Wednesday, December 05, 2007

Vichaa waongezeka Dar





















Nimesoma habari kwenye ippmedia.com kuwa vichaa wameongezeka mjini Dar es Salaam. Lazima wataongezeka kwa jinsi maisha yalivyobadilika Tanzania. Tamaa ya vitu pia unafanya watu warukwe na akili. Maisha magumu na ukosefu wa fedha unachangia.

Na wanawake pia wanakuwa kichaa. Juzi nilisoma habari ya mama moja aliyelala barabarani huko anaomba wanaume wafanye naye ngono. Mwingine zilifyatuka baada ya kuwatopeza mume wake na mtoto. Mwingine alitembea uchi Kimara hadi Ubungo alipokamatwa.

Nilipokuwa nasoma Zanaki kuna kichaa alikuwa na mchezo wa kukaa karibu na geti na kuonyesha wasichana ume wake. Huyo alikuwa anavaa nguo safi, asingekuwa anafanya maajabu usingejua ni kichaa. Kulikuwa na jamaa moja alikuwa anajifunga shuka tu na kusimama kwenye kona ya Morogoro Road na United Nations. Kazi yake kutazama wanafunzi. Watu walisema zilimfyatuka akibukua mtihani wa Form 6!
Pia watu kupoteza imani na waganga wa kienyeji na idadi yao kupungua inachangia. Waganaga gao walichangia sana kupunguza idadi ya watu wenye ugonjwa wa akili, maana tiba yao mara nyingi ni 'psychological'.

Kuna haja ya kuongezeka kwa tiba ya psychiatric, huko Tanzania.

***********************************************************************

Wenye matatizo ya akili Jijini Dar waongezeka


2007-12-05

Watu 28,900 mkoani Dar es Salaam, wameugua ugonjwa wa akili mwaka jana. Mratibu wa Afya Wilayani Temeke, Bi. Mary Mgaya ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari. Akasema takwimu hizo na zinahusu wagonjwa waliofikishwa katika vituo mbalimbali vya afya Jijini.


``Mwaka 2000, wagonjwa 6,000 waliugua ugonjwa huu wa akili... Hawa ni wale waliofikishwa katika vituo vya afya na kupatiwa matibabu,``akasema. Kuhusu siku ya wagonjwa wa akili itakayoadhimishwa leo Jijini, Katibu Mkuu wa Chama cha Afya ya Akili, ?Dk. Scolastica Ndonde amesema sikukuu hiyo inafanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke.

Akasema ujumbe wa mwaka huu ni``Afya ya akili na mabadiliko:Mwingiliano wa tamaduni, imani, maadili, desturi na tofauti za kijamii,``. Akasema matibabu ya ugonjwa huo yanahitaji mawasiliano mazuri katika jamii.

Akakemea tabia ya watu kuwafunga kwa kutumia kamba wagonjwa wa akili kwani hiyo ni kutowatendea haki. Aidha, akasema Watanzania wamekuwa wakikimbia kwa waganga ambapo wanaambiwa kuwa wagonjwa hao wamelogwa ama wamepagawa. Akasema jambo hilo limekuwa likiwafanya wagonjwa kuzidi kuumwa.

Akawataka kuwawahisha hospitali wagonjwa hao ili waweze kupatiwa matibabu yaliyosahihi kwa ajili ya afya zao. Akasema baadhi ya watumishi katika sekta ya afya wamekuwa hawasimamiii huduma za wagonjwa wa akili kwa namna inavyotakiwa.

Akasema wengine wanashindwa kufanya maamuzi mazuri kuhusu tiba ya wagonjwa wa akili kutokana na fikra zao juu ya umuhimu wa huduma hizo. ``Wamaweza kujua wajibu wao lakini mazoea yao na tabia walizozizoea zinawafanya washindwe kutimiza majukumu yao vizuri,``akasema.

Tuesday, December 04, 2007

Bongoland II, Maswali na Majibu

BOFYA HAPA KUSOMA MASWALI NA MAJIBU KUHUSU SINEMA YA BONGOLAND II.

Maswali na majibu kuhusu sinema ya Bongoland II.

Kwa habari za sinema za Kibira films Bofya hapa:

http://www.kibirafilms.com/index.html

Kuona posts zangu zote kuhusu sinema ya Bongoland II BOFYA HAPA:

BONGOLAND II

Hii ndo jinsi ya kucheza 'First Dance'


Hii ndo jinsi ya kucheza ngoma ya kwanza baada ya kufunga ndoa.

Mwalimu Gibbons arejea Uingereza!


Mwalimu Gibbons na watoto wake


Mwalimu Gillian Gibbons (54), yuko Uingereza na familia yake. Alirejea leo asubuhi na ndege ya Emirates.
Mwalimu Gibbons, alisifia waSudani na alisema yaliyompata yasiwakatishe moyo wengine kwenda huko. Anasema hakujua nini inatokea duniani na jinsi kesi yake ilivyogusa wengi maana alifungwa peke yake (Solitary). Baadaye kuna mtu alimdokeza kuwa kesi imekuwa kubwa.

Kwa sasa anataka kupumzika na kushrekea Christmas na familia yake. Halafu atatafuta kazi.

Imegundulika kuwa chanzo cha matatizo yake ni visa vya dada moja aliyekuwa anafanya kazi kwenye shule hiyo, Unity High School. Sarah Khawad, alikuwa karani kwenye hiyo shule. Alifukuzwa kazi Novemba na aliahidi kuifunga hiyo shule ili kulipiza kisasi!
Mweza Septemba Khawad aliwaomba wazazi wa watoto wa darasa la Mwalimu Gibbons (darasa la pil) kwenda polisi kumshitaki. Walikataa.

Khawad ndo aliwaambia polisi kuhusu darasa la Mwalimu Gibbons kuita mdoli, Mohamed na kusababisha matatizo yote. Unity High School imefungwa kwa muda.

Kwa habari zaidi someni:



Monday, December 03, 2007

Rais wa Sudan amsamehe Mwalimu Gibbons!



UPDATE 1:29PM Eastern - Mwalimu Gibbons ameondoka Sudan, kurejea Uingereza.
****************************************************************************
Rais wa Sudan, Omar Al-Bashir, amemsamehe mwalimu mwingereza Gillian Gibbons (54)! Mwalimu Gibbons alifungwa Sudan wiki iliyopita baada ya kuruhusu darasa lake la wanafunzi wa darasa la pili kuita mdoli wa darasa, Mohamed.

Wasudan walisema kuwa ilikuwa kashfa kwa waislamu. Wengine walidai auliwe. Baada ya mwalimu huyo kufungwa wabunge wawili waislamu kutoka Uingereza walienda Sudan kuongea na rais Al-Bashir. Msamaha huo umetolewa leo asubuhi.

Mwalimu Gibbons naye ameomba msamaha kwa watu wa Sudan na kusema kuwa hakuwa na nia ya kuwakashifu. Hivi sasa yuko chini ya ulinzi ya waingereza ubalozini mwao kwa usalama wake. Ataondoka kwenda Uingereza hivi karibuni.

Wakati huo huo, Serikali ya Sudan bado inaendelea kuua waDinka (waafrika) huko Darfur.

Kwa habari zaidi someni:

http://www.cnn.com/2007/WORLD/africa/12/03/sudan.teacher/index.html

http://www.thestar.com/comment/article/281848

http://www.news.com.au/heraldsun/story/0,21985,22865462-663,00.html

Saturday, December 01, 2007

Siku ya UKIMWI Duniani




Leo ni siku ya UKIMWI Duniani. Hakuna mTanzania asiyejua mtu aliaathirika au kufa kwa ugonjwa huo. Kama umetoka Tanzania siku nyingi halafu unarudi na unaanza kuuliza watu unaambiwa, "yule kafa, yule kafa zamani, yule tulimshasahau!" inasikitisha!

Afrika ugonjwa huo bado ni tishio. Juzi Tanzania walitangaza kuwa UKIMWI unaua kuliko malaria, maana watu 400 wanakufa kwa siku shauri ya huu ugonjwa. Zambia walisema idadi ya watoto waliopoteza wazazi wote wawili kwa UKIMWI unaongezeka. Afrika Kusini wanaume wanatembea na watoto wadogo wa hata miezi kusudi eti wapone ugonjwa huo!

Tatizo la Afrika ni kuwa inasambaza hasa kwa ngono. Waafrika wanapenda ngono. Utamsikia mtu anasema yuko tayari ku-risk kwa ajili ya raha ya muda mfupi. Na atasema "Oh, kila mtu atakufa!" Hiyo ni kweli lakini kwa nini ufupishe maisha yako kwa ajili ya raha?

Tumieni kondomu basi acheni kupenda kwenda Tigo, bila soxi! Utasikia msichana kakubali kufanya bila kondomu kwa vile mpenzi wake kamwambia, "Kama hutaki kavu ina maana hunipendi!"

Idadi ya watu wanaokufa na ugonjwa huo katika nchi ziliaoendelea zimepungua sana. Wagonjwa wapo. Nimeona wazungu waliothirika. Na hapa Marekani wengi ya waathirika ni weusi!

Tuombe Mungu kuwa Tiba ya kudumu ipatikane haraka. Dawa zipo za kurefusha maisha lakini hakuna dawa ya kuitibu kabisa ipotee mwilini mwa mtu.

Mungu atunusuru!

********************************************************************************
Kwa habari zaidi someni:

http://www.aids.org/

http://en.wikipedia.org/wiki/AIDS

http://aids.about.com/

Ajisalimisha


Kichaa aliyeteka ofisi ya kampeni ya Senator Hillary Clinton huko Rochester, New Hampshire, Leeland Eisenberg, alijisalimisha jana jioni. Aliachia mateka wote huru kabla ya kujisalimisha kwa polisi.

Eisenberg alisema alifanya hivyo kwa sababu anahitaji matibabu ya ugonjwa wa akili na hana pesa za kulipia. Alisema watu wenye ugonjwa wa akili wanateseka Marekani hasa kama hawana bima au hela za kulipia matibabu.
Senator Clinton anasema kuwa anaelewa kuwa Eisenberg aliteka ofisi yake kwa ajili ya kutoa mwanga kwenye hiyo swala. Alisema pia kuwa anashukuru hakuna mtu aliyeumia au kufa katika tukio hilo.
Kwa habari zaidi someni:

Friday, November 30, 2007

Ofisi ya Hillary Clinton imetekwa nyara New Hampshire

Senator Hillary Clinton
UPDATE: 4:14Pm Eastern - Mateka wote wawili wameachiwa huru
*********************************************************************************

Watu wawili wametekwa katika ofisi ya mgombea rais wa chama ca Democrats wa Marekani, Senator Hillary Clinton. Ofisi enyewe ni ya kampeni yake na iko Rochester, New Hampshire.

Sakata umeanza saa 7 mchana huu na hivyo navyoandika bado inaendelea. Mama moja aliyekuwa ndani ya hiyo ofisi na mtoto wake wa miezi sita aliachiwa huru pamoja na mtoto.

Jamaa aliyeteka nyara ofisi amejifunga mkanda ambayo anasema ina bomu! Ofisi sasa imezungukwa na polisi, SWAT (FFU) na Secret Service. Kama jamaa hajisalimishi msishangae mkisikia kuwa jamaa katunguliwa kwa kupigwa risasi kichwani na FFU.

Pia polisi wameamuru ofisi za wagombea rais wengine maDeomcrats, Barack Obama na John Edwards zifungwe kwa usalama wa raia na wafanyakazi.

Marekani bwana!

http://www.cnn.com/2007/POLITICS/11/30/clinton.office/index.html

Msosi



Je, msosi kama huu unafaa kulika kwa bia au soda? Ila hiyo nyama ya pembeni hapo ni mafuta tupu.

