Showing posts with label Michuzi. Show all posts
Showing posts with label Michuzi. Show all posts

Sunday, May 15, 2016

Shukurani Kutoka Kwa Familia ya Michuzi - Msiba wa Maggid Muhidin

Familia ya Ankal Muhidin Issa Michuzi inapenda kutoa shukrani nyingi sana sana kwa ndugu, jamaa, majirani, marafiki na wafanyakazi wenzie kwa kujitoa kwa hali na mali katika wakati huu mgumu wa msiba wa mawanae Maggid (pichani) aliyefariki huko Durban, Afrika Kusini Jumapili ya wiki iliyopita na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam juzi Jumamosi.
Ni vigumu mno kumshukuru mtu mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila mmoja wenu alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe tumehitimisha robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu. Hivyo tunaomba radhi kwa yoyote ambaye hatutomtaja, kwani wafadhili wetu nyie mko wengi mno.
Pamoja na hayo shukrani za kipekee ziwaendee Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli na familia yao yote, Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete na familia yao yote, Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake yote, Rais Mstafu wa awamu ya Tatu Mzee Benjamin William Mkapa na Mama Anna Mkapa na familia yao yote, Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Familia yake yote, Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Allan Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Ombeni Sefue pamoja na wafanyakazi wenzie wote wa baba mfiwa kwa kuwa karibu naye katika wakati wote, na kuhakikisha kuwa kila kitu katika msiba huu kinaenda sawasawa. TUNAWAOMBEA KWA MOLA AWAPE BARAKA ZAKE ZOTE...

Salamu zingine za kipekee ziwaendee watumishi wote wa Ubalozi wetu Afrika kusini mjini Pretoria ambao wakiwa chini ya Brigedia Jenerali Kimaryo na Afisa wa Ubalozi kaka Awesi walisimamia maswala yote ya kuusafirisha mwili kutoka Durban kuja Dar es salaam. MOLA AWAONGEZEE PALE MTAPOPUNGUKIWA...

Vile vile shukrani za kipeke ziwaendee Viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Watanzania waishio Durban pamoja na Muslim Burial Society ya hapo hapo Durban ambao walihakikisha mwili wa marehemu unahifadhiwa, unakafiniwa na unasafirishwa kwa heshima zote. ALLAH AWAJAALIE KATIKA KILA JAMBO...

Kwa Uongozi wa msikiti wa Maamur uliopo Upanga Dar es salaam pia familia inatoa shukurani za kipekee kwa yote mliotutendea ikiwa ni pamoja na mwongozo wa kidini katika wakati wote wa msiba na mazishi.
Tutakuwa watovu wa fadhila endapo kama hatutatoa shukurani za kipekee kwa magrupu ya WhatsApp yote ambayo baba mfiwa Ankal ni mwanachama. Shukurani hizi maalum ziwaendee Ma-Admin na wanachama wa Kariakoo Family Group (KFG), Dar es salaam Old Friends (DOF), Ma Best Group (MBG), Wanahabari, Tasnia ya Habari, Uongozi, Siasa na Matukio Mix, The New Team, TSJ Alumni, Zama Zile, The Brain Team, Jazz Fans, The Kop in Tanzania, LFC Bongo, Uswazi Academia, Tanzania Bloggers Network (TBN), The Legends Family, SID Tanzania Chapter, Mawasiliano, Team Michuzi, Amani Kwanza Group, Photojournalists TZ, PPAT Members, P Mamas, RUBY 15, Warembo wa KA, Mambachoz Group, Ndanshau Group, Empress Group kwa Fundi Mussa na wengi wengine wote katika Social media wakiongozwa na Jamii Forum na VIJIMAMBO BLOG ya Marekani. TUMEHEMEWA MNO NA KUFARIJIKA SANA KWA MICHANGO YENU YA HALI NA MALI. WE ARE HUMBLED. MBARIKIWE SANA, SANA, SANA...
Mwisho, lakini sio kwa umuhimu bali kwa nafasi na mpangilio, tunatoa shukrani za kipekee kwa shirikia la ndege la Emirates kwa kufanikisha usafiri wa mwili wa marehemu, hali kadhalika kampuni mahiri ya SWISSPORT kwa kusaidia logostics zote katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.

HATUNA CHA KUWALIPA ZAIDI YA KUTOA SHUKURANI NA KUSEMA ASANTE SANA NA KUWAOMBEA KWA MOLA KILA MMOJA WENU AWABARIKI KATIKA SHUGHULI ZENU ZOTE...

Inna Lillahi wa inna ilaihi raji'un

AMIN!




Saturday, May 14, 2016

Mazishi ya Maggid Muhidin Leo

CODES:
Mwili wa marehemu ukiingizwa katika msikiti wa Maamur Upanga jijini Dar es salaam leo tayari kwa kuswaliwa kabla ya mazishi.
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete (kushoto) akimfariji baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi.
Mama wa marehemu (aliyevaa nguo nyeupe) akiwa na ndugu wa karibu wakiomboleza.
Baba wa marehemu akiwa na viongozi wa dini wakiombea mwili wa marehemu dua.
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa na ndugu wa marehemu.
Baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi akipata chakula.
Mke wa Rais mama Janeth Magufuli (kulia) akiwasili msibani Wazo hill akiwa na baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi.
Baba wa marehemu akiwa na Balozi Cisco Mtiro na baadhi ya waombolezaji.
Baba wa marehemu (mwenye kofia), Ankal Issa Michuzi akipewa pole na baadhi ya waombolezaji mara baada ya maziko ya mtoto wake Maggid Muhidin Michuzi (18)yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akimpa pole Issa Michuzi.
Rais Mstaa mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete akimfariji Ankal Issa Michuzi.
Issa Michuzi (mwenye kofia) akifuatiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe Ombeni Sefue. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi, Katibu Mkuu Ikulu Mhe. Peter Ilomo wakati maziko.
Waumini wakiomba dua.
Baba wa marehemu Issa Michuzi (katikati) akiwa na huzuni akiwa na Rais mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, kulia kwake ni Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Sinde
Baba mkubwa wa marehemu, Ismail Issa Michuzi akitoa shukrani kwa walioshiriki mazishi ya mtoto wao.
Mroki Mroki ambaye aliyekuwa MC akitoa ya muongozo wakati wa mazishi.
Waombolezaji wakiweka udongo kwenye kaburi la marehemu.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Mhandisi John Kijazi akiweka udongo.
Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba akiweka udongo kaburini.
Rais mstaafu Jakaya Kikwete akiweka udongo kaburini.
Baba wa marehemu Ankal Issa Michuzi akiweka udongo kaburini.
Mwili wa marehemu ukiwekwa kaburini.
Mwili ukiwasili makaburini.

Rais mstaafu Jakaya Kikwete akimpa pole baba wa marehemu, Ankal Issa Michuzi. Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi. Picha zote na Francis Dande


Wednesday, September 09, 2015

Sunday, March 01, 2015

Team Michuzi Production Yarekodi Kwa Weledi wa Hali ya Juu Mnuso wa Tanzania Bloggers Party Serena Hotel Jijini Dar es Salaam

Ankal akiwa na MD wa Michuzi Media Group (kulia kwake) pamoja na kikosi kazi cha Team Michuzi Production chini ya Production Manager Barbra Kilugira (wa tatu kushoto) ambayo ilipata heshima ya kurekodi mnuso wa kihistoria wa Tanzania Bloggers Network (TBN) Meet and greet Party katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia March 1, 2015. Mnuso huu ulifanikiwa sana kwa udhamini mkubwa wa VODACOM TANZANIA (wadhaini wakuu), NMB, COCACOLA, RAHA.COM na SERENA HOTEL. 

