Showing posts with label Adam Kuambiana. Show all posts
Showing posts with label Adam Kuambiana. Show all posts

Sunday, May 25, 2014

Mama Bishanga Amlilia Kuambiana

OHIO: USA, MAMA BISHANGA AMLILIA KUAMBIANA

Nimepokea kwa huzuni taarifa ya kifo cha msanii mwenzagu wa fani ya filamu marehemu Adamu Philip Kuambiana, ni pigo kubwa kwa tasnina yetu na kwa taifa pia kwa kuondokewa na mtaalamu mahiri kama yeye, namuombea usingizi wa milele wa amani.

Adamu alikuwa mtoto wa mwalimu Philip Kuambiana mwalimu wangu wa major yangu chuoni Theater Arts, alikuwa director na producer mkali sana. Na kama itakumbukwa nilihojiwa mwaka 2001 baada ya kupokea  Award ya The Best Actress wa mwaka wa 2001, nilieleza mengi pamoja na production tuliocheza  mbele ya wabunge na  Rais wa kwanza Mwl Julius Nyerere, Marehemu Mwalimu Philip kuambiana ndie aliidirect, na alisimamia Nyanja zote, mandhari, costumes, sound, na hata lebasi za ulibwende (wale tuliokuwa darasa moja mnaikumbuka hiyo?), na alikuwa very serious kazi inapoanza, alikuwa akitutania kila tunapoanza mazoezi kuwa kila mtu aende chooni kabisa kwani kazi ikianza ni moto moja kwa moja, kazi moja tu, na hakika matokeo ya production zake yalikuwa mazuri sana. Na ndio hapo nilimjua Adamu akiwa mdogo sana mwaka 1982-83.

Mwaka 2011 niliporudi tz kufunga ndoa ndipo nilipoonana tena na Adamu akiwa mkubwa kabisa, na tulipanga kuicheza tena jukwaani ile production ya mtihani wetu wa mwisho, alisema pamoja  kuwa alikuwa mdogo sana lakini anakumbuka ile production ya mfalme Odepasi (The King Odepus) kutoka kwenye kitabu cha Shake Spear, ambayo kwa kifupi mfalme Odepas alifungwa miguu na mikono kwenye mti na kupewa wafugaji wakamtupe mtoni akafe maji, Odepus alikuja kuwa mfalme baada ya miaka mingi, alimuua baba yake bila kujua kuwa ni baba yake na alimuoa mama yake na kuzaa nae watoto wawili bila kujua! ni production nzuri sana na ninasikitika kuwa Adamu amefarika na ndoto ya kuicheza hii production tena jukwaani sijui ndio vipi! Pamoja na yote namuombea Amani ya kudumu,

Mwisho nawapa pole kwa familia yake, na kwa taifa Zima.

 Bwana alitoa, Bwana ametwaa; Pumzika kwa Amani Adamu Philip Kuambiana.

Christina Innocent Marolen
Mama Bishanga
OHIO  

The Late Adam Kuambana

Saturday, May 17, 2014

Msanii Adam Kuambiana Afariki Dunia

Wadau, leo nimepokea habari za kusikitisha za kifo cha Msanii, Adam Kuambiana.  Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.


 KUTOKA LUKWANGULE BLOG

The Late Adam Philip Kuambiana

HABARI  haziko wazi lakini marafiki w akaribu wamethibitisha kwamba dairekta anayekuja juu, muigizaji na mwandishi wa sinema Adam Phillip Kuambiana PICHANI amefariki saa chache zilizopita.

Mkali huyo mwenye tabia 'ngumu ' (hana simu ya mkononi) labda sasa, ameshiriki kama muigizaji au dairekta katika sinema Lukuki na amekufa akikimbizwa hospitali ya Sinza palestina.

    Hizi ni baadhi tu ya kazi zake njema:
    Danija
    Faith More Fire|
    Bad Luck
    Scola
    The Boss
    Mr.Nobody
    Radhi ya Mke
    Lost Sons
    Chaguo Langu
    My Fiance
    Jesica
    Life of Sandra
    Basilisa
    My Flower
    Regina
The Late Adam Kuambiana
    Born Again
    Its Too Late
    Fake Pastors


Nilimpenda sana kuambiana katika filamu ya Fake Pastors.

Vijana watanashati Vicent Kigosi (Patric) na Adam Philip Kuambiana (Petro) waliohitumu Chuo Kikuu cha Mzumbe, Morogoro Vichwani mwao wanaelewa kitu kimoja tu walichoambiwa tangu utotoni kuwa ukiwa na digree masiha yatakuwa rahisi jambo ambalo baada ya kuingia mitaani wanakuta ni tofauti kwani hakuna ajira na maisha yanakuwa magumu sana kwao.

Baada ya kutembea katika ofisi moja hadi nyingine wakitafuta kazi bila mafanikio, hatimaye wanagundua kuanzisha kanisa ndio suluhisho pekee walilobakiza hivyo wanaamua kuwa wachungaji wa uongo (Fake Pastors) na kuanzisha kanisa kwa lengo la kujitajirisha badala ya kumtumikia Mungu, kazi yao inakuwa ni kuwakamua waumini fedha na mali walizonazo. 
Kwakufanya hivyo wanajikusanyia utajiri mkubwa hasa baada ya misaada kuanzia kuingia kutoka nje kwa wahisani, baadala ya kufanya kazi ya Mungu wao wanazitumia fedha hizo katika anasa wakilewa pombe na kununua Malaya usiku na ifikapo asubuhi wanahubiri injili kama kawaida na kuwafanya waamini wazidi kuwakubali.  Baadae walijingiza katika biashara haramu dawa za kulevya ndipo Mungu Mbinguni alipoamua kuingilia kati na kuwaadhibu vibaya.

Cast: Adam Philip Huambiana (Petro), Vicent Kigosi (Ray),  Jokette Mwegelo (Jach), Lisa Jensen (Lisa), Blandina Chagula

Producer- Vicent Kigosi, Executive Producer- Eric Shigongo, Director- Gervas Kasiga