Showing posts with label Father Evaristus Mushi. Show all posts
Showing posts with label Father Evaristus Mushi. Show all posts

Friday, March 29, 2013

Mtuhumiwa wa Mauaji ya Father Evaristus Mushi Akamatwa Zanzibar!

BREAKING NEWS: MTUHUMIWA WA MAUAJI YA PADRI EVALIST MUSHI AKAMATWA ZANZIBAR

Jeshi la polisi linamshikilia Omari Musa Mkame Mkazi wa Mwanakwerekwe Zanziba anaye sadikiwa kuwa ni muuaji wa padre Evalist Mushi. Amekamatwa alasiri hii maeneo ya Kariakoo, Zanzibar.

Ni kwa msaada wa mchoro wa mfano wa muhusika ulioachorwa na FBI.

Suspect in Father Mushi Killing




Tuesday, February 19, 2013

Taarfif ya Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) - Kuwawa kwa Father Mushi

TAARIFA YA JUMUIYA YA MAIMAMU ZANZIBAR (JUMAZA) TAREHE 18/2/2013 KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSIANA NA TUKIO LA KUUWAWA KWA KUPIGWA RISASI PADRI EVARIST MUSHI WA PAROKIA YA KANISA KATOLIKI MJINI UNGUJA

Shukurani njema zote anastahiki Allah Ambaye ametuwezesha kuwa hai tukiwa na afya njema. Tunamuomba Allah atuwafikishe kufanya mema na aujaalie uhai wetu wote uwe kwa ajili ya kumtumikia Yeye katika Dini hii ya Kiislamu. Rehema na amani ya Allah zimwendee kipenzi chetu, mtukufu wa viumbe Mtume Muhammad (Sallallaahu ‘alayhi wasallam), masahaba zake, jamaa zake na wale wote waliomfuata kwa wema mpaka Siku ya Malipo.

Ama baada ya hayo,Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) inachukua fursa hii kutoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari kufuatia tukio la kupigwa risasi na kuuwawa kwa Padri Mushi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mjini jana tarehe 17/2/2012 Beit – El – Ras.

JUMAZA kwa mshtuko mkubwa imepokea kwa masikitiko taarifa ya kuuwawa kwa Padre Mushin na inalaani kwa nguvu zote kitendo hicho cha kiharamia ambacho kinaashiria kuitia doa Zanzibar kisiwa cha amani na ukarimu tokea enzi na enzi. Kufuatia kadhia hii JUMAZA inawataka Wanzanzibari wote wa dini na madhehebu zote kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu na kuendelea kutunza amani na mshikamano tulionao chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa na kutotoa mwanya kwa watu au vikundi ambavyo vina nia mbaya ya kutaka kuleta kutokuelewana kwa wananchi kwa malengo yao binafsi.

Aidha JUMAZA inaungana na kauli iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuliagiza Jeshi la Polisi nchini kufanya uchunguzi wa kina na waharaka ili kubaini nani waliohusika na tukio hili na hatimaye sheria ichukue mkondo wake.

Aidha JUMAZA inaliomba Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa kiuadilifu na usioambatana na shindikizo la mtu au kikundi chochote ili hatimae ukweli halisi ujulikane na bila ya kuwadhuru wasiohusika.

JUMAZA inakemea vikali kauli za baadhi ya vyombo vya habari vinavyonasibisha waislamu na tukio hili na kuvitahadharisha vyombo vya habari ikwemo magazeti na redio hizo kutoanza kutoa taarifa ambazo kwa makusudi zinaweza kupandikiza chuki na uhasama katika jamii na hatimae kuotesha mizizi ya fitna na kupelekea Taifa kuingia kwenye machafuko bali viachiwe vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi wake na kutoa taarifa sahihi. Aidha JUMAZA inaziomba Serikali zote mbili kuwa waamgalifu sana katika kipindi hiki kwa kujizuia kutoa maneno yanayoashiria kuhusisha tukio hili na upande fulani wakati bado uchunguzi unaendelea.

Imesaniwa na:
KATIBU WA JUMAZA
MUHIDDIN ZUBEIR MUHIDDIN.

