Thursday, May 31, 2007

Jeff Koinange afukuzwa kazi CNN


Photo from CNN.com

Leo nimesikia habari za kusikitisha kweli. Jeff Koinange, amefukuzwa kazi CNN. Wanasema kuwa mwanamke aliyemtaka kamfanyia mbaya. Haya. Kweli wamepoteza mwandishi aliyejua Africa, na aliyetoa habari za kuaminika. Ni vizuri kuona mwafrika mweusi anaongelea habari za Africa na siyo mzungu. Kweli wamepata hasara na kama kafukuzwa shauri ya mwanamke ni hasara kwa CNN.
Huyo mwanamke anakataa kuwa yeye ndiye alisababisha afukuzwe. Soma habari zake na e-mail walizokuwa wanatumana hapa:

Monday, May 28, 2007

Flaviana afika Top Ten - Miss Japan ashinda!






Kwanza nampongeza Miss Tanzania, Flaviana, Matata kwa kufika katika Top Ten (kumi bora) ya mashindano ya Miss Universe. Ingawa hakufika katika Top 5 atafika mbali maana mabilioni ya watu wamemwona. Pole zake Miss USA, alianguka jukwaani kwenye evening gown segment.

Nilijua Miss Japan atashinda. Alivyopita na swimsuit yake alivyokuwa anatingisha matako, kwa swing, macho yote yalikuwa kwake. Flaviana alivyovaa ili bikini niliona kama ana aibu fulani, bora angetembea kama anacheza ngoma watu wangemshangilia. Flaviana alijitahidi sana lakini kuna wakati niliona kama alikuwa nervous hasa pale kwenye Evening gown, na hata mwanzo walivyokuwa 77 na alikuwa jukwaani.

Lakini kunyoa kipara kilimsaidia kwa kiasi fulani, ila ingekuwa vigumu ashinde awe Miss universe maana moja wa wadhamini wakuu ni kampuni inayotengeneza manukato ya nywele. Miss Jamaica naye alishindana na nywele za rasta.

Lakini leo jioni waTanzania tuliweza kujivunia si mchezo, maana ni mara ya kwanza kuona Miss Tanzani anafika mbali kiasi hicho katika hayo mashindano. Naomba Flaviana akirudi Tanzania afundishe na atoe ushauri kwa wasichana wengine kuhusu jinsi ya kushiriki katika hayo mashindao na kushinda.

Natumaini Trump Model Agency watampa contract.

Good Luck Flaviana! -

(Miss Tanzania Flaviana Matata akipiga pozi na Miss Italy na Miss Nigeria. Photo from Michuzi Blog)

Msisahau kutazama mashindano ya Miss Universe leo jioni. Flaviana anasifiwa kweli, hasa kwa vile amenyoa kipara na anajiita 'natural African woman'.

Kwa habari na picha zaidi nenda:

http://tv.yahoo.com/miss-universe-2007/show/41744/photos/1

http://www.elpasotimes.com/entertainment/ci_6006480

Saturday, May 26, 2007

Umecheza Slots?


Hivi karibuni nilienda kwenye Casino cha Foxwoods, huko Connecticut na nilicheza na hizo slots. Usipokuwa mwangalifu inakula hela yako. Kama unabahati unarudi na kibunda. Niliona watu wakipata vibunda lakini wanarudishia casino!

Kila mtu na bahati yake lakini!

Bongowood





Katika dunia ya sinema, mfalme na wa kuiga ni Hollywood. Maelfu ya sinema zimetengenezwa na Hollywood tokea miaka ya 1910's. Lakini siku kila kona ya dunia sinema zinatengeneawa. Wahindi wana Bollywood na waNigeria wana Nollywood. Sasa sisi waTanzania tuna Bongowood.

Ndiyo, tuna BONGOWOOD! Sinema zinaanza kutengenezwa kwa wingi Tanzania, na watu wana hamu ya kujifunza namna ya kuzitengeneza. Si muda mrefu iliyopita, enzi Ujamaa utengenezaji sinema ilikuwa si kitu muhimu kwetu. Wakati huo kutenegeza sinema ilikuwa ghali na serikali ya Ujamaa ilikuwa na kazi muhimu kama kuwapatia wananchi maji safi, elimu na huduma ya afya.

Lakini ziku hizi asante 'digital technology' bei ya kutengeneza sinema imeshuka sana.

Kama makao makuu ya Hollywood iko Los Angeles, California USA, ninapendekeza studio kubwa iwe Bagamoyo. Bagamoyo ni penyewe kwa mambo ya usanii. Kuna Chuo cha wasanii huko Bagamoyo, na mambo mengi.

Baadhi ya Sinema za KiTanzania, zilizotengenezwa Tanzania ni:


1. Simu ya Kifo (2007)
2. Tusamehe (2005) http://www.kibirafilms.com/tusamehe
3. Bongoland (2003) http://www.kibirafilms.com/bongoland
4. Maangamizi the Ancient One (2001) http://www.grisgrisfilms.com/html/maangamizi_-the_ancient_one.html
5.Arusi ya Mariamu (1985) http://www.grisgrisfilms.com/html/marriage_of_mariamu.html
6. Mama Tumaini (1987)
7. Mogambo (1953) http://www.imdb.com/title/tt0046085/
8. YombaYomba (1985)
9. Darwin’s Nightmare (2005) http://www.imdb.com/title/tt0424024/
10. Surrender (2000) http://www.newsreel.org/nav/title.asp?tc=CN0132&s
10. These Hands (1992)
11. Gubu la Wifi
12. Four Weeks in Tanzania (2004) http://www.studentfilms.com/film/get.do?id=978
13. These Hands (1992)13. Girlfriend (2004)
14. Fimbo ya Mnyonge (1974)
15. Tumaini -Childhood Robbed (2005) http://www.abantuvisions.com/StoryPage.php?StoryID=3

Thursday, May 24, 2007

Postcard from Bagamoyo


Nimeona hii POSTCARD ya Bagamoyo Beach, kwenye neti.

Kuna picha zingine hapa: http://www.rlw-photography.com/blog/category/contests/

Mshindi wa American Idol 6 ni Jordin


Natoa pongezi kwa Jordin Sparks aliyeshinda American Idol 6 jana. Ana miaka 17 tu na anasoma darasa la 11 (Form 3). Ni mshindi mwenye umri mdogo kuliko wote waliowahi kushinda.

Baba yake ni mcheza footbal (American style) mweusi, na mama ya ni mzungu. Huyo Jordin ni mrefu na ana mwili. Alifmfanya Ryan Seacrest aonekane kama pygmy kwake.

Kwa uimbaji, sijamfurahia sana. Ila aliimba vizuri kuliko aliyebaki, Blake, kijana wa kizungu aliyependa kutia ma beatbox kwenye nyimbo zake.

Wenye sauti nzuri Melinda na Lakisha walitolewa wiki kadhaa zilizopita. Wanasema watazamaji wa America Idol walipungua kwa vile show mwak huu haikuwa nzuri. Nsiyohaikuwa nzuri, maana walitoa waliojua kuimba mapema. Wengi walikuwa wanaume weusi. Tungojea January 2008, kuona American Idol y itakuaje.

Tuesday, May 22, 2007

Kama Huoni Blog

Wapendwa wasomaji blog sizifuti. Hapana zinaingia Archives, na kila mtu anaweza kuziona. Kama kuna blog uliyopenda na kwa sasa huoni, uangalie upande wa kushoto wa blog, halafu u-clik kwenye Archives. Kama unakumbuka mwezi ulioiona u-click kwenye mwezi na mwaka. Pia, unaweza kufanya Search hapo juu kwenye upande wa kushoto.

Monday, May 21, 2007

Sinema ya Arusi ya Mariamu


Umewahi kuona sinema iitwayo, ‘Arusi ya Mariamu’? Sinema hiyo ilitengenezwa 1985 nchini Tanzania na Ron Mulvihill na marehemu Nangayoma Ng’oge.

Sinema hiyo ni fupi, dakika 36. Lakini ni hadithi tamu sana. Mariamu (Amadina Lihamba) ana funga ndoa na Sekondo (Godwin Kaduma). Wanapendana sana, lakini Mariamu anaanza kuugua ugonjwa ambao madaktari wanashindwa kumtibu. Sekondo anashauriwa ampeleke kwa mganga wa kienyeji atiibiwe. Huko inakuwa balaa maana kumbe Mariamu ana waoga wa waganga wa kienyeji. Kwani alishuhudia kifo cha baba yake ambaye naye alikuwa mganga wa kienyeji. Alifariki akikusanya mitishamba kwa ajili ya kutibu wagonjwa. Je, Mariamu atapona?

Sinema hiyo inapatikana http://www.grisgrisfilms.com/html/marriage_of_mariamu.html
Ron Mulvihill alirudi Tanzania 1994 kutengeneza sinema ya Maangamizi the Ancient One.

Misuko





Kuna wakati wanawake waafrika walipenda nywele zao walizozaliwa nazo, yaani nywele za kipilipili. Walikuwa wanazisuka kwa mitindo mbalmbali na kuzipamba na vitu kama 'rafia'.

Jamani, mnakumbuka yale mabunda ya rafia yalikuwa yanauzwa bei ya juu pale Kariakoo na hata kuuzwa kwa magendo baada ya 'Miezi 18' kile kipindi baada ya vita vya Kagera. Na ilikuwa mtu akisuka nayao basi ndo anaonekana mtu wa maana. Siku hizi ni weave! Zamani Tanzania walikuwa wanaita wigi, 'nywele ya maiti'. Sasa zinauzwa kila kona.

Kulikuwa na klabu/ saluni maalum za kusuka nywele. UWT (Umoja wa Wanawake Tanzania) nao walikuwa na sehemu zao za kusuka nywele.

Nakumbuka nilivyokuwa nasoma Zanaki, mwanafunzi mwenzangu Margaret Makame, alinisuka mtindo wa mistari, lakini iliyogeuzwa (mfano hapo juu). Walimu walikuja juu, eti nimesuka kizungu! Duh, siku hizi si kitu cha kushangaa.

Friday, May 18, 2007

Mheshimiwa Sumaye akipokea DVD za Bongoland na Tusamehe



Wiki hii nilibahatika kumkabidhi aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania enzi za Rais Mkapa, Mheshimiwa Frederick Sumaye, DVD za sinema ya Tusamehe na Bongoland. Yeye ni jirani yangu hapa Cambridge, Massachusetts. Anasoma Harvard University.

Mheshimiwa Sumaye alifurahi sana kuona DVD hizo na alisema ingekuwa vizuri vijana wote Tanzania wazione kwani zina ujumbe nzito sana.

Katika sinema ya Tusamehe waTanzania waliofanikiwa kimaisha Marekani wanakumbwa na ugonjwa wa UKIMWI, na katika Bongoland, MTanzania anapambana na maisha Marekani.

Sinema hizo zimetengenezwa na mwanafilamu wa kiTanzania aishio huko Minnesota, Josiah Kibira. Kwa habari zaidi za sinema hizo na hata kununua DVD zake, tembelea....
http://www.kibirafilms.com/index.html

Thursday, May 17, 2007

Wasio na Makaratasi wataweza kupumua sasa!

Habari njema kwa wasio na makaratasi Marekani. Kwa haabri zaidi someni:

http://www.cnn.com/2007/POLITICS/05/17/immigration.ap/index.html

Excerpt

The key breakthrough came when negotiators struck a bargain on a so-called "point system" that would for the first time prioritize immigrants' education and skill level over family connections in deciding how to award green cards.

The draft bill "gives a path out of the shadows and toward legal status for those who are currently here" illegally, said Sen. Dianne Feinstein, D-California.
The immigration issue also divides both parties in the House, which isn't expected to act unless the Senate passes a bill first.


The proposed agreement would allow illegal immigrants to come forward and obtain a "Z visa" and -- after paying fees and a $5,000 fine -- ultimately get on track for permanent residency, which could take between eight and 13 years. Heads of household would have to return to their home countries first.

Jua lachomoza

Photo from http://www.abantuvisions.com/PictureGallery.php

Jua lachomoza eh kijana we
Jua lachomoza eh kimbia kimbia x2

Ikiwa wewe kuruta
-Kimbia Kimbia

Ikiwa wewe afande
-Kimbia Kimbia

Mchakamchaka
-CHINJA!

Mchakamchaka
-CHINJA

Aliyesema
-Alia
Aliyesema
- Alia

Jua lile literemke mama!
Ai ai ai ai ai Mama!

Mchakamchaka
-CHINJA

Kwa Heri Melinda! American Idol IMEOZA!

American Idol imepoteza watazamaji wengi baada ya kutolewa kwa Melinda Doolittle (29) jana.
Waliobaki sasa ni kijana wa kizungu Blake na shombe Jordin. Blake sijapenda staili yake maana anaimba huko anafanya ma beat box, halafu Jordin basi tu ndo wiki hizi za mwaisho ndo kajitahidi sana lakini sijaona kama anasthahili kushinda.

Nimechukia sana kwa sababu hakuna wiki tangu walivyoanza kuonyesha msimu huu kuwa Melinda alikosea wimbo. Ana sauti nzuri ajabu na majaji wote walikubali hivyo. Yeye kati wa wote waliochaguliwa katika Top 24, ndiye alishahili kushinda.

Lakini mshndi anachaguliwa na watazamaji. Na tunajua kuwa bado kuna ubaguzi Marekani. Ukiingia kwenye bodi ya American Idol utaona wanavyotukana waimbaji weusi. Insikitisha kweli kweli.

Haya tuone nani atashinda wiki ijayo, lakini mimi sitazami. Nitaona matokeo kwenye taarifa ya habari. Kwa nini nipoteze muda kuangalia watu wasiostahili kuwa Idol wawe pale? No nitangalia Sopranos reruns! Huenda Tony ataweza kuwawahack hao producers wa show!

Msimu wa sita wa American Idol umeoza kweli kweli.

For the benefit of non Swahili speaking readers, I say that American Idol is rotten and stinks! Is it a talent contest or a popularity contest?

Tuesday, May 15, 2007

Aftershock: Beyond the Civil War

Hii ni trailer ya sinema ya Aftershock. Ilionyeshwa kwenye History Channel mwanzoni mwa mwaka huu mara kadhaa. Mimi niliigiza kama mtumwa aliyeachiwa huru, lakini nilijikuta bado niko utumwani pamoja na watumwa wengine. Sinema inahusu kipindi mara baada ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, miaka ya 1865.

http://store.aetv.com/html/product/index.jhtml?id=77017

Asante Sana Wana Mahusiano.com!


Ninatoa shukrani zangu kwa wana mahusiano.com kwa muziki walioposti kwenye site yao. Site hiyo ilianzishwa na bwana Christopher Makwaia.

Yaani wana nyimbo kibao za nyumbani. Kuna nyimbo za Bongo Flava, Taarab, Zilipendwa, Nyimbo za Injili na Bongo Dance! Lazima utafurahia!

Watembelee www.mahusiano.com mfaidi muziki wa homu!

Saturday, May 12, 2007

Mrs. South America/ Miss Guyana wa Zamani ni Muuaji?



Anayeshika taji la Mrs. South America kwa sasa, Bibi Carolan Lynch anashikiliwa na polisi huko Guyana kwa shutuma la kumwua mume wake.

Mume wake, mfanyabiashara maarufu wa Guyana, Farouk Razac, alikutwa amekufa kwenye chumba chao cha kulala. Ama kweli duniani kuna mambo!
Kwa habari zaidi soma:

Miss Universe 2007 - Je, atakuwa Flaviana Matata wa Tanzania?




Kwa kweli mwaka huu nangojea kwa hamu siku ya May 28th. Siku hiyo NBC itonyesha Live mashindano ya Miss Universe itakayofanyika huko Mexico City.

Mwakilishi wa Tanzania, Flaviana Matata yumo. Kwa kweli weusi kutoka nchi zingine wana weave na wigi kichwani, lakini yeye kanyoa upara! Kama vile kusema, napenda uafrika wangu! Naomba afike mbali katika hayo mashindano.

Na hata kama hata pita msishangae mkisikia kuwa amepata modelling contract, au yuko kwenye matangazo ya magazeti na TV. Sasa hivi hao models weusi wa kiafrika ni mali kweli hapa. Washukuru akini Alek Wek, na Iman kwa kupendwa waafrika katika u-model hapa USA. Zamani ilikuwa model mweusi lazima awe mweupe karibia ya mzungu na awe na nywele ndefu!

Black Beauty juu! Waafrika tujipende!

Friday, May 11, 2007

Wanamlaumu Rubani - Kuanguka kwa Kenya Airways Flight 507


Bado uchunguzi unafanywa kuhusu kuanguka kwa ndege ya Kenya Airways huko Cameroon. Kwa sasa wanamlaumu Rubani hiyo, marehemu Capt. Francis Mbatia Wamwea. Wanasema huenda aliamua kuondoka kwa vile ilibidi abiria wawahi connections Nairobi. Marubani wa ndege zingine mbili zilizokuwa pale uwanjani wa Air Moroc, na Cameroon Airlines waliamua kusubiri.

Mimi sikuwepo lakini huenda aliamini kuwa kwa vile hiyo ndege ni ya kisasa kama wanavyoisifia 'Ultra-Modern' haiwezi kuanguka. Tusisahau kuwa meli ya Titanic ilizama 1912 wakati walisema haiwezi kuzama kwa vile ilikuwa 'Ultra-Modern' kwa wakati huo. Lakini siku yako ya kufa ikifika, imefika! Hakuna cha Ultra-modern wala nini. Kila ukipanda ndege au hata kuingia kwenye gari lako ni kuomba ufike salama.

Lakini bado hawajapata Black Box ya Cockpit ambayo itatoa habari zote na maneno ya hao rubani. Maskini ya Mungu msaidizi wake, Andrew Kiuru, alikuwa ana miaka 23 tu. Alikuwa amemaliza kusoma urubani Afrika Kusini mwaka jana.

Habari zinasikitisha kweli. Moja ya abiria waliokufa alikuwa Mtaalam wa UKIMWI, Dr. Albert Henn, wa Harvard University.

Kwa habari zaidi soma:

http://seattlepi.nwsource.com/local/6420AP_Cameroon_Planes_Last_Moments.html

http://allafrica.com/stories/200705110439.html

Thursday, May 10, 2007

Kwa Heri Lakisha!


Jana kwenye American Idol, Lakisha Jones alitolewa kwenye mashindano. Kwanza nashukuru kuwa aliweza kufika mpaka kuwa namba 4! Nilikuwa na wasiwasi angetolewa mapema maana wtau walikuwa wanamwita 'Fantasia Part 2' kwa vile ana mtoto. Na kwa kweli sikufurahi kuona Simon Cowell anampiga busu kwenye mdomo wiki iliyopita. Nilijua wazungu watachukia kuona hivyo. Wengi hawajui kuwa mchumba wa Simon Cowell ni mweusi.

Watu wanasema kuwa Show siyo nzuri mwaka huu, kwa vile waimbaji wengi hawana sauti za kuvutia mno kama za mastaa. Nalaumu majaji wa American Idol kwa sababu kulikuwa na waimbaji wzuri lakini hawakuchaguliwa. Kulikuwa na vijana wengi wa kiume wenye sauti za ajabu, lakini hata hatukuwaona kwenye finals! Badala yake walichagua wahuni kama yule malaya Antonella, na Sanjaya asiyeweza kuimba kusudi ratings ziwe juu. Watu wamechukia na ratings zimeshuka! Wameahidi mwaka kesho watakarabati jinsi wanavyochaga waimbaji.
Kwa kweli Lakisha ana suaiti nzuri, anaweza kushindana na Jennifer Hudson. Nina imani kuwa atenda mbali. Tutasikia ana contract hivi karibuni.

Bado wiki mbili za mashindano. Je, mshindi atakuwa Blake, Melinda au Jordin?

Ningependa kuona Melinda akishinda. Kwa kweli ana sauti nzuri mno na hakuna wiki aliimba vibaya.

Wednesday, May 09, 2007

Mpakanjia sasa yuko Hoi!

Duh, ni majuto, maneno ya watu, mapenzi, au nini kinachomsumbua Bwana Mpakanjia?
Hivi majuzi kampa mke wake, Mheshimiwa Amina Chifupa, talaka na leo tunasikia yuko hoi kitandani! Mungu ampe nguvu maana mambo ya ndani yakianikwa hadharani yanaweza kuleta presha!



********************************************

From: http://www.ippmedia.com/ipp/alasiri/2007/05/09/90143.html



Mumewe Amina hoi!



2007-05-09 Na Badru Kimwaga, Jijini

Siku chache tu baada ya `kumlima` talaka mkewe kwa tuhuma za kutokuwa muaminifu, katika ndoa, mfanyabiashara maarufu nchini, Bwana Mohammed Mpakanjia almaarufu kama `Meddy` imedaiwa kuwa hivi sasa yuko hoi bin taaban kitandani.


Akizungumza na Alasiri kwa njia ya simu mapema leo asubuhi, mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mkandarasi wa kutengeneza barabara, amesema hivi sasa yu hoi kitandani kutokana na kusumbuliwa na maradhi ambayo hakuweza kuyafichua.

Rest in Peace JWTZ Captain Leticia Oswald


Afisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania, Kepiteni Leticia Oswald (pichani), ni mmoja ya abiria waliokufa katika ajali ya ndege ya Kenya Airways, iliyoanguka huko Cameroon, usiku wa kuamkia Jumamosi 5/5/07. Alipandia ndege Abidjan.


Kepiteni Oswald alikuwa Ivory Coast kwenye shughuli za kulinda amani (UN Peacekeeping Force). Alikuwa anakuja Dar es Salaam kwenye likizo.


Mungu amlaze mahali pema mbinguni. Amen.


Pia naomba Mungu ampe nguvu, mume wake, Keptieni John Jumla, katika kipindi hiki kigumu. Habari zinasema kuwa Kepiteni Kumla alienda Uwanja wa Ndege Dar es Salaam kumpokea mke wake. Ndege ya Kenya Airways ilitua salama, lakini mke wake hakuwemo katika abiria walioshuka. Ndipo kwenda kuulizia akambiwa kuwa alikuwa abiria kwenye hiyo ndege iliyoanguka Cameroon.

Habari kutoka kwenye gazeti la Daily News Tanzania, inasema kuwa Kepiteni Jumla amekwenda huko Cameroon, kujaribu kutambua maiti ya marehemu mke wake.
Kwa habari zaidi soma:

Tuesday, May 08, 2007

Pole sana Mheshimiwa Dada Amina Chifupa






Natoa pole, tena pole sana kwa Dada Amina Chifupa (Mbunge Viti Maalum). Miaka mingi nimekuwa nikifuatilia habari zake. Lakini hii miaka ya ya karibuni maisha yake yameanikwa hadharani na kushabikiwa kama vile maisha ya hao stars wa Hollywood. Yaani maisha yake imekuwa kama Tanzanian Soap Opera. Ni kama vile papparazzi wanavyofuatilia maisha ya Paris Hilton hapa Marekani..oh sijui kavaa hivi, katembea na huyo, alionekana sijui wapi! Khaa! Na inaelekea watu hawatosheki na habari wanazaopata kuhusu Dada Amina, wanataka zaidi na zaidi.

Kwa kweli tangu jana nilisikitika sana nilivyosikia kuwa mume wake kampa TALAKA! Nilidhania wana ndoa safi sana. Lakini tena ndoa yao naona imekuwa kama hizi ndoa za Hollywood, hazidumu!

Nampongeza Baba yake Luteni Chifupa kwa kuzuia Amina kufanya Press Conference kuhusu yaliompata. Ni mapema mno. Ngojea apoe kidogo maana lazima atakuwa ameshutuka mno, anaweza kuwa na hasira na kusema maneno ya ajabu na baadaye kujuta.

Sijui kama habari nilizosikia juu ya kisa cha Dada Amina kuachika ni kweli. Lakini kama ni ya kweli basi ni aibu kwa huyo mwanaume. Je, alishindwa kumtosheleza mke wake kwenye mambo ya unyumba? Hatimaye ukweli utajulikana.
Dada Amina, kumbuka kuwa watu watasema na mwisho watachoka! Nyayua kichwa juu ukitembea barabarani wala usijali maneno ya watu. Unajua maisha yako mwenyewe. Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu. Pia wanaume wako wengi katika dunia hii, na dunia ya leo si lazima uwe na mwanaume. Wakati mwingine mwanaume ni mzigo na mzuia maendeleo ya mwanamke. Samahani nimeingiza 'women's lib' hapa!

Na ambaye anatarajia kuolewa na huyo Bwana Mpakanija ajue kuwa atamtendea kama alivyomtendea Dada Amina. Kwa bahati mbaya ndivyo wanaume walivyo...wakimtendea mwanamke moja hivi na mwingine atatendewa vile vile.
Pamoja na kuwa nimemsema Bwana Mpakanija natoa pole kwake maana ni hatua kubwa aliyochukua na maisha yake pia yameanikwa hadharani. Jamani, mbona mlivyofunga ndoa mlionekana mna mapenzi mno.

Karibuni mtoe maoni.
Kwa habari zaidi ya Mheshimiwa Dada Amina Chifupa someni:
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=2787

Sinema ya Tusamehe

Hii ni trailer ya sinema ya Tusamehe.

Kwa habari zaidi ya sinema ya Tusamehe tembelea:

http://www.imdb.com/title/tt0480032/


http://www.kibirafilms.com/tusamehe/

Monday, May 07, 2007

SPIDERMAN




SINEMA YA SPIDERMAN 3, imevunja rekodi kwenye Box Office ya Marekani. Imeingiza dola $104 milioni kwenye premiere yake. Lazima wahisani wanafurahia! Je, Tobey Maguire (aliyeigiza kama Spiderman) atapata percentage?

Kwa habari zaidi ya spiderman 3 nenda http://www.imdb.com/title/tt0837564/
Cheki Spiderman mwenyewe anayofurahia!


Ajali ya Ndege ya Kenya Airways














Photos from:
Usiku wa kuamkia jumamosi May 5, 2007, ndege ya Kenya Airways ilianguka huko Cameroon, mara tu baada ya kutake-off kwenye uwanja wa ndege ya mji mkuu wa nchi hiyo Douala. Lakini ilichukua masaa 40 kuona ndege ilianguka wapi. Ajabu zaidi, huko Cameroon sijui hawakujua ndege imeanguka. Watu walienda kwenye airport Nairobi na ndege haikuonekana! Ilikuwa itue Nairobi saa 12 asubuhi. Kwneye hiyo ndege kulikuwa na abiria 115 kutoka nchi 23 na mmoja alikuwa MTanzania.

Hapa kazini kwangu wazungu wanasema, ehe mnaona huko Africa ni Bush/Jungle mpaka wanashindwa kujua ndege imanguka wapi. Japo comments inchukiza lakini ni kweli kwa nini ilichukuwa muda wote huo kuona mabaki ya hiyo ndege. Na kama mtu aliponea, huenda alikufa akingojea waokozi! Africa ina sifa mbaya sana kwenye suala ya usafiri wa ndege.

Hata hivyo, nimesisitiza kwa hao wazungu kuwa Kenya Airways ni airline nzuri hawatumii zile ndege za kirusi za zamani, bali wanatumia ndege za kisasa. Hata hiyo ndege iuliyoanguka ilikuwa mpya maana ilikuwa na miezi sita tu.

Na tusisahau kuwa miaka sita iliyopita ndege ya Kenya Airways, ilianguka huko Abidjan, Ivory Coast. Katika ajali hiyo watu kumi kati ya 169, waliponea.

Kwenye hii ajali nchi za France, South Africa, Kenya na Marekani walituma watu kwenda kusaidia kutafuta mabaki ya hiyo ndege. Jamani, Cameroon enyewe imeshindwa kuona ndege iliyoanguka kilomita 20 kutoka mji mkuu wao. DOH!

Na kwa sababu ya joto, maiti na mabaki ya abiria waliokuwemo kwenye hiyo ndege zimeanza kuoza. Wanasema kuwa hata wakipata maiti ambayo ni nzima, wakinyanyua inadondoka vipande!

MUNGU AWALAZE MAHALI PEMA MBINGHUNI. AMEN/AMIN.

Kwa wanaotafuta habari zaidi:

Kenya Airways advised relatives seeking information to call +271 12071100, which is an international line, and 3200353, 3200354, 3274349.
Stories zinazohusiana na hii ajali:

http://allafrica.com/stories/200705070649.html
Majina ya Crew ya Ndege hiyo:
• Wamwea Francis Mbatia - Captain • Wanyoike Andrew Kiuru - First Officer • Kiiru Phylis Njeri - Flight Purser • Njoroge Allan Njenga - Flight Attendant • Nyakweba Lydia Mocheche - Flight Attendant • Ong’ondo Elizabeth Achieng - Flight Attendant • Wakhu Shantaben Niriza - Flight Attendant • Kadurenge Cyprian Mande - Flight Attendant • Kisilu William Muia - Flight Engineer

Sinema ya Simu ya Kifo


(Pic 1) Mwongozaji Hammie Rajab, akipungia Camera.
(Pic 2) Ganda la DVD la Simu ya Kifo
(Pic 3) Baadhi ya walioigiza katika sinema la Simu ya Kifo
All Photos courtesy of Michuzi Blog.



Wikiendi hii sinema mpya ya Bongo iitwayo, Simu ya Kifo, ilizinduliwa. Premiere ilikuwa katika ile kumbi maarufu la wasanii, The Little Theatre, pale Oyster Bay.

Kwa vile siko Bongo, bado sijauona. Lakini nasikia ilikuwa nzuri na watengenezaji wamejitahidi sana kusudi iwe sinema na si video. Hongera sana.

Wengi tunafahamu kile kitabu cha Simu ya Kifo, na hii ndo sinema yake. Nitapenda kuona kama sinema ni nzuri kama kitabu. Mara nyingi inakuwa vigumu kwa sinema kushinda kitabu maana kwenye kitabu wanaelezea kwa undnani zaidi na mambo mengi zaidi.
Mlioiona naomba maoni yenu.
Kama hamfahamu zamani Little Theatre ilikuwa 'Exclusive' kwa ajili ya wazungu. Waafrika walikuwa wafanyakazi tu pale. Hata bei ya tiketi waliweka juu kusudi waafrika washindwe kununua. Kulikuwa na sisters, Erica Khuri na Tony Khuri (wote marehemu) walikuwa wanaandaa michezo mara kwa mara pale. Nafurahi kuona weusi kwenye Stage hiyo.


Saturday, May 05, 2007

Ndege ya Kenya Airways imeanguka huko Cameroon!




Ndugu wa abiria huko Kenyatta Aiport Nairobi.



Kuna habari kuwa ndege ya Kenya Airways enye abiria 115, imeanguka huko Cameroon. Ilikuwa inatoka Ivory Coast (Cote d'Ivoire) kwenda Nairobi lakini ilipitia Cameroon kuchukua abiria wengine. Mungu awalaze marehemu wote mahali pema mbinguni. AMEN/AMIN.

****************************

NAIROBI, Kenya (AP) -- Kenya Airways has lost contact with a commercial airliner carrying more than 100 passengers that took off from Cameroon early Saturday, the airline said.

"The last message was received in Douala after takeoff and thereafter the tower was unable to contact the plane," Kenya Airways CEO Titus Naikuni said Saturday.

The Boeing 737-800 was carrying 106 passengers, eight crew members and a flight engineer, he said. The plane is capable of carrying 189 passengers.

"We have no details about what has happened to the aircraft," Naikuni said.The flight departed Douala at 12:05 a.m. and was to arrive in Nairobi at 6:15 a.m. The flight originated in Ivory Coast but stopped in Cameroon to pick up more passengers, the airline said.

The airline opened a crisis management center near the airport. Relatives of those on the plane were instructed to go to a downtown airport, where they would be provided information as it became available.

The last crash of an international Kenya Airways flight was on Jan. 30, 2000, when Flight 431 was taking off from Abidjian, Ivory Coast, on its way to Nairobi. Investigators blamed a faulty alarm and pilot error for that crash, which killed 169 people.

Thursday, May 03, 2007

Barack Obama yuko chini ya ulinzi wa Secret Service


Mgombea wa raisi wa Marekani katika uchaguzi ujao, Senator Barack Obama wa Illinois, amewekwa chini ya ulinzi ya Secret Service. Kazi ya Secret Service ni kulinda watu wazito katika serikali ya Marekani kama Raisi na familia yake na makamu wake, na pia wagombea raisi lakini walioteuliwa na vyama vyao.

Obama bado hajateuliwa, hivyo ina maana kuwa lazima Secret Service wamepata habari kuwa maisha yake iko hatarini. Kama tunavyojua Obama ni mweusi na bado kuna wabaguzi hapa Marekani amabao wasingependa kuona mtu mweusi anashika uraisi. Ametokea kupendwa na watu wa kila rangi na kuna watu ambao hawafurahii kabisa! Tusisahau viongozi weusi waliouliwa na hao wabaguzi kama Martin Luther King Jr., na Medgar Evers.

Mungu amlinde na abariki Barack Obama!


********************************************************************

Thursday, May 03, 2007


(CNN) Democratic presidential hopeful Barack Obama has been placed under secret service detail, according to a statement from the U.S. Secret Service."Secretary Chertoff has, after consultation with the congressional advisory committee, authorized the United States Secret Service, to protect presidential candidate Senate Barack Obama. "As a matter of procedure, we will not release any details of the deliberations or assessments that led to protection being initiated. For security reasons we will not release the timing, scope or details of any protective operations."

Zanzibar International Film Festival - ZIFF






The Zanzibar International Film Festival (Festival of the Dhow Countries) ZIFF will be held June 29th, to July 8th, 2007 in Zanzibar, Tanzania.
ZIFF ni tamasha inayofanyika kila mwaka huko Zanzibar. Wanaonyesha sinema na pia vikundi mbalimbali vya kisanii na muzuki kutoka nchi mbalimbali zinashiriki katika maonyesho kadhaa. Lasiki hasa ni maonyesho ya sinema zinatoka nchi za mwambao ya bahari ya hindi. Huu ni mwaka wake wa kumi. Mwaka huu wataizindua Dar katika hoteli ya Holiday Inn.