Showing posts with label U.K.. Show all posts
Showing posts with label U.K.. Show all posts

Friday, November 21, 2008

Kipanya Asema....

UK Counsulate Official: Get out of my way! As of today, all your visa requests will be processed in Kenya!

Kipanya (Rat Character): You're sucking up to Obama!? Why don't you just close down the Counsulate!

Tuesday, July 08, 2008

Rudini Zimbabwe - Uingereza!


Loh! Kumbe waingereza ni wakatili. Wameamuru wakimbizi 11,000 walioko Uingereza warudi Zimbabwe. Hali ilivyo mbaya huko Zimbabwe hao wakimbizi watakuwa salama kweli? Washenzi wa Mugabe watawauliza, "ehe mlikimbia nini?" halafu watanyanyaswa ile mbaya.

Nashangaa waingereza kwa uamuzi wao. Wanajua kabisa kuwa Zimbabwe kuna matatizo sana hasa kuhusuiana na haki za binadamu. Na wenyewe wamesemea serikaliya Mugaba si ya halali. Waingereza si wanadai wao ni watetezi wakuu wa haki za binadamu. Lakini hawashutuki kurudisha watu kwenye hali ambayo inahatarisha maisha yao.

Hali ya waZimbabwe wakimbizi huko Uingereza ni mbaya. Hawapati huduma ya serikali (welfare) na pia hawaruhusiwi kufanya kazi. Kutokana na hali hiyo wengine wanazagaa mitaani na kuwa ombaomba huko Uingereza.

Nauliza wangekuwa wakimbizi kutoka nchi ya kizungu kama Bosnia wangewarudisha kweli?

Kwa habari zaidi someni: