Showing posts with label Gari. Show all posts
Showing posts with label Gari. Show all posts

Saturday, November 12, 2016

Wananchi Wajeruhiwa Katika Ajali Iliyohusisha Magari Manne Kongowe Temeke jijini Dar es Salaam Leo

div class="separator" style="clear: both; text-align: center;">
 Wananchi wakiangalia ajali iliyohusisha magari manne na pikipiki iliyotokea daraja la Mzinga Kongowe, Temeke jijini Dar es Salaam leo mchana. Katika ajali hiyo watu kadhaa walijeruhiwa.
 Wananchi wakiangali basi dogo aina ya Coster ya abiria namba T 415 DCC ikiwa imeharibika vibaya baada ya kugongwa.
 Wananchi wakiwa eneo la ajali
 Wananchi wakiwa eneo la ajali.
 Ofisa wa Jeshi la Polisi akiwa eneo la ajali akichukua taarifa.
Prado yenye namba  T 177 AHH iliyohusika katika ajali hiyo.

Na  Dotto Mwaibale

WATU kadhaa wamejeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha magari manne na pikipiki iliyotokea daraja la Mzinga Kongowe Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo ilitokea saa sita mchana na kuhusisha magari hayo lori la mafuta aina ya Scania lenye namba T 617 AQQ, Coster ya abiria namba T 415 DCC inayofanya safari zake kati ya Kilwa Masoko na Mbagala, Prado yenye namba  T 177 AHH, pikipiki na lori jingine. 

Ofisa wa Polisi aliyekuwepo eneo la ajali ambaye alitambulika kwa jina moja la Emanuel alisema chanzo cha ajali hiyo bado hakijafahamika.

"Nimefika sasa hivi bado hatujajua chanzo cha ajali wala watu waliopoteza maisha na kujeruhiwa" alisema ofisa huyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto alipopigiwa simu ili kuthibitisha ajali hiyo alikiri kutokea  hata hivyo alisema alikuwa hajapata taarifa kamili kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Usalama wa Wilaya hiyo ambaye alikuwepo eneo la tukio.

Kwa mujibu wa mashuhuda walioshuhudia ajali hiyo walisema majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Manispaa ya Temeke kwa matibabu.

The great escape.

Saturday, June 21, 2014

Ajali Mbaya Imetokea Lugalo Leo - Watu Saba Wamakufa






 Taarifa na picha kitoka kwa Mdau OS:


Ajali mbaya ya gari imetokea mchana huu, katika maeneo ya Lugalo jijini Dar es Salaam. Katika ajali hiyo, inakadiriwa zaidi ya watu saba wamefariki dunia.

Mashuhuda wanasema, ajali hiyo imesababishwa na gari aina ya dalala iliyokuwa ikitokea maeneo ya Tegeta kuja Mwenge. Gari hiyo ililigonga dalala nyingine kabla ya kulivamia roli na baadaye gari nyingine aina ya Toyota Discover.

Friday, June 29, 2012

Ogopa Magari enye Madirisha Tinted!

Nimepata kwa email, lakini hii kali!  Mambo ya ushirikina yataisha lini!!!!


*************************************************************

Dear Friends:

Leo nimeona ni vyema nika-share nanyi kisa hiki cha kutekwa mfanyakazi mwenzetu ambaye ni cashier siku ya jumatano jioni wiki iliyopita. Ni kama movie lakini ni ukweli, cashier wetu aliomba ruhusa siku hiyo ya tukio aende kwenye mkutano wa wasabato uliokuwa uliendelea viwanja vya biafra.

Yeye pia ni msabato aliyeishika dini ya Sabato haswa, kwa hiyo aliondoka saa kumi kamili badala ya saa kumi na moja. Baada ya dakika 40 tulianza kupokea sms zinazosema mwenye namba xxx amepata ajali na kufa papo hapo na kwa taarifa zaidi twende muhimbili hospital. Baada ya kutazama hiyo namba xxx ilikuwa ni ya cashier wetu. Tulijaribu kuipiga iliita tu bila kupokelewa, na pia tulipiga namba iliyotutumia sms iliita bila majibu. Ilipofika saa kumi na moja tuliamua kuelekea muhimbili, ma baada ya kufika pale emergence tukaambiwa tuelekee chumba cha kuhifadhia maiti. Tulioneshwa mwili wa mtu aliyepata ajali lakini haukuwa wa cashier wetu, tukawatuma wenzetu waende hospitali zote lakini hapakuwa na taarifa zake.

Baada ya kuzunguka bila mafanikio tulitoa taarifa makao makuu ya usalama barabarani na baada ya dk kumi wakatwambia kuwa hakuna taarifa za ajali mbaya iliyotokea jioni hiyo. Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutoa taarifa polisi juu ya tulio hilo na ndipo waliposema kwa kuwa ni mtu mzima tusubiri hadi siku inayofuata.

Wakati huo huo ndugu zake pamoja na wafanyakazi wenzetu walikuwa pamoja wakiendelea na jitihada za kumtafuta hadi saa sita usiku.

Kilichokuwa kinatia wasiwasi zaidi ile namba iliendelea kutumia sms namba takribani zote zilizokuwa kwenye phonebook yake na ndugu zake hawakuwahi kuona ndugu yao akichelewa kiasi hicho.

Ilipotimu mida kama ya saa sita na nusu walisikia mtu akigonga mlango, alikuwa kaumizwa na amejaa matope, hakuwa na uwezo wa kuzungumza sana, ilibidi wampeleke kituo cha polisi na baada ya muda hospitali ya mwananyamala. Alipopata nguvu alianza kuwasimulia nduguze kilichotokea. Alipotoka ofisini alikwenda moja kwa moja kwenye kituo cha daladala cha karakana, pale kituoni walikuwa abiria wawili
yaani yeye na mama mmoja. Baada ya dk chache ilikuja coaster iliyoandikwa mbele Kawe na ilikuwa na tinted nyeusi, yule mama hakupanda sababu alikuwa anaelekea posta ila yeye alipanda. Ndani ya gari kulikuwa na watu watatu pamoja na dereva, wawili wakiwa wamekaa nyuma na mmoja akiwa amekaa karibu na driver. Gari hiyo hiyo ilikuwa ni mpya, mmoja wa abiria alimumba simu cashier apige simu
moja kwa jamaa yake maana alidai kuwa simu yake illiishiwa charge na walikuwa wametoka mtwara kupeleka maiti, alimuuliza cashier umri wake na kama ameoa na anafanya kazi wapi, cashier akamjibu hajaoa na hana kazi pia ana miaka 32.

Walipofika Tazara hawakutaka kupakia abiria yoyote na walikuwa wote wamevaa miwani myeusi, na ndipo akaanza kuingiwa na mashaka akaomba ashuke, wao wakamwambia watapita biafra na hawana mpango wa kusanya kwa kuwa hata yeye walimpa lifti tu.

Gari ilipokaribia taa za buguruni akainuka ili ashuke, jamaa wale wa nyuma wakamkalisha chini kwa nguvu, na sio kwenye viti yaani chini kabisa. Mmoja wao akafunga kitambaa cheusi kwenye macho na mikono ikafungwa kwa nyuma na mipira, baada ya muda akasikia kama wamempulizia perfume. Akihisi fahamu kumtoka polepole na neno lamwisho analokumbuka alisikia kuwa waelekee misitu ya Kibaha wakamalize kazi. Kilichomwamsha ni kofi zito alilopigwa na kusukumwa hadi nje ya gari. Alianza kulia na kuwasihi wasimdhuru, wakaanza kumrusha kichurachura huku wakimkanyaga.

Walikuwa wameshamfungua kitambaa machoni na waliacha gari umbali kama wa dk kumi na lilikuwa ni pori zito na giza, wao walivaa vitu usoni na walikuwa wamevaa gloves.

Wakamwekea simu yake mfukoni wakiwa wametoa simcard, walichomwambia wanachohitaji ni sehemu zake za siri na sio kitu kingine. Mmoja wao akaambiwa alete kisu kikali wanachokitumia, na walipompigia boss wao akawasisitiza nyeti zinazotakiwa lazma ziwe za mtu wa miaka 40 na kuendelea.

Mwenzao mmoja akasema cashier alisema alikuwa na miaka 32, baada ya kumkagua wakakuta card yake inaonyesha kazaliwa mwaka 1979. Kulingana na yeye asemavyo ndicho kilichomwokoa ila waliendelea kumkung'uta kwa hasira. Wakamrudisha kwenye gari na baada ya mwendo wakampakia kwenye gari nyingine ndogo iliyokuwa na watu wawili ambao walimchukua na kumtelekeza maeneo ya sayansi.

Hawakuchukua kitu hata kimoja wala kumwambia lolote, siku iliyofuata alipelekwa agakhan kwa uchunguzi zaidi na kwa sasa anaendelea vizurr. Kwa ufupi ni hayo, ukweli mwenyezi Mungu atulinde na tumwombe pia
abadilishe mioyo ya watu ambayo imekuwa migumu mno kwa ajili ya kupata vyeo na utajiri wa haraka.

Tuesday, March 09, 2010

Tuogope magari ya TOYOTA!!!!

(pichani - gari aina ya Toyota Prius ambayo ilipata ubongo na kuanza kwenda mwendo wa kasi mno, hata breki haikufanya kazi!)

Leo mzee James Sikes (61) karibu auliwe wakati gari yake aina ya Toyota Prius, ilivyoanakwenda mwendo wa kasi ghafla. Bila shaka mmesikia kwenye taarifa ya habari, habari ya magari ya Toyota kuua watu baada ya kuanza kwenda mwendo wa kasi ghafla. Spidi zinakaribia kilomita 100 kwa saa! Watani wanasema eti jini ailingia kwenye injini! Gari inakosa breki...inakuwa balaa. Unaweza kusoma habari zaidi hapa!

http://news.yahoo.com/s/ap/20100309/ap_on_bi_ge/us_runaway_prius

Thursday, March 05, 2009

Yaliyompata Wema Sepetu

Sijui niseme nini. Naona macelebrity wetu wanataka kuanza kuwa na maskandali kama za Hollywood. Sina habari kamili lakini inaelekea Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu, alichukua gari ya mwigizaji maarufu Steven Kanumba aka Denzel wa Tanzania, na kuliharibu. Kama ilikuwa ajali si amsamehe na wapatane kuhusu matengenezo? Kwa sasa macho yote kwao.

*********************************************************
mrembo wema sepetu akipewa pole na rafiki yake baada ya kuachiwa kwa dhamana leo mahakamani kinondoni anakikabiliwa na shtaka la kuharibu gari la mwigizaji steve kanumba. mrembo huyu aliyepata kuwa miss tz alikuwa rumande toka wiki iliyopita baada ya kukosa dhamana alipofikishwa kizimbani kwa mara ya kwanza
mama mzazi wa wema sepetu akisaidiwa na nduguye wa kiume ilibidi watumie nguvu wema aondoke nao wao na sio rafikiye ambaye alifika hapo mahakamani

**********************************************************************************


Former Miss Tanzania Charged

2009-03-04

By Hellen Nachilongo

Miss Tanzania 2006 Wema Sepetu was yesterday brought before the Kinondoni Resident Magistrate`s Court over allegations of malicious damage to a motor vehicle.

Sepetu (20), a resident of Tabata Senene, and Aisha Jumbe (23) appeared before the magistrate in charge Emilius Mchauru to answer the charges levelled against them.

Inspector of Police Nassoro Sisiwaya told the court that willfully and unlawfully the accused maliciously damaged a motor vehicle wind screen with registration no T 993 ASD Toyota RAV 4 brand, the property of actor Kanumba Stephen.