Saturday, December 06, 2014

TAHADHARI MUHIMU KUTOKA MICHUZI MEDIA GROUP



MKURUGENZI MTENDAJI WA KAMPUNI YA MICHUZI MEDIA GROUP (MMG) ANAPENDA KUTAHADHARISHA WADAU POPOTE WALIPO KUHUSIANA NA UJUMBE (PICHANI) AMBAO UPO KWENYE FACE BOOK NA HATA KWENYE TWITTER) KWAMBA UJUMBE HUO  HAUHUSIANI KWA LOLOTE NA ANKAL MUHIDIN ISSA MICHUZI,  WALA MMG AMA WAKALA WAKE. 

HIVYO TUNAWASIHI TUSIHUSISHWE NAYO NA PIA TUNAWAOMBA KUWA MACHO NA MAMBO KAMA HAYA, MAANA ULAGHAI NA UTAPELI MITANDAONI NI MWINGI MNO.

AHSANTENI SANA
ANKAL

Saturday, October 18, 2014

Chemi Katika Sinema, HIstoria ya Khanga 1994



Mwaka 1994, TAMWA, walitengeneza sinema kuhusu Historia ya Khanga. Mimi nilikuwa mmoja wa waigizaji pamoja na Issa Michuzi.  Mnaweza kuona Clip yote YOU TUBE:

CHEMI & MICHUZI IN HISTORY OF KHANGA

Saturday, August 24, 2013

Mombasa Port Loses Business as Exporters Opt for Dar es Salaam

--
Kenya Port Authority (KPA) is losing business to rival Dar es Salaam port as delay in cargo clearance in Mombasa prompts traders from neighbouring countries to turn to Tanzania.
Data from KPA shows that the Mombasa port handled 18.9 per cent less or 552,449 tonnes of cargo from Tanzania, Burundi, Rwanda and the DRC in the nine months to September.
As a result, the port relied on Uganda and South Sudan—that have little choice on their logistic corridor—to grow its export cargo volumes to 3.9 million tonnes in the nine months compared to 3.8 million tonnes in the same period last year.
Shippers attribute the trend to the shorter period it takes to transport cargo from the port of Dar es Salaam compared to Mombasa which is facing congestion that has seen transporters take more than a month to reach Rwanda from three weeks.
“We are losing business to Tanzania because of inefficiency at the port,” said Gerald Kagumo, the vice chairman of East Africa Freight Forwarders Association.
Kwa hisani ya Kaka Michuzi

Saturday, June 22, 2013

Kaka michuzi Aishukuru Hospitali ya KiLutheri ya Haydom

 Wadau, hivi karibuni mtoto wa Kaka Michuzi, ally aliugua vibaya malaria.  Hospitalia y a Kilutheri ya Haydom waliokoa maisha yake. Kaka Michuzi anatoa shukurani kwa Hospitali hiyo na wafanyakazi wake:

***********************************************

ANKAL AISHUKURU HOSPITALI YA KILUTHERI YA HAYDOM KWA KUMHUDUMIA VYEMA MWANAE

Nachukua nafasi hii kutoa shukurani zangu za dhati kutoka katika kilindi cha moyo wangu kwa Hospitali  ya Kilutheri ya Hydom iliyoko mkoani Manyara kwa matibabu waliyompatia mwanangu Ally Hassan (16) aliyelazwa hospitalini hapo tokea siku ya Alhamisi Juni 13, 2013 akiwa hajitambui  (in a coma) kwa muda wa siku nne mfululizo baada kuugua malaria.

Shukurani maalum ziwaendee madaktari na wauguzi wote wa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) ambao kwa siku hizo nne tulikesha nao kumuuguza Ally ambaye aliletwa hapo toka Katesh alikoenda kumtembelea mama yake wakati huu wa likizo akiwa hana fahamu. Kwa upendo, weledi na utaalamu wenu hatimaye mlifaniklwa kupambana na malaria hiyo kwa ukamilifu. Hivi sasa Ally hajambo na anaendelea kupata nafuu kila dakika.

Mama mzazi, Baba mlezi, mjomba, shangazi, mamdogo na mamkubwa mliojitoa kumsaidia Ally nawashukuru sana sana kwa upendo wenu.

 Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Kilutheri ya Haydom sina cha kuwalipa zaidi ya kutoa ahsante kwa wote mliomshughulikia Ally pamoja na wagonjwa wengine waliolazwa hapo (nilishuhudia kwa macho yangu jinsi mlivyokuwa mkiwashughulikia wagonjwa wote kwa upendo na weledi kila dakika walipohitaji uangalizi) na kupata nafuu.

Kwa niaba ya wagonjwa wengine waliopata huduma na kupata nafuu, natoa pia ahsante kwa kazi njema, ya weledi na upendo mnaoonesha kwa kila mgonjwa anayefika kutibiwa hapo Hydom. Ninyi ni mfano wa kuigwa katika mahospitali yetu yote hapa nchini.

 NAOMBA MOLA AWALIPE KWA  KUWAZIDISHIA.PALE MLIPOPUNGUKIWA. MBARIKWE SANA.


Kaka Michuzi na Mwanae Ally




Monday, October 03, 2011

Sinema 'Historia ya Khanga" Cheki Mimi na Kaka Michuzi!

MaStaa wa Bongowood 1991 Michuzi & Chemi


Kabla ya Kanumba na Ray kulikuwa na Chemi na Michuzi!

Wadau, kwenye mwaka 1992 nilishiriki katika sinema ya TAMWA, "The History of Khanga".  Hebu itizame, Utaniona mimi na Kaka Michuzi, "Tunajiandaa kulala"

Mwongozaji alikuwa Dada Fatma Alloo. Pia kuna mahojiano na marehemu Bibi Titi Mohamed.

Sinema sasa iko YOU TUBE kwa hisana ya Dada Fatma na Kaka Michuzi:

http://www.youtube.com/watch?v=jAuhAB0HeeA&feature=player_embedded

Monday, August 29, 2011

Happy Birthday Kaka Michuzi!

Namtakia Kaka Michuzi Happy Belated Birthday! Birthday yake ilikuwa jana Jumapili August 28th. (Pichani Blogger No.1 from Tanzania, Muhidini Michuzi)

KWA MAJAALIWA YAKE MWENYEZI MUNGU MTUKUFU LEO ANKAL ANASHEREHEKEA SIKU YA HEPI BESDEI YA KUZALIWA KWAKE.

ANAMSHUKURU MOLA KWA KUMJAALIA KUFIKISHA SIKU YA LEO SALAMA, NA ANAMUOMBA AMUAFU YEYE NA FAMILIA YAKE PAMOJA NA WADAU WOTE MAISHA MEMA NA YA AFYA, NA KUMPA NGUVU KUENDELEA KUITUMIKIA JAMII KWA MOYO MMOJA BILA KUCHAGUA WALA KUIBAGUA KWANI ATAYEMZIKA HAMJUI.

