Saturday, July 19, 2008

Tanzia - Esther Katua (Mwandishi wa Habari)


Kutoka Mjengwa Blog:

MWANDISHI wa habari wa magazeti ya Uhuru,Mzalendo na Burudani,Esther Katua (pichani), amefariki dunia.Esther alifariki katika hospitali ya Lugalo Dar es Salaam juzi ,alikokuwa amelazwa kwa matibabu baada ya hali yake kuwa mbaya.

Alifikishwa hospitalini hapo Jumatatu ya wiki hii baada ya kuzidiwa alipokuwa akijiuguza nyumbani kwao Ilala,Dar es Salaam. Kifo cha mwanahabari huyo kimetokea siku ambayo pia alichaguliwa kuwa Katibu wa Umoja wa Wanawake Tanzania(UWT)Tawi la Uhuru na mjumbe wa UWT wa tawi kuwakilisha vijana.

Wakati wa uhai wake,mbali ya magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Esther aliwahi kuandikia magazeti ya ZanzibarLeo na Mwananchi. Esther alijiunga na magazeti ya Uhuru katikati ya miaka ya 1990.

Kwa waliomfahamu Esther wakati wa uhai wake,alikuwa ni mkarimu, mchapakazi hodari,mchangamfu na aliyependa kushirikiana na watu katika shughuli mbalimbali za kijamii. Hadi jana jioni ilikuwa haijafahamika maziko ya marehemu Esther yatafanyika lini na wapi.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi Amen.

Friday, July 18, 2008

Call for Proposals

Call for Proposals

Title of the Call for Proposals : : ACP-EU cooperation support programme for the ACP cinema and audiovisual sectors (ACP Films)- 9 ACP RPR 43

Publication reference: Europaid /127212/D/ACT/ACP

The African, Caribbean and Pacific Group of States Secretariat (ACP Secretariat) launches a call for proposals financed by the “ACP-EU cooperation support programme for the ACP cinema and audiovisual sectors”, to support projects in the intra-ACP cinema and audiovisual fields, aiming at contributing to the development and structuring of the ACP States’ cinema and audiovisual industries, so that they can create and distribute their own images more effectively. It also aims to enable more promotion of cultural diversity, the networking of ACP cultural identities and intercultural dialogue.

The current call for proposals will award grants to three types of Actions in the cinema and audiovisual fields:

Production projects of cinema and audiovisual (television) works ( Lot 1)
Promotion, distribution, dissemination and networking of the cinema and audiovisual sector in the ACP States ( Lot 2)

Professional development and training of ACP professionals in the cinema and audiovisual sector projects ( Lot 3)

The full Guidelines for applicant can be consulted on the Programme website (http://www.acpfilms.eu), on the ACP Secretariat website (http://www.acp.int), and on the EuropeAid Calls for proposals and tenders website

(http://ec.europa.eu/europeaid/work/funding-opportunities/index_fr.htm).

The deadline for submission of proposals is 5 September 2008.

Toa Maoni Juu ya sinema Bongoland II

E Film Critic wamefungua ukurasa kuhusu sinema Bongoland II. Kwa walioiona mnaweza kuta maoni hapa:

http://efilmcritic.com/review.php?movie=17693

Mnaweza pia kupiga kura hapo Internet Movie Database imdb.com.

http://www.imdb.com/title/tt1125797/

Reuben and Julie Kigame Ministering in Boston 7.19.08


Tamasha la Taa Boston

Wasichana kutoka China wakijiandaa kucheza densi ya kwao.
Taa zikielea kwenye maji ya Ziwa Hibiscus hapo Forest Hills Cemetery

Wasichana wa China wakicheza densi
Grand Master Kuobta ambaye ni 11th generation Samurai kutoka Japan
Watu wakivizia nafasi ya kuweka taa kwenye ziwa
Kikundi cha Grand Master Kubota (Huyo aliyekaa kushoto mwa Grand master alijaribu kuvunja tofali ya cement kwa mguu, kashindwa) Jamaa mweusi alivunja mbao kwa kichwa!
Baadhi ya taa kwenye ziwa!

