asilimia 18.5 na kuchangia katika kupanda kwa gharama za uzalishaji katika nchi na kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.
Ombi la TANESCO la wakati huo la kupandisha umeme lilikuwa ni asilimia 34 likakataliwa na EWURA na kushushwa mpaka asilimia 18.5, sasa Rais Kikwete, Waziri Mkuu Pinda na Waziri Ngeleja wanapaswa kuwaeleza watanzania sababu za kufanya ombi hilo la dharura kuwa la wastani wa asilimia 155 ili wananchi waweze kutoa maoni kwa kuzingatia mzigo ambao umma unataka kubebeshwa.
Pamoja na matatizo ya kifedha ya TANESCO ambayo serikali inapaswa kuyashughulikia kwa pamoja na mambo mengine kutoa ruzuku katika kipindi hiki cha mpito; gharama kubwa za uzalishaji zinazolikabili shirika zinachangiwa na ufisadi wa muda mrefu katika mikataba ikiwemo ya uzalishaji wa gesi na ukodishaji wa mitambo ya kufua na pia maamuzi ya kukopa kibiashara katika kutekeleza mpango wa dharura wa umeme.
Kabla ya kuongeza bei ya umeme kwa watanzania wa kawaida, Serikali iwaeleze wananchi imewapunguzia mzigo kiasi gani kwa kupitia upya mikataba ya kifisadi inayolinyonya Shirika la Umeme Tanzania kama ilivyopendekezwa kwenye ripoti mbalimbali ikiwemo katika maazimio ya Bunge ya mwaka 2008 juu ya mkataba wa ukodishaji wa mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Richmond Develepment Company LLC ambapo orodha ya mikataba na makampuni mengine ilitajwa.
Aidha, umma uelezwe pia ukweli iwapo uamuzi wa kuchukua mikopo ya kibiashara yenye riba kubwa umeongeza zaidi gharama za uzalishaji wa umeme na hivyo kuifanya TANESCO iongeze zaidi bei ya umeme kwa wateja ikizingatiwa kuwa tarehe 15 Julai 2011 na 13 Agosti 2011, nilisisitiza bungeni serikali ipunguze bajeti katika maeneo mengine yasiyokuwa ya lazima na kuelekeza rasilimali nyingi zaidi kwenye umeme bila kuongeza mzigo mkubwa wa riba utakaolipwa na wananchi kupitia ongezeko la bei.
Uamuzi huu wa kupandisha kwa kiwango kikubwa bei ya umeme utasababisha ongezeko la ziada la mfumuko wa bei hali ambayo ni tishio wa usalama na uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla.
Serikali izingatie kwamba mfumuko wa bei nchini hivi sasa umefikia asilimia 17.9 na bidhaa zinazochangia mfumuko huo kwa kiwango kikubwa ni vyakula, mafuta na umeme. Kupanda kwa bei kwenye sekta ya nishati pekee kumekuwa kwa asilimia 37.4 na kusababisha kupanda kwa gharama za maisha, sasa viongozi wajiulize itakuwaje umeme ukapopanda kwa wastani wa asilimia 155.
Wananchi wakumbuke kwamba katika hotuba yake kwa taifa tarehe 18 Novemba 2011 Rais Kikwete ameelezea kwamba mfumuko wa bei na kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola kwa ujumla kumetokana na uchumi wa nchi mbalimbali duniani hususani za Ukanda wa Sarafu ya Ulaya (Eurozone) kuwa katika kipindi kigumu na cha mashaka na kueleza kwamba suluhisho la matatizo la uchumi wetu litategemea uchumi wao.