Thursday, November 29, 2007

Mwalimu Mwingereza afungwa Sudan!

Mwalimu Gillian Gibbons


Macho ya waiingereza yamekuwa Sudan tangu jumapili kwa sababu ya mwalimu kutoka Uiingereza anayefundisha katika shule ya International huko. Mwalimu Gillian Gibbons ana miaka 54. Wanafunzi wake wana miaka saba na lazima bado wako kwenye umri wa kupenda toys (vitu vya kuchezea). Walikuwa na mdoli wa darasa. Aliwapa zoezi la darasa kumpa jina. Wengi walichagua jina Mohamed. Kwa kidemokrasia wengi wanashinda. Hao watoto wa miaka 7 ndo waliochagua jina la Mohamed. Majina mengine yaliyopendekezwa ni Hassan na Abdullah.

Huyo mwalimu namhurumiwa sana. Lazima hakuelewa uiislamu vizuri. Hakuna picha ya mtume Mohamed na wala hakuna sanamu yake. Hivyo kumwita huyo mdoli Mohamed ilikuwa tusi kubwa kwa waislamu. Pia kaanza kufundisha Sudani juzi juzi tu. Kwa wazungu kutoa jina kwa midoli ni kawaida. Sasa anashitakiwa kwa kosa la kutukana uislamu.

Sasa nauliza hivi, hao waSudani hawakuweza kumwelezea kuwa kafanya kosa na kumwelimisha. Baadala yake walitishia kumchapa viboko 40 na kufungwa jela.

Leo mahakama huko wameamuru afungwe siku 15 na awe deported akitoka. Tayari waSudani wanaonekana wabaya duniani kwa kuua raia wao wanye asili ya Afrika hasa kabila la Dinka huko Darfur.

Nawauliza wasomaji waislamu, je, walivyofanya waSudani ni sawa au walizidisha kipimo na hii tukio?

Na hao watoto je, waadhibiwe kwa kuchagua hiyo jina au waelimishwe sheria za uisilamu? Lazima wataathirika maishani mwao wakikumbuka mwalimu wao mpendwa alivyonyanyaswa kwa kosa hiyo.

Hii kesi inasisitiza umuhimu wa watu wanaoenda nchi zingine kuelewa mila na desturi na dini za huko!

Kwa habari zaidi someni:

http://www.cnn.com/2007/WORLD/africa/11/29/sudan.bears/index.html

http://www.abcnews.go.com/International/story?id=3931681&page=1

http://www.cfnews13.com/News/International/2007/11/29/briton_convicted_in_sudan_blasphemy_case.html

Wednesday, November 28, 2007

Simu ya Kifo kweli!


Siku hizi watu wengi wana simu za mkononi. Lakini zina athari zake. Siku nyingi watu wamesema zinapunguza nguvu za kiume au kuua mayai ya mwanamke! Mara waseme zinaleta tumours (uvimbe) kwenye ubongo.

Sasa leo kuna habari kuwa baba moja huko Korea ya Kusini kafa kazini kwake baada ya simu yake ya mkononi kulipuka kwenye sharti yake na kumwua. Wanasema betri ndo ililipuka ndani ya poketi kwenye sharti aliyovaa. Simu enyewe iliyeyuka kifuani mwake! DOH!

******************************************************************************

SEOUL, South Korea (AP) -- An exploding mobile phone battery apparently killed a South Korean man in the first such known case in this gadget-obsessed country, police say.

The man, identified only by his family name Suh, was found dead at his workplace in a quarry Wednesday morning and his mobile phone battery was melted in his shirt pocket, a police official in Cheongwon, 135 kilometers (85 miles) south of Seoul, told The Associated Press.

"We presume that the cell phone battery exploded," the police official said on condition of anonymity.

The official said the phone was made by South Korea's LG Electronics, the world's fifth-biggest handset maker.

LG Electronics confirmed its product was involved in the accident but said such a battery explosion and death was virtually impossible.


Duniani wawili wawili!

Mwigizaji maarufu wa Namibia marehemu 'N!xau' katika sinema ya The Gods Must be Crazy!


Huyo Usher kafanana sana na yule mwigizaji mkuu wa sinema ya The Gods Must be Crazy! Utadhani ndugu yake! Ama kweli duniani wawili wawili!

Tuesday, November 27, 2007

Mhindi aingia benki Florida na kudai tiketi ya kwenda India!

DUH! Habari kutoka Orlando, Florida zinasema kuwa mhindi aliingia kwenye tawi la Wachovia bank na kudai tiketi ya ndege kwenda India. Alikaa kwenye kiti na kusema kuwa haondoki mpaka apate hiyo tiketi!

Wazungu wasiojua tofauti katia ya mhindi au mwarabu waliita polisi wakidhani katumwa na Al Qaeda. Alikaa mle masaa mawili akisema anataka kwenda India.

Polisi walituma SWAT team (FFU)! Mtu mwenyewe hata hakuwa na silaha alikaa kwenye kiti na kudaia tiketi ya ndege tu. Huyo baba angekufa bure! SWAT walimchukua na anashikiliwa na polisi!

******************************************************************************

Man Demanding Plane Ticket To India Forces Bank Evacuation In Orlando

November 27, 2007

ORLANDO, Fla. -- An Orlando bank was evacuated Tuesday when an East Indian man walked into a bank and demanded a plane ticket to India, according to the Orange County Sheriff's Office.

Investigators said bank workers inside the Wachovia Bank located on Sand Lake Road in Orlando noticed the man acting suspiciously and called 911.

When officers arrived, the man refused to leave the bank and said "he wanted to go to India," Orange County sheriff's representative Jim Solomons said.

A bank worker who flagged down an officer said the man sat in a chair and did not moved after entering the building. Witnesses said they saw the man praying inside the bank.

A SWAT team took the man into custody after a two-hour standoff at the building.

There were no injuries in connection with the standoff.

A lane of traffic near Orange Blossom Trail and Sand Lake was closed over the incident.

http://www.local6.com/news/14704846/detail.html

Obama - Nimevuta bangi na kutumia unga!

Mgombea nafasi ya rais wa Marekani kutoka chama cha Democrats, Senator Barack Obama, amekiri kuwa alitumia madawa ya kulevya akiwa kijana.

Akiongea na vijana wa NewHampshire alisema kuwa akiwa anasoma shule ya sekondari alitumia unga aina ya Cocaine na pia alivuta bangi. Alisema kipindi hicho hakufanya vizuri shule na ni sababu ya hayo maovu. Anasema kuwa ana majuto na kipindi kile. Anasema alivyoacha alianza kufanya vizuri shuleni mpaka aliweza kusomea sheria chuo kikuu cha Harvard na kuwa mhariri wa Harvard Law Review.

Si mara ya kwanza kusema kuwa alitumia madawa ya kulevya. Akigombea uSenator alisema, na pia kwenye kitabu chake, ' Dreams from my Father, A story or Race and Inheritance' anasema pia.

Obama si mgombea wa kwanza kukiri kuwa walitumia madawa ya kulevya. Rais Bill Clinton alisema kuwa alijaribu kuvuta bangi, na rais Bush wa sasa anasema alikuwa mlevi wa pombe (bado ni mlevi)! Pia kuna watu ambao wanadai kuwa Bush alitumia unga.

Navyoona Obama aliamua kusema alifanya nini akiwa kijana maana kuna watu wangemwumbua. Aliona ni bora aseme mwenyewe kulikoni aonekane kama alijaribu kuficha. Sasa kuna watu ambao wanadai kuwa Obama si mfano mzuri kwa vijana maana wao wataona kuwa ni sawa kutumia madawa ya kulevya maana baadaye wataweza kugombea urais! Haya!