Wasichana wa Japan wakicheza ngoma
Baadhi ya watu waliojitokeza kwenye Tamasha la Taa wakiangalia show

Wadau, jana jioni nilenda kwenye makaburi ya Forest Hills hapa Boston kwenye Tamasha la Taa. Ni sherehe ya kukumbuka wafu. Watu wanaandika ujumbe kwenye karatasi maalum kwa wapendwa wao waliofariki na zinawekwa kwenye 'lantern' Ni mbao ambao inaweza kuelea kwenye maji. Katikati ya makaburi hayo kuna ziwa ndogo na 'park' sehemu ya kupumzika na kufanya sherehe.

Tuliburudishwa na wanamuziki wanaoimba nyimbo za injili na wacheza ngoma kutoka China na Japan. Giza ilivyoingia watu waliweka hizo 'lantern' taa kwenye maji ya Ziwa Hibiscus. Ilipendenza sana kuona mataa yanaelea juu ya maji, huko bata wanaogelea kwa mshangao kuna nini leo.
Bahati mbaya giza iliingia na sikuweza kupiga picha nzuri. Zingine zimetoka nyeusi kabisa!
*************************************************
The Lantern Festival
Once a year, Forest Hills hosts the Lantern Festival, an extraordinary community event attended by 3,000 people in 2000. Inspired by Buddhist traditions, this non-denominational ceremony offers a magical way to remember family and friends. After enjoying a program of music and dance, people inscribe the paper shades of simple wooden lanterns with greetings. At dusk, we light the lanterns and watch them float across Lake Hibiscus, bearing their messages to the world of the spirits.

Kwa habari zaidi za Forest Hills Cemetery Bofya hapa:

Wednesday, July 16, 2008

NASA inatafuta Mikojo!


NASA ile shirika inapeleka astronauts (wanasayari) huko Mwezini na Mars inatafuta mikojo. Imeomba msaada kutoka kwa wafanyakazi wanaofanya kazi huko! Wanahitaji zaidi ya lita 30 za mkojo kwa siku!
Huo mkojo utasaidi katika kubinu choo chema ambacho kitatumika na wanasayari wakiwa kwenye safari zao ndani ya Space Station na Space Shuttle.
************************************************************************

NASA contractor: Give us your urine

WASHINGTON (AP) -- The No. 1 need right now for some of the builders of the nation's next spaceship: Lots of urine.

A NASA contractor is seeking urine from space-program workers to test the toilets on the Orion space capsule.

Space program contractor Hamilton Sundstrand is seeking urine from workers at the Johnson Space Center in Houston, Texas, as part of its work on the new Orion space capsule that eventually would take astronauts to the moon, according to an internal memo posted on the Web site Nasawatch.com.
The need is voluminous: 30 liters a day, which translates into nearly 8 gallons. Even on weekends.

Designers of the Orion, which will park unoccupied in space for up to six months while astronauts work on the moon, have to solve a pressing issue of getting rid of stored urine, said John Lewis, NASA's head of life support systems for Orion.for dumping pee, so keeping the waste disposal system clear is "really a challenge," he said.


"Urine is a mess because urine is full of solids," Lewis said. Those solids clog the venting system
NASA has a long-standing tradition of collecting samples from its workers to help design better space toilets because "you can't make fake urine," Lewis said.

The Connecticut-based company building the Orion toilet needs the large volume of urine (about the daily output of 30 people) to work on urine acidity problems, said spokesman Leo Makowski.
The memo seeking daily contributions from July 21 to July 31 was not meant to go public, he said.

Tuesday, July 15, 2008

Uraia wa Nchi Mbili (Dual Citizenship)

Nimeona hii story ippmedia.com.


Law on dual citizenship coming

2008-07-15

By Bilal Abdul-Aziz, Dodoma

The government yesterday said it was in the process of drafting a new law that would allow Tanzanians to have dual citizenship. Home Affairs deputy minister Khamis Kagasheki told the House that the Union and Zanzibar governments were jointly looking into the matter.

The deputy minister was responding to a question posed by Mwadini Jecha (Wete, CUF) who had wanted to know when the government would table a bill proposing the enacting of a new law on the matter.

``The Union government and that of Zanzibar are carefully looking into the matter. When the process has been completed, my ministry will bring the bill in the House for approval,`` said Kagasheki.

Earlier on, the deputy minister told Parliament that under the Union constitution, dual citizenship was illegal. He said the law denied the people of Tanzania a chance to possess dual citizenship, and their Tanzanian citizenship ceased once they opted for other citizenship.

