Maandamano nje ya Ofisi za INS mwaka 2005Yaani kuna ushenzi na washenzi kwenye ofisi za INS (Uhamiaji) hapa Boston! Leo tumepata habari kuwa Mwalimu Obain Attou0man (raia wa Ivory Coast) alikuwa DEPORTED jana. Tena INS walimtorosha kimya kimya!
Kisa, mwaka juzi walipotaka kumdeport wanafunzi wake na watu wengine waliandamana kwenye ofisi za INS Boston. Pia walimwomba Senator Kerry na Senator Kennedy waingilie kusimamisha deportation order. Senator Kerry aliingilia na walitoa amri kuwa apewe residency (haki ya kukaa Marekani). Congress walilalia na ile order ilikwisha juzi, haikupita. Hivyo Mwalimu Obain alivyoenda kureport kama kawaida huko Ofisini INS Boston walimkamata!
Ameonewa huyo kaka! Ni mtu mwema, ni mwalimu mzuri sana wa hesabu Fenway High School (na hapa Marekani kuna upungufu). Ajabu ameoa mMarekani lakini bado wamemfukuza.
Haya sasa kampeni imeanza ya kumrudisha Marekani. Arudi kwa wanafunzi wake hapa. Yaani wanalia si mchezo. Na lazima niseme, siku hizi ni walimu wachahe sana hapa wanaopendwa na wanafunzi.
Kwa kifupi alfika Marekani kama mwanafunzi miaka ya tisini. Aliomba hifadhi (political asylum). Alikosea kusoma tarehe ya hearing kwenye notisi. Ndo walianza kumdeport.
Habari zinasema kuwa amefika salama huko Ivory Coast.
STAY STRONG Mr. OBAIN! You are not a criminal, you are a law abiding, caring and skilled person who does not deserve to be treated like you have. Our children need postive black role models like you!
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:



