Showing posts with label Housegirl. Show all posts
Showing posts with label Housegirl. Show all posts

Sunday, January 25, 2015

Mwanaume Ajifanya Mwanamke Ili Apate Kazi Dar

 Kutoka Facebook

 
LAHAULA UMEISIKIA HII??? Katika hali isiyo ya kawaida kijana mmoja mwenye jina la Naftaeli Mbowe ameibua mapya jijini Daresalam. Kijana huyu ambaye ni graduate wa sociology katika moja ya vyuo hapa nchini alimaliza chuo mwaka 2011 na kufaulu vizuri sana. Kutokana na maisha ya kuiga akiwa chuoni alijitumbukiza kwenye siasa na kujidai ni mwanaharakati wa chadema hivyo kutokana na uwezo wake darasani aliweza kujenga hoja zilizomfanya akajulikana na uongozi wa juu wa CDM.

Alipomaliza chuo kijana huyu alichukuliwa na viongozi hawa wa ufipani kwa ahadi kuwa aendelee kukisaidia chama ambapo alipangwa kwenye department ya matusi mtandaoni kwa ujira wa kulipiwa chumba jijini daresalam na kulipwa shilingi laki moja kama posho ya mwezi. Chakula na vinywaji walikuwa wanapata kwenye getho walilopangiwa mtaa wa kimara Bucha. Kijana huyu amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda mrefu na yupo humu humu kundini kwa jina bandia. Kutokana na chama kufilisika siku za hivi karibuni kwa kuendekeza kesi za kupinga kila jambo la serikali na safari za viongozi zisizokuwa na tija vijana hawa walitelekezwa.

Kijana huyu toka mwaka 2013 amekuwa akisota mtaani bila mafanikio yoyote ndipo alipoamua kujibadilisha jinsia kwa kuvaa nguo za kike na kusuka rasta ili aombe kazi za uhasegirl na azma yake hii ilitimia. Aliajiriwa na mama mmoja asiyekuwa na mume maeneo ya ubungo msewe na hakuweza kumshtukia kwa muda wa miezi miwili kwani aliishi kwa umakini mkubwa sana. Juzi ijumaa limemtokea la kumtokea baada ya mtoto wa kiume wa mwenye nyumba kwenda kumpiga chabo akioga ili afaidi kuona maumbile ya beki tatu huyo.

Alishangazwa na alichokiona ikabidi amkasirikie mama yake sana kwa kumleta mwanamme ndani ya nyumba yao huku akisingizia ni mwanamke. Gadhabu zilimpanda zaidi kwa kuwa njemba hilo lilikuwa likilala na dada yake ndipo njama za kumuumbua bila mama yake kujua ziliposukwa.Alipotumwa sokoni mtoto wa mama wa kazi ambaye ni wa kiume aliamua kufuatilia nyuma ili kumuumbua, huku akiwa na wenzanke walimsimamisha na kumshushia kipigo cha maana ndipo alipoelezea kisa kizima.

Vijana wa chadema mliopo kwenye magetho mbali mbali okokeni sasa njooni ccm. mtaumbuka mjini hapa.

Tuesday, August 11, 2009

Da Flora Aongelea Suala la Mahausegeli

Wadau, hii suala la mahausegeli kugeuza nyumba danguro lipo siku nyingi. Pia mahausgeli kupata mimba za baba mwenye nyumba au vijana wa kiume kwenye nyumba ni jambo la kawaida. Tufanye nini ili kutokomeza hiyo tabia chafu?

***********************************************************************
Na Flora Wingia
9th August 2009

Mpenzi msomaji, lipo jambo moja nimesimuliwa nikaona ni vema nawe nikumegee pengine huna habari kama hata hayo yanatendeka nyumbani kwako bila kujua.

Ndani ya familia zetu nyingi, hazikosi mtumishi wa nyumbani awe ni hausigeli au shambaboi. Katika nyumba hizi, zipo zenye watoto wadogo au zingine zina wazee ambao wanatunzwa na mahausigeli hao.

Pia zipo ambazo hazina wazee wala watoto bali ni mahausigeli pekee ambao hubakia nyumbani baada ya matajiri zao kwenda kazini. Hizi ndizo nitakazozungumzia leo, nikigusia kidogo zile zenye watoto wadogo.

Ipo familia moja jirani na kwa rafiki yangu pale Makonde, Mbezi Beach inafanyiwa shere na hausigeli wao lakini hawajui kwa kuwa wote ni wafanyakazi.

Rafiki huyu akanisimulia kwamba binti huyo ambaye anaishi na familia moja yenye watoto ambao wote wanasoma shule za bweni, amekuwa akialika rafiki zake wa kiume pale nyumbani bila woga.

Majirani zake wamekuwa wakimtizama kwa jicho moja na hata walipomtaarifu mama mwenye nyumba kuhusu tabia hiyo, yeye alipinga kwa maelezo kuwa huenda wanamuonea gere kwa kumpata hausigeli mzuri na mchapakazi. Kumbe anasahau msemo kuwa ‘kikulacho kiko nguoni mwako’

Msichana huyu toka moja ya mikoa ya Kusini mwa nchi, anachofanya ni kuamka alfajiri na kuhakikisha kuwa anawaandalia matajiri zake kila kitu wanachohitaji ili wanapoondoka tu majira ya saa 12 asubuhi aweze kurudi kulala kwa saa kadhaa.

Hiyo ndiyo imekuwa ratiba ya bibie huyo kila siku isipokuwa Jumamosi na Jumapili ambapo wenye nyumba wanakuwa nyumbani. Lakini katika siku zingine yeye ndiyo hujipangia ratiba ya kujirusha na yule ampendaye.

Jirani huyu anasema kuwa yupo baba mmoja wa makamo ambaye amekuwa akionekana karibu kila siku nyumbani kwa familia hiyo kuanzia majira ya saa moja asubuhi hadi baada ya mlo wa mchana.

Swali ni je, baba huyu anayedhihirisha kuwa ameoa na anao watoto, haoni aibu kuzoea nyumba hiyo yenye wenyewe? Isitoshe, umri wa binti anayemmendea ni mdogo ikilinganishwa na ule alionao. Na wenyewe wakiibuka ghafla atajitetea vipi? Au ndio amekolewa na ule msemo kuwa inzi kufia kidondani ni halali yake’?

Hicho ni moja ya vimbwanga vya mahausigeli. Tena wengine, huthubutu hata kuleta wanaume zao ndani ya nyumba kama huyo niliyemzungumzia na kudiriki kujirusha juu ya kitanda cha bosi wake.

Eti naye aone raha kama ile aipatayo bosi akiwa na mamsapu wake. Na ukiona hivyo, binti wa aina hiyo huenda analala chumba cha ovyo ovyo, hivyo kujiongezea thamani anaamua kujiliwaza katika mandhari wanayofurahia matajiri zake.

Mahausigeli wengine bila aibu, hujipitishapitisha mbele za mabosi wao wa kiume ili waweze kunasa kwenye ulimbo. Ushawishi huu ni ushetani usiokubalika lakini unazitesa sana baadhi ya familia zetu. Ukweli ndio huo.

Matokeo yake, wanawavuruga vichwa baadhi ya kinababa na hivyo kutamani bila kupenda. Ndio hao unaosikia kuwa mama kamfumania mumewe na hausigeli.

Au mama anamtilia shaka hausigeli kuwa ana mahusiano na mumewe hivyo anamtimua. Wapo kina mama waliowafukuza mahausigeli kibao, kisa macho hayatulii wanapokuwa nyumbani na hasa akiwepo baba mwenye nyumba. Maisha Ndivyo Yalivyo! Au siyo? Kwamba purkushani za aina hii hazikosekani.

Mahausigeli wengine wanapoibukia kwenye nyumba zenye mashambaboi au wengine huwaita mahausiboi, inakuwa kama wamefungishwa ndoa za mikeka. Mabosi wakiondoka kwenda kazini wao ndiyo huanzisha nyumba zao za muda. Wapo waliobebeshana mimba kwa mtindo huo.

Bila kusahau wale wanaotoroka usiku kwenda kujirusha na washikaji wao na kisha kurejea alfajiri bila matajiri wao kung’amua. Hii ni hatari kwani wanaweza kutoa mwanya kwa wezi na kuiba.

Naam. Mpenzi msomaji, hapa nilitaka kuonyesha kuwa pamoja na umuhimu wa watumishi hawa katika kuhudumia familia zetu, lakini wengi wana madhaifu yao kama binadamu. Yapo yanayovumilika lakini mengine hakika hayakubaliki.

Kwa mfano kwa zile familia zenye watoto, wapo baadhi ya mahausigeli wameharibu watoto. Kwa mfano atamleta mshikaji wake nyumbani halafu kwa raha zao wanapigana mabusu huku watoto wakishuhudia. Haya sio malezi mazuri kwani badala ya kuwajengea watoto nidhamu nzuri anawaharibu kwani wataiga matendo yake

Mpenzi msomaji, kwa kifupi nilitaka kuwatahadharisha wazazi wenzangu kuhusu hawa wafanyakazi wetu wa majumbani. Pamoja na umhimu wao, lakini wanahitaji uangalizi wa karibu ili mabosi wanapokuwa makazini, na nyumbani nako kuwe na heshima yake badala ya kugeuzwa nyumba za wageni au sehemu za kufanyia maasi ya kimya kimya.

Tusiwape uhuru wa moja kwa moja. Ikiwezekana katika nyakati fulani mmoja wao, awe baba au mama afanye ziara ya kushtukiza. Yapo mambo mengi yanayoweza kubainishwa na ikiwezekana kuzimwa mapema badala ya kuachwa na hatimaye yakatokea madhara.

Wanapogundua kuwa zipo ziara za kushtukiza, sidhani kama wale waliozoea kuleta washikaji mara tu mabosi wanapoondoka watathubutu kufanya hivyo tena. Pia taarifa za majirani zisipuuzwe kwani wao ndio walioko karibu na wanaona mengi yanayotendeka wakati wenye nyumba hawapo. Au siyo? Huo ni ushauri wa bure, waweza kukubalika au kukataliwa lakini ukweli unabakia pale pale kwamba, lisemwalo lipo na kama halipo linakuja.

Msomaji wangu, kama unayo maoni au mchango wowote nikandamizie kupitia

flora.wingia@guardian.co.tz