BEHIND THE SCENES OF THE HARLEM RENAISSANCE REVISTED WITH A GOSPEL FLAVOR PLAY
Wadau, wiki iliyopita nilikuwa kwenye mchezo wa kuigiza (tamthiliya)hapa Boston. Tulicheza May 7-9. Show ya mwisho ilijaa watazamaji mpaka ilibidi wengine wasimame. Show inahusu kipindi cha Harlem Renaissance miaka ya 1920-39. Ni kipindi ambacho wasanii waMarekani weusi walistawi Marekani na Ulaya.
Kabla sijavaa costume. Kwenye mchezo mimi niliigiza kama Mama, Bibi na Ms. Thelma.
Joe Banks (Steve Lucky) na Mwongoza mchezo Lee Smith wakitaniana
Ron Murphy (Father Africa) akipumzika Dressing Room kabla ya kwenda stage
Ona nilivyokuwa tajiri kwenye mchezo, binti Sidney ananiibia.
Ron Murphy, Ruby Hill (Bag Lady) na Charles Jackson
Ms. Thelma (Mimi) na Joe the Bartender (Charles Jackson). Kwenye mchezo Joe anampenda Ms. Thelma lakini namkataa halafu baadaye namkubali.
"Mko Tayari!" Mwongoza mchezo Lee Smith na msaisdizi, Stanley Everett (Weldon Johnson) wakihakisha wachezaji wako tayari.
Ms. Thelma
Baba Afrika (Ron Murphy) na Mama Afrika (Irene O'Bannon)
Mimi na Lee Smith (Hapo nimevaa costume ya kwanza. Mimi ni mtumwa na tunafanyakazi shambani, halafu ghafla mwanangu wa kike anachukuliwa kwenda kubakwa, naishia kulia na kuzuiliwa kwenda kumfuata mwanangu)
Mapacha Dariana na Dashiana na Nia (Katikati)
Costume yangu kwenye scenes za mwisho. Ms. Thelma amekubali kufunga ndoa na Joe. Kwa habari zaidi someni:
http://www.dotnews.com/2009/harlem-renaissance-revisited-three-shows-lilla-g-frederick



