Showing posts with label Bibi Titi Mohamed. Show all posts
Showing posts with label Bibi Titi Mohamed. Show all posts

Friday, February 11, 2022

SAHIHISHO - CORRECTION Pichani siyo Mh. Anna Makinda

 Kuna mtu ameposti hii picha mtandaoni akidai aliyesimama ni Mh. Spika Mstaafu wa Bunge la Tanzania, Mrs. Anna Makinda. Si kweli, aliyesimama ni Mama yangu mzazi Mrs. Rita Che-Mponda.  Picha ilipigwa mwaka 1965, Biti Titi alivyokuja Marekani kwenye mkutano wa akina Mama.  Baba alimwalika nyumbani, Washington D.C. kwa ajili ya chakula na mahojiano.  




CORRECTING THE RECORD - SAHIHISHO!!

Since last night, there has been a photo of my Mom with the Late Pioneer Female Leader of Tanzania, Bibi Titi Mohamed. My Mom is identified as a young Former Speak of the Tanzania Parliament, Mama Anna Makinda.
I'd like people to see the original photo that was cropped by someone. The young lady standing is my mother, Mrs. Rita Che-Mponda and NOT Mh. Mama Anna Makinda.
The photo was taken in 1965, Bibi Titi was in the USA for a Women's Meeting. My father was an Announcer at the Voice of America - Swahili Service at the time, He invited Bibi Titi to the house and interviewed. I originally published in my 'Swahili Time Blog' in 2010.

Monday, October 03, 2011

Sinema 'Historia ya Khanga" Cheki Mimi na Kaka Michuzi!

MaStaa wa Bongowood 1991 Michuzi & Chemi


Kabla ya Kanumba na Ray kulikuwa na Chemi na Michuzi!

Wadau, kwenye mwaka 1992 nilishiriki katika sinema ya TAMWA, "The History of Khanga".  Hebu itizame, Utaniona mimi na Kaka Michuzi, "Tunajiandaa kulala"

Mwongozaji alikuwa Dada Fatma Alloo. Pia kuna mahojiano na marehemu Bibi Titi Mohamed.

Sinema sasa iko YOU TUBE kwa hisana ya Dada Fatma na Kaka Michuzi:

http://www.youtube.com/watch?v=jAuhAB0HeeA&feature=player_embedded

Wednesday, January 27, 2010

Bibi Titi Alivyotutembelea Mwaka 1965


Wadau, nilivyokuwa Tanzania mwaka jana, nilichukua hii picha kutoka nyumbani. Ni wazazi wangu Dr. Aleck & Rita Che-Mponda na marehemu Bibi Titi Mohamed. Naona alikuwa kwenye ziara Marekani. Picha ilipigwa Washington D.C., wakati huo baba alikuwa Mtangazaji wa Voice of America Swahili Service na pia mwanafunzi Howard University. Picha naona ilipigwa 1965, baba anamhoji kwa ajili ya kipindi chake. Nakumbuka kulikuwa na picha Bibi Titi amenipakata lakini sikuiona. Nikiipata mbona nitafurahi mno.

Thursday, September 24, 2009

Maneno ya Wimbo 'Hongera Mwanangu'

Bibi Titi na Mwalimu Nyerere

Kuna mdau kaniomba nimtafutie maneno (lyrics) za wimbo, Hongera Mwanangu ambayo tulisikia sana Radio Tanzania enzi zile ukiimbwa na marehemu Bibi Titi Mohamed. Sasa naomba nisaidie, ni lugha gani wanaiyotumia. Naona maneno ya kiswahili na sijui ni kilugha gani.


******************************************************************

HONGERA MWANANGU

Hongera mwanangu eh hongera.
Nami nihongeree hongera.

Hongera mwanangu eh hongera.
Nami nihongeree hongera.

Mama uchungu, Mama uchungu.

Nyamara mwanangu. Oyee.

Nyamara mwanangu tumbo la udere linauma mno eh!