Showing posts with label Umoja Church. Show all posts
Showing posts with label Umoja Church. Show all posts

Wednesday, April 20, 2011

MKutano wa Pasaka Dallas Texas

Unakaribishwa kwenye Easter Revival Conference kwa watu wote itakayofanyika Dallas Texas kuanzia siku ya Ijumaa April 22 hadi Jumapili April 24 katika ukumbi wa Kanisa La Umoja.

Semina hii itafuatiwa na Marriage Revival—maalum kwa wana-ndoa ambayo itaongozwa na Ev. Douglas Mmary kutoka Minneapolis, MN siku ya Jumamosi katika ukumbi wa Staybridge Hotel - Dallas TX

Umoja Praise and Worship Band itakuwepo. Hakuna kiingilio, huduma kwa watoto (Day Care) itatolewa bure. Karibu upokee muujiza wako. Wote mnakaribishwa!!!
Kwa maelezo zaidi wasiliana.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na uongozi wa kanisa:

214 554 7381 / 682 552 6402 / 469 279 1762 / 972 506 7780


Wednesday, April 06, 2011

Krystaal Watakuwa Texas Jumapili 4/10/11



The Award-Winning and International Acclaimed Trio will be performing LIVE at the Umoja Church Auditorium Sunday
April 10th 2011 Evening from 5:30PM through 8:00PM
This is a FREE concert, All are Welcome!


6411 LBJ FREEWAY DALLAS TEXAS,75240

Mawasiliano ni;Pastor Absalom Nasuwa; 214 554 7381, Nicholus Chove 682 552 6402, Matthew Mille 469 279 1762,

Saturday, July 17, 2010

PASTOR ABIUD & CATHERINE Watakuwa Texas


Kwa heshima na unyenyekevu, ninapenda kuwatangazia watanzania na watu wote wanaoishi katika katika jiji hili la Dallas -Texas kwamba kutakuwa na SEMINA ya siku mbili ya neno la Mungu katika jiji letu la Dallas-Texas. Semina hii itaendeshwa na watumishi wa Mungu PASTOR ABIUD & CATHERINE PAMOJA NA EV.LENATA KUTOKA TANZANIA. Watumishi wa Mungu Mr&Mrs Abiud wanaheshimika ndani na nje ya mipaka ya Tanzania kutokana na wito wao wa kumtumikia Mungu kwa upendo na unyenyekevu mkubwa.

Kwa sasa hawa watumishi wameweka maskani yao katika jiji la Kansas -Missour (USA).Ninaomba kwa kila mtu atakaesoma tangazo hili amkaribishe mwenzake.Pamoja na semina ya Mungu, watumishi hawa watapata nafasi ya kutoa ushauri kwa watu wanye matatizo binafsi na kuwaombea.Kama unahitaji ushauri wa ndoa,uchumba, mahusiano na mambo kama hayo usisite kutujulisha ili utengewe muda wa kukutana nao ana kwa ana..

Kumbuka tarehe ni 17-18/7/2010-Jumamosi na Jumapili ya wiki hii.

Mahali ni-Umoja Church,127217 Hillcrest Rd,Dallas Texas 75230

Muda ni:Saa kumi na moja mpaka saa mbili usiku (11-2 usiku) 5pm 8Pm.

Maelezo zaidi;214 554 7381,682 552 6402,214 773 6697.

NB:Kutakuwa na chakula maalumu pamoja na vinywaji kila baada ya semina ili kufahamiana zaidi.

Karibuni wote
Uongozi wa kanisa la Umoja Dallas Texas.

Thursday, May 20, 2010

Mtumishi wa Mungu Mama Habiba Atakuwa Dallas!

Wapendwa katika shamba la Bwana. Ninayoheshima kukukaribisha ili uweze kukutana na mtumishi wa Mungu Mama Habiba.Inawezekana umewahi kumsikia huyu mtumsihi kwa namna moja au nyingine au hujawahi kumsikia.Mama Habiba ni mama aliyepewa karama ya maombezi na Mungu na amekuwa akiifanya hii kazi kila Mungu alipompeleka.Watanzania wengi wanaoishi hapa Marekani wamekuwa wakisafiri kwenda Houston ili kuombewa na mama huyu na wengine wengi kwa mamia wemekuwa wakiombewa kwa njia ya simu.Mama Habiba atakuwa mgeni wetu kuanzia Jumamosi mpaka Jumapili (22&23/5).

Mama Habiba atafuatana na ujumbe wa watu kama 20 ukiongozwa na Dr.Jerrry Mng'wamba.
Kutokana na uwezo wa ukumbi wetu na ushauri tuliopewa hatutaweza kuchukua watu zaidi baada ya ukumbi kujaa.Ninakushauri ujitahidi kuwahii ili uwe na uhakika wa kupata nafasi ya kukaa bila usumbufu.Milango itakuwa wazi kuanzia saa kumi na moja kamili jioni.

Kwa Maelezo zaidi; 214 554 7381, 682 552 6402, 214 773 6697

Mungu akubariki sana na naomba ufoward huu ujumbe kwa kila mtu bila kujali dini,kabila au nchi anayotoka.

Pastor
Venue:
Trinity Church
12727 Hillcrest Road
Dallas, Texas 75230

Jumamosi kuanzia saa 12 jioni 6:00PM

Jumapili 9:00AM to 11:00AM (saa tatu hadi saa tano asubuhi)
na 5:00PM - 8:00PM (saa 11 hadi saa mbili jioni)

Friday, April 25, 2008

Umoja Church Texas


Habari zimetoka kwa Pastor Absolom wa Umoja Church, Dallas Texas:

Kwa niaba ya kanisa lenu la Umoja,tunapenda kumkaribisha kila moja wenu katika mkutano wa kesho ambao mtumishi wa Mungu Mama Newstar Ngereja atahudumia.
Mbali na mkutano huu, tunapenda pia kutangaza msiba wa BIBI BUPE MWAIJANDEM ambae ni bibi mzaa mama wa mwanajumuia, na mshirika wa kanisa la Umoja dada BAHATI na WINNIE. Msiba huu umetokea jana huko nyumbani Mbeya, Tanzania. Tunaomba wanajumuia watakaoweza kufika kanisani kwa ajili ya ibada na kuwafariji wafanye hivyo kesho siku ya jumamosi saa moja jioni.Kwa watakaoweza kuwapigia simu na kuwafaraji wanaweza kufanya hivyo kwa namba hizi;214 779 4469,214 576 8903, 214 989 8778,214 554 7381. Kwa direction ya kanisa angali juu ya tangazo letu.
Umoja