Hapa Marekani, ukiwa mgombea nafasi ya siasaa hasa hizi kubwa kubwa uwe msafi! Maana yangu si msafi wa nguo au mwili. Uwe msafi kabisa na usiwe na kitu cha kuficha. Viongozi wengi wameabikia baada ya kugundulika walikuwa na vimada pembeni au walitembea na malaya! Usiwe umezaa nje ya ndoa yako! Usiwe unatumia madawa ya kulevya au mlevi.

Watu kama Newt Gingrinch, Henry Hyde, Gary Hart, waliaibika baada ya siri zao na kuwa na vimada kugundulika! Na lazima unakumbuka kuwa Rais Clinton karibu avuliwe urais shauri ya kunyonywa ume wake na Monica Lewinsky ofisini kwake!

Kwa habari zaidi someni:

http://www.cnn.com/2007/POLITICS/11/27/costello.drug.use/index.html

http://www.iht.com/articles/2006/10/24/news/dems.php

http://www.washingtonpost.com/wp-dyn/content/article/2007/01/02/AR2007010201359_pf.html


Mtaa wa Bagamoyo

Hii picha nimeona kwa Michuzi. Ni ya barabara mpya huko Bagamoyo. Sasa nauliza hii ni barabara ya matofali ni ya magari au ya waenda kwa mguu? Naona kuna watu wanatembea kwa mguu na nyuma naona gari inakuja. Sasa hii njia itadumu kweli kama ni ya magari? Hebu nyie wahandisi tuambie.

Sasa wakarabati na nyumba basi papendeze.

Monday, November 26, 2007

Chalene









Ama kweli nimeona matako makubwa leo! Huyo dada anataka kuwa Model wa wanene.

Saturday, November 24, 2007

Bi Kidude ana miaka mingapi?

Hivi Bi Kidude ana miaka mingapi? Sasa anadai kuwa ana mika 113. Lakini anasema hajui alizaliwa lini. Mimi nilimwona Zanzibar mwaka 1993 na wakati huo alisema ana miaka 80. Kwa hiyo nahisi kama ana miaka 94.

Aliolewa kwa mara ya kwanza katika miaka ya 1930's. Alikuwa mwanafunzi wa marehemu Siti Binti Saad ambaye alifariki 1950.

Ni Kungwi na mwenyewe kwa mafundisho ya Unyago. Huenda ni kweli wazungu wanavyosema, "sex makes you younger" (yaani ngono inakufanya uwe kijana).

Je, umemwona kwenye show zake. Ngoma zikianza kulia anageuka kijana!

GO BI KIDUDE!

Rappers wamtukana Dr. Jan Adams



Rappers hawana dogo. Wametoa wimbo wa kumtukana Dr. Jan Adams aliyemfanyia mama yake mzazi Kanye West, upasuaji wa urembo na kusababisha kifo chake.

- Dr. Jan Adams alikuwa na TV show kwenye Discovery Channel, Plastic Surgery Before & After
- Alikuwa siyo Board Certified
- Oprah amekaa kimya. Alimwalika kwenye show yake kama mtalaam wa upasuaji wa urembo kumbe jamaa ni feki! Watu wengi waliamini 'utalaamu' wake kwa vile alikuwa kwenye Oprah.

http://www.drjanadams.com/

Cheki website ya jamaa, mambo mengi eti yako "down for maintenance" LOL!

Kinachonisikitisha katika hii kesi ni kuwa huyo jamaa ni mweusi, alikuwa anaonekana kama mtaalamu wa mambo ya plastic surgery. Kumbe jamaa tapeli!

Friday, November 23, 2007

Sofia Productions wataandaa Fimbo ya Mnyonge Awards


Kampuni ya Sofia Productions, inayoshugulika na mambo ya filamu na muziki Tanzania imechaguliwa kuandaa tuzo za filamu Tanzania zitakazoitwa 'Fimbo ya Mnyonge Film Awards 'kutoka Baraza la Sanaa la Taifa. Naona ndo zitakuwa Oscars zetu Tanzania!