Kagasheki said the current laws particularly affected Tanzanian children born outside the country, who on reaching 18 years, were required to denounce the citizenship of one of their parents if they wanted to keep the Tanzanian citizenship.

``The system is not much known by our people. For that reason, at times, children encounter problems when they apply for passports or seek sponsorship for higher education,`` he said.

SOURCE: Guardian

Josiah Kibira alinganishwa na Sembene Ousmane!

Wadau, Mtengeneza sinema wa kiTanzania, Josiah Kibira amelinganishwa na mtengeneza sinema maarufu wa kiafrika, marehemu Sembene Ousmane. Gene Siskel Film Center ambayo inatambulika hapa Marekani kama sehemu maarufu inayotoa maoni juu ya sinema inasema kuwa sinema, Bongoland II ni kama aina ya sinema ambazo alitengeneza marehemu Sembene. Inafanya mtazamaji afikirie kwa undani.

Kati ya watengeneza sinema wote wa kiafrika, Sembene ndiye anajulikana zaidi kwa ajili ya sinema zake kama Moolaade, Xala na Faat Kine.

Bongoland II itaonyeshwa Chicago mwezi ujao, na Detroit hivi karibuni, tarehe za Detroit bado hatujapata.

**********************************************************************


BONGOLAND II: THERE’S NO PLACE LIKE HOME 2008,
Josiah Kibira, Tanzania, 100 min.
With Peter Omari, Thecla Mjatta

In his first film BONGOLAND (2003), Josiah Kibira related the misadventures of Juma, a Tanzanian immigrant in Minnesota. In this self-sufficient sequel, Juma returns to Tanzania (aka Bongoland) to manage a company. His American-style ideas about efficiency and motivation meet with a less than enthusiastic response, and, when Mom’s visit produces some jaw-dropping revelations, he discovers that his relationship to his homeland has become even more tenuous. The film’s sharp, angry satire recalls such Ousmane Sembene classics as XALA and GUELWAAR. In Swahili with English subtitles. DV-CAM video. (MR)

Itaonyeshwa mjini Chicago:

164 North State Street
Chicago, Illinois 60601

Tel: 312-846-2600

MOVIE HOTLINE: 312-846-2800

Itaonyeshwa mara mbili:

Ijumaa/Friday, August 15, 6:15 pm
Jumatano/Wednesday, August 20, 6:15 pm

Monday, July 14, 2008

TPN Mouns the Death of Simbo Ntiro

Simbo Ntiro

Dear Wazalendo and my fellow members of TPN;

It is with deepest sympathy I announce the death of our brother, friend and colleague Simbo Ntiro who was also a Vice-Chairperson of TPN ICT Division.

Let us all pray for the family of the deceased so that God can give them strength to face The reality in this tragedy.

Sanctus Mtsimbe
TPN, President

Kanumba Bongo


Kaka Michuzi, hivi karibuni alibahatika kukutana na wacheza sinema maarufu wa Bongo, Steven Kanumba na Ray. Alipiga picha hii huko Msasani Club. Cheki Kanumba anavyoonekana sasa...very handsome na hiyo ndevu!
Kuona picha zaidi mtembelee Kaka Michuzi kwa kubofya HAPA.

Mh. Zitto Kabwe hajambo sasa.

Picha kwa hisani ya http://bongopicha.blogspot.com/

Wadau, kuna habari njema. Mh. Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini - Chadema) hajambo sasa na ametoka hospitalini siku ya Alhamisi wiki iliyopita.
*************************************************
Zitto atoka hospitali

Thursday, July 10, 2008

Mbunge Machachari nchini Zitto Zuberi Kabwe (Kulia) akiwa na ndugu yake mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya taifa ya Muhimbili leo jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa siku mbili.Mh Kabwe mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya matumbo.


Saturday, July 12, 2008

Bongoland II Review - Beda Msimbe

Nimeona hii review ya sinema, Bongoland II huko Lukwengule Entertainment. Imeandikwa na mwandishi wa habari maarufu Beda Msimbe. Aliiona leo kwenye Tamasha la filamu huko Zanzibar.