Kauli hii imedhihirisha kwamba Serikali haina mpango wa haraka wa kukabiliana na mfumuko wa bei, kuporomoka kwa shilingi na kupanda kwa gharama za maisha. Hali itakuwa mbaya zaidi iwapo tutaruhusu pamoja na sababu za nje ya nchi yetu tukaongeza vyanzo vya ndani vya kuongezeka kwa gharama za uzalishaji na bei za bidhaa kwa kupandisha bei ya nishati ya umeme ambayo chanzo chake ni hapa hapa nchini. Hivyo, mpango huu wa kupandisha bei ya umeme kwa wastani wa asilimia 155 unapaswa kusitishwa ama kubadilishwa kwa kulinda maslahi ya makundi mbalimbali kwa kuzingatia aina za matumizi.
John Mnyika (Mb)
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
1/12/2011
Sunday, July 31, 2011
Serikali Iombe Wananchi Msamaha - Mgao wa Umeme
*******************************************************************
Imeripotiwa kuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, ameitaka serikali iwaombe radhi wananchi kwa mgao wa umeme unaoendelea. Kauli hiyo ya Sitta imewafanya maadui wake ndani ya serikali, CCM na baadhi ya vyombo vya habari vinavyotumiwa kuibuka na kumuita waziri huyo kuwa ni msaliti na lazima afukuzwe kazi.Lazima tukubali kuwa tuna tatizo kubwa sana la uwajibikaji katika nchi hii. Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata umeme kwa ajili ya kuhakikisha ukuaji wa uchumi, upatikanaji wa huduma za jamii na maisha ya kila siku ya wananchi.
Leo hii, wastani wa asilimia 15 tu ya Watanzania milioni 44 wanapata umeme. Na serikali imeshindwa kuhakikisha kuwa asilimia hiyo ndogo ya wanaopata umeme wanapata huduma ya uhakika. Hapa ndipo dhana ya uwajibikaji inapokuja.
Kitendo cha serikali yenyewe kulazimika kuitoa bajeti ya wizara ya nishati na madini Bungeni ili
wakajipange upya ni ishara nyingine kuwa serikali haiko makini kwenye kutatua mgao wa umeme. Ni baada tu ya kuona kuwa Wabunge wamekuja juu na huenda hawatapitisha bajeti hiyo ndiyo serikali ikashituka usingizini na kusema wanahitaji muda wa kujipanga zaidi.
Wakati serikali imeongeza bajeti ya miundombinu kwa asilimia 85 na kufikia shilingi trilioni 2.78 ($1.73 billion), ilitenga shilingi bilioni 402.4 ($250m) tu kwa wizara ya nishati na madini katika kipindi hiki ambacho taifa liko kwenye janga kubwa la umeme. Ni kweli tunahitaji barabara, bandari, reli na airport, lakini ni lazima tuweke vipaumbele sawa. Kama pesa hazitoshi kufanya vyote kwa wakati mmoja, serikali makini ingetatua tatizo la umeme kwanza ndipo ijenge barabara.
Narudia tena, tatizo la umeme nchini si ukame. Ni matokeo ya serikali kutotoa kipaumbele kwa suala hili tangu ilipoingia madarakani. Ndiyo maana serikali imekiri yenyewe kuwa katika kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano, imeongeza megawati 145 tu kwenye gridi ya taifa. Lazima kuwe na hatua za dharura, muda mfupi na muda mrefu (immediate, medium-term na long-term) za kukabiliana na tatizo hili. Serikali inabidi isimamishe safari za nje, posho, semina, manunuzi ya Landruiser VX, na matumizi mengine ya anasa ili pesa zote ziende kwenye umeme. Na ikibidi hata ikope pesa nje ili kuwekeza kwenye umeme. Kwenye global financial crisis, serikali ilitoa 1.7 trillion shillings (over $1 billion) na kugawa pesa hizi kwa kampuni zenye utata. Leo hii serikali inasemaje haina pesa za kuzalisha umeme na kutoa $250m tu? Athari za mgao wa umeme ni kubwa mara dufu kuliko zile za global financial crisis.
Serikali inabidi ifanye budget re-allocation kubwa na kutoa pesa kwenye wizara na mufungu mengine na kuzipeleka kwenye umeme.