Sunday, February 17, 2013

Padri Auwawa Zanzibar Akielekea Kanisani Leo!

TAARIFA  KUTOKA JAMII FORUM:

Default Update: Watatu wahojiwa Zanzibar kuhusiana na mauaji ya Padre na Taarifa ya Polisi


17/02/201




Padre Evaristus Mushi


UPDATE/TARIFA MPYA (saa nane u nusu mchana) Taarifa ya Polisi:

Watu watatu wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za mauaji ya Padre Mushi. Tafadhali bofya vipande vya picha zilizopachikwa hapo ili kuvikuza na kusoma taarifa ya Polisi inayoonekana hapo (shukurani kwa Francis Dande).









UPDATE/TAARIFA MPYA (saa saba mchana) Taarifa ya habari Radio One Stereo:

Taarifa ya habari ya Radio One Stereo iliyosomwa saa 7 mchana imeripoti kuwa Padre Mushi aliuawa na watu walipolisimamisha gari la Padre huyo alipokuwa akielekea katika kanisa la Mtakatifu Theresia lililoko eneo la Mtoni, na alipopunguza mwendo ili awasikilize, ndipo alipopigwa risasi kichwani na kusababisha gari alilokuwamo kukosa uelekeo na kuigonga nyumba iliyokuwa jirani. Watu walioshuhudia tukio hilo walimchukua Padre Mushi ili kumwahisha hospitalini katika jitihada za kuokoa uhai wake, lakini alifariki dunia. Waliomwua Padre Mushi bado hawajakamatwa.
-----------------------


Akina mama wakilia kwa uchungu kuomboleza kifo cha ghafla cha kupigwa risasi Padre Evaristus Mushi kilichotokea leo asubuhi muda mfupi kabla ya kuanza Misa ya Jumapili kwenye kanisa la Kigango cha Mtoni, Zanzibar. (Picha na Martin Kabemba via Lukwangule blog)
Taarifa kutoka Zanzibar zikiripotiwa na mwanahabari Donisia Thomas wakati kipindi cha Patapata cha WAPO radio FM kinaendelea, zinasema kuwa Padre Evaristus Mushi wa Kanisa la Parokia ya Minara Miwili huko Zanzibar amepigwa risasi majira ya saa moja asubuhi -na watu wasiofahamika- na kufariki dunia.

Taarifa za kufariki kwake zimethibitishwa na madaktari kutoka hospitalini alikopelekewa katika harakati za kuuokoa uhai wake.


Padre Mushi aliuawa akiwa anashuka kwenye gari lake tayari kuingia Kanisani kwa ajili ya kuendesha misa ya kawaida ya Jumapili katika kanida la Mtoni, mjini St. Joseph. Inaelezwa kuwa gari lisilofahamika lilifika na kufyatua risasi zilizomlenga Padre Mushi sehemu ya kichwani na hivyo kumsababisha majeraha yaliyokuwa yakivuja damu nyingi.


Mwanahabari anasema tukio hilo limezua taharuki kubwa miongoni mwa waumini ambao wamekataa kuahirisha ibada iliyokuwa iendeshwe na Padre huyo na kusema ikiwa kusudio ni kuwaangamiza Wakristo wote, basi na waangamizi wafike Kanisani wawaangamize wakiwa pamoja.


Jeshi la Polisi limeshafika katika eneo la tukio na kuanza uchunguzi.


Wakizungumza kuhusu hilo, raia wamesema hawana imani na Polisi wala Madaktari na hawatarajii jipya zaidi ya ripoti kuwa suala hili ni la uhalifu kwa kuwa tukio kama hili liliwahi kutokea mwishoni mwa mwaka jana kwa Padre Ambrose kupigwa risasi na taarifa zilisema lilikuwa ni tukio la kihalifu na kwamba risasi hazikutumika jambo ambalo halikuwa kweli kwani Padre Ambrose alikutikana na risasi alipohamishiwa katika hospitali ya Taifa, Muhimbili.

Kwa taarifa zaidi, tafadhali fuatilia vyombo mbalimbali vya habari.


Father Mushi Alipokuta mauti yake