Showing posts with label Fidel Castro. Show all posts
Showing posts with label Fidel Castro. Show all posts

Saturday, December 17, 2016

Kongamano la Kumuenzi Fidel Castro


Nilibahatika kuhudhuria japo kwa muda mfupi Kongamano ya Kumuenzi Marahemu Rais Fidel Castor wa Cuba, iliyofanyika mjini Dar es Salaam, Tanzania, jumapili iliyopita December 11, 2016 kwenye hall ya Taasisi ya Watu Wazima. (Symposium to Honor the Legacy of Fidel Castro).  Waliongolea jinsi Castor alivyotoka kwenye familia ya matajiri lakini alipenda kusaidia na kunyanua maskini.  Pia jinsi Cuba ilivyosaidia Tanzania.


Jenerali Ulimwengu Akiongea
Audience Participants
The Symposium Leaders

Saturday, November 26, 2016

Aliyekuwa Rais wa Cuba , Fidel Castro Afariki Dunia

Rais Castro na Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1977
Aliyekuwa Rais wa Cuba, Fidel Castro, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90.  Castro alifariki usiku wa kuamkia leo.  Mdogo wake, Rais Raoul Castro aliwatangazia waCuba kuwa Castro amefariki saa nne na nusu usiku.  Alisema kuwa maiti ya kaka yake itachomwa moto leo (cremation) huko Cuba. Kutakuwa na Misa ya kumkumbuka  Taifa la Cuba itakuwa na siku kadhaa za kuomboleza.
Rais Raoul Castro alivyowantangazia wananchi:
The commander in chief of the Cuban revolution died at 22:29 hours this evening (03:29 GMT Saturday)," he said. "Towards victory, always!" he added, using a revolutionary slogan.
Marehemu Castro anakumbukwa kwa kuwa Dikteta. Alipindua serikali ya Cuba mwaka 1959, na hakutoka madarakani hadi mwaka 2006.  Alimwachia madaraka mdoo wake Raoul.  Castro alifanya mengi kusaidi nchi za Afrika ikiwemo Tanzania. Nchi ya Marekani waliweka vizuizi vingi juu ya Cuba ili kujaribu kumkomesha Castro lakini walishindwa.
Video ya Ziara ya Rais Castro nchini Tanzania kwa hisani ya AP



Saturday, July 25, 2015

Nabii Fidel Castro

Wadau, Kumbe Rais Fidel Castro wa Cuba ni Nabii. Mwaka 1973 alitabiri kuwa Marekani itazungumza na serikali ya  komunisti Cuba wakipata Rais mweusi na Papa anatoka nchi za Marekani ya kusini. Ona Raisi wa Marekani ni mweusi, Papa anatoka Argentina!  Sasa kuna Ubalozi wa Cuba Washington D.C. na US wanatuma Balozi Cuba! Duh! Vita Baridi imekweisha sasa.


Monday, March 02, 2009

Rais Castro wa Cuba alipotembelea Bongo 1977

Mimi nilikuwa Form One Zanaki Girls, wakati huo 1977. Tulikuwa tunasoma darasani kama kawaida. Ghafla Mwalimu Mkuu katuambia lazima tuende Ikulu kumpokea Rais Castro wa Cuba. Tuliaacha masomo, na kukaguliwa uniform. Tulitembea hadi Ikulu, na tulipangwa ndani ya geti ya Ikulu upande wa bahari. Nakumbuka Castro alikuwa amevaa magwanda ya kijani na mandevu yake halafu alionekana mrefu kweli alivyonipita. Alitupita sisi wanafunzi huko tukishangalia 'CASTRO - NYERERE'! Baadaye kulikuwa na maneno kuwa eti Rais Castro alijialika Bongo ndo maana watu walikuwa hawajajiandaa vizuri. Sijui kama ni kweli lakini. Lakini nikicheki uso wa Mwalimu kwenye hii picha...sijui.

*********************************************************

Kwa habari zaidi soma:

Tuesday, February 19, 2008

Rais Castro wa Cuba Ajiuzulu!

Cuban President Fidel Castro with his host Tanzanian President Julius Nyerere in Tanzania in 1978. I was there!


Rais Fidel Castro, wa Cuba amejiuzulu urais. Castro aliongoza nchi hiyo kwa miaka hamsini! Alipindiua serikali ya kibepari ya Batista siku ya mwaka mpya mwaka 1958! Castro alikuwa mgonjwa muda mrefu, hajaonekana hadharani kwa miaka miwili sasa. Kulikuwa na uzushi kuwa amefariki dunia, lakini habari hizo si kweli.

Alikuwa adui mkubwa wa Marekani shauri ya siasa zake za Communism. Mdogo wake, Raoul Castro atakuwa rais sasa.

Nakumbuka mwaka 1978, nilimwona laivu. Alikuja Dar es Salaam kumsalimia Mwalimu Nyerere. Wakati huo nasoma Zanaki secondary Form II. Tuliambiwa tukajipange pale Ikulu kumpokea. Alikuwa bado fiti wakati huo. Sasa ni mzee kabisa. Nakumbuka watu walisema eti, Castro alijialika kutembea Tanzania. Sijui walikuwa na maana gani. Tulitolewa haraka darasani na kuambiwa tuwahi Ikulu.

***********************************

Kwa habari zaidi soma:

http://www.cbsnews.com/stories/2008/02/19/world/main3843492.shtml?source=mostpop_story

http://ap.google.com/article/ALeqM5jo_74bCqDvop0iQubmaRzy42RadwD8UTE7E00

http://blogs.guardian.co.uk/politics/2008/02/so_fidel_castro_has_finally.html