Huko Afrika Kusini mwaka 2008 wakati nchi hiyo ilipokutwa na tatizo la umeme, aliyekuwa Rais wa wakati huo, Thabo Mbeki, alikuwa na uungwana wa kwenda mbele ya Bunge la nchi hiyo na kuwaomba radhi wananchi kwa mgao wa umeme. Sijaona mkuu wa nchi yetu akichukua hatua kama hii.
Thabo Mbeki alisema kuwa Eskom (TANESCO ya Afrika Kusini) ilikuwa inaomba pesa serikalini kila siku iwekeze kwenye umeme serikali ikakataa na kuwambia wasubiri mpaka baadae. Mbeki akakiri kuwa Eskom ilikuwa sahihi na serikali ilikosea. Na akaomba radhi. Wataalamu wa TANESCO waliikataa Richmond, vigogo serikalini wakalazimisha wapewe mkataba na matokeo yake tumeyaona. Hakuna aliyeomba radhi, na mhusika kuu akabaki kusema hajutii maamuzi yake na kujisifu kuwa yeye ni hodari wa kufanya maamuzi magumu. TANESCO kila siku imekuwa ikiomba pesa za miradi mikubwa ya umeme lakini serikali imekuwa ikiwaambia waendelee kusubiri tu. Hakuna aliyekiri kosa, kuomba radhi wala
kuwajibika.
Angalia:
http://www.news24.com/SouthAfrica/Politics/Mbeki-apologises-for-power-cuts-20080208-2
http://www.iol.co.za/news/politics/mbeki-apologises-for-sa-power-cuts-1.382421
http://www.southafrica.info/about/government/stateofnation2008-electricity.htm
Idara ya hali ya hewa iko pale kufanya utabiri wa hali ya hewa. Hivyo basi, tangu mwaka 2005 walitabiri kuwa 2010/11 kutakuwa na upungufu wa mvua. Hata hii leo wanaweza kutoa utabiri wa hali ya hewa ya mwaka 2015/16 itakuwaje. Serikali ilikuwa na taarifa tangu miaka mitano au hata kumi iliyopita kuwa mwaka huu kutakuwa na mvua chache na hii itaathiri uzalishaji wa umeme, upatikanaji wa chakula, mfumuko wa bei, nk. Serikali iache kusingizia ukame. Iombe radhi kwa taifa kuwa mgao huu wa umeme unatokana na serikali yenyewe kutotoa kipaumbele kwa tatizo hili na kutojipanga kukabiliana nalo. Na iseme ukweli chanzo cha mgao ni nini, umeleta athari gani kwa taifa, serikali inafanya nini na tatizo hili litaisha lini. Serikali sikivu ingewaomba radhi wananchi wake. Na wananchi makini na wazalendo wangedai uwajibikaji kutoka serikalini, si visingizio vya ukame!
Mdau
Tuesday, July 26, 2011
Maoni - Umeme: Mahojiano Ya BBC Na JK
(pichani: Makao Makuu yaTANESCO HQ Ubungo)Umeme: Mahojiano Ya BBC Na JK; Tafsiri Yangu
Ndugu zangu,
Kuna mengine yamenipita hapa kati. Leo nimesikiliza mahojiano ya mwandishi wa BBC na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tatizo la upatikanaji wa umeme Tanzania.
Nimefuatilia pia maoni ya Watanzania mtandaoni juu ya majibu ya Kikwete. Tafsiri yangu; uongozi wa nchi ni kitu kigumu sana. Wengi wamemshambulia Kikwete kwa majibu yake kiasi wengine wamediriki kuandika; kuwa hatuna Rais.
Tunafanya makosa sana kutoa hukumu zenye kusukumwa na hisia hasi. Nimesikiliza mara mbili majibu ya Rais. Sikuona mahala pa kumshutumu Rais isipokuwa nimesikitishwa na maswali ya mwandishi wa BBC ambayo kwa Kikwete ilikuwa kama penalti alizokuwa akipigiwa mikononi na yeye kuzidaka huku akitabasamu.
