Showing posts with label Universal Studios. Show all posts
Showing posts with label Universal Studios. Show all posts

Tuesday, November 24, 2009

Ubaguzi Mpaka kwenye Poster!

Wadau, hivi kribuni ilitoka sinema, Couples Retreat.

Walianza kuionyesha Marekani halafu walianza kuionyesha nchi za Ulaya. Producers (Universal Studios) waliamua kuondoa weusi katika bango la sinema. Hebu cheki bango la Marekani (picha ya juu), na bango la Ulaya (Picha ya chini). Waliona wakiweka weusi kwenye bango watu hawataenda kuoiona huko Ulaya nini? Baada ya zozo kubwa hapa Marekani waliamua kutumia ile bango la awali!



Kwa habari zaidi BOYA HAPA:

Monday, June 02, 2008

Moto Universal Studios Hollywood!


Seti kadhaa za sinema huko Universal Studios Hollywood, ziliangamizwa kwa moto jana. Baadhi ya seti zilizoungua ni zote za New York City, ile ambayo unaona kwenye sinema za Back to the Future na exhibit ya King Kong.

Pia kanda za sinema zaidi ya 40,000 ziliangamizwa wakati vault ambako zilihifadhiwa iliungua. Sinema hizo nyingi ni za tangu miaka ya 1920's! Kwa bahati nzuri Universal wanasema kuwa wanazo copy za sinema zote zilizoungua!

Kwa habari zaidi someni:



Sunday, January 13, 2008

Steven Kanumba yuko Hollywood!








Wadau mliuliza na hii ni jibu:

Mcheza sinema maarufu wa Tanzania, Steven Kanumba aka. Denzel wa Tanzania, yuko ziarani Marekani. Kwa sasa yuko Hollywood. Amenitumia picha za safari yake na nazi-share na wadau.
Ametembelea Warner Brothers na Universal Studios.
* Steven Kanumba allitutuembelea kwenye seti ya sinema ya Bongoland II tulivyokuwa tunashuti Magomeni. Alitambulishwa kwa crew wetu kama Denzel Washington wa Tanzania. Naona hiyo nickname ni sawa maana amecheza kama lead kwenye sinema/video kadhaa, sijui kama yupo aliyemfikia.