*********************************************************

Bongoland ll full uzushi full kupendeza

Ndio kwanza natoka kuangalia filamu iliyotengenezwa na watanzania ya Bongolandll katika ukumbi wa sinema wa wazi ndani ya Ngome Kongwe. Nyumba ilikuwa imeshiba, nataka kusema kwamba sinema hii ilipata mapokezimakubwa kwani ilishangiliwa na vile vijembe viliandaliwa kama vinavyostahili,maeneo ya manzese yalionyesha utofauti mkubwa wa maisha ndani ya Bongo ukilinganisha na mahali kazi zinapofanyika, dauni tauni.

Naam kama kuna wakati nilijisikia raha ni pale ambapo nilimuona dada Chemi akiwana waigizaji wazoefu sana nchini kama mama Mjata wakifanya vitu vyenye uhakika.Nilimaliza kuona filamu iliyojaa utata mkubwa wa maisha Bongoland ll nikiwa najisikia kuwapa Hi watanzania ambao wameonyesha tofauti kubwa ya maisha, akili,uwezo na kupozi maswali ambayo yanamgusa mtazamaji.

Ama hakika kazi ya Mtanzania huyu Josiah Kibira anayeishi huko Ughaibuni, Marekani ina maana kubwa na changamoto kwa waandazi wengine wa filamu nchini.Picha ya Bongoland 11 ambayo ni mwendelezo wa picha nyingine iliyoandaliwa naMtanzania huyo Bongoland ni ukakasi wa mapenzi, machungu, uzushi nauwongo,uzembe na kutojali maisha.

Ni filamu iliyoonyeshwa nchini kwa Mara ya kwanza ikiwa pia miongoni mwa filamuza kitanzania chache zilizofikishwa ZIFF kwa ajili ya kushindanishwa. Ikiwa inatumia dakika 109 inazungumzia umaskini kwa namna nyingi.

Umaskini uliomo ndani ya filamu hii ni wa mawazo, akili na swali kama kweli sisi ni mafukara linatawala kila mahali.hivi kama watu hawataki kazi watakuwaje mafukara?

Juma baada ya kurejea nchini akajikuta anatapeliwa, anadanganywa na pia anapata habari nyignine si nzuri, anapambana na bosi wake ambaye ana vibanda na vijumba basi mambo juu ya mambo.Naam ilikuwa filamu ya kuona kwani inasema wazi na ghasia zote sisi tu maskini wa mawazo.

Mboga za Majani huko Chang'ombe

Bustani za Mboga za Majani Chang'ombe
Wanamwagilia kwa 'can'

Maji Machafu huko Chang'ombe karibu na hiyo bustani...ndo wanachotea maji ya kumwagilia

Bustani ya mboga za majani Chang'ombe


Mdau wa Joseph N. Kutoka Dar es Salaam kaniletea picha hizi za mboga zinazomwagliwa na maji machafu huko Chang'ombe, Dar es Salaam. Kitu gani kinaelea juu ya hayo maji? Na hao wanaotumia kumwagilia wanadhani mchanga unatosha kuwa 'filtration system'?

"Rejea makala uliyo post 'Mboga za majani zaua Dar" kuhusu mboga za majani. Nimeamua kukutumia pix za moja ya sehemu dar eneo la chang`ombe jirani na uwanja mpya wa taifa. Sijajua hasa nini kinapita kwenye mtaro huo sijui mazagazaga ya kiwanda cha serengeti bia au vinyesi ndio wana palilia mboga then watu wanakula, duhh hii ni sumu tena kali sana ina ku kill soft taratibu." - Joseph N.

Friday, July 11, 2008

Msaada Kwenye Tuta - Chombeza Time


Mzalendo mwenzangu nikiwa kama mdau wa kublog na host wa http://www.mwakilaga.blogspot.com/naomba msaada kwenye tuta, unitangaziye ujio wa kitabu changu cha mahaba, Chombeza Time kiatakachoingia mtani Julai 21, nashukuru kwa kunisaidia katika hili.

Chombeza Time kitakuwa kimesheheni mada kali za mahaba na meseji zenye hisia kali za mapenzi zaidi ya 500 ili kuwawezesha wasomaji kupata vitu adimu vitakavyowasaidia kutumisha uhusiano wao!!Si kitabu cha kukosa kitapatikana kwenye meza za magazeti nchini kote kwa bei ya Tsh. 1500/- tu .

Asante,
brazatk@yahoo.com
Mobile: 0715 888887
http://www.mwakilaga.blogspot.com/

Michuzi Globu

Wadau,

Nimewasiliana na Kaka Michuzi kuhusu globu yake kutokupatikana.

Anasema kuna matatizo ya kiufundi na anawahakikishia kuwa itarudi hivi karibuni.


- Chemi


BOFYA HAPA ILI UENDE MICHUZI GLOBU

Hakuna Sumu! - Skandali ya 'Uchawi' Bungeni


Sijiui kama wabunge watakaa wakiamini kuwa wako salama sasa. Mkemia mkuu wa serikali anasema kuwa ule unga uliyomwagwa bungeni haukuwa na sumu. Lakini kwa wanaojua uchawi, huo sumu hauwezi kuonekana kabisa kwa binadamu wa kawaida. Kwa hiyo bado tutasikia mbunge fulani atakaa sehemu fulani huko Bungeni na baada ya muda kidogo atasema kuwa anajiskia kachoka kichwa kinamwuma nk.. Hii siyo mwisho wa skandali ya uchawi/juju Bungeni.


***************************************************************************


Unga uliomwagwa Bungeni hauna lolote-Mkemia

2008-07-11

Na Jackson Kalindimya, Dodoma

Hakuna ushahidi wowote uliopatikana wa mtu kuona au picha za mitambo ya kamera maalum-CCTV unaothibitisha kumwagwa sumu ndani ya ukumbi wa Bunge kama ilivyodaiwa.

Taarifa iliyotolewa jana mjini hapa na Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma, Naibu Kamishia wa Polisi, Bw. Omari Mganga, ilisema kuwa baada ya sampuli kukusanywa na kutumwa kwa Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye baada ya uchunguzi wake hakuweza kuona sumu yoyote ile inayotambulika.

``Kwa maana hiyo basi hakuna ushahidi wowote ule, uliopatiakana wa ama mtu kuona au poicha za mitambo ya CCTV au wa kisayansi unaothibitisha kufanyika vitendo kama hivyo`` ilisema taarifa hiyo.

Wakati wa kikao cha Mkutano wa kumi na mbili cha Bunge la Tanzania lilipoanza mkoani Dodoma, kulitokea minong\'ono au uvumi kuwa kuna Mbunge mmoja na Afisa Mmoja walionekana ndani ya Ukumbi wa Bunge wakizunguka kwenye viti vya waheshimiwa Wabunge huku wakinyunyizia vitu/unga uliohisiwa ulikuwa kwa ajili ya kudhuru binadamu au imani za kishirikina.

Kamanda Mganga alisema, katika taarifa yake kuwa, baada ya kuenea kwa uvumi hadi kwenye vyombo vya habari, uchunguzi ulifanyika kwa kukusanya ushahidi mbalimbali. ``Watu mbalimbali walihojiwa na hakuna hata mmoja aliyeweza kuthibitisha kuwa aliona watu wa aina hiyo wakifanya hayo yaliyokuwa yakiongelewa,`` ilifafanuliwa.

Alisema, uchunguzi pia ulifanywa na wataalamu wa kampuni ya SSTL GROUP wakisaidia na Maafisa wa Usalama wa Taifa na Polisi kwa kupitia picha zinazochukuliwa na mitambo ya CCTV ndani ya ukumbi wa Bunge, milango ya kuingilia na kuzunguka eneo lote la Bunge waliona kuwa hakuna kamera zilizozimwa tangu mwaka 2006 na katika kumbukumbu hizo za picha hakuna iliyuoonyesha mtu/watu wakifanya vitendo vilivyokuwa vinavumishwa.

Alisema pia sampuli mbalimbali zilichukuliwa kutoka katika ukumbi wa Bunge pamoja na vumbi lililopatikana kutoka ndani ya mashine ya kusafishia ndani ya ukumbi wa Bunge (hoover) ambao kama kungekuwa na kitu kilichokuwa kimenyunyuziwa ndani ya ukumbi huo tangu tarehe 9/6/2008 na kuendelea ingesaidia kwa kiwango kikubwa.

Thursday, July 10, 2008

Familia ya watumwa Marekani - 1862


Familia ya watumwa South Carolina, 1862.
(Picha iko kwenye maktaba ya Library of Congress)
Kuna kitu ambacho nalalamika sana hapa Marekani. Ni kwamba wengi wa waMarekani weusi wamesahau au hawataki kutambua asili yao ya Afrika. Ninfanya utafiti kwa ajili ya screenplay ambayo naandika. Nikaona hii picha iliyopigwa 1862, yaani miaka 146 iliyopita.
Ukitazama vizuri unaweza kusema ni waafrika kabisa. Naona hao walikuwa bado hwajachanganya damu na wazungu. WaMarekani weusi wengi ni weupe weupe shauri ya kuchanganya damu na wazungu. Leo utasikia waMarekani weusi wanatania, "She/He black like coal" Yaani mweusi kama mkaa. Na hao weusi tii wanadhauruliwa ile mbaya.

