Showing posts with label Jennifer Hudson. Show all posts
Showing posts with label Jennifer Hudson. Show all posts

Tuesday, June 02, 2009

Umbea - Jennifer Hudson ana Mimba!

Pichani Jennifer Hudson na David Otunga

Habari zinasema kuwa mwimbaji na mcheza sinema, Jennifer Hudson ana mimba ya miezi saba. Niliona picha kwenye TV leo na kweli alikua na 'mtumbo' hasa. Nampongeza yeye na mchumba wake, David Otunga. Lazima Jennifer atakuwa na furaha. Kwa sasa wameficha kwa umati kama ni mtoto wa kike au wa kiume.

Mtakumbuka mwaka jana, shemeji yake Jennifer aliwaua, mama yake mzazi, kaka yake na mpwa wake.

Kwa habari zaidi someni:


Monday, October 27, 2008

Maiti ya Mpwa wa Jennifer Hudson Yapatikana

William Balfour (Kushoto mwneye kofia) na mke wake Julia Hudson (Katikati) William ameshikiliwa na polisi kwa sasa. Inaelekea yeye ndiye aliyewaua Familia ya Jennifer Hudson.
Mama yake Jennifer Hudson, Darnell Donerson
Mpwa wa Jennifer Hudson, Julian King (7)
Kaka yake Jennifer Hudson, Jason Hudson (29)


Maiti ya mpwa wa Jennifer Hudson, Julian King (7), ulikutwa ndani ya SUV iliyokuwa imegeshwa upande mwa Magharibi mwa Chicago (West Side) leo asubuhi. Polisi wanasema kuwa mtoto alikuwa amebakwa na alipigwa risasi mara kadhaa.

Kwa kweli sijaweza kulala vizuri tangu nisikie habari za mama na kaka yake Jennifer kuuwawa siku ya Ijumaa iliyopita. Na sasa huyo malaika mwenye miaka 7 tu kauliwa kikatili hivyo.

Kwa sasa polisi wanamshikilia mume wa dada yake Jennifer, William Balfour (26). Habari zinasema kuwa wiki kadhaa zilizopita aliiba gari ya mke wake Julia Hudson, na kuiuza bila ruhusa yake. Ugomvi ulizuka hasa Julia alipokataa kumpa 'title' ya gari. Balfour alimtishia Julia kuwa atamwua mtoto wake na familia yake yote. Julia hakutoa taarifa polisi maana hakutegemea atatenda maovu yake ingawa jamaa aliwahi kufungwa miaka saba kwa kosa la kutaka kuua mtu.

Mungu alaze roho za marehemu mahala pema mbinguni. AMEN.

Kwa habari zaidi someni:

http://omg.yahoo.com/news/fbi-says-body-found-is-that-of-hudsons-nephew-7/14640

http://www.chicagotribune.com/chi-julian-king-1027,0,7364921.story

http://edition.cnn.com/2008/SHOWBIZ/10/27/jennifer.hudson.profile/?iref=hpmostpop

http://www.abcnews.go.com/Entertainment/story?id=6114149&page=1

http://www.chicagotribune.com/chi-jennifer-hudson-1028,0,7284673.story

Saturday, October 25, 2008

Mama na Kaka wa Jennifer Hudson Wameuawa!

Jennifer Hudson ma Mama yake mzazi

Kuna habari za kusikitisha. Mama yake mzazi Jennifer Hudson, Darnell Donerson (57), na kaka yake Jason Hudson (29), walmeuawawa kikatili jana nyumbani kwao huko Chicago. Mpwa wake mwenye miaka 7 anatafutwa na polisi wametoa Amber Alert (tangazo maalum kwa ajili ya watoto waliohatarini). Polisi wanamshikilia William Balfour (27) ambaye ni mume kwa mdogo wake.

Jennifer Hudson alipata tuzo la Oscar mwaka jana kwa ajili ya sinema, Dreamgirls. Aliigiza kama Effie White ambaye alikuwa mwimbaji mkuu wa kikundi cha Dreamgirls kabla ya kupinduliwa na Deena Jones (Beyonce). Jennifer alipata umaarufu kwenye American Idol.

Wiki iliyopita sinema, The Secret Life of Bees, ilitoka. Jeenifer anaigiza mle na akina Queen Latifah, Alicia Keys na Sophie Okonedo. Hivi karibuni kachumbiwa na mwanasheria na mwigizaji, David Otunga.

Mungu awalaze roho za marehemu mahala pema mbinguni. Amen.

Watu wanauliza kwa nini Jennifer hawakuhamisha familia yake kutoka South side ambayo inajulikana kwa kuwa eneo hatari sana huko Chicago. Habari zinasema kuwa mama yake hakutaka kuhama maana alikaa pale maisha yake yote.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.latimes.com/news/nationworld/nation/la-na-hudson25-2008oct25,0,4062243.story

http://hollywoodinsider.ew.com/2008/10/jennifer-hudson.html?iid=top25-20081025-Jennifer+Hudson

http://ap.google.com/article/ALeqM5iIqSbmp7cCrnSvw1FIMxIvjQa8AQD941DLG80