Showing posts with label Ubungo. Show all posts
Showing posts with label Ubungo. Show all posts

Sunday, January 25, 2015

Mwanaume Ajifanya Mwanamke Ili Apate Kazi Dar

 Kutoka Facebook

 
LAHAULA UMEISIKIA HII??? Katika hali isiyo ya kawaida kijana mmoja mwenye jina la Naftaeli Mbowe ameibua mapya jijini Daresalam. Kijana huyu ambaye ni graduate wa sociology katika moja ya vyuo hapa nchini alimaliza chuo mwaka 2011 na kufaulu vizuri sana. Kutokana na maisha ya kuiga akiwa chuoni alijitumbukiza kwenye siasa na kujidai ni mwanaharakati wa chadema hivyo kutokana na uwezo wake darasani aliweza kujenga hoja zilizomfanya akajulikana na uongozi wa juu wa CDM.

Alipomaliza chuo kijana huyu alichukuliwa na viongozi hawa wa ufipani kwa ahadi kuwa aendelee kukisaidia chama ambapo alipangwa kwenye department ya matusi mtandaoni kwa ujira wa kulipiwa chumba jijini daresalam na kulipwa shilingi laki moja kama posho ya mwezi. Chakula na vinywaji walikuwa wanapata kwenye getho walilopangiwa mtaa wa kimara Bucha. Kijana huyu amekuwa akifanya kazi hiyo kwa muda mrefu na yupo humu humu kundini kwa jina bandia. Kutokana na chama kufilisika siku za hivi karibuni kwa kuendekeza kesi za kupinga kila jambo la serikali na safari za viongozi zisizokuwa na tija vijana hawa walitelekezwa.

Kijana huyu toka mwaka 2013 amekuwa akisota mtaani bila mafanikio yoyote ndipo alipoamua kujibadilisha jinsia kwa kuvaa nguo za kike na kusuka rasta ili aombe kazi za uhasegirl na azma yake hii ilitimia. Aliajiriwa na mama mmoja asiyekuwa na mume maeneo ya ubungo msewe na hakuweza kumshtukia kwa muda wa miezi miwili kwani aliishi kwa umakini mkubwa sana. Juzi ijumaa limemtokea la kumtokea baada ya mtoto wa kiume wa mwenye nyumba kwenda kumpiga chabo akioga ili afaidi kuona maumbile ya beki tatu huyo.

Alishangazwa na alichokiona ikabidi amkasirikie mama yake sana kwa kumleta mwanamme ndani ya nyumba yao huku akisingizia ni mwanamke. Gadhabu zilimpanda zaidi kwa kuwa njemba hilo lilikuwa likilala na dada yake ndipo njama za kumuumbua bila mama yake kujua ziliposukwa.Alipotumwa sokoni mtoto wa mama wa kazi ambaye ni wa kiume aliamua kufuatilia nyuma ili kumuumbua, huku akiwa na wenzanke walimsimamisha na kumshushia kipigo cha maana ndipo alipoelezea kisa kizima.

Vijana wa chadema mliopo kwenye magetho mbali mbali okokeni sasa njooni ccm. mtaumbuka mjini hapa.

Sunday, June 30, 2013

President Obama's Schedule/Ratiba in Tanzania

Ratiba ya President Obama Bongo

Monday, July 1, 2013
On Monday afternoon, President Obama takes part in a formal arrival ceremony in Dar es Salaam, Tanzania.

President Obama participates in a bilateral meeting and joint press conference with President Jakaya Kikwete of Tanzania.

In the evening, President Obama participates in a CEO roundtable and business leaders forum.
President Obama and President Jakaya Kikwete of Tanzania participate in an official dinner.

Tuesday, July 2, 2013

On Tuesday morning, President Obama takes place in a Consulate meet and greet.
President Obama visits the Ubungo Power Plant.

Mpokee Rais Obama kwa Shangwe!

Tuesday, June 19, 2012

Msimamo wa John Mnyika Juu ya Bajeti!

Msimamo wangu wa sasa juu ya Kauli yangu!


Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya Urais.

Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la mawaziri ikafanyiwe marekebisho!

http://mnyika.blogspot.com/2012/06/msimamo-wangu-wa-sasa-juu-ya-kauli.html

John Mnyika
19 Juni 2012

Sunday, October 02, 2011

Mzee Mark Kisamecha Mfunguo Ampeotea


UPDATE:  MZEE MFUNGUO AMEPATIKANA YU SALAMA!
Mzee Mark Kisamecha Mfunguo

Ndg. Mark K. Mfunguo mkazi wa Ubungo Msewe(karibu na kanisa la Deeper Life) amepotea tangu tarehe 01/10/2011 kabila lake ni mchagga wajihi wake ni maji ya kunde na ana mvi kichwani ana umri wa miaka 65 na ana tatizo la kupoteza kumbukumbu (Dementia). Mara ya mwisho kuonekana ilikuwa ni tarehe 01/10/2011 siku ya jumamosi maeneo ya UBUNGO-EMAUS alipokwenda kwa ajili ya huduma ya maombi.


Mwenye taarifa zozote za kuonekana kwake atoe taarifa kwenye kituo chochote cha Polisi kilichopo karibu naye na namba zifuatazo

0786-871720

0688-871720

0754484947

0713698240

0754-455176

ASANTENI!