Tusisahau, kuwa Kikwete ni mwanasiasa mahiri. Mwandishi anayekutana na Kikwete ni vema akajiandaa vilivyo juu ya namna ya kumbana Kikwete ndani ya majibu yake. Afanye hivyo ili kupata maswali mapya na hivyo basi habari mpya kutokana na majibu ya Rais.
Niseme tu, mahojiano yale ya Kikwete na BBC hayakutoa maswali mapya wala kuja na habari mpya. Na huo si udhaifu wa Kikwete bali mwandishi wa BBC aliyemhoji Kikwete.
Si tumemwona? Kikwete aliweza kucheza anavyotaka kwenye mahojiano yale. Na umahiri wake ulijidhihirisha pale alipogeuza sura ya mahojiano yale na Kikwete kuchukua nafasi ya mwandishi kwa kumbana mwandishi na husuan juu ya maarifa ya mwandishi katika eneo husika;
Wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo - tungeweza kufanya hivyo. Kikwete anamwambia mwandishi wa BBC.
Katika mahojiano yale Kikwete alikwenda na takwimu zake mfukoni. Kama moja ya mbinu katika sanaa ya mawasiliano ili kufikisha ujumbe, mara tatu ndani ya mahojiano yale Kikwete alizungumzia MW 600 zilizozalishwa tangu uhuru na MW 145 zilizozalishwa tangu 2009, na MW 160 zitakazozalishwa ifikapo Desemba mwaka huu. Jumla zitakuwa MW 305 tangu 2009. Na hapo ndipo kwenye hoja ya msingi ya Kikwete. Ana haki kuwashangaa wasioona jitihada zake.
Na Kikwete hakosi majibu ukimwuliza juu ya umeme wa jua, upepo na mvuke. Ana hoja anaposema kuwa umeme huo pia unahitaji mipango na kuwa huwezi kupata umeme wa jua kesho kwa vile jua linawaka.
Kama msikilizaji ningependa mwandishi ambane Kikwete kwenye maeneo ya ufisadi kwenye mikataba ikiwamo yenye kuhusiana na nishati ya umeme. Hakika, kama tungedhibiti ufisadi kwenye mikataba, basi, ni imani ya wengi kuwa tungejenga uwezo wa kuzalisha MW nyingi zaidi za umeme na kwa kasi kabisa, kulifanya tatizo la umeme kuwa ni historia. Tungeweza pia kupunguza gharama za mtumiaji wa umeme.
Tuna tatizo pia la baadhi ya wanasiasa kujiingiza katika kuwekeza kwenye eneo la nishati ya umeme. Wachague kati ya uongozi na uwekezaji. Kiongozi huwezi kuwa na hisa kwenye kampuni binafsi ya kuzalisha umeme na wakati huo huo ukalinda maslahi ya umma badala ya kampuni yako.
Vinginevyo, kwa waliokuwa na utayari wa kuelewa, mahojiano yale ya BBC na Kikwete yamempa nafasi Kikwete ya kujenga hoja ya msingi juu ya nini alichofanikiwa kufanya tangu aingie madarakani katika jitihada za kutatua tatizo la umeme nchini.
Nawasilisha.
Maggid,
Sweden, Jumanne, Julai 26,2011
http://mjengwa.blogspot.com/
Tuesday, March 01, 2011
LUKU Za TANESCO Zina Mambo!
Nasikia "wajanja" wa Tanesco wana-program LUKU, wewe unalipa Shs 1,000 kwa mwezi lakini unapata umeme wa kuweza kuwasha tanuru (kama unalo).
Malipo tofauti mnalipana chembaz na programmer.
Habari hizi umeshazipata au wewe hawakukufundisha hii programming pale Chuo cha Tanesco.
Sasa kama Tanesco wananunua umeme Dowans na kukuuzia wewe, hasara na faida tunajua napata nani :-)
Maelezo zaidi kuhusu THAMANI na BEI utatupiga "tuisheni" baadaye :-)
Halafu mnataka kutulaumu sisi tulioko Florida ........ati makosa yetu hatukusomea Chuo cha Tanesco.
