Showing posts with label Cambridge MA. Show all posts
Showing posts with label Cambridge MA. Show all posts

Saturday, November 12, 2016

Kumbukumbu - Mh. Samuel Sitta Alipokutana na WaTanzania Cambridge, MA Mwaka 2014

Mh. Samuel Sitta akiwa nyumbani kwangu Cambridge, MA, USA
Siku ya jumamosi, 6/15/14 jioni, Mheshimiwa Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba na Waziri wa Afrika Mashariki​​, Mheshimiwa Samweli Sitta alikutana na baadhi ya viongozi wa Jumuiya za waTanzania wa New York na Massachusetts. Mkutano ulifanyika Cambridge, Massachusetts.  Katika mkutano huo Mh. Sitta aliongea kuhusu maswala ya Katiba na Uraia Pacha.  Pia aliongea kuhusu jinsi waTanzania wa diaspora watakavyoweza kusaidia kuijenga Tanzania. Mh. Sitta alikuwa Boston kwa ajili kozi fupi katika Chuo Kikuu cha Harvard.

Kwa picha na habari zaidi tembelea VIJIMAMBO BLOG. 


Kutoka Kushoto - Mr. Sangiwa, Mr. Temba, Dr. Malima, Mh. Sitta, Mr. Sangiwa, Mr. Tome, Mr. Mhellla, Chemi
Mh. Sitta akiwa mwingi wa furaha baadaya kuongea na WaTanzania mjini Cambridge, MA


Saturday, October 19, 2013

Mwanangu Ameingia Siasa za Marekani.


Elechi Kadete




 Wadau, nafurahi kuwatangazia kuwa mwananagu, Elechi Kadete, ameamua kufuata nyayo za Babu yake, Dr. Aleck Che-Mponda, na kuingia katika dunia ya siasa. Anagombea kiti katika Baraza la Maashule (School Committee) katika mji wa Cambridge, Massachusetts. Akifanikiwa baadaye itakuwa rahisi kugombea nafasi katika City Council na kwenye ngazi za State. Kutokana na katiba ya Marekani hataweza kugombea Urais kwa vile hakuzaliwa Marekani. Alizaliwa Tanzania. Lakini ataweza kugombea nafasi zingine kama Congress, Senator na Gavana.

Baba mzazi wa Elechi, ni marehemu Prof. Henry Kadete aliyekuwa kuwa Mkuu wa Idara ya Uhandisi Umeme Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alifariki mwaka 1995.  Kwao Prof. Kadete ni Tabora.

Kwa kweli naona watu Cambridge wanamchangamkia,  Tunaomba maombi na dua zenu Ashinde!

Kwa habari zaidi za kampeni ya Elechi:

-->
Email:ekfocusedonfuture@gmail.com
Facebook: The committee to Eelect Elechi Kadete
Twitter: Kadete_1
Telephone Number: (617)504-1679
Website: http://vote.cambridgecivic.com/kadete.htm


http://www.cambridgeday.com/2013/10/04/elechi-kadete-announces-candidacy-for-school-committee/

 Wadau, kampeni ni ghali, mabango, literature, simu, huduma kwa ajili ya wasaidizi zina gharama.

Ukitaka kutuma mchango tuma:

The Committee to Elect to Elechi Kadete
10 Laurel St. #4
Cambridge, MA 02139

Uchaguzi ni Jumanne, Novemba 5, 2013. 

Tuesday, October 30, 2012

Hurricane Sandy Ilivyotupiga Cambridge, MA!

Wadau, jana Kimbunga Sandy kilipita kwetu. Upepo mkali sijawahi kuona. Hiyo kelele utadhani treni inapita.  Mtaa wa jirani, Howard St., Cambridge, MA walikipata!  Tuliruhusiwa kuondoka kazini mapema jana kwa vile  MBTA walikuwa wanasimamisha huduma ya basi na treni. Nilivyofika Howard St. nilikuwa mitawi ya mti imeanguka na kuponda magari kadhaa. Dirisha zao zilivunjwa.  Leo asubuhi nikapita tena na kukuta usiku mtu wote umeanguka! Yaani imevunjika kwenye kisiki. Bahati mbaya gari iliyokuwa upande wa pili wa barabara umepondwa kabisa! Duh! Lakini uzuri hakuna aliyeumia. Sasa sijui kama bima itamlipa jirani yangu hela ya kutosha kununua gari nyingine.

Tazama picha nilizopiga, Howard St., Cambridge, Massachusetts.


10/29/12 Howard St. Mitawi ya miti imeanguka na kuvunja vio vya magari




10/30/12  Upepo mkali ulivunja ule mti!

Maskini gari ya watu

Mti ulikatika kwenye kwenye kisiki!

Wednesday, June 01, 2011

Sisi Wazima! - Vimbunga Massachusetts

Asanteni wadau walionipigia simu kunijulia hali. Sisi ni wazima na Mungu yu mwema hatujapigwa na kimbunga hapa mjini Boston/Cambridge. Maeneo ya Springfield, Westfield, Massachusetts yamepigwa vibaya! Magari yamepinduka, nyumba kadhaa zimebomolewa na nyumba kadhaa hazina umeme. Bado tuko chini ya Tornado Watch mpaka saa 5 (11:00PM). Nimepiga ka kideo muone hali ilivyokuwa kwenye saa 3:30 (9:30PM). Nimepiga kutoka kwenye back porch ya fleti yangu.

Tuesday, February 01, 2011

Snow Imezidi Boston! Tumechoka!



Yaani leo ni siku ya kwanza ya Februari. Tunapigwa na snow tena. Kesho tutapigwa tena. Ikiisha tutakuwa na karibu futi mbili na nusu ya snow! Hiyo ni juu ya ile snow ambayo ilianguka majuzi! Hatuna pakuiweka. Ni hatari kutembea na kuendesha magari shauri ya milima ya snow. Watu wameonywa kuwa ikianza kuyeyuka kutakuwa na mafuriko!

Thursday, January 13, 2011

Tunapambana na Theluji na Barafu!






Ni msimu wa winter (Baridi) hapa Marekani. Tunatamani joto la Dar. Hizi picha nilipiga hapa Cambidge, Massachusetts leo asubuhi.

Sunday, September 13, 2009

Caribbean Festival Kwetu Cambridge Leo! Part II

Mara parade ilivyoisha hawakuchelewa kuanza usafi!
Kulikuwa na polisi kibao kutulinda! Bila shaka mmesikia habari za fujo wanazofanya kwenye hiyo parade wakiwa Boston, hata watu wamepigwa risasi na kuchomwa visu, na hata kufa. Kwetu Cambridge, mambo shwari! Tatizo hao wanaume wanaolinda wanawake zao kwenye parade. Umtizime GF au mke wa mtu utakoma! Wanaume wao wako karibu! Lakini wengine wako karibu uchi utaweza kuacha kuwtazama kweli?
Hao walipita kwenye sidewalk, maana hawakuwa official. Walikuwa wananuka bangi, ile mziki wao ulinikumbusha muziki wa asili ya waKulya.




Nimeshika bendera ya Jamaica, ni nchi alikozaliwa mama yangu. Huyo baba sijui nitammwona wapi nimpe picha yake!

Huyo baba alikuwa amelewa. Alikuwa anasakata rhumba, alisema yeye ni mzuri wa ajabu (Most handsome Man) na wanamwita Denzel Washington au Billy Dee Williams. Jirani yangu anayetoka Jamaica kamwambia, "don't kid yourself!" Alisema anatoka Trinidad.

Huyo jamaa alichukua bendera yangu, aliomba apige picha nao. Alikuwa amelewa mno, na kaongea lugha ambao sielewi!

Hao wameikumbusha ngoma ya Sindimba!



Huyo dada alihangaika mno na hiyo costume. Mpaka tukapiga bets kuwa hata fika mbali kwa maan ilikuwa nzito na alikuwa hoi! Alivyofika mbele yetu kwenye taa walimpa mtu mwingine aivae! Huyo alikuwa karibu kuzimia!

Hao walichelewa na walikuwa wanaenda kujiunga na wenzao.

Caribbean Festival Kwetu Cambridge Leo!

Wadau, leo hapa Cambridge, Massachusetts, tulivamiwa na watu wa Boston. Walikuwa hapa kwa ajili ya Caribbean Carnival ambayo infanyika kila mwaka. Mwaka huu walichelewa kuifanya, kawaida wanafanya August na ndo tunaaga summer (kipindi cha joto). Nimepiga picha kadhaa kwa ajili yenu.