Showing posts with label Harvard University. Show all posts
Showing posts with label Harvard University. Show all posts

Sunday, June 15, 2014

Mh. Samuel Sitta Akutana na WaTanzania Cambridge, MA

Mh. Samuel Sitta akiwa nyumbani kwangu Cambridge, MA, USA
Siku ya jumamosi, 6/15/14 jioni, Mheshimiwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba na Waziri wa Afrika Mashariki​​, Mheshimiwa Samweli Sitta alikutana na baadhi ya viongozi wa Jumuiya za waTanzania wa New York na Massachusetts. Mkutano ulifanyika Cambridge, Massachusetts.  Katika mkutano huo Mh. Sitta aliongea kuhusu maswala ya Katiba na Uraia Pacha.  Pia aliongea kuhusu jinsi waTanzania wa diaspora watakavyoweza kusaidia kuijenga Tanzania. Mh. Sitta alikuwa Boston kwa ajili kozi fupi katika Chuo Kikuu cha Harvard.

Kwa picha na habari zaidi tembelea VIJIMAMBO BLOG. 


Kutoka Kushoto - Mr. Sangiwa, Mr. Temba, Dr. Malima, Mh. Sitta, Mr. Sangiwa, Mr. Tome, Mr. Mhellla, Chemi
Mh. Sitta akiwa mwingi wa furaha baadaya kuongea na WaTanzania mjini Cambridge, MA


Tuesday, June 29, 2010

Mashushushu wa KiRusi wakamatwa kwetu Cambridge

Kunbe Cold War haijaisha. Wadau, mbavu sina. Tangu jana jioni habari kubwa hapa Boston ni kuwa mashushushu kutoka Urusi wamekamatwa Cambridge. Watu wanashangaa. Walikuwa wanaishi kama mke na mume na eti walionekana kama watu wa kawaida. Of course walikuwa wazungu! Mwanamke eti alikuwa mrembo kweli mwenye nywele blonde! Mnaweza kuona picha yake HAPA. Kwenye taarifa ya habari wakati wa editorial wakiwaongelea, waliweka na muziki wa sinema za James Bond.

Kinachoniudhi ni kuwa kama wewe ni mweusi na unakaa Cambridge hao jirani zako wa kizungu wantakufanyia background check! Ukipita kwenye mitaa kadhaa wanaita polisi maana wanadhani mwizi au una nia mbaya! Kuna siku mimi na marehemu mume wangu tulikuwa tunatembea kwa mguu kwenye mtaa fulani. Nyumba ilikuwa inauzwa tukasimama mbele na kuliangalia. Tukaendelea na safari, si tulifuatwa na mzungu na kuulizwa maswali ya jela. Aliona aibu alipogundua kuwa tulikuwa jirani zake.

Anyway, nirudi kwa hao waRusi. Hao kwa vile walikuwa wazungu hakuna anayesema kitu. Ndo FBI wameshutua watu jana kusema hao walikuwa mashushushu! Na mimi ningesema si hao tu, wako na wengine. Walikuwa wanavizia wasomi wa Harvard na MIT. walikuwa wankaa nyumba fulani enye rangi ya njano huko Trowbridge St. karibu na Harvard Square na Cambridge Rindge & Latin High School.

Wanasema kuwa nia ya hao mashushushu ilikuwa kuishi kama waMarekani na kujuana na watu wenye uhusiano na siasa na mambo ya kitaaluma. Habari walizokuwa wanapata eti walikuwa wanatuma Urusi katika picha.

Mbinu waliotumia ni kukaa nyumba ambayo wanakaa wanafunzi. Wanafunzi wamahama hama hivyo watu jirani wanaokaa muda mrefu katika eneo hawapati nafasi ya kuwajua, na ukiwaona una sema wanafunzi tu.

Haya wazungu hebu acheni kushuku kila mweusi kuwa ni mbaya, wacheki na wazungu wenzenu! Tumechoka!

Kwa habari zaidi someni:

http://www.foxnews.com/us/2010/06/29/authorities-arrest-alleged-russian-spies-massachusetts/

http://www.cnn.com/2010/CRIME/06/29/russian.spying.arrests/?hpt=T2

http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2010/06/29/AR2010062902062.html

Tuesday, July 21, 2009

Kukamatwa kwa Prof. Gates.

Aliyeanza hii sakata la Prof. Henry Louis Gates Jr. ni Bi Lucia Whalen (40) wa Malden, Ma. Yeye ndiye alipiga simu polisi na kusema aliona wanaume wawili weusi wenye backpacks mgongoni wakijaribu kufungua mlango wa hiyo Nyumba Ware St. Nami nauliza huyo Bi Whalen alikuwa anafanya nini Cambridge?

Hii habari ya kukamatwa kwa Prof. Gates nyumbani kwake, imekuwa gumzo sehemu nyingi na kwenye taarifa ya habari. Hasa ni je, ni kitendo cha kibaguzi? Naona ni sawa ni kitendo cha kibaguzi, maana huko Harvard na hapa Cambridge weusi wanaonewa kila siku. Sema hii imekuwa habari kwa vile Prof. Gates ni mtu maarufu.

Soma habari zaidi hapa:

http://www.racismreview.com/blog/2009/07/21/racism-in-cambridge-harvard-prof-gates-arrested/

Tuesday, May 19, 2009

Rest in Peace Justin Cosby

UPDATE : 5.26.09

Mnaweza kupata taarifa zaidi hapa! Yaani tunashangaa kama hizi habari ni kweli. Yaani alikuwa haelekee kabisa! Na huyo ambaye wanadai walimwua ni Jabrai Jordan Copney, mtoto wa polisi mstaafu wa New York. Nadhani na hao mabinti wa Harvard hawasemi wanachojua!http://www.nydailynews.com/news/ny_crime/2009/05/22/2009-05-22_harlem_man_arrested_in_murder_in_harvard_university_dorm.html


(pichani Justin na mpenzi wake)


Wadau, nina habari ya kusikitisha. Kijana ambaye namfahamu tangu akiwa mdogo na rafiki wa mwanangu ameuawa katika bweni Harvard University. Navyosikia alikuwa anawakimbia hao waliomwua. Kwao ni karibu na napokaa mimi. Lazima niseme kuwa huyo kijana alikuwa mpole na hakuwa na matatizo niliyofahamu. Nimesikitishwa mno. Alikuwa anasoma Chuo Kikuu cha Salem State, lakini wanasema kwa sasa alikuwa hasomi pale. Tutasikia mambo yalivyokuwa. Yaani siwezi kuamini.

REST IN PEACE JUSTIN

***********************************************************

CAMBRIDGE, Mass. — A 21-year-old man shot inside a Harvard University dormitory Monday while students studied for finals died Tuesday.

Justin Cosby, of Cambridge, was shot in the abdomen late Monday afternoon while standing on a stairway leading to a common area inside the Kirkland House, an undergraduate dorm. He was found outside the building by police.

The dorm has an electronic security system, and Middlesex District Attorney Gerry Leone said authorities were looking into how Cosby got into the building.

Cosby's mother, Denise, said her son attended Salem State College. He lived a few blocks from the Harvard campus.

"It's just so strange. He was fine, healthy yesterday," Denise Cosby told The Boston Globe. "I just can't believe my son is not here today. Inside I'm just torn up, I feel like someone has murdered me."

No arrests had been made by Tuesday afternoon.
Harvard referred all questions to the district attorney. Leone said it appeared the shooting was isolated.

After the shooting, students were told to remain in the dorm for several hours as police interviewed potential witnesses.

Harvard police added security, mainly as a precaution, and students were allowed to move freely inside the dorm Tuesday.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.thecrimson.com/article.aspx?ref=528246

http://www.boston.com/news/local/breaking_news/2009/05/man_dies_after_1.html

Monday, March 17, 2008

Ajali Central Square Leo - Part 2

Police wakikagua vipande vya nyama na mifupa barabarani

State Police akipima urefu wa ajali ilipotokea hadi lori iliposimama. Unaona alama ya damu jamaa alivyoburuzwa.
Lori kwa mbele! Ilisimama kwenye crosswalk nyingine mbele na ingendelea kumburuza jamaa kama watu wasingemsimamisha!
Kipande kilichofunikwa!
Lori iliposimama! Imesajiliwa Maine Namba yake ni #908655


Hizi ni picha nilizopiga leo asubuhi wakati polisi wanafanya uchunguzi kuhusu hiyo ajali mbaya Central Square iliyomtoa roho mwanafunzi wa chuo kikuu cha Harvard. Alikata roho saa 6 na dakika ishirini mchana. Marehemu ametambulika kama Isaac Meyers, mwenye miaka 28. Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. Amen.
Kuna watu ambao wanadai kuwa marehemu alikuwa anasikiliza Ipod yake ajali ilipotokea. Mwingine anasema alikuwa anatazama kuelekea MIT na hakuwa natazama mbele ndo maana alizolewa na matairi ya nyuma ya lori. Dereva wa lori hajafunguliwa mashitaka.
Wadau, hapo jamaa lipogongwa ni pa hatari sana, maana wenye magari mara nyingi hawaheshimu waenda kwa miguu! Dawa wasimamishe magari ndo watu waruhusiwe kupita!
Kwa habari zaidi someni: