Showing posts with label Wedding Gown. Show all posts
Showing posts with label Wedding Gown. Show all posts

Sunday, November 30, 2014

Wafunga Ndoa Uchi

Haya jamani, kwa nini mnapoteza kununua nguo za harusi wakati mnaweza kusevu pesa kwa kufunga mkiwa uchi?  Hao wazungu walisema hela ya nguo watatumia kwa ajili ya kulipa mortgage ya nyumba! Ingekuwa safi kama wageni nao wangekuwa uchi.  Kutoka https://www.facebook.com/pages/Ijebu-News-Xtra/121224847988714?fref=photo


Saturday, November 02, 2013

Fesheni Mpya ya Picha za WanaHarusi Bongo

Wadau, naomba maoni yenu kuhusu hii picha. Mimi nasema Tarzan angefurahi sana kuona wanaharisu kwenye miti! Bibi harusi alipandaje na hiyo gauni na heels?

Thursday, July 25, 2013

Vazi la Nusu Uchi Lazuia Ndoa Kufungwa Kanisani St. Peter Dar!

Binafsi sioni shida ya kuvaa nguo ya harusi ya mabega wazi, ndo fesheni sehemu nyingi. Mbona, tunavaa khanga na vitenge na tunakuwa mabega wazi? Lakini kama umeambiwa mapema kuwa nguo hiyo haifai kanisani basi msikilize Padri au tafuta Kanisa lingine!

***************************************
KUTOKA  GAZETI LA HABARI LEO

VAZI LA NUSU UCHI LAZUIA NDOA KUFUNGWA JIJINI DAR....PADRI AGEUKA MBOGO NA KUWATIMUA WAPAMBE


KIVAZI cha ndugu wa maharusi, kimesababisha patashika katika Kanisa  Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Peter, baada ya Paroko Msaidizi wa Kanisa hilo, Padri Paulo Haule, kusitisha ibada mpaka mhusika atoke akavae vizuri.

*“Ninatoa dakika 10 kwa aliyeingia na mavazi ambayo hayatakiwi kanisani humu kutoka mara moja akavae vizuri, la sivyo ndoa yao haitafungwa,”* alisema Padri Haule wa Kanisa hilo lililoko Oysterbay, Dar es Salaam.

Awali vurugu hizo zilizotokea Jumamosi iliyopita, zilianzia nje, wakati Katekista wa Parokia hiyo, Yohane Maboko, alipotangazia wanandoa na ndugu zao waliokuwa mabega wazi au kuvaa nguo fupi, kutafuta nguo za kujifunika au wasiingie kabisa kanisani.

Maharusi walikubali kutekeleza ombi hilo, wakavishwa vitambaa mabegani vya rangi tofauti na gauni jeupe la harusi, wakaruhusiwa kuingia kanisani, tayari kufunga pingu zao za maisha.


Aliyegoma kutoka na nguo yake ya nusu uchi

Hata hivyo, mmoja wa ndugu wa maharusi hao ambaye jina lake halikupatikana mara moja, alipotaka kulazimisha kuingia na kivazi chake cha mabega wazi, alizuiwa na Katekista Maboko. Katekista huyo alimfuata mwanamke huyo ili kumrudisha akavae vizuri, lakini aliibua zogo na kulazimisha kuingia na
vazi hilo.

Zogo hilo lilipoendelea, wanandugu waliingilia kati, wakitetea vazi hilo ambapo mmoja wa wanandugu, alimvua miwani Katekista Maboko na kuipiga chini ikavunjika huku yeye na wenzake wakimtolea maneno makali ya kumtaka asimzuie ndugu yao kuingia kanisani.

Wakati ndugu hao wakimdhibiti Katekista Maboko, mwanamke huyo alitumia mwanya huo na kupenya hadi ndani ya Kanisa, ambamo Padri Haule, alikuwa akijiandaa kuanza ibada.

*Baada ya Padri Haule kupata taarifa, alitangaza kuwa ndoa ya maharusi wa msichana huyo, haitafungwa hadi awe ametoka. *

Licha ya Paroko kutangaza hivyo, bado ukaidi uliendelea jambo lililomfanya Katekista Maboko kumfuata tena dada huyo na kumwamuru atoke nje, ambapo aliendelea kupinga na baadaye akatekeleza amri hiyo ya Paroko.

Baada ya hapo shughuli za kufungisha ndoa ziliendelea kwa amani na utulivu hadi mwisho maharusi wakatoka kwenda kuendelea na mambo mengine.

Akizungumza na mwandishi wetu, Katekista Maboko alisema waumini hao walikiuka maadili ambayo Kanisa lina wajibu wa kulinda na kuyasimamia ili  waumini wake wayafuate.

Alisema miwani yake iliyovunjwa ilikuwa na thamani ya Sh 90,000 na baada ya  ibada hiyo, aliyetenda kosa hilo alimwendea na kumwomba radhi na kulipa Sh 50,000 na kuahidi kumalizia kiasi kilichobaki wakati wowote.

Maboko alisema uvaaji wa mavazi yasiyotakiwa kanisani hapo, umekuwa ukipigiwa kelele mara kwa mara, na hata katika mafundisho ya ndoa huambiwa lakini ukaidi unaendelea.

*“Maharusi wakati wa mafundisho ya ndoa tunawaambia kuhusu mavazi yao na hata ya ndugu zao watakaowasindikiza kanisani, kuwa wavae kistaarabu lakini  hawasikii,”* alisema Katekista Maboko.

Makanisa mengi siku hizi yamekuwa yakipiga marufuku uvaaji wa nguo fupi na  zinazoacha mabega wazi kwa wasichana na wanawake, wakati wa ibada za kawaida na za ndoa.

Habari Leo

Hii fesheni inapendwa na vijana wengi

Friday, February 15, 2008

Gauni ya Arusi zilizotengenzwa na Toilet Paper






Kama mnavyofahamu kununua gauni ya arusi ni ghali. Kumbe si lazima ununue gauni kwa bei ya juu wakati unaweza kutengeneza na kitu ambacho bei ni rahisi kidogo tena ukitumia coupon ni bei rahisi zaidi.

Hapa Marekani ukienda dukani kununua toilet paper kuna kila aina. Kuna Charmin, kuna double ply, kuna quilted, zenye michoro na ngumu na laini. Mwaka jana kulikuwa na mashindano ya kutengeneza gauni ya arusi na Toilet paper baadala ya kitambaa. Ila nauliza hivi, ukitoka majasho hiyo gauni haitayeyeyuka huko umeivaa. Maana Toilet paper inaanza kuharibika (disintergrate) mara mkitia maji!

Hizi ni baadhi ya picha zilizoshinda. Kuona design zingine bofya hapa: