Showing posts with label Mwenge. Show all posts
Showing posts with label Mwenge. Show all posts

Saturday, September 17, 2016

Mwenge wa Uhuru Wawasili Mkoani Singida na Ishara ya Uhuru wa Tanganyika

MWENGE wa Uhuru baada ya kuwasili mkoani Singida Mwenge huu ni ni kitu mfano wa kikombe chenye mpini mrefu na utambi ambacho aghalabu huwasha na kukimbizwa katika kusheherekea au kutukuza tukio fulani
Askari wa Jeshi la Polisi wakiulinda Mwenge ishara ya kuwasili muda mfupi kabla ya kukabidhi kwa uongozi wa Mkoa wa Singida

Kushoto ni Katibu tawala wa Mkoa wa Singida Dkt Angelina M. Lutambi akimkabidhi Mwenge Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Mhe Geofrey Mwambe tayari kwa ajili ya kumulika Miradi 18 katika Wilaya hiyo

Saturday, August 09, 2014

Kibonde wa Clouds FM Akamatwa na Polisi Leo

Ni mara chache sisi waandishi wa habari, tunakuwa habari!

********************************
 Habari na picha kutoka FACEBOOK:

Askari wa Trafiki Akimkamata Ephraim Kibonde

Ephraim Kibonde ndani ya Lock Up


Mtangazaji Mahiri wa Redio 88.5 Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi, Ephrahim Kibonde akipingana na Askari wa Usalama barabarani wakati alipotakiwa kutii sheria bila shurti,mapema asubuhi hii jijini Dar es salaam.

Kibonde anadaiwa kusababisha ajali asubuhi hii eneo la Makumbusho, ikiwa gari aliyokuwa akiendesha kuigonga gari ya dereva mwingine kwa nyuma. Trafiki walifika eneo la tukio na kupima ajali, Kibonde alipoona hivyo akarudi nyuma na kuendesha gari lake kuondoka eneo la tukio bila kufuata taratibu za usalama barabarani,hali iliyomlazimu yule Trafiki katumia gari lililogongwa kumfukuzia.

Walifanikiwa kumkamata eneo la Mwenge na Trafiki aliingia katika gari lake na kumwomba arudi eneo la ajali ili wakapime na kuchora mchoro wa ajali. Kibonde aligoma na kumtaka trafiki ashuke katika gari lake,Trafiki naye hakutana kufanyi kwa maana ya kuwa aligoma kushuka na kumuamuru Kibonde arudi eneo la tukio.

Kibonde aliondoa gari na kuendelea na safari yake huku yule Trafiki akiwa ndani ya gari hiyo, Trafiki aliwasiliana na wenzake ambao walianza kuifuatilia gari hiyo ya Kibonde kama walivyopewa maelekezo na mwenzao aliopo ndani ya Gari hiyo.

Mara Kibonde akatokea maeneo ya mataa ya Ubungo, hapo kulikuwa na Trafiki mwingine aliyekua eneo hilo akaipiga mkono gari ya Kibonde na ambapo inasemekekana hakusimama na badala yake ikaja gari nyingine na kuichomekea kwa mbele na hapo ndipo alipotiwa mbaroni! Aligoma kuendesha gari ikabidi livutwe hadi polisi Urafiki na yeye kuwekwa chini ya ulinzi na baadae akahamishiwa Kituo cha Oystabay ambako yupo mpaka sasa.

Inadaiwa kuwa Kibonde alikuwa amelewa sana,hali iliyopelekea kufanya hayo yote ikiwa ni pamoja na kuwajibu vibaya Askari hao.

Friday, July 26, 2013

Onyo Kwa Wanapoenda Kusuka Mwenge

Nimetoa hii onyo Facebook. Sijui kama kuna ukweli ndani yake lakini miaka ya 1980's kitu kama kii ilitokea Manzese.


Monday, December 22, 2008

Shujaa wa Taifa - Major Alex Nyirenda Afariki Dunia


Kutoka Michuzi Blog:

MAJOR ALEX GWEBE NYIRENDA, SHUJAA ALIYEPANDISHA MWENGE WA UHURU JUU YA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO SIKU YA MKESHA WA UHURU WA TANZANIA BARA, HATUNAYE TENA.

HABARI ZILIZOINGIA SASA HIVI TOKA KWA FAMILI YAKE ZINASEMA MAJOR NYIRENDA ALIFARIKI JANA SAA MOJA JIONI KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOLAZWA. ALIKUWA NA UMRI WA MIAKA 72.

ALIKUWA AKISUMBULIWA NA MARADHI YA KANSA KWA MUDA MREFU NA AMESHAKWENDA MARA KADHAA NCHINI INDIA KWA MATIBABU.

KWA MUJIBU WA HABARI HIZO ZA KIFAMILIA, MAZISHI YATAFANYIKA DAR JUMATANO KATIKAMAKABURI YA KINONDONI. MSIBA UKO NYUMBANI KWA MAREHEMU MBEZI BEACH, FLETI ZA NATIONAL MILLING, KUCHEPUKA NJIA YA KWENDA AFRICANA, DAR.

GLOBU YA JAMII INATOA RAMBIRAMBI KWA FAMILIA, NDUGU, JAMAA NA RAFIKI WA MAJOR NYIRENDA AMBAYE ATAKUMBUKWA DAIMA KWA HISTORIA ALIYOIWEKA SIKU YA MKESHA WA KUPATA UHURU DESEMBA 9, 1961.

SOMA MAHOJIANO ALIYOFANYA NA BONGO CELEBRITY HIVI KARIBUNI KWA KUBOFYA HAPA:
************************************************************
Wadau,
Mnakumbuka ule wimbo wa halaiki, maneno sikumbuki vizuri hivyo naomba mnisahishe:
Sisi tumeuwasha Mwenge
na kuiweka Mlima Kilimanjaro
Kuwasha Mwenge
Kuwasha Mwenge

Na kuiweka Kilimanjaro

Wednesday, September 24, 2008

Bongoland itaonyeshwa Dar (Mwenge)


Kutoka Kibira Films:


Haya wadau mlioko Bongo, tunawajulisha kuwa sinema ya Bongoland (Original) stelingi wake ni Mukama (Jimmy Morandi) itaonyeshwa Bongo mwezi ujao hapo mjini Dar katika tamasha la filamu za Ulaya. (European Film Festival 2008) Shoo itakuwa katika ukumbi wa sinema wa New World Cinema katika kitongoji cha Mwenge.

Bongoland itaonyeshwa siku ya Jumamosi Ocktoba 18 saa nane kasoro robo. (14.45). Kwa habari zaidi wasiliana na British Council hapo mjini Dar au piga simu namba 0755-481374

Kama unavyokumbuka sinema hii ni ya hadithi ya kijana Juma Pondamali aliyekuwa anaishi ughaibuni. Baada ya kupatwa na mizengwe mingi na milolongo ya kazi, ubaguzi na shida nyingi tu..akaanza kujiuliza ni kwa nini aendelee kuumia? Je angekuwa Bongo kweli hali ingekuwa hivi? Marafiki zake walimshauri kuvumilia na hadithi hii inamwonesha Juma akikabiliwa na swala la uamuzi ...ataendelea kuumia mpaka lini?

Kwa habari zaidi kuhusu sinema hii BOFYA HAPA

Kwa kuona trela ya sinema hii BOFYA HAPA

Kwa habari zaidi za Kibira Films International BOFYA HAPA


Mipango ya kileta Bongoland II iko mbioni...kwa sasa BONGOLAND II itaonyeshwa Scotland mwezi huu wa Oktoba mwishoni. Habari zaidi BOFYA HAPA