Wadau, ndo Uselebriti huo, Uzushi mwingi! Saida Karoli yu Hai! Mungu azidi kumbariki!
Hakuwemo kwenye boti iliyopata ajali, Ziwa Victoria!
*********************************************
Taarifa ya Neville Meena kuwa ingawa ni kweli kuna ajali ya
boti iliyotokea, mwanamuziki Saida Karoli hakuwa mmoja wa waliokuwemo
kwenye boti hiyo na yuko hai!Taarifa hiyo imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa
Saida Karoli ni mzima, yupo jijini Dar es Salaam: “Nimetafuta namba yake
ya simu sijaipata, ila taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa
Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli…” ameandika Meena.
Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “…ni kweli kwamba kuna boti
imezama katika Ziwa Victoria, na kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba
na Wilayani Muleba kuhusu
mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa
mmoja wa abiria.”Nayo Upland FM
radio, Kwa kupitia Facebook page yake, imekanusha taarifa za kufariki
Saida kalori na kusema msanii huyo ni mzima wa Afya. “TAARIFA: Kumezuka
habari zisizo rasmi juu ya mwanamuziki SAIDA KALORI. Tunaomba
kuthibitisha kwa Mwanamuziku huyo ni MZIMA wa afya kabisa. Usidanganywe
na uzushi wowote. ASANTE.” imesema taarifa hiyo ya Upland FM
Showing posts with label Saida Karoli. Show all posts
Showing posts with label Saida Karoli. Show all posts
Tuesday, June 18, 2013
Subscribe to:
Comments (Atom)