Hebu DM atufafanulie kama anaujua huu mpango wa ku-program LUKU za Tanesco ili kujipatia umeme wa chee.
Huu ndiyo mpango wa UMEME KWANZA kwani KILIMO KWANZA ni kwa ajili ya Ng'wakitolyo
Uchakachuaji hadi kwenye LUKU.
Tanesco pandisheni bei ya umeme, watumiaji tuna mbinu zetu .....mechi droo.
Sijui "kisowia" ni nani kati ya Tanesco na wateja?? :-)
Mdau O.S. M.
Tuesday, January 05, 2010
TANESCO Mwogopeni Mungu!!!!
(Pichani: Askofu Zakaria Kakobe Akiongea na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam)5th January 2010
Akizungumza jana na Nipashe kwenye Kanisa hilo, Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Zacharia Kakobe, alisema vijana wake wamehamasika na wameamua kulinda kanisa lao kwa saa 24 hivyo Tanesco wasijidanganye kuwa wanaweza kuyaondoa mabango hayo.
"Vijana kama unavyowaona wako hapa kwa saa 24 kuhakikisha tingatinga likija kutaka kuyaondoa halifanikiwi maana huu ni uonevu dhidi ya Kanisa, na wamevaa sare ili iwe rahisi kutambulika kuwa ni waumini wa hapa," alisema Kakobe.
Fulana walizovaa waumini hao zilikuwa zimeandikwa “Tanesco mwogopeni Mungu, baada ya Richmond sasa mmeligeukia kanisa”.
Askofu Kakobe alisema mabango hayo yametengenezwa kwa Sh. milioni 120.
Alisema Tanesco ilijaribu kupitisha nyaya hizo upande wa pili lakini baada ya kujadiliana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilikataa baada ya kubaini hatari ya kupitisha umeme huo mkubwa karibu na makazi ya watu.
"Wasomi walikataa maana wanaujua umeme na madhara yake, sasa walipoona wameshtukiwa kule wakaona waje wapitishe huku kwetu ambako walidhani waumini ni watu wasiojua kitu, cha kushangaza walianza kwa kutwambia kuwa umeme huo hauna madhara baadaye wakasema wakishaweka nyaya zao itabidi mabango haya yaondoke maana ni hatari yakiendelea kuwepo sasa wanajichanganya wenyewe," alisema na kuongeza kuwa yeye ni msomi wa sayansi na anaufahamu vilivyo umeme.
Alisema shirika hilo limekuwa likitoa fidia tangu Ubungo zitakazopita nyaya hizo lakini walipofika kwenye Kanisa hilo hawakuona hata umuhimu wa kuzungumza na waumini ili kufikia muafaka.
Tanesco imeshasema kuwa itatekeleza mpango huo mapema mwaka huu, baada ya utafiti wa wataalamu na ushauri wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), kwamba hauna madhara kwa wakazi wa eneo hilo.
CHANZO: NIPASHE
Wednesday, October 14, 2009
Tatizo la Umeme Tanzania
Someni maoni ya mhariri wa Nipashe.
********************************************************************
Tunahitaji umeme wa uhakika si malumbano
Na Mhariri
13th October 2009
Ukifuatilia kwa karibu yanayotokea katika sekta ya nishati ya umeme nchini, huwezi kuepuka kufikia hitimisho jepesi tu, kwamba hakuna anayejali kinachotokea.
Kama taifa tumekosa ujasiri si tu wa kutenda, bali hata wa kusema. Tumekosa hata soni ndani ya nafsi zetu, kiasi cha kubakia kupiga domo mwaka hadi mwaka.
Taifa kwa sasa lipo kwenye mgawo mkali wa umeme wa zaidi ya saa 14 kwa siku kokote ambako gridi ya taifa imepita. Ni kero, shida na kila aina ya kuvunjika moyo, kwamba mwaka baada ya mwaka tunabakia pale pale, watu tusioweza si tu kujifunza kwa makosa ya watu wengine, bali hata kwa yetu wenyewe.