ANATOA SHUKRANI PIA KWA TIMU NZIMA YA GLOBU YA JAMII KWA KUENDLEZA UTUMISHI ULIOTUKUKA, WADAU KWA KUENDELEA KUMSAPOTI PAMOJA NA WAFADHILI WOTE AMBAO KWA PAMOJA ASINGEFIKA HAPA PADOGO ALIPO KWA URAHISI. MOLA NA AWABARIKI NA AWAZIDISHIE KILA PENYE MAPUNGUFU.

Friday, July 01, 2011

Taarifa ya MO Blog kwa Wadau

MO BLOG INAPENDA KUWAFAHAMISHA WADAU NA WASOMAJI WA BLOG HII KUWA TUMESIKITISHWA NA KUHUZUNISHWA NA TABIA INAYOENDELEA YA KUHUJUMIWA NA WAPINZANI WASIOPENDA MAENDELEO YETU KWA SABABU ZAO BINAFSI.

KWA MUDA MREFU TUMEKUWA KATIKA HARAKATI NA MSTARI WA MBELE KUHAKIKISHA TUNAWAHABARISHA, ELIMISHA NA KUJADILIANA NA WADAU MBALIMBALI WA BLOG HII BILA KUINGIA UHURU WA WENGINE WALA KUKOSOA WENGINE, KWANI MAENDELEO YA KWELI YANATOKANA NA KUJIAMINI.

KWA MANTIKI HII TUNAOWAMBA RADHI WADAU WETU KWA KUTOKUWEPO HEWANI KWA SAA KADHAA LAKINI SASA MO BLOG IMERUDI NA ITAENDELEA KUWALETEA HABARI NA BURUDANI MBALIMBALI NANYI MSISITE KUTUSHAURI NA KUTUONGOZA KWA MAWAZO YA KUJENGA.

IKIWA NI MARA KWA MARA TATIZO HILI LA KUPOTEA NA KUPOTEZA KAZI ZETU KUTOKEA KATIKA BLOG YETU ,TUNAJIULIZA NI WAPI TUNAKOSEA AU KUHARIBU KATIKA UHABARISHAJI WETU WA HABARI NA MATUKIO ,AU KUFANYA HIVI NI MAKOSA..?!!! KWA KIFUPI MOBLOG INATEMBELEWA NA WATU 20,000 KWA SIKU NA HILI LINATUPA NGUVU NA KUFAHAMU KUWA WADAU WETU WANARIDHISHWA NA KUPENDEZWA NA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, BIASHARA, MICHEZO, BURUDANI NA INTERVIEWS ZA WATU MAARUFU WANAOJULIKANA NA WALE PIA WENYE VIPAJI WASIOJULIKANA. WADAU HILI NI KOSA…???

KWA MASIKITIKO MAKUBWA TUNAPENDA KUWATAARIFU KUWA KAZI ZOTE ZA MWAKA HUU 2011 ZILIZOPENDWA NANYI WADAU NA NYINGINE ZIKITOKANA NA MCHANGO WA NINYI WADAU NA WASOMAJI ZIMEPOTEA KWA LUGHA NYINGINE (ZIMEFUTWA/ZIMEPOTEZWA) KWA SABABU AMBAZO ZINATUTIA SHAKA NA KUTUPA HISIA KUWA NI ZA KIPINZANI.

TUSINGEPENDA KUSEMA MENGI NA WALA KUTAJANA MAJINA ILI KWA WEMA KABISA NA HEKIMA TUNAPENDA KUSISITIZA KUWA UPINZANI WA KUHARIBIANA SI MZURI NA HAUJENGI WALA KULETA MAFANIKIO KWANI MWISHO WA UBAYA NI AIBU.

HAIPENDEZI KUONGEA HAYA YOTE HAPA ILA YAKIZIDI NI AFUENI YA MOYO NI KUONGEA NA KUSEMA WAZI TUMECHOKA KUHUJUMIWA.

ASANTE KAKA MAKWAIYA KWA MSAADA WAKO, MKUBWA MICHUZI TUNAKUSHUKURU BILA KUMSAHAU MZEE WA FULL SHANGWE NA WENGINE KWA MISAADA MBALIMBALI NA USHAURI MLIOTUPA KWETU.

WADAU WA MOBLOG TUKO PAMOJA NATUTAENDELEA KULIJENGA TAIFA LETU KWA AMANI, UPENDO NA MATUMAINI.

TUNAWAPENDA, TUNAWATHAMINI, TUNAWAHESHIMU NA TUTAFANYA KAZI PAMOJA NA TUTAFIKA PALE TUNAPOKUSUDIA.
MUNGU IBARIKI MO BLOG NA WADAU WAKE WOTE.
Endelea kuperuzi MO BLOG www.mohammeddewji.com/blog

Wednesday, June 22, 2011

Society for International Development - Tanzania Chapter Election Results
















Society for International Development, Tanzania Chapter Elects New Office Bearers

The Society for International Development (SID) Tanzania Chapter on Saturday 18th June 2011 elected new office bearers for its chapter.

Mahmoud Thabit Kombo (pichani) has been appointed chapter’s President while Richard Kasesela will serve as Vice-President. June Warioba becomes the chapter’s Secretary General, Muhidin Issa Michuzi, Programs Officer and Yasmin Said Chali is Treasurer.

The following were elected members of the Executive Council: Ally Masoud (Kipanya), John Ulanga, Fatma Alloo, Salma Moulid and Chambi Chachage.

SID Tanzania is one of chapters of SID International and acts as an independent platform organisation, bringing together policy makers, academics, NGOs, the private sector, journalists and others to drive forward the development debate in Tanzania, and subsequently influencing the policy discussion.

Ambassador Juma Mwapachu, Vice President of SID’s Global Governing Council, said: "We are thrilled to have such thoughtful and knowledgeable members to lead SID Tanzania during this challenging period."

“We need to provide a forum for individuals and institutions that are seeking long-term solutions to issues such as good governance, food security and agriculture and gender in development to name a few” he added.

On his appointment, the in-coming President thanked members for the honor to serve SID Tanzania. “More than ever, we need the kind of forum that SID provides for enhanced collaboration, informed debate, and a steady focus on learning and innovation. I look forward to working in these areas with other members.”

“My colleagues and I are committed to broadening the dialogue on crucial development issues and promoting effective economic growth for our people” said Kombo.

Mr. Kombo succeeds His Lordship Chief Justice, Mohammed Chande Othman.

Founded in 1957, SID is an international association of individuals and organizations concerned with sustainable economic, social and political development. SID has over 3,000 individual and institutional members in 125 countries and over 65 local chapters worldwide, including in Tanzania.

For more information on SID Tanzania, contact:
June Warioba,
Tel: 0782/0655 004436
Email: sidtanzania@gmail.com
sidtanzania@yahoo.com

Friday, March 18, 2011

Lowassa Naye Apata Dawa ya Babu Loliondo

Bila shaka mmesikia habari za dawa ya Loliondo. Kuna mchungaji mstaafu ambaye amegundua dawa ya mitishamba inayotibu magonjwa karibu yote. Watu wanahaha kwenda Loliondo, wengine wamekodi hata helikopta! Na serikali ya Tanzania imebariki dawa ya babu! Sasa wagonjwa wanatoroka Muhimbili kwenda kufuata dawa Loliondo!

*****************************************************************************


Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile aka. BABU akipima dozi

Msongamano wa wangonjwa na wananchi wakienda kupata dosi. Dozi ilikuwa shs 500/- tu. Sijui kwa sasa ni bei gani.

Picha na Habari kutoka Michuzi blog:

Lowassa apata kikombe Loliondo, huduma zaimarishwa, bei ya mabasi Ubungo zapanda
Source: Gazeti la Mwananchi

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa juzi alipata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo, mkoani Arusha.

Lowassa alifika katika eneo hilo mchana akiwa na viongozi kadhaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Serikali kisha kupata kikombe kimoja chenye dawa kinachotolewa na mchungaji huyo kwa ajili ya tiba.

Tofauti na viongozi wengine, Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), Jimbo linalopakana na Kijiji cha Samunge, alikwenda huko akiwa na viongozi mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini na baadhi ya wapigakura wake.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Lowassa alithibitisha kwenda Loliondo na kuwataja viongozi wa dini alioambatana nao katika msafara wake kuwa ni Askofu Msaidizi wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Dk Frederick Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha), Mchungaji John Nangole.
Katika ramani ya utendaji kazi ya KKKT, Jimbo la Masai Kaskazini ndipo kilipo Kijiji cha Samunge ambako ni makazi ya Mchungaji Mwasapile.

“Ni kweli, nimekwenda pale na wapigakura wangu pamoja na viongozi wa dini, Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dk Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Mchungaji Nangole,” alisema Lowassa na kuuliza: “Kwani hiyo nayo ni habari jamani?”

Baada ya Lowassa kufika katika kijiji hicho akiwa na ujumbe wake, aliongoza moja kwa moja hadi kwa Mchungaji Mwasapile na kuzungumza naye kisha akapata kikombe cha tiba na kuondoka.

Kabla ya Lowassa kwenda kupata tiba, amekuwa akitoa msaada wa nauli kwa wagonjwa mbalimbali wa jimbo lake kwenda kwa mchungaji huyo ambaye dawa yake inadaiwa kutibu magonjwa ya saratani, kisukari, pumu, shinikizo la damu na Ukimwi.

Kwa habari zaidi BOFYA HAPA:

Tuesday, August 17, 2010

Michuzi Post


Habari Muhimu Kutoka kwa Kaka Michuzi

*********************************8
Asalaam Aleikhum Wadau,

Kwa furaha, heshima na taadhima naomba kutangaza rasmi libeneke jipya
la www.michuzipost.com ambalo wikiendi ilopita lilipaa hewani katika
kile kiitwacho uzinduzi laini (soft launch). Kunradhi kwa
kutowataarifu mapema, kwani ilibidi mambo kadhaa yawekwe sawa kwanza
kabla ya kuthubutu kutia neno kama nifanyavyo sasa.

Wadau wa Globu ya Jamii naomba baraka zenu pamoja na maoni juu ya
libeneke hili ambalo azma ya kulianzisha ni ile ile ya Kuendeleza
Libeneke kwa njia ya kisasa zaidi na kwa upana mkubwa. Hivyo
nakaribisha maoni, ushauri pamoja na neno lolote lile litalonkisaidia
kuboresha libeneke hili.

Kama nilivyotamka awali, bado niko katika uzinduzi laini, kwani kama
ujuavyo libeneke kama hili halitaki papara. Linahitaji subira, sikion
sikivu la neno toka kwa wadau ambao sapoti yao naithamini kama lulu
kwa muda wote huu.

Globu ya Jamii itaendelea kuwepo hewani kama kawaida, na itaenda
sambamba na Libeneke hili la www.michuzipost.com pamoja na lile la
www.michuzi-matukio.blogspot.com. Hivyo wadau Globu ya Jamii
itaendelea kudunda kama kawaida, ikiwa ni chapuo la Libeneke jipya
ambalo kama utavyoliona, litakuwa na habari na taarifa motomoto kwa
mapana na undani zaidi.

Inshaallah panapo majaaliwa Libeneke hili jipya litazinduliwa rasmi
mnamo September 8, mwaka huu - ikiwa ni siku ya kuadhimisha miaka
mitano kamili ya kuzaliwa kwa Globu ya Jamii kama link hii
inavyojionesha http://issamichuzi.blogspot.com/2005/09/michuzi-and-ndesanjo.html#comments.

Namshukuru Muumba wa Yote kwa kunipa nguvu na uwezo kufikia hapa
nilikofikia. Pia natoa shukrani kwa kila mdau ambaye amekuwa akinipa
sapoti ya nguvu kila siku kwa kutembelea Globu ya Jamii. Ni mategemeo
yangu kwamba baada ya kwikwi ya kuwa na Libeneke jipya wakati fulani
huko nyuma, sasa mambo yanaonekana kuwa mswano na Libeneke litaendelea
kama kawa.

Libeneke hili jipya la www.michuzi.post.com limewezekana kwa ushauri
na msaada pamoja na ushirikiano mkubwa wa Bw. Zubeir Masabo na Bw.
Alistair Horsburgh, washirika wangu walio Uingereza ambao kwa pamoja
tutaendesha Michuzi Post Ltd. kampuni rasmi itayosimamia uzalishaji wa
bidhaa za www.michuzipost.com. Sambamba nasi pia kuna kikosi kazi
kikubwa ambacho kitakuwa kinashughulika katika kuendeleza Libeneke
hili.


Muhidin Issa Michuzi
Mkurugenzi
Michuzi Post Ltd

Tuesday, June 08, 2010

MDurban the King Atuma Salamu kwa Mjomba Kamau

Imeandikwa na Mdau MDurban the King Kutoka Algeria.

MDurban anatoa dukuduku lake kuhusiana na mada kwa Kaka Michuzi....

SALAMU KWA MJOMBA KAMAU :

MJOMBA MICHUZI NAFURAHI SANA UMELETA HOJA NZURI SANA!!ME HII HABARI NIMEISOMA JUZI KWENYE IPP MEDIA!!NA ILINIGUSA NIKACHANGIA MAONI.

KWANZA NASIKITISHWA SANA NA KAULI ZA HAWA WAKENYA !!BINAFSI HASA ZA BROTHER KAMAU MAANA KAMA NI KWELI KAMAU NINAYEMJUA MWANDISHI WA HABARI WAKIKENYA NDIYE ALIYEFANYA HICHI NI AIBU KWAKE NA JAMII YAKE !!MAANA KAMAU NA WENZAKE WAANDISHI WA HABARI WA VITUO MBALIMBALI VYA KIKENYA WAPATAO ZAIDI YA 15 MWISHONI MWA MWAKA JANA (2009) WAKIWEMO WA KITUO CHA KBC KENYA KWENYE SHEREHE ZA PAN AFRICANISM ALGERIA, NIMIMI NDIYE NILIYEWAPOKEA NA NILIKUWA NDIYO TOUR GUIDE WAO NA INTERPRETER WAO KUTOKANA HAWAKUWA WANAFAHAMU LUGHA YA KIFARANSA !!NA SIO KWAMBA WALIKUWA WANANILIPA ILA ILIKUWA NI VOLUNTEER TU NA KWA USHAHIDI HUO WALIKUWEPO WAANDISHI WENGINE WA KITANZANIA KUTOKA KAMPUNI YA MAGAZETI YA SERIKALI NA KAMPUNI YA NEW HABARI COPARATION !!NAO WALIFIKIA HAPA EL-AURASSI HOTEL ALGIERS.

HAWA WAKENYA WALIFURAHISHWA SANA NA UKARIMU NILIOWAFANYIA NIKIWAWAKILISHA WATANZANIA WENZANGU POPOTE WALIPO DUNIANI NDANI NA NJE YA NCHI !!SIO KAMA WAKENYA WENZAO HAWAKUWEPO ILA NI WATU WAMASLAHI !!! SASA HII INAONESHA NI JINSI GANI TULIVYOKUWA CIVILISED ZAIDI YAO.

SASA KAMA KAWAIDA YETU SISI NDIYO WAZALENDO WENYEWE TUTAILINDA NCHI YETU KWA NAMNA YEYOTE ILE KUTOKA KWA ADUI!!TAIFA LOLOTE LILE LILILOKOSA WANANCHI WAZALENDO SIKU ZOTE WATAKUWA WATUMWA!!LITAKUWA TAIFA LA MACHAKUBIMBI NA WANAFIKI ILI WAWEZE KUWAPREZIR WENYE NGUVU YANI HAO MABWANA ZAO!!SASA SISI TUKIWA KAMA WAZALENDO TUNAIPENDA NCHI YETU, NI KWELI NCHI YETU NI MOJA YA NCHI MASKINI DUNIANI NA TUNAMATATIZO MENGI SANA TU LKN SIO MKENYA WAKUTOSEMA SISI!!KILA LINALOTUSIBU KENYA LINAWASIBU MARA MIA ZAIDI YA SISI!NAONGEA HIVI KUTOKANA HUU NDIYO UKWELI KWA MTU ANAYEIFAHAMU KENYA VIZURI ATANIUNGA MKONO, WALIO WENGI KENYA WANATAABIKA KAMA WAPO JAHANAMU!!RAIA WAKENYA WALIOWENGI HAWANA HATA MAJI YA KUNYWA USHAHIDI UKAME ULIOPITA ULIUA MAELFU YA MIFUGO KENYA ILE ILIKUWA AIBU NA KIELELEZO TOSHA CHA KUWA KENYA SIO WAKUTUSEMA SISI WATZ.

PIA UNAKUMBUKA VURUGU ZA MUNGIKI? ZILE NI ISHARA TOSHA WATU WAMESHATAABIKA VYA KUTOSHA NA IMEFIKIA KIPINDI HAWAOGOPI KIFO!!MAANA MJOMBA MALCOM X ALISHASEMA U CANT SEPARATE PEACE FROM THE FREEDOM BEACAUSE NO ONE CAN BE IN PEACE UNLESS HE HAS HIS FREEDOM!!KWA KULITIZAMA HILI KWANZA NDIYO MAANA HAWA WAKENYA HAWANA AMANI KWAO COZ HAWANA UHURU WA KUIKOSOA SERIKALI YAO SASA HII LEO WAJE WAIKOSOE SERIKALI YETU? SASA WATUPE UHURU WETU NASI ILITUWE NA AMANI NAO!!MAANA KITENDO CHA KUTUNYIMA UHURU WA KUFANYA MAMBO YETU NI KUTUNYIMA UHURU WETU KWAHIYO HATUTOKUWA KWENYE AMANI NAO!!TUSIWE WANAFIKI KWA KUJIFANYA ETI TUNAWAWAPENDA WAKENYA WAKATI WAO HAWATUPENDI !! HATA MBWA AU PAKA UKIMCHUKIA NAYE ATAKUCHUKIA SEMBUSE SISI AS HUMAN BEING HILO NI GUMU NA ZITO !!HALAFU MJOMBA MALCOM X AKAMALIZIA KUWA HAKUNA AMANI KWENYE NCHI YENYE NJAA NA ISIYO NA HAKI !!HIKI NI KIELELEZO TOSHA KUWA KENYA NI NCHI YA NJAA NA ISIYO NA HAKI NA NDIYO MAANA HAKUNA AMANI KWAO KILA KUKICHA TUNASHUHUDIA VURUGU MAUAJI YA HALAIKI NA WANASIASA ILA SISI TUMENYAMA KIMYA HATUWAONGEI VIBAYA !!MIMI NAMARAFIKI WENGI TU WAKIKENYA NA TUNAHESHIMIANA NA HAWANA KEJELI. SISEMI WAKENYA WOTE WANATABIA MBOVU.

NAUNGA MKONO RISALA YA MH : RAISI WETU JAKAYA ALIYOITOA KWAO KUWA TUHESHIMIANE WALA TUSITOLEANE KEJELI HUO NDIYO UJIRANI MWEMA ILI TUSIJENGE TENSION MIONGONI MWETU !!HII ILIKUWA ELIMU TOSHA KWAO !!LKN WENZETU HAWAELEWI NA HII KUTOKANA KWAMBA NA VIONGOZI WAO NDIYO HULKA ZAO WANAFURAHIA HILI !!NAKUMBUKA MWAKA 2006 MWISHONI MWA MWEZI WA 10 NILIKUWA VACATION KENYA KILA REDIO UTAYOFUNGUA WALIKUWA WAKITUKEJELI HAWA WATU KTK MAMBO MENGI TU !!SASA HILI HALIKUANZA LEO !!

UNAJUA SIKU ZOTE ADUI HAKUSIFII KWENYE ZURI UTAKALOFANYA ZAIDI YA KUKUPONDA ILIUWEDISCOURAGE USIENDELEE NA MAZURI YAKO !!JUU NIMEFURAHI KUONA KUWA LEO MJOMBA WANGU MASHAKA KAONESHA UZALENDO KWA KUWAAMBIA UKWELI KUWA ANATEGEMEA KTK MAMIA YA WAKENYA WATAKAO KUJA KUWAONA BRAZIL ANATEGEMEA KUWA BROTHER KAMAU NAO ATAKUWA MIOGONI MWAO !!WAJE WATULETEE FOREIGNE CURRENCY NA WATUPATIE AJIRA NA NDILO LINALOWAUMIZA VICHWA HILO.

KUWAALIKA BRAZIL KUJA TZ KWA SISI WATAALAMU WA UTALII TUNALIITA NI STRATEGIQUE MARKETING TOURISTIQUE WAKENYA WANALIJUA HILI NA NDIYO MAANA WANAANZA KUTAPATAPA MAANA WANAJUA FAIDA ZAKE NI NYINGI MNO MAANA WAO WALISHAANZA KUIPA KIPAUMBELE SECTEUR YA UTALII SIKU NYINGI MFANO WA BAADHI YA FAIDA NI KAMA IFUATAVYO :
KWANZA KABISA TANZANIA ITAPATA FAIDA YA KUJITANGAZA NJE YA NCHI HII KUTOKANA SOKA NI MOJA YA MCHEZO UNAOPENDWA SANA DUNIANI NA WASHABIKI WENGI WASOKA WANA CULTURE YA UTALII NA KUFANYA RESEARCH !!KWA HIYO WAPENZI WOTE WA SOKA WATAJUA KWAMBA BRAZIL IPO TZ !!NA HAPO NDIPO WATAKAPOANZA KUJUA RESOURCE N CIRCUITS TOURISTIQUE ZOTE ZILIZOPO TZ !!

PILI TELEVISION ZOTE MASHUHURI ZA HABARI NA VYOMBO VYA HABARI VYENGINE VITAITANGAZA HII MECHI NA PIA KUNA VITUO VITALIPIA HII MECHI ILIWAWEZE KUIONESHA KWAHIYO HII ITAKUWA NI MOJA YA MBINU ZA BURE KUJITANGAZA KWA NCHI YETU !!

PILI NCHI ITAPATA FOREIGN CURRENCY WAKIWEMO HAO WAKENYA WATATULETEA PESA ZA KIGENI !!TUTAINGIA MAPATO YA KIINGILIO NA HOTELI ZETU ZITAPATA MAPATO !!

PIA WANANCHI WETU KTK SECTEUR TOFAUTI WATAPATA AJIRA MFANO WATU WA USAFIRI WATAFANYA KAZI KWA UHAKIKA, WAFANYABIASHARA, MAHOTELINI NA WAKULIMA WATAUZA MAZAO YAO N.K
HIZO NI BAADHI YA FAIDA TUTAKAZO ZIPATA !!NA NDIYO LINALOWACHANGANYA VICHWA BINAMU ZETU WAKENYA !!

TZ HAINA TOFAUTI KUBWA NA UCHUMI WAKIKENYA KWENYE MAKARATASI !!MKITAKA STATISTIQUE ZA INSTITUTE ZA UMOJA WA MATAIFA UNKALE NITAKUTUMIA !!

WATANZANIA TUSHUKURU KWAMBA TUMEPATA RAISI MZALENDO ALLIYEFUNGA KILA AINA YA JANJA NA DANGANYA TOTO ZA KIKENYA NA LINAWAUMIZA HILI.

PIA KUNA SUALA NINGEPENDA KUISHAURI SERIKALI YETU KUANGALIA SUALA LA AJIRA NA KULINDA AJIRA KWA WATANZANIA SIDHANI KAMA KENYA INGAWA WATAINGIA KWENYE COMMUNITY LKN WATAMUACHA MTZ ACHUKIE AJIRA KIRAHISI HIVYO NA PIA SUALA LA ARDHI TUSIKUBALI KUWAUZIA WAGENI MAANA ARDHI HAIUZWI, UKIMWONA MTU ANAUZA ARDHI UJUE ANAJIANDAA KUWA MTUMWA NYUMBANI KWAKE.

PIA SERIKALI YETU ITIZAME VIZURI HIVI VYOMBO VYA HABARI VYOTE VINAVYOMILIKIWA NA WAKENYA NCHINI KWANI NDIYO VIMEKUWA VIKIONGOZA KUTUPONDA NA KUKEJELI VIONGOZI WETU !!PIA VIMEKUWA VIKIJA NA STYLE YA KUTULETEA SIASA ZA MAKUNDI NA SUPPORT KWA BAADDHI YA WANASIASA NA PIA KAMA MNAFUATILIA VIZURI VIMEKUWA MSTALI WA MBELE KULETA ITIKADI ZA UCHONGANISHI WA KIKABILA NA UDINI.

TUKUMBUKE KTK KILA NCHI DUNIANI KUNA AINA KUU 3 ZA POUVOIRS PUBLICS (NGUVU YA DOLA) IKIWEWO POUVOIRS EXECUTIVE, LEGISLATIVE NA POVOIRS JURIDIQUE LKN TUNASAHAU KUWA KUNA AINA NYENGINE YA NGUVU YA DOLA NA NDIYO NI HATARI ZAIDI KTK USHWAWISHI KTK JAMII AMBAYO NI MEDIA !!VYOMBO VYA HABARI VIKITUMIWA VIBAYA VINAATHARI KUBWA KTK JAMII KAMA VIKITUMIWA VIBAYA !!ANGALIA MFANO WA RWANDA NA BURUNDI VYOMBO VYA HABARI VILILETA MTAFARUKU MKUBWA NA KUJIKUTA WATU WAKIINGIZA NCHI KTK UMWAGAJI DAMU !!TIZAMA HISTORIA YA ISRAEL NA PALESTINA, UJERUMANI WKT WA HITLER NA WAKATI WA VITA BARIDI YA DUNIA.

SASA TUSIJE TUKAJIKUTA TUMESHACHELEWA KUVIZIBITI NA BADALA YAKE TUKAANZA KUVIDHIBITI BAADA YA MADHARA KAMA ILIVYOKUWA KWA ZE UTAMU !!

UNKAL NAOMBA USINIBINYIE HUU UTAKUWA NI KIJIMCHANGO CHANGU KIDOGO KWA WATANZANIA WENZANGU NA NDIYO MAANA NIMEJARIBU KUIANDIKA KWA KISWAHILI ILI WATANZANIA WENZANGU WANIELEWE.

MWISHO NALITAKIA KILA LA KHERI TAIFA LETU LA WAMATUMBI NA TUKITUKUZE KIMATUMBI CHETU KIDUMU DAIMA !!MAANA KILIMKOSTI NYERERE KTK KUKIKUZA NA KIKAWAUNGANISHA WAMATUMBI NA BADALA YAKE TUNAWAACHIA WAKENYA KILA MAHALI UTAKAPOPITA AMA UTAKAPOSOMA UTAONA KIMATUMBI NI CHA WAKENYA !!WANAPATA MALAKI YA WATALII KWA AJILI YA CIVILISATION ZA KIMATUMBI TUAMKE WTZ NA NDIYO MAANA HAWA JAMAA WANATUTUKANA KWA KUMONOPOLI KILA KITU CHETU KIZURI KUANZIA MLIMA KILIMANJARO, TANZANITE YETU, KARAFUU, SERENGETI, ZANZIBAR VYOTE NI VYAO.

NATUMAI WATANZANIA TUTAKUWA WASTAARABU KTK KUCHANGIA MADA NA HII TUWAONYESHE KUWA CIVILISATION ILIZALIWA NA KUKULIA KWETU NA NDIYOMAANA HATA KWAO WANAOPAKANA NASISI KAMA MOMBASA WAMESTAARABU.

BY MDURBAN

******************************************************

Mnaweza kusoma Mada kwa MICHUZI HAPA:

Monday, May 17, 2010

Kaka Michuzi Anahamisha Blogu Yake!


Kutoka Kwa Kaka Michuzi:

Asalaam Aleikhum, Bwana Asifiwe, Tumsifu Bwana, Shalom, Namaste, konnichiwa, Nihao, olá.....
kwa heshima na taadhima nawaamkia wadau wote popote mlipo ulimwenguni. Salamu nilizotoa hapo juu naomba ifahamike kuwa hizo nilizozimudu ni kama kielelezo kwamba nia ni kumuamkua kila mmoja kwa nafasi yake popote alipo. Mie sijambo na naendelea na Libeneke kama kawaida.

Waama, baada ya salamu, napenda kuwafahamisha kwamba Globu ya Jamii hivi karibuni itaingia kwenye awamu mpya ya dot com, ikiwa katika jitihada za kuboresha Libeneke zaidi.

Imechukua muda kuchukua hatua hii kutokana na mazoea kwani toka September 8, 2005 hadi leo si kidogo ati. Hivyo mabadiliko kama yapo inabidi yafanywe kwa uangalifu wa hali ya juu ili kutoleta usumbufu wa aina yoyote kwa wadau wa Globu ya Jamii ambao kwangu ndiyo waajiri wangu wakuu.

Naam, wakati wowote kuanzia sasa libeneke la issamichuzi.blogspot.com litaingia katika awamu ya www.imichuzi.com. unakaribishwa kujaribu na kutoa maoni yako.
Mabadiliko haya tayari yameshaanza na sasa yako katika hatua za nchani. Kilichosalia ni kuhamisha 'mzigo' wote toka issamichuzi.blogspot.com na kuutua katika www.imichuzi.com ili libeneke liendelee vile vile kama siku zote, ukaicha mabadiliko kiasi ya muonekano.
Ni kweli jina litabaki lile lile la 'MichuziBlog' lakini si uwongo kwamba hivi sasa itakuwa tovuti kamili ila katika sura ya globu kama siku zote. Hii yote ni katika juhudi za kuongeza ufanisi, tija na vionjo vingi zaidi pamoja na kuondoa kero ya kusaka mitundiko iliyopita. Nadhani sasa itaeleweka kwa nini kulikuwa na kwikwi katika kutafuta posti za zamani.

Mdau usihofu kwamba labda utapata shida kusaka www.imichuzi.com. La, hasha. hautopata shida kwani hata kama utaingia Globu ya Jamii kwa kutumia issamichuzi.blogspot.com ama hata kwa kutumia 'michuzi' pekee utapelekwa moja kwa moja kwenye kurasa mpya bila matatizo. Isitoshe, posti zitabakia kwenye ukurasa wa mwezi husika na kuingia kwenye 'archive' baada ya mwezi huo kwisha.
Hivyo basi, kwa unyenyekevu naomba niwashukuru wadau wote popote mlipo kwa kampani yenu wakati wote huu ambayo kwa kweli bila nyie Libeneke lisingefikia hapa lilipo, hususan katika wakati huu wa kulifanya bora zaidi.

Maoni, ushauri na mawazo vinakaribiushwa kwa mikono miwili, pasina kusahau kukosoana kwa kujenga na mawazo mbadala ili kieleweke na Libeneke liendelee mbele.

Kwa kuwa nawapenda wadau wote, nitakuwa mtovu wa fadhila endapo kama sintowaonjesha Libeneke litalokuja kwa muonekano mpya. Hapo hapo naomba radhi kwa usumbufu wowote utaotokea kwani kama inavyofahamika si rahisi kwa binadamu kuwa sahihi kwa kila jambo. Hivyo n penye kwikwi na tusameheane na tushtuane haraka iwezekanavyo kupitia anuani ile ile ya issamichuzi@gmail.com ambayo nayo itabadikika mambo yakikaa sawa muda si mrefu ujao itakuwa info@imichuzi.com

Tuesday, March 23, 2010

Michuzi Safarini Uingereza


Mwasisi wa habari za jamii mtandaoni (social media) nchini Bw. Muhidin Issa Michuzi (pichani) anaondoka leo Jumatano kuelekea London, Uingereza, kuhudhuria kongamano la pili la Watanzania wanaoishi nchi za nje (Diaspora 2 conference) kwa mwaliko maalumu akiwa kama blogger.

Bw. Michuzi, ambaye ametoa mchango mkubwa katika kupromoti habari za jamii mtandaoni kupitia blog yake maarufu ndani na nje ya nchi iitwayo issamichuzi.blogspot.com, amealikwa huko mkutanoni na ubalozi wetu Uingereza ili kutoa mada inayohusu umuhimu wa habari za jamii mtandaoni katika kujenga daraja kwa walio ndani na nje ya nchi.

Akiongea nasi leo kabla ya kukwaa pipa la shirika la ndege la Emirates, Bw. Michuzi ambaye pia ni maarufu kwa majina kama Mzee wa Libeneke, Mdau na Ankal, amesema amefarijika sana kuona kumbe kuna wanaotambua mchango mkubwa unaoletwa na vyombo vya habari za jamii mtandano, hasa blogs.

Amesema anajisikia mwenye furaha sana kuona azma yake ya kuifanya tasnia hii ya kupashana habari kwa njia ya intaneti kwa waandishi wa hapa nyumbani unatambulika na kukubalika na kupewa heshima stahili kama ilivyo kwa vyombo vya kawaida kama vile magazeti, redio na luninga.

Bw. Michuzi, anayeweka rekodi ya kuwa bloga wa kwanza nchini kualikwa kama bloga kwenye mkutano muhimu kama huo, anaushukuru ubalozi wetu Uingereza chini ya Balozi Mh. Mwanaidi Maajar ambaye naye anakuwa miongoni mwa wazalendo wa kwanza kuutambua hadharani mchango wa wanahabari za jamii mtandaoni kwa kutoa mwaliko huo.

"Nilijua iko siku wanahabari za jamii mtandaoni tutatambulika na mwaliko huu hakika umekuja wakati muafaka kwani msisimkmo na mwitikio wa jamii kuikubali njia hii ya mawasiliano hapa nyumbani umekuwa mkubwa kuliko ilivyotarajiwa.

"siku hizi habari za jamii mtandaoni zinachukua kiti cha mbele katika kusomwa na wenye kuwa na intaneti kutokana sio tu na habari kuwa za uhakika, zisizochujwa na za haraka bali pia kwa kule wasomaji kupata fursa ya kuchangia habari waionayo tofauti na ilivyo kwa magazeti, redio na luninga.

"dunia imezidi kuwa kijiji kimoja kidogo kwa teknohama hii ambayo hata Rais Jakaya kikwete yuko mstari wa mbele kutaka iendelezwe mijini na vijijini ili kuwezesha wananchi wawe na habari za uhakika, za haraka na zenye kutoa fursa ya wasomaji kuchangia maoni" alisema Bw. Michuzi.

Blog ya issamichuzi.blogspot.com ilianza rasmi Septembe 8, mwaka 2005 katika jiji la Helsinki, Finland, ambako alikwenda kuhudhuria mkutano wa Helsinki Conference akiwa kama mwandishi na mpiga picha wa gazeti la Daily News.

Alikuwa ni bloga wa siku nyingi aliyekuwa anaishi Marekani wakati huo, Bw. Ndesanjo Macha, aliyemshawishi Bw. Michuzi kufungua blog yake na kuwa bloga wa kwanza wa Tanzania kuupasha ulimwengu ya kila linalojiri nchini, kazi ambayo ameifanya kwa ustadi mkubwa kiasi ni hivi majuzi tu ameweza kufikisha wasomaji milioni 8, kati ya hao asilimia 30 wakiwa ni wasomaji wa hapa hapa Tanzania.

Bw. Michuzi ameweka wazi kwamba amefurahi na kusisismkwa sio kwa sababu anakwenda ulaya, kwani ameshatembelea karibu miji mikubwa yote duniani, ukiondoa Australia na New Zealand, ila amefarijika kwa sababu hatimaye blog zimeanza kutambuliwa rasmi.

Anatoa masikitiko yake kwamba pamoja na fanaka hiyo, lakini bado hapa nyumbani jamii, hasa ya mahafidhina (conservatives) wasiotaka mabadiliko wamekuwa wazito kukubali kwamba vyombo vya habari za jamii mtandaoni vimeshapata nguvu sawa na vyombo vya kawaida kutokana na wingi wa wasomaji na hata kupelekea kujitokeza kwa wadhamini wanaotangaza biashara zao humo.

Pamoja na mambo mengine, Bw. Michuzi amesema anatamani sana kuanzisha umoja wa wanahabari za jamii mtandaoni ili kutetea na kulinda maslahi yao pamoja na kuindeleza tasnia hii ambayo inakua kwa kasi za ajabu.

Kwa mahesbu ya haraka haraka hivi sasa kuna blog zinazotumia lugha ya kiswahili zipatazo 200 ambapo pia blog takriban 10 zinaanzishwa kila siku, na kuifanya Tanzania kuw nchi zinazoendelea katika tasnia ya habari kwa njia ya mtandao.

Monday, October 12, 2009

Kaka Michuzi Kwenye Harusi Juzi

Wadau, hebu cheki kaka Michuzi anavyonengua kwenye arusi ya Jackson Mbando wikiendi hii iliyopita. Kujua nani kashinda BOFYA HAPA:

Monday, May 18, 2009

Kaka Michuzi Yu Salama USA!

Wadau, kwa kweli tumshukuru Mungu kwa mkono wake uliosaidia ndege ya KLM aliyokuwa anasafiria Kaka Michuzi na wengine kutua salama Amsterdam Schipol. Ndege ilikuwa ikitoka Schipol kwenda San Francisco direct, kwa hiyo lazima ilimwaga mafuta mengi kweli.


Kaka Michuzi alipiga hii picha akiwa ameshika roho mkononi. Ndege ina mwaga mafuta kusudi iweze kutua salama kwenye Emergency landing. Habari alizonitumia ni kuwa yuko salama na kwa sasa yuko San Francisco, California.

Mnaweza kupata picha na maelezo zaidi hapa:

http://issamichuzi.blogspot.com/2009/05/vekesheni.html#comments

Wednesday, December 03, 2008

Sasa Aninitwa ' Hasheem the Dream'

Wadau, kijana wetu Hasheem anapanda kwenye charts za Basketball hapa Marekani. Naona karibu tutamsikia kwenye NBA!

*************************************

Kutoka Sports Illustrated.com


Hasheem The Dream

The odyssey of Hasheem Thabeet began in one of the most remote hoops hinterlands. Soon, perhaps, it will take the UConn 7-footer to an unimaginably big stage -- bigger even than the first round of the NBA draft.

Living up to a name that means "destroyer of evil" in Arabic, Thabeet is a record-breaking shot blocker.

Thabit Manka is up on the back step of his house in Dar es Salaam, Tanzania, for good reason: If he posed on level ground with his eldest son, their height difference would be accentuated to the point of absurdity. Even like this, in the last photo they would ever take together, the top of Thabit's kufi only meets the giant boy's shoulders. It's April 2004, and the son, 17-year-old Hashim Thabit Manka, as his name was written then, is seven feet of limbs drowning in baggy jeans and a retro Philadelphia 76ers shirt, staring straight into the camera with only the faintest hint of a smile. The father's billowy kanzu and the gray edges of his facial hair give him a regal air at the age of 56; he is grinning, with his gaze fixed slightly off to the left.

Thabit was an architect, educated in England at the University of Bath and Oxford. He was a lover of soccer, world geography and English Scrabble, all of which he taught to Hashim. Thabit was also a diabetic, and when he fell ill in the days after the photo was taken, complications led him to be hospitalized and, in a week's time, took his life.

Hashim kept the picture in a scrapbook under his bed during his freshman year at Connecticut but has since returned it to his mother, Rukia, for safekeeping in Tanzania. He remembers his father now for his wisdom. Thabit had showed him maps of his travels through Africa, Europe and Australia, and said that their family identity -- being Tanzanian, Swahili-speaking, Muslim -- should never be a limitation. "You can live anywhere as long as you can get along with anybody," he told the boy. "You just have to adapt and overcome."

Four years ago Thabit couldn't have foreseen the odyssey in store for Hashim, who was in just his third year of organized basketball in soccer-mad Tanzania, which had never sent a soul to the NBA, much less the NCAA. Who could concoct a narrative that begins with a boy doing runway modeling in Dar es Salaam to earn money for his fatherless family, continues with him trying to get a basketball scholarship by e-mailing U.S. colleges he randomly Googled in an Internet café and ends with him in Storrs, Conn., as the starting center on a Top 5 team?

E-mail was not the solution; it wasn't until Hashim left Makongo High in Dar es Salaam to take a scholarship at Laiser Hill Academy in Nairobi, Kenya, that he was noticed by someone with international basketball connections. French businessman Oliver Noah, who organized the NOGA African All-Stars AAU team, saw Hashim play and offered to take him to the U.S., and, with Rukia's blessing, handled the paperwork for an I-20 visa.

Seven-foot-three Hasheem Thabeet -- the new, Americanized name on his passport -- arrived wide-eyed in Los Angeles in January 2005 and was placed at Stoneridge Prep, where neither the housing conditions (four players were packed into coach Ron Slater's home) nor the transcript situation (they designated him as an 11th-grader, rather than a 12th-) was ideal. By April he was on the move again, to Picayune, Miss., to live with a host family and attend a public high school. Transcript issues arose once again, prompting a move in June to Houston, where Mark McClanahan, a coach Thabeet had met at the Kingwood (AAU) Classic in Houston that spring, found him another host family and a spot as a senior on the Cypress Christian School team for the '05-06 season. By the following summer Thabeet was at UConn, where he is now a junior majoring in geography. The bedroom walls of his campus apartment are decorated with SpongeBob SquarePants dolls, and his dresser doubles as a trophy stand for being last season's Big East Defensive Player of the Year and NABC Defensive Player of the Year.

In Arabic, Hashim means "destroyer of evil," and the shot blocking that earned those awards (147 swats as a sophomore, breaking Alonzo Mourning's Big East single-season blocks record) is an instinctual talent. The crash course in post offense that Thabeet received at UConn has helped him grow from a comedic liability to someone who, says Huskies graduate assistant Justin Evanovich, "is conscious of his ability to dunk everything." Huskies coach Jim Calhoun laughs at his first memory of Thabeet ("He would get a rebound in Houston, throw it and then watch nine guys run") and beams with pride when he says that "no player I've ever had at UConn has improved to the level that Hasheem has improved."

Since his father's passing, all Thabeet has done is change cities five times, countries twice and his name once. He basically learned how to play offense from scratch while establishing himself as the nation's premier defensive game-changer. Thabeet has adapted, and he has overcome.

If Uconn, which finished 24-9 last season, were to win a national championship in April, it would be the first basketball team to visit the White House under Barack Obama, whose absentee father was an economist in the Kenyan Ministry of Finance -- only nine miles from the Nairobi school where Thabeet was discovered. The gravity of this African connection is not lost on Thabeet, but it wouldn't be his first presidential encounter, either.

On Sept. 21 he arrived at the Intercontinental Hotel in New York City wearing a Euro-cut suit, and he joined Tanzania's president, Jakaya Kikwete -- who was in town for the opening of the U.N. General Assembly -- in breaking Ramadan fast. This was their third meeting, and it came with a reminder from Kikwete "to keep representing the country well." At their first meeting, in Boston when Thabeet was a freshman, he showed up in a fitted New York Yankees hat, brown sweater and jeans. ("I wasn't grown up yet," he says sheepishly.) When a photo of him appeared on Michuzi, the highest-trafficked Tanzanian blog, he was lambasted by some Swahili-speaking commenters for being disrespectful and undeserving of such attention.

Kusoma story nzima BOFYA HAPA: