Showing posts with label River St.. Show all posts
Showing posts with label River St.. Show all posts
Sunday, September 12, 2010
Sunday, September 13, 2009
Caribbean Festival Kwetu Cambridge Leo! Part II
Mara parade ilivyoisha hawakuchelewa kuanza usafi!
Kulikuwa na polisi kibao kutulinda! Bila shaka mmesikia habari za fujo wanazofanya kwenye hiyo parade wakiwa Boston, hata watu wamepigwa risasi na kuchomwa visu, na hata kufa. Kwetu Cambridge, mambo shwari! Tatizo hao wanaume wanaolinda wanawake zao kwenye parade. Umtizime GF au mke wa mtu utakoma! Wanaume wao wako karibu! Lakini wengine wako karibu uchi utaweza kuacha kuwtazama kweli?
Hao walipita kwenye sidewalk, maana hawakuwa official. Walikuwa wananuka bangi, ile mziki wao ulinikumbusha muziki wa asili ya waKulya.


Nimeshika bendera ya Jamaica, ni nchi alikozaliwa mama yangu. Huyo baba sijui nitammwona wapi nimpe picha yake!
Huyo baba alikuwa amelewa. Alikuwa anasakata rhumba, alisema yeye ni mzuri wa ajabu (Most handsome Man) na wanamwita Denzel Washington au Billy Dee Williams. Jirani yangu anayetoka Jamaica kamwambia, "don't kid yourself!" Alisema anatoka Trinidad.
Labels:
Cambridge MA,
Caribbean Carnival,
River St.
Caribbean Festival Kwetu Cambridge Leo!
Wadau, leo hapa Cambridge, Massachusetts, tulivamiwa na watu wa Boston. Walikuwa hapa kwa ajili ya Caribbean Carnival ambayo infanyika kila mwaka. Mwaka huu walichelewa kuifanya, kawaida wanafanya August na ndo tunaaga summer (kipindi cha joto). Nimepiga picha kadhaa kwa ajili yenu.


Saturday, May 17, 2008
Zimamoto Kazini Cambridge Leo I
Nyumba ikiungua moto kwenye kona ya River St. na William St., Cambridge MA leo.
Zimamoto Kazini Cambridge Leo III
Karibu na napokaa kuna nyumba ulianza kuunga moto. Bahati wameiwahi. Tunasikia harufu ya moshi. Zimamoto na polisi wamefanya evacuation ya nyumba karibu na pale. Nyumba iliyoungua iko karibu na sehemu ya kufua nguo (laundromat) mtaani River St.
Gari ya Polisi ikizuia magari kupita mtaa wa Pleasant St. kwenda River St.
Gari ya Polisi ikiuia magari kupita River St. Hiyo basi No. 70 ilikwama hapo hapo! Abiria walishuka na kutembea kwenda Central Square.
Zimamoto juu ya nyumba inayoungua River. St.

Mzimamoto akivaa nguo zake haraka kwenda kuwasaidia wenzake
Gari ya Zimamoto, Chifu wa Zimamoto wa Cambridge ni yuke aliyevaa koti ya njano
Fire Hydrant (Bomba la maji) ambayo walitumia kupata maji kuzima moto. Wadau Mareknai mnajua ni mwiko kuegesha magari mbele au karibu sana na hydrant maana utapata faini kali! Iko kwenye kona ya River na Pleasant St.
Subscribe to:
Comments (Atom)






