Tangu mwaka 2006 serikali ilipoamua kuachana na mchakato wa kubinafsisha Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) tulitarajia kuona watu wakikimbizana usiku na mchana kuiondoa nchi katika adha hii ya umeme wa mgawo.
Tuliona juhudi za kutafutwa kwa umeme wa dharura wa megawati 100 wa kampuni hewa ya Richmond, ambayo ilipewa kandarasi ya kuzalisha nishati hiyo kwa kutumia gesi asilia.
Kwa bahati mbaya, umeme huo uliingia ruba, haukupatikana kwa wakati, kwa hakika ulipatikana wakati dharura ikiwa imekaribia kufikia ukingoni, lakini kwa kutambua ukiukaji wa taratibu za kumpata mkandarasi Richmond, mkataba wake ulivunjwa na hivyo, Richmond na mrithi wake, Dowans wakatakiwa wafungashe virago.
Tangu hatua hizi za kuvunja mkataba zichukuliwe, si tu kumekuwa na ngonjera za kutakiwa kwa mitambo ya Dowans, bali pia juhudi za lazima kabisa za kutaka Tanesco inunue mitambo hiyo, hoja inayojengwa ni moja, mitambo ni mizuri na kwamba mitambo si mkataba, kweli inawezekana kuna ukweli wa jambo hilo.
Lakini kwa bahati mbaya, nchi haiendeshwi tu kwa uhalali wa kisheria na ubora wa hiki au kile, bali pia na siha ya kisiasa ya wakati husika. Kwa maana hiyo kama siha ya kisiasa si mwafaka kwa wakati fulani si vema wala busara kung’ang’ana na jambo fulani.
Kwa hali hii haijalishi kwamba eti mitambo ya Dowans ni mizuri kiasi gani, kama siha ya kisiasa si mwafaka kwa mitambo hiyo kuchukuliwa, na kwa sababu wahusika serikalini na ndani ya Tanesco walikwisha kuonywa juu ya hali hiyo, tulidhani kwamba nguvu zao zingeelekezwa kwa mbadala wa Dowans.
Lakini inavyoelekea watu wamejaza vifua visasi na vinyongo vya kutaka kuonyeshana nani zaidi. Nguvu kubwa hazijaonekana zikielekezwa huko na huko kusaka mitambo mengine kama mbadala wa Dowans, hata kama ilijulikana wazi kwamba mkataba wa Richmond kuanzia mapema ulikuwa ni wa miaka miwili tu, sasa kufikiri kwamba bila wao (Dowans) adha ya umeme haiwezi kutatuliwa, tunashawishika kuuliza kuna nini Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini?
Kama taifa hatuwezi kukamatwa mateka wa Dowans na siasa zote zinazohusu Richmond na wote waliokuwa kondoo wa kafara kwa utendaji mbovu wa baadhi ya watendaji serikalini na au maamuzi dhaifu ya wanasiasa; tunataka umeme.
Tanesco ni lazima itambue kwamba inawajibika kutupa umeme, ni lazima iumize kichwa kutupa umeme, kutupa sababu za mgawo wa umeme na ratiba ya mgawo, si vitu vinavyosaidia taifa hili kusonga mbele.
Tunahisi kwamba kwa kitambo kirefu mno, Tanesco si tu wameachwa hadi kulewa vilivyo ukiritimba wa kuzalisha na kusambaza umeme nchini, bali pia wamebobea mno katika uzembe na kutokujali kwa kiwango cha hali ya juu.
