Showing posts with label Simba. Show all posts
Showing posts with label Simba. Show all posts

Monday, March 07, 2011

Simba Hajatoroka Dar es Salaam Zoo!

Kumbe ule uzushi kuwa simba wa Dar es Salaam katoroka na anazurura mjini Dar es Salaam si kweli! Ifuatayo ni Tamko Rasmi kutoka Dar es Salaam Zoo
**********************************************************************
Habari

Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu wananchi wa maeneo ya kibanda, kigamboni na maeneo ya jirani na Zoo na Dar es Salaam nzima kwa Ujumla, Kua Taarifa za kutoroka kwa kati ya Simba wetu kwenye Zoo sio za kweli.

Simba wetu wote wako salama pamoja na Wanyama wengine wote. Simba alie patikana maeneo ya Mbagala na huyo mwingine anaesemekana kuepo maeneo ya huko hatoki kwenye Zoo yetu.
Kuhusisha Dar esSalaam Zoo na wanyama hao ni Uzushi na Tetesi za mtaani.

Karibuni Sana Dar es Salaam Zoo
Akhsanteni Sana.

Mr. Salim Hassan
Marketing manager
Dar Es Salaam Zoo
+255 784 524285

Tuesday, June 09, 2009

Shindano kwa Kaka Michuzi


Wadau, kuna shindano ya kutunga caption ya hii picha kwa Kaka Michuzi!

Mbavu sina! Sasa huyo simba anashangaa au?

Monday, July 28, 2008

Yanga - Rest in Peace

Upinzani kati ya timu za soka, Simba na Yanga ni kali sana huko Bongo. Yaani nakumbuka watu wamepigana na hata ajali za gari na vifo zimesabishwa na upinzani huo. Lakini si mchezo jamani? Kwa nini watu wanachukulia 'serious'?

Hebu cheki washabiki wa Yanga walivyowatania timu ya Yanga leo! Wamebeba jeneza la Yanga! DUH!

*********************************************************
Kutoka Michuzi Blog:



Yanga yafungiwa miaka 3, na faini dola 35,000

KLABU ya Yanga imefungiwa kushiriki michuano inayoandaliwa Shirikisho la vyama vya soka vya nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) kwa miaka mitatu sambamba na kupigwa faini dola za Kimarekani 35,000 kutokana na kugomea mchezo wa kuwania nafasi ya mshindi wa tatu ya michuano ya kombe la Kagame.

Akitangaza uamuzi huo uliofikiwa na kikao cha kamati ya uendeshaji wa michuano hiyo ya Kagame jana usiku mara baada ya michuano hiyo kukamilika, Katibu Mkuu wa Cecafa, Nicolas Musonye alisema mbali na adhabu hiyo ya kufungiwa pia Yanga imepigwa faini hiyo ambayo inatakiwa kulipwa katika kipindi kifupi iwezekanavyo.

Musonye ambaye alikuwa akizungumza huku akionyeshwa kukerwa mno na kitendo hicho cha Yanga kugomea mchezo huo, alisema jambo walilofanya Yanga ni kitendo cha aibu na ndio maana wameamua kuchukua hatua hiyo ili iwe onyo na fundisho kwa timu nyingine.

"Adhabu hii haina suala la kukata rufaa na adhabu hiyo itakuwa ikitekelezwa pale tu Yanga itakapokuwa imefuzu kucheza michuano ya Cecafa na endapo hatalipa faini yake iliyotozwa haitoshiriki michuano yoyote ile ya Cecafa hadi ilipe faini hiyo" alisema Musonye.

Musonya aliongeza kuwa wao kama Cecafa wameliomba pia Shirikisho la soka Tanzania ambao ndio walikuwa wenyeji wa michuano hiyo ya Kagame kwa mwaka huu kuichukulia hatua Yanga kutokana na utovu huo wa nidhamu iliyoonyesha.

Aidha Musonye alisema pamoja na kuwapa adhabu hizo mbili pia italiandikia Shirikisho la soka la Afrika (CAF) kuielezea juu ya kitendo hicho cha utovu wa nidhamu kilichofanywa na klabu ya Yanga ili kuonyesha ni jinsi gani timu hiyo haina nidhamu.

"Unajua kitendo walichofanya Yanga kinaonyesha upambavu wa viongozi wa klabu hiyo na kwa kweli wana bahati sana mimi si kiongozi wa soka hapa la sivyo ningewafungia maisha" Musonye alisema.

Musonye aliongeza kuwa uongozi wa Yanga mbovu wa Yanga umeiletea hasara Cecafa na TFF kwa sababu ya uamuzi wa viongozi wachache wa klabu hiyo na wasipoangalia klabu hiyo ina hatari ya kuporomoka kabisa katika soka.

Aidha Musonye alikanusha kuwepo makubaliano ya aina yoyote kati ya Cecafa, TFF na klabu za Simba na Yanga za kupeana fedha kama ilivyodaiwa na viongozi wa Yanga na kusema huo ni uongo wa mwaka kwani kanuni za Cecafa zinajulikana wazi kabisa kuwa hakuna suala la timu kupewa mgao wa mechi na timu zote zinatambua hilo.

Tuesday, April 08, 2008

Tangazo toka enzi za Ukoloni


Tangazo la baiskeli enzi za Ukoloni!