Kwa nini waMarekani weusi wengi wamechanganya damu? Wazungu walitembea sana na wanawake weusi na kuzaa nao enzi za utumwa. Enzi hizo uliweza kukuta Mzungu (Master) ana familia ya watoto wa kizungu na mke wake, na hapo kwenye backyard kazaa watoto kibao mashombe na mtumwa/watumwa wake. Wengine walitunza hao watoto vizuri kidogo kwa kuwapa nguo na chakula zaidi ya wengine. Master wengine waliona hao watoto sawa na watumwa wengine na kuwauza na kuwapiga na kuwatesa.
Si siri kuwa wazungu walitumia wanawake weusi kwa ajili ya raha zao za ngono na pia kujifunzia habari za ngono. Wanawake weusi wengine waliona sifa kuzaa na wazungu kuliko mweusi mwenzake maana alidhani mtoto atakuwa na maisha bora. Master wengine walisema kuwa wataua wanawake ambao hawazai watoto waliochanganya damu. Kweli ilikuwa balaa enzi hizo.

Maneno ya Rev. Jesse Jackson juu ya Obama

Senator Obama na Rev. Jesse Jackson (Picha ya kinafiki)


Reverend (Mchungaji) Jesse Jackson, ni mtu aneyeheshimika sana hapa Marekani na duniani hasa kwa kutetea haki za watu weusi.

Kumbe Rev. Jackson ana usongo na Senator Barack Obama ambaye ni mgombea rais wa upande wa Democrats. Rev. Jackson alikuwa anahojiwa kwenye TV Fox News siku ya jumapili. Alidhani microphone imezimwa, ndo akamwambia huyo mtu aliyekuwa amekaa naye, " Huyo Obama anadharau watu weusi, natamani nimkate mapumbu!"

Duh! Kutoka kwenye mdomo wa mtu wa Mungu.

Rev. Jackson ameomba msamaha kwa maneno yake.

Hivi karibuni, Sen. Obama, alihimiza 'familia' kwa watu weusi wa Marekani. Watoto wengi wamezaliwa nje ya ndoa na akina baba wanakimbia wajibu wao kama wazazi. Jambo ambayo ni kweli. Takrimu kwa watu weusi hapa zinaonyesha kuwa watoto wengi wamezaliwa nje ya ndoa kuliko waliozaliwa katika ndoa.

Lakini tukisoma ndani zaidi si siri kuwa waMarekani weusi wengi wanachukia watu waliotoka Afrika ingawa mababu zao walitoka huko huko. Kuna wakati walisema kuwa Obama si mweusi halisi maana mamab yake ni mzungu na baba yake ni Mkenya.

Kwa habari zaidi someni:

http://firstread.msnbc.msn.com/archive/2008/07/10/1190777.aspx

http://www.smh.com.au/news/us-election/treacherous-sound-bite--jacksons-offcolour-words-about-obama/2008/07/10/1215658037955.html

http://blogs.usatoday.com/onpolitics/2008/07/whats-new-6.html

Wednesday, July 09, 2008

Wanaogombea Miss Vodacom TZ 2008


Hao akina dada wanagombea taji la Miss Vodacom 2008. Wamekwenda kambini leo Bagamoyo.
Kwa habari na picha zaidi mtembelee Kaka Michuzi.

70's Boat Party Minneapolis, Minnesota


Hivi karibuni wadau wa Midwest walikumbuka enzi za miaka ya 70 kwa '70's Boat Party' huko Clear Water, Minnesota. Ama kweli walijitahidi kuonekana kama ni 1973! Cheki hizo Afro wigs!
Umoja society, waliandaa hiyo sherehe siku ya 4th of July.

Hapo kushoto ni stelingi wa sinema, Tusamehe, Fundi Kibwana aka Bilantanya, Thomas Kibwana, Yolanda Kibwana, Tuma Mutua, Peter Mutua na Nguzo.