Uongozi wa Tanesco umeamua kubweteka, si leo wala jana, ila kwa miaka na miaka, wameruhusiwa kuishi kwa kuamini wananchi ndio wanaowahitaji na si vinginevyo, ndiyo maana Tanesco daima hawashituki wanaposikia mteja wao kapata hasara kwa sababu ya kuunguliwa na nyumba kutokana na huduma zao mbovu, wala hawasumbuki wanapokuwa na mlolongo wa maombi ya wananchi wanaohitaji huduma yao. Tanesco wakikosa kabisa mkakati wa kumaliza kero hizo.
Tanesco walitutisha kwamba kwa kuikataa Dowans tutajuta, na sasa wameanzisha mgawo, ndiyo kusema walikusudia kuliadhibu taifa, walipanga na sasa wametekeleza. Hii haikubaliki, kama wapo walioshindwa kazi Tanesco wanasubiri nini, hili ni shirika la umma si kampuni binafsi, ni vema na haki wakapisha wengine watakaothubutu kujaribu na hivyo kutatua kero ya umeme nchini.
CHANZO: NIPASHE
Thursday, September 18, 2008
Matatizo na Luku Dar
****************************************************************************
Panic as LUKU meters collapse
2008-09-18
By Correspondent Felister Peter
Tanzania Electric Supply Company`s (Tanesco) automatic vending machines in Dar es Salaam collapsed on Monday, putting customers using pre-paid meters popularly known as LUKU at risk of going without power for days.
A survey conducted by this paper in the city up to yesterday afternoon showed that nearly all LUKU (pay-for-power-as-you-consume-it) vending stations have fallen dead since Monday night.
Services are said to have returned to normal on Tuesday night before collapsing again yesterday morning.
Tanesco Communication Manager Badra Masoud said in an interview yesterday that the problem was caused by technical faults in the network linking up the machines.
Technicians from the giant state-run monopoly have been making frantic efforts to solve the problem, she explained.
``Our technicians have been working non-stop to solve the problem to spare our esteemed customers a protracted blackout that would also adversely affect the company financially,`` noted Masoud, without saying how much revenue the company had lost following the system failure.
``I cannot at the moment say exactly how dearly the problem has cost us. I will be in a position to speak about it later because we need to make some computations first``, she added.
According to the official, only Dar es Salaam is affected and vending stations in all other regions where they are in use are functioning normally.
Dar es Salaam apart, the LUKU system is in use in Arusha, Dodoma, Mara, Mwanza and Shinyanga regions and several major urban centres elsewhere.
Our survey shows that Dar es Salaam has more than 100 LUKU vending stations and Tanesco technicians managed to restore services at Mikocheni station late yesterday.
Meanwhile, scores of people were seen moving from one vending station to another in a futile attempt to purchase emergency power. Most of those interviewed wondered why Tanesco was tight-lipped over such a sensitive development, the first of its magnitude to hit its LUKU consumers.
The LUKU vending machines first came into use in Tanzania in 1995, with most installed in Dar es Salaam. They were chiefly meant for residential and commercial consumers but they are used by several other segments of the public.
Most other Tanesco consumers still use conventional electricity meters but the company has not been able to give any figures.
As we went to press, Tanesco apologised to its LUKU customers who had failed to purchase vouchers at various selling points in Dar es Salaam after the sudden malfunctioning of its computer network.
``The problem first occurred at 11.00 am on Monday
and repeatedly occurred until today (yesterday) when it was eventually resolved,`` read the statement issued by public relations manager Badra Masoud.
The Tanesco management also informed customers who had unsuccessfully tried to purchase LUKU vouchers through the National Microfinance Bank and been erroneously debited, that they would get back their money.
The statement advised city power consumers to purchase LUKU vouchers at the following selling points:
-BP Posta/Upanga petrol station
-Fuel station at Swahili Street, Kariakoo
-Magomeni petrol station.
-Tandika Maghorofani
-BP Sinza Kijiweni
-Tegeta Kibaoni
-Buguruni filling station
-Oryx Fire filling station, Morogoro Road.
-BP Airport filling station
-Oilcom, Kijitonyama
The Tanesco management concluded by giving phone number 0783 313342 for queries in case of any problems.