Habari hizo zimethibitishwa na meneja mkuu wa Sofia Productions, Bwana Musa Kissoky.

Tuzo hizo wanatarajia kuzifanya mapema mwakani kati ya mwezi March na April.

Kwa kweli fani ya sinema inashamiri siku hizi Tanzania, tunangojea kwa hamu kuona washindi wa Awards!

Producer wa Big Brother Africa II Amefukuzwa Kazi!


LOH! Fall-out ya Big Brother II inaendelea! Producer wa Big Brother II, Bwana Martins Ngubane amefukuzwa kazi kutokana na vituko vilivtyotokea kwenye Big Brother Africa II na kuonyeshwa kwa umati wa waafrika na dunia kwa ujumla! Nawaambia 'Fingergate' haijaisha!

Walisema kuwa Ngubane, alikuwa na sheria za kufuata lakini hakuzifuata! Na bado tutasikia mengine!

Yalioyofanyika ni mazito, japo watu wanaona matendo ya Richard ya kunyanyasa wanawake ni ya kishujaa wengi wanaona sivyo!

****************************************************************************
Nigeria: MNet Sacks BBA Producer

From Allafrica.com

Posted to the web 23 November 2007

Stanley Nkwazema in Abuja

Mulitichoice yesterday confirmed that the producer of the Big Brother Africa (BBA) Programme, Martins Ngubane who produced the show on the day the Nigerian representative in the programme Ofunneka Molokwu was harassed by one of the Housemates has been relieved of his duties.

This followed pressure from the House of Representatives that the Nigerian girl was not adequately protected and the viewers treated with obscene pictures during the period.

The Operations Director of MNET Africa, Mr Joseph Hunda who appeared in the House Committee Room 13 with eight other officials of the company including Ofunneka apologised to Nigerians that there were certain editorial guidelines spelt out for the producers of the programme which were not adhered to and we have relieved the producer of the programme of his job and the superior who was supposed to supervise the day has equally been sanctioned accordingly.

Ngubani apologised to Nigerians "that those things were not supposed to come on anyway and we are sorry that it appeared and we will not allow it again".

He explained to the House of Representatives committee on Information and National Orientation that "we commissioned MNET to come out with something that will project the image of Africa. We agree that there were certain things that were not acceptable to a large part of Nigerians. We had discussions with NBC and agreed that we are going to continuously use parental control on all DSTV channels. Our customers should be able to control their homes. "

Chairman of the Committee Honourable Dino David Melaye who represents Buunu/Kaaba federal constituency of Kogi state told the Multichoice officials that Nigerians were fed with too much pornography during the period the programme lasted. NBC actually invited Multichoice twice but they never honoured the invitation.

"We will not allow our image to be dragged on the floor.Ofunneka projected the image of Nigeria and we are proud of her. We earlier banned clips, preview and full airing of the programme and we want you to apologise to Nigerians over what happened,"

Hundah however explained to the lawmakers that Multichoice has made serious efforts towards encouraging more local content in the programmes while confirming that six local stations, AIT, Channels, Silver Bird, MITV, NTA and Minaj broadcast International are already collaborating with Multichoise to improve on the content. He also disclosed that Hollywood, has not only become a household name in Africa, but acceptable the world over while a new Programme Moments with Mo aired thrice daily and produced in Nigeria is now on the DSTV channels.

Melaye also wants the company to join the Nigerian stock exchange so that Nigerians can buy into the company as they have done in NewYork andJohannesburg where the company's shares are being traded.

He also told Hundah that Nigerians would want his company to go into more serious poverty reduction programmes so that the subscribers could have a sense of belonging that at least the heavy money they are paying is being ploughed back in some way.

Ofuneka Molokwu , the runner up of the 2007 Big brother Africa show who was at the hearing said she is" proud to be a Nigerian and Delta state origin. I thank Multichoice for giving me the opportunity and the Nigerians that kept me on. I take every stride as they come. And am proud to show that am a true Nigerian and African woman"

http://allafrica.com/stories/200711230975.html