Showing posts with label Asylum. Show all posts
Showing posts with label Asylum. Show all posts

Sunday, March 29, 2015

Watanzania - Wakimbizi Ulaya!

 
Malazi ya Wakimbizi huko Ujerumani


Nimepata kwa E-Mail:

 Hivi karibuni nilikuwa safarini Nchini Ujerumani. Na moja ya mambo niliyoyakuta ni kwamba siku hizi nchini humo kumefunguliwa makambi sehemu mbali mbali ya wakimbizi. Wengi wao ni kutoka nchi za Afrika. Nadhani mnasikia mara kwa mara kuhusu wakimbizi hawa ambao huenda Ulaya kwa njia ya hatari ya Meli. Wengi hufa bahari kwa hali mbaya ya hewa au hata kwa kutoswa.

Nchini Ujerumani nilikuwa katika Jiji la Munich. Nilibahatika kuona moja ya kambi hiyo, ila kwa bahati mbaya sikuruhusiwa kuingia. Niliambiwa kadiri ya orodha yao kuna WATANZINIA WAWILI. Nilipopata habari hiyo nilishituka sana. Hata aliyenipa habari hiyo aliona sikuwa tena katika hali ya kawaida. Ndipo akaniuliza nchini kwenu kuna matatizo gani hata watu wakimbie huko? Hakika sikuwa na jibu. Sababu za ukimbizi nchini mwako zinaweza kuwa za Kisiasa, yaani kutokana na utawala mbovu watu wanaamua kukimbia kuokoa maisha yao. Au hali hali nyingine yoyote inayohatarisha maisha. Mimi ninajiuliza nchini Tanzania kuna hali gani ya kuhatarisha maisha ya watu hadi wakimbie wakaishi kwenye makambi Ugaibuni? Hakika nilisikitika sana.

Ila kwa vyovyote wanazo sababu zao za kimsingi kukimbia na hata kujiorodhesha kama wakimbizi. Wito wangu kwa vijana; hakika wengi wanadhania Ulaya ni sehemu poa. Kuna fedha za kumwaga na maisha huko ni rahisi. Kiukweli ni kujidanganya. Hapa Tanzania unaweza kwenda sokoni ukaokota hata matunda au mbogamboga ukaponea. Ukafanya kibarua chochote kitu hata kufanya usafi kwenye zizi au bustanini au hata kuiba kwa wale wenye ujuzi huo. Kwa wenzetu hayo hayapo. Hakuna cha kibarua. Hakuna mazingira unayoweza kuiba kirahisi. Kila duka na soko kuna makamera. Hali ya hewa ni mbaya. Muda mwingi katika mwaka ni baridi kali. nk. Witoa kwa vijana kama unataka kuteseka maisha yako yote kimbilia Ulaya.

Walioko kule wako makambini. Hawaruhusiwi kusafiri, hawaruhusiwi kufanya kazi ila wanafugwa tu kwa kupatiwa chakula na mahitaji mengine ili waishi. Wanangoja ufanyike utaratibu wa kurejeshwa makwao. Je huko si kupoteza muda na kuhatarisha maisha zaidi. Kinachoniuma zaidi ni je, hapa Tanzania kuna mazingira gani magumu kiasi hicho hata wajiorodheshe kuwa wakimbizi? Kama kuna mwenye maelezo ya sababu ningeshukuru.

K

Tuesday, May 18, 2010

Shangazi wa Rais Obama apewa Asylum Marekani!


Hatimaye, Zeituni Onyango (57) mkazi wa Boston, Massachusetts na pia shangazi yake rais Obama kapewa ruhusa ya kukaa Marekani kihalali. Amepewa 'asylum' kutokana na afya yake mbaya na pia fujo za kisiasa huko Kenya. Kesi yake ilifuatiliwa kwa makini tangu Rais Obama alivyokuwa anagombania uraisi. Wazungu wenye fikra za kibaguzi walimtumia kama mfano na kusema eti Kenya nzima itahamia Marekani kama Obama atachuguliwa kuwa rais!