It was alleged that the offence was committed at Magomeni Mikumi area in Kinondoni District on January 1, this year.

However, the accused pleaded not guilty just after the charge was read to them and were returned to remand custody after failing to meet bail conditions.

The court required two reliable sureties working from any recognised or established company to sign a bond of 500,000/- for each of the accused. No body stepped up to rescue the charged duo.
The case was adjourned to March 18, this year when it comes up for mention. Investigation is still in progress.

SOURCE: Guardian
****************************************************************

Wema Sepetu atupwa Segerea

2009-03-04
By Adam Fungamwango

Miss Tanzania wa mwaka 2006, Wema Sepetu (20), jana alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam akikabiliwa na shitaka la kuharibu mali baada ya kuvunja kioo cha gari chenye thamani ya Sh. milioni moja, mali ya muigizaji wa filamu, Steven Kanumba.

Sepetu alisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Emilius Mchauro, analiyesikiliza kesi hiyo.

Mwendesha Mashitaka Insepkta wa Polisi Nassoro Sisiwaya alidai mahakamani hapo kuwa, Sepetu na mwenzake Aisha Jumbe (23) wanadaiwa Janauari 29 mwaka huu, saa 3:00 usiku huko Magomeni Mikumi, walivunja kioo cha mbele cha gari la mlalamikaji chenye thamani ya Sh 1,000,000.

Ilidaiwa kuwa gari hiyo aina ya Rav 4, lenye namba za usajili T 990 ASD, ilivunjwa kioo na washitakiwa hao na kusababisha hasara ya fedha hizo.

Mahakama iliwataka washitakiwa kudhaminiwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. 500,000 kila mmoja.

Washitakiwa hao walikana shitaka hilo, na wamepelekwa gereza la Segerea baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.

Aidha, mlalamikaji wa kesi hiyo Kanumba hakutokea mahakamani hapo.

Hakimu alimhoji mmoja wa aliyejitokeza kuwa mdhamini kama ana hati za dhamana, ambapo badala ya kuzitoa alidai kuwa amezisahau ndani ya gari.

Kwa kutumia busara, Hakimu Mchauro alimtaka mdhamini huyo azifuate, lakini alitumia zaidi ya dakika tano bila kurejea.

``Hii ni mpya, hakimu anamsubiri mdhamini aliyesahau hati ndani ya gari!.

Labda huyu mheshimiwa alitaka watu wajue tu kama na yeye ana gari,`` alisema Hakimu Mchauro. huyo.

Baada ya kusubiri vya kutosha Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Machi 18 mwaka huu na hapo ndipo pakawa na ugumu wa wadhamini kukubaliwa dhamana kwa sababu tayari hakimu alikuwa ameshasaini.

Sepetu muda wote wa kesi hiyo ilipokuwa inasikilizwa alionekana kutokujali kufikishwa kwake mahakamani hapo, alikuwa yuko kawaida kama vile hakuna kilichotokea na hata baada ya kesi kusomwa alisikika akiwapigia kelele waandishi hasa wapiga picha wampige picha wanazotaka.

Na hata alipotolewa kwenye mahabusu ya polisi kupelekwa kwenye basi la jeshi la magereza, bado alikuwa akipiga kelele kwa waandishi akitaka waandike huku akiwataka askari waache wapiga picha wampige wanavyotaka, lakini haikueleweka alikuwa akisema hivyo kwa hasira au alipenda mwenyewe.

Kwa mara ya kwanza, kesi hiyo ilifikishwa kwenye kituo cha polisi Magomeni mwezi uliopita na Kanumba, ambapo Wema alitiwa mbaroni na kulala kituoni hapo kwa muda wa siku mbili.
Kesi hiyo itatajwa tena, Machi 18, mwaka huu.

SOURCE: Nipashe

Pia soma DAILY NEWS: http://www.dailynews.co.tz/home/?n=632