Showing posts with label Vincent Urio. Show all posts
Showing posts with label Vincent Urio. Show all posts

Sunday, June 21, 2015

Wapiga Picha wa Vyombo Vya Serikali Enzi Hizo!

 Nilifanya kazi nao wapiga picha nikiwa mwandishi wa habari Daily News miaka ya 1980's! Enzi zile tulikuwa wachache na wote tulijuana.  Mzee Makwaia alikuwa Mwalimu wetu TSJ. Alifariki tukiwa mwaka wa kwanza baada ya kugongwa na gari Morogoro Road.

 Kwa hisani ya Kaka Juma Dihule:

WAFAHAMU WAPIGAPICHA WA VYOMBO VYA SERIKALI ENZI HIZO.
Wapigapicha wa wakati huo ambapo vyombo vya habari vilimilikiwa na Serikali pamoja na chama tawala. Waliosimama nyuma toka kushoto marehemu Max Madebe (Mpigapicha Mkuu gazeti la Mfanyakazi, Marehemu Sam Mbando, mpigapicha mwandamizi Shirika la Habari Tanzania (SHIHATA), Marehemu Vincent Urio (Mpigapicha Mkuu magazeti ya Serikali ya Daily News & Sunday News, Marehemu John Makwaia ndiye aliyekuwa mwalimu wetu sisi wote na mpigapicha mkuu wa Serikali katika Idara ya Habari (MAELEZO), akifuatiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye pia ni marehemu, David Saileni ambaye wakati huo akiwa mpigapicha mwandamizi wa Sinema, upande wa Idara ya Habari, (Film Unit), Juma Dihule, Mpigapicha Mkuu SHIHATA, Marehemu Adnani Mihanji, Mpigapicha Mwaandamizi, SHIHATA na Moshy Kiyungi, Mpigapicha mwandamizi ( Idara ya Habari).
Walioketi toka kushoto, Steven Kasange, IKULU, Charles Kagonji , Mkutubi Mkuu wa maktaba ya picha MAELEZO na pia akiwa mpigapicha, Gaspar Msilo, Daily News, Mwanakombo Jumaa, MAELEZO, Hatib Ali Mpichapicha Mkuu (Uhuru na Mzalendo) Raphael Hokoro , ambaye hivi sasa ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO).

Wednesday, December 19, 2007

Wapiga Picha wa enzi zile!

agosti, 1985: *mwalimu nyerere akila pozi na paparazi wa enzi hizo. toka shoto juu ni *max madebe (mfanyakazi), *sam mmbando (shihata), *vicent urio (daily news - huyu ndiye kanifundisha kazi), *mzee makwaia (maelezo), mwanakombo jumaa (maelezo) juma dihule (shihata), mzee nanihii (maelezo), adinani mihanji (shihata) na john lukuwi (maelezo)
chini toka shoto: mdau simfahamu, charels kagonji (shihata), boaz mpazi (shihata) moshy kiyungi (maelezo) na raphael hokororo (maelezo). wenye nyota * wote ni marehemu
******************************************************************************

Kabla ya Michuzi. Hao ni baadhi ya wapiga picha maarufu wa Tanzania. Huyo Boaz Mpazi alikuwa ni mchapa kazi kweli kweli na mwenye moyo wa kazi.

Mzee John Makwaia alipiga portrait kadhaa 'official' za Mwalimu. Pia alikuwa mwalimu wangu wa Photography nikiwa nasoma TSJ. Kwa bahati mbaya aligongwa na gari Morogoro Road maeneo ya Magomeni 1989. Alikufa papo hapo. Tulikosa mwalimu mzuri sana.

Vincent Urio alikuwa mpiga picha mkuu wa Daily News kwa miaka mingi. Alienda kwenye vita vya Kagera. Wengine walioenda kwenye vita ni Juma Dihule na Ben Kiko. Alivyorudi alikuwa analalamika kichwa kinamwuma na alishindwa kufanya kazi vizuri. Alistaafu na aliaaga dunia si muda mrefu baada ya kustaafu. Mzee Urio anaigiza kama Baba Mariamu katika sinema, Arusi ya Mariamu.