Watu wengi kutoka nchi za Afrika wana asylum hapa Marekani. Pia kuna waBongo waliopewa. Wanapata kutokana kuhofia maisha yao wakirudi kwao, fujo za kisiasa, kuteswa kutokana na imani za kidini nk. Hata wanawake kuogopa kutahiriwa.
Sasa ataweza kuleta familia aliyoacha huko Kenya kihalali.
Rais Obama anasema hakuhusika kabisa na uamuzi wa jaji.
HONGERA SHANGAZI ZEITUNI!
******************************************************************

Obama's aunt can stay in U.S.
Posted: May 17th, 2010 01:42 PM ET
From

Washington (CNN) - President Barack Obama's Kenyan aunt can stay in the United States, a U.S. immigration judge has ruled, ending a more than six-year legal battle over her status.
Judge Leonard Shapiro made the decision Friday, court officials told CNN.

Two government sources confirmed Monday that the ruling will give legal status to Zeituni Onyango, 57, allowing her to remain in the country.

Onyango's attorneys held an afternoon news conference on the matter in Ohio.
Onyango, who is the half-sister of the president's late father, applied for political asylum in 2002 due to violence in her native Kenya. She was a legal resident of the United States at the time and had received a Social Security card a year earlier.

Onyango's asylum request was turned down in 2004. She appealed the rejection of her request twice, but was denied each time and ordered to leave the country. Onyango remained in the country illegally until April of 2009, when Judge Shapiro gave her permission to stay in the United States while he considered her case.In February, Onyango arrived at an immigration court in a wheelchair and testified before the judge for more than two hours, her representative, Amy Cohn, told CNN at the time. Two doctors, including her personal physician, also testified on her behalf. Onyango's medical condition was part of her legal defense against expulsion.
White House officials said during the appeals that Obama was staying out of the matter.

"The president believes that the case should run its ordinary course," the officials said.
Onyango's immigration status came to light in the final days of the 2008 presidential race.

Thursday, May 22, 2008

Mwalimu Obain amekuwa DEPORTED!

Maandamano nje ya Ofisi za INS mwaka 2005
Mwalimu Obain (pichani)



Yaani kuna ushenzi na washenzi kwenye ofisi za INS (Uhamiaji) hapa Boston! Leo tumepata habari kuwa Mwalimu Obain Attou0man (raia wa Ivory Coast) alikuwa DEPORTED jana. Tena INS walimtorosha kimya kimya!
Kisa, mwaka juzi walipotaka kumdeport wanafunzi wake na watu wengine waliandamana kwenye ofisi za INS Boston. Pia walimwomba Senator Kerry na Senator Kennedy waingilie kusimamisha deportation order. Senator Kerry aliingilia na walitoa amri kuwa apewe residency (haki ya kukaa Marekani). Congress walilalia na ile order ilikwisha juzi, haikupita. Hivyo Mwalimu Obain alivyoenda kureport kama kawaida huko Ofisini INS Boston walimkamata!

Ameonewa huyo kaka! Ni mtu mwema, ni mwalimu mzuri sana wa hesabu Fenway High School (na hapa Marekani kuna upungufu). Ajabu ameoa mMarekani lakini bado wamemfukuza.

Haya sasa kampeni imeanza ya kumrudisha Marekani. Arudi kwa wanafunzi wake hapa. Yaani wanalia si mchezo. Na lazima niseme, siku hizi ni walimu wachahe sana hapa wanaopendwa na wanafunzi.
Kwa kifupi alfika Marekani kama mwanafunzi miaka ya tisini. Aliomba hifadhi (political asylum). Alikosea kusoma tarehe ya hearing kwenye notisi. Ndo walianza kumdeport.

Habari zinasema kuwa amefika salama huko Ivory Coast.

STAY STRONG Mr. OBAIN! You are not a criminal, you are a law abiding, caring and skilled person who does not deserve to be treated like you have. Our children need postive black role models like you!
Kwa habari zaidi BOFYA HAPA: