Showing posts with label Mvua. Show all posts
Showing posts with label Mvua. Show all posts

Saturday, March 18, 2017

Mbinu Hizi zitakusaidi Kukabiliana na Mvua Jijini Dar es Salaam

Na Jumia Travel Tanzania

Hivi kuna mkazi yeyote wa jiji la Dar es Salaam ambaye ni mgeni wa adha zitokanazo na mvua zinazonyesha? Sidhani kama kuna mtu yeyote hafahamu ya kwamba mvua ikinyesha kutakuwa na foleni zisizokwisha, barabara na mitaa tofauti jijini kujaa maji, mafuriko na matamko kadha wa kadha kutoka kwa viongozi wa serikali kuwataka wananchi wahame mabondeni.

Lakini ni wangapi wametafakari watawezaje kukabiliana na mvua zitakaponyesha? Zipo mbinu nyingi tu ambazo Jumia Travel inakushauri uzizingatie ili kipindi cha mvua nyingi za Dar es Salaam kwako kiwe ni cha kawaida katika mwaka. 


Amka mapema kukabiliana na foleni ili uwahi shughuli zako
Hakuna wakati ambao kunakuwa na foleni kubwa na zisizopungua kwa muda mrefu jijini Dar es Salaam kama kipindi cha mvua! Lakini jambo hili sio la kushangaza kwa sababu kila mwaka hali hii inajirudia. 

Na hiki ni kipindi ambacho mabosi wengi huchukia sana pengine kuliko vipindi vyote vya mwaka maana visingizio vya wafanyakazi wao kuchekelewa kazini kwa sababu ya mvua huwa haviishi. Kwa hiyo unakabiliana vipi na hali hiyo? 

Kwanza kabisa lazima uwe makini katika kuwahi kuamka mapema na pia njia ya usafiri utakayoitumia. Inakubidi kuwahi kuamka mapema sana kama unategemea usafiri wa umma au binafsi. Kwa sababu ukifanya hivyo kama kutakuwa na foleni barabarani basi utaziwahi ukilinganisha na ukichelewa kuingia barabarani. Lakini pia kama unategemea usafiri wa umma, mabasi ya mwendokasi ni mkombozi mkubwa kwenye kipindi hiki. Hivyo kwa maeneo ambayo usafiri huu unapatikana ni vema kuutumia ipasavyo kwa sababu yenyewe hayakai foleni kutokana na kuwa na njia zao pamoja na kupewa kipaumbele.    

Nunua vifaa vya kujikinga na mvua
Kutokana na jiji la Dar es Salaam kuwa na vipindi virefu vya jua na joto kali, imekuwa ni nadra sana kuwakuta wakazi wake wana vifaa vya kujikinga na mvua kama vile mwamvuli, koti, sweta au viatu vya mvua. Inashauriwa kuwa na vifaa hivi nyumbani kwako ili kujikinga ifikapo kipindi cha mvua na sio kuanza kufikiria kununua kwani inawezekana usiwe na bajeti hiyo pindi unapovihitaji. Vifaa hivyo ni muhimu kwani hukukinga na baridi, kutolawana, magonjwa na hata kutunza mavazi yako kutokana na maji ambayo huweza kusababisha kuharibika.
Umakini kwenye chombo chako cha usafiri 
Kwa wenye vyombo vya usafiri wanajua wenyewe ni kadhia gani wanayokumbana nayo ikifika kipindi cha mvua. Kipindi hiki ni jambo la kawaida kukuta magari kadhaa yamezimika au kukwama barabarani kutokana na sababu mbalimbali za kiufundi. Lakini pia barabara nyingi huharibika na kutopitika kabisa hivyo kulazimisha chombo chako kupita ni kujitafutia kuingia gharama zisizohitajika siku za usoni. Kama inawezekana tafuta njia mbadala ya usafiri katika kipindi hiki au pita kwenye njia ambazo una uhakika ni salama kwa chombo chako.

Kuwa makini na vifaa vyako vya umeme
Siyo vifaa vyote vya umeme vimetengenezwa vikiwa na uwezo wa kuzuia maji kutokuingia ndani yake. Licha ya makapuni mbalimbali kuja na teknolojia hiyo lakini unashauriwa kuwa makini sana aidha kwa kuvivika vifaa maalumu vya kuzuia maji au kuvikinga kabisa na maji. Kipindi hiki ndicho ambacho wengi hupatwa na majanga ya kuharibikiwa na simu, kompyuta, radio pamoja na luninga huko majumbani.

Kuwa makini na vyakula utakavyokula
Kama huwa unakuwa makini na aina ya vyakula unavyokula basi kipindi hiki inabidi uwe makini zaidi. Mvua zikinyesha jijini Dar es Salaam ndiyo kipindi ambacho pia kunakuwa na mlipuko wa magonjwa kadha wa kadha kama vile kipindupindu. Inashauriwa kula chakula sehemu ambayo unaiamini na inayozingatia usafi wa hali ya juu au kama inashindikana uwe unabeba chakula unachopika mwenyewe au kutokula kabisa.  

Tumia muda wako kusoma vitabu
Sio watu wote wana utaratibu wa kusoma vitabu kwenye siku zao za kawaida badala yake wanatazama filamu, kusikiliza muziki, kutoka wikendi au kupendelea kutembea. Lakini katika kipindi hiki ambacho mvua zinanyesha, barabara hazipitiki, hali ya hewa ni baridi na sehemu nyingi za starehe au kutembelea zinakosa watu ni vema ukajaribu kusoma vitabu. Amini usiamini kuwa hata kutazama filamu na kusikiliza muziki hufikia mahala vinachosha, hiki kinaweza kikawa ni kipindi kizuri cha kujaribu kitu tofauti, nunua vitabu na usome ili uongeze maarifa. 

Hivyo basi tusiifanye mvua ikawa ni kisingizio cha kutofanya shughuli zingine au majukumu mengine yanayotukabili. Kila kipindi huja na changamoto pamoja na fursa zake, ni vema kupambana nazo na kuzitumia ili kusonga mbele.

Saturday, March 05, 2016

Tahadhari Kuhusu Hali ya Hewa Nchini

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini TMA Dkt.Agness Kijazi (Katikati) akitoa taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016. Kushoto ni Samwel Mbuya ambae ni Meneja Kitengo Kikuu cha Habari TMA Dar es salaam na Kulia ni Dkt.Hamza Kabelwa ambae ni Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Mamla ka ya Hali ya Hewa nchini TMA imewatahadharisha Wananchi pamoja na Taasisi mbalimbali ikiwemo za Uokoaji, kujiandaa juu ya namna ya kukabiriana na athari zinazoweza kujitokeza kutokana na mvua za masika ambazo tayari zimeanza kunyesha hapa nchini.

Mkurugenzi wa mamlaka hiyo Dkt.Agness Kijazi alitoa tahadhari hiyo juzi Jijini Mwanza, wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa Mvua za Masika kwa Kipindi cha kuanzia mwezi Machi hadi mwezi Mei Mwaka huu.

Dkt.Kijazi alisema kuwa mvua za Masika zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza nay a pili ya mwezi machi mwaka huu, katika maeneo ya Ukanda wa Ziwa na kusambaa katika maeneo mengine yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

Alisema Mvua hizo zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi nchini, na kwamba zinaweza kusababisha athari mbalimbali ikiwemo mafuriko hivyo ni vema wananchi pamoja na mamlaka za uokozi zikajiandaa kikamilifu ili kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza.
Mkutano baina ya Wanahabari pamoja na TMA uliofanyika Jijini Mwanza, ambapo TMA ilikuwa ikitoa taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.

Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Wanahabari wakifuatilia taarifa ya Mwelekeo wa hali ya Mvua nchini kwa kipindi cha mwezi machi hadi mwezi Mei, 2016.
Bonyeza HAPA Kutazama Semina Kwa Wanahabari.

Saturday, May 09, 2015

Habari ya Tsumani Tanzania Si ya Kweli

 Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 08 Mei, 2015



TAARIFA KWA UMMA: TAARIFA ZA UWEPO WA TSUNAMI SI ZA KWELI.

Tahadhari ya Tsunami inayosambazwa kwenye mitandao ya Jamii sio ya kweli.
Kumekuwapo na taarifa zinazosambazwa kwa njia ya mtandao wa simu kuhusiana na uwepo wa tsunami kati ya kuanzia saa 1 usiku na saa 3 usiku leo hii siku ya Ijumaa tarehe 8/5/2015.Taarifa hiyo imemtaja Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa na Televisheni ya Taifa (TBC) kutoa tangazo hilo.

Taarifa hizo si za kweli unaombwa umjulishe na mwenzio.

Aidha, Mamlaka inapenda kutoa wito kwa umma kuacha kutoa taarifa za kupotosha katika mitandao ya kijamii.

Imetolewa na:
Kitengo cha Uhusiano
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania

Tuesday, January 29, 2013

Kimbunga Felleng Kutua Afrika Mashariki - Tropical Cyclone Felleng


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF TRANSPORT
TANZANIA METEOROLOGICAL AGENCY

Telegrams:"METEO"DAR ES SALAAM.
Telephone: 255 (0) 22 2460706-8
Telefax: 255 (0) 22 2460735 P.O. BOX 3056
E-mail: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM.
http//www.meteo.go.tz

Our ref: TMA/1622 29th January, 2013

Information to the Public: Heavy Rainfall expected

Information No. 20130129-02

Time of issue(Hour)
EAT 6:00pm

Category:

1:Information  2: Advisory 3:Alert   4:Warning:

Advisory Valid from: Date 30th January, 2013

Valid to:Date 1st February, 2013

Phenomena/Hazard/Disaster Heavy rainfall (above 50 mm in 24hrs)

Level of Confidence: Medium

Expected affected Areas :

Some areas of Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Morogoro, Lindi, Pwani, Mtwara regions and neighboring areas.

Text:

Existence of Tropical cyclone “FELLENG” over the North-eastof Madagascar which pulls moisture-rich air from Congo through above mentioned areas.

Advisory:

Residents of high-risk areas, users of land and sea; and Disaster management institutions are advised to take necessary precaution

Remarks: Updates regarding the mentioned Tropical cyclone will be issued when necessary

ISSUED BY TANZANIA METEOROLOGICAL AGENCY   *****************************************

Taarifa kwa umma: Uwezekano wa matukio ya mvua kubwa

Taarifa Na. 20130129-02

Muda wa Kutolewa Saa za Afrika Mashariki Saa 12:00 Jioni

Daraja la Taarifa:

1:Taarifa 2:Ushauri 3:Tahadhari 4:Tahadhari Kubwa:

Ushauri

Kuanzia:

Tarehe 30 Januari, 2013 Mpaka: Tarehe  01 Februari, 2013

Aina ya Tukio Linalotarajiwa

Mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kilasiku)

Kiwango cha uhakika: Wastani

Maeneo yatakayoathirika Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe,Ruvuma, Morogoro, Lindi, Pwani, Mtwara na maeneo jirani na mikoa hiyo.

Maelezo:

Kuwepo kwa kimbunga “FELLENG” kaskazini-mashariki mwa,Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu.kutoka Congo kupitia maeneo tajwa hapo juu.

Angalizo:

Wakazi wa maeneo hatarishi, watumiaji wa Bahari na nchi kavuwanashauriwa kuchukua tahadhari. Aidha taasisi zinazohusika na Maafa zinashauriwa kuchukua hatua stahiki.

Maelezo ya Ziada

Mamlaka inaendelea kufuatilia mwenendo wa kimbunga hicho,na kutoa mrejeo (updates) kila itakapobidi.

IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA