Devin, Mimi Augustin, Chemi na Charles Jackson aka Mzee MatumbiWiki iliyopita niligiza katika sinema fupi iitwayo 'The Gift' (Zawadi). Inatengenezwa na wanafunzi wa filamu wa Emerson College hapa Boston.
Sinema inahusu familia ya kiislamu ambao wanakaa Marekani halafu wanamchagulia binti yao mchumba. Awali ilikuwa sinema iigizwe na wahindi lakini waiigazji walikosekana kukamilisha familia katika sinema. Hivyo waliamua kufanya familia wawe waafrika. Sinema imepigwa katika 35MM format hivyo inabidi ipelekwe lab kusafishwa. Wamechanganya mambo ya kihindi ya kiafrika. Mfano kwenye arsui Bibi harusi kavaa nguo ya kihindi halafu kuna chakula cha kihindi. Natumaini itapendeza lakini. Huenda ikakamilika kabla ya mwezi wa sita.
Katika sinema hiyo, mimi niligiza kama Mama, Charles 'Matumbi' Jackson aliigiza kama Baba, Mimi Augustin aliigiza kama binti Anum, na Devin ndo Mchumba/Mume.















