Showing posts with label Wema Sepetu. Show all posts
Showing posts with label Wema Sepetu. Show all posts

Saturday, July 19, 2014

Wema Sepetu 'Amlipua' vibaya Kajala -





Wema Sepetu (R) na Kajala

Kutoka BONGO MOVIES. COM

Ikiwa ni siku chache zimepita baada ya mwigizaji  Kajala kudai kuwa mrembo Wema Sepeteu ni Mnafiki, hatimaye Mwanadada Wema Sepetu , amemlipua aliyekuwa shosti wake, Kajala Masanja ‘K’ ambaye wiki iliyopita alimwita mnafiki, habari  ambayo  ilisambaa  katika  mitandao  mbalimbali  ya  kijamii.

Katika habari hiyo, Kajala alikaririwa akisema kwamba licha ya watu wengi kuamini wamepatana, hakuna ukweli kwani rafiki yake huyo ni mnafiki kufuatia kutomthamini na kutokuwa karibu naye kama zamani likiwemo suala la kumsifia mtu ambaye alikuwa na ugomvi na Kajala (Dacutee).

Akizungumza na mwanahabari wetu, Wema alisema alishangaa kuona Kajala anamwita mnafiki wakati hakuwahi kupatana naye tangu walipotofautiana kipindi cha nyuma kama alivyosema.
“Nashangaa Kajala ananiambia mimi ni mnafiki ‘ok fine’ na huo unafiki wangu unakuja pale nilipomu-wish Dacutee siku yake ya kuzaliwa, alitakaje eti? Yaani kwa kuwa yeye ana bifu la kumchukulia bwana’ke na mimi nijiingize kwenye bifu lao?

“Au tofauti zangu mimi na yeye, Aunty Ezekiel aingilie, itakuwa sahihi kweli kama wanavyofanya hao watu wake anaozurura nao siku hizi? Wanaingilia vitu ambavyo hawavijui kiundani wake? Nasema siyo sahihi kabisa mimi nitabaki kama Wema Sepetu na yeye atabaki kama Kajala Masanja na asifikirie kuwa nitakuja kuwa kama zamani na yeye halafu kama anamaindi kuhusiana na Dacutee mbona Petit Man ambaye ana uhusiano naye aliweka picha.

BOFYA HAPA KUSOMA HABARI KAMILI BONGO MOVIES.COM

Friday, May 07, 2010

Kanumba Aja na Sinema Mpya - White Maria!


Wadau, mcheza sinema maarufu wa Tanzania Steven Kanumba aka. The Great Kanumba au Denzel wa Tanzania atatoa sinema mpya mwezi ujao.

Sinema itaitwa White Maria. Stelingi wake ni Kanumba mwenyewe, Wema Sepetu aliyewahi kuwa Miss Tanzania.

Mnaweza kupata habari zaidi kwenye Blog ya Kanumba:
http://kanumbathegreat.blogspot.com/
Naingojea kwa hamu! Wadau huko Bongo mtuletee reviews.

Friday, March 06, 2009

Steven Kanumba na Wema Sepetu


(Picha kutoka Global Publishers)

Wadau, wengi wetu tunaelewa mapenzi yanavyoenda. Leo unampenda mtu kupita kiasi, kesho unamchukia, huna hamu naye. Unaweza kumwona mtu na kumpenda mpaka unaona unachangayikiwa huwezi kufikiria kitu kingine. Na pia tunaelewa kuwa kuna yale mapenzi ambayo si mapenzi ila kutaka raha ya kimwili tu. Mtu akitosheka anaanza kwenda pengine. Unaweza kumpenda mtu mapaka ukaona wengine wana sura mbaya kama Chakubanga. Yaani mapenzi ni kitu cha aina yake. Lakini yakifa....mhhhh!!!




Hii picha ilipigwa mwezi Novemba mwaka jana. Unaweza kusoma maelezo hapa:
http://worldhotstars.blogspot.com/2008/11/mapenzi-ya-wema-sepetu-na-kanumba.html

Thursday, March 05, 2009

Yaliyompata Wema Sepetu

Sijui niseme nini. Naona macelebrity wetu wanataka kuanza kuwa na maskandali kama za Hollywood. Sina habari kamili lakini inaelekea Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, alichukua gari ya mwigizaji maarufu Steven Kanumba aka Denzel wa Tanzania, na kuliharibu. Kama ilikuwa ajali si amsamehe na wapatane kuhusu matengenezo? Kwa sasa macho yote kwao.

*********************************************************
mrembo wema sepetu akipewa pole na rafiki yake baada ya kuachiwa kwa dhamana leo mahakamani kinondoni anakikabiliwa na shtaka la kuharibu gari la mwigizaji steve kanumba. mrembo huyu aliyepata kuwa miss tz alikuwa rumande toka wiki iliyopita baada ya kukosa dhamana alipofikishwa kizimbani kwa mara ya kwanza
mama mzazi wa wema sepetu akisaidiwa na nduguye wa kiume ilibidi watumie nguvu wema aondoke nao wao na sio rafikiye ambaye alifika hapo mahakamani

**********************************************************************************


Former Miss Tanzania Charged

2009-03-04

By Hellen Nachilongo

Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu was yesterday brought before the Kinondoni Resident Magistrate`s Court over allegations of malicious damage to a motor vehicle.

Sepetu (20), a resident of Tabata Senene, and Aisha Jumbe (23) appeared before the magistrate in charge Emilius Mchauru to answer the charges levelled against them.

Inspector of Police Nassoro Sisiwaya told the court that willfully and unlawfully the accused maliciously damaged a motor vehicle wind screen with registration no T 993 ASD Toyota RAV 4 brand, the property of actor Kanumba Stephen.

It was alleged that the offence was committed at Magomeni Mikumi area in Kinondoni District on January 1, this year.

However, the accused pleaded not guilty just after the charge was read to them and were returned to remand custody after failing to meet bail conditions.

The court required two reliable sureties working from any recognised or established company to sign a bond of 500,000/- for each of the accused. No body stepped up to rescue the charged duo.
The case was adjourned to March 18, this year when it comes up for mention. Investigation is still in progress.

SOURCE: Guardian
****************************************************************

Wema Sepetu atupwa Segerea

2009-03-04
By Adam Fungamwango

Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu (20), jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la kuharibu mali baada ya kuvunja kioo cha gari chenye thamani ya Sh. milioni moja, mali ya muigizaji wa filamu, Steven Kanumba.

Sepetu alisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Emilius Mchauro, analiyesikiliza kesi hiyo.

Mwendesha Mashitaka Insepkta wa Polisi Nassoro Sisiwaya alidai mahakamani hapo kuwa, Sepetu na mwenzake Aisha Jumbe (23) wanadaiwa Janauari 29 mwaka huu, saa 3:00 usiku huko Magomeni Mikumi, walivunja kioo cha mbele cha gari la mlalamikaji chenye thamani ya Sh 1,000,000.

Ilidaiwa kuwa gari hiyo aina ya Rav 4, lenye namba za usajili T 990 ASD, ilivunjwa kioo na washitakiwa hao na kusababisha hasara ya fedha hizo.

Mahakama iliwataka washitakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. 500,000 kila mmoja.

Washitakiwa hao walikana shitaka hilo, na wamepelekwa gereza la Segerea baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Aidha, mlalamikaji wa kesi hiyo Kanumba hakutokea mahakamani hapo.

Hakimu alimhoji mmoja wa aliyejitokeza kuwa mdhamini kama ana hati za dhamana, ambapo badala ya kuzitoa alidai kuwa amezisahau ndani ya gari.

Kwa kutumia busara, Hakimu Mchauro alimtaka mdhamini huyo azifuate, lakini alitumia zaidi ya dakika tano bila kurejea.

``Hii ni mpya, hakimu anamsubiri mdhamini aliyesahau hati ndani ya gari!.

Labda huyu mheshimiwa alitaka watu wajue tu kama na yeye ana gari,`` alisema Hakimu Mchauro. huyo.

Baada ya kusubiri vya kutosha Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 18 mwaka huu na hapo ndipo pakawa na ugumu wa wadhamini kukubaliwa dhamana kwa sababu tayari hakimu alikuwa ameshasaini.

Sepetu muda wote wa kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa alionekana kutokujali kufikishwa kwake mahakamani hapo, alikuwa yuko kawaida kama vile hakuna kilichotokea na hata baada ya kesi kusomwa alisikika akiwapigia kelele waandishi hasa wapiga picha wampige picha wanazotaka.

Na hata alipotolewa kwenye mahabusu ya polisi kupelekwa kwenye basi la jeshi la magereza, bado alikuwa akipiga kelele kwa waandishi akitaka waandike huku akiwataka askari waache wapiga picha wampige wanavyotaka, lakini haikueleweka alikuwa akisema hivyo kwa hasira au alipenda mwenyewe.

Kwa mara ya kwanza, kesi hiyo ilifikishwa kwenye kituo cha polisi Magomeni mwezi uliopita na Kanumba, ambapo Wema alitiwa mbaroni na kulala kituoni hapo kwa muda wa siku mbili.
Kesi hiyo itatajwa tena, Machi 18, mwaka huu.

SOURCE: Nipashe

Pia soma DAILY NEWS: http://www.dailynews.co.tz/home/?n=632