Showing posts with label Maggid Mjengwa. Show all posts
Showing posts with label Maggid Mjengwa. Show all posts

Tuesday, August 26, 2014

Facebook ya Zitto Kabwe imekuwa Hacked!

Kutoka kwa Maggid Mjengwa - Facebook

*******************************

TAHADHARI: KUNA MTU AMEHACK FACEBOOK ACCOUNT YA ZITTO KABWE

Muda mchache uliopita nimepokea ujumbe kwa anayejifanya Zitto Kabwe ( Impersonate) unaosomeka hapo chini ambao niliutilia mashaka kutoka sentesi ya kwanza. Usome....

"Habari, samahani kwa ujumbe huu endapo kama utakukera ila napenda kukurekebisha lengo kukuweka sawa na kukuepusha katika matatizo. Kuna taarifa umepost katika group ya facebook view timeline kupitia link hii hapa www.facebook-view-timeline.wapka.mobi kiukweli sio taarifa nzuri inaleta uchochez wa vita ya kidini,siasa na mfarakano wa ubaguzi kua makini nimepata taarifa jesh la polisi wanafatilia hz ripot na wapo ktk msako wa kukutafta ili utoe maelezo yakina. Nimezipa hzo hapa www.facebook-view-timeline.wapka.mobi mtu akilogin hapo akiingza email na password anaona yote. Kua makini"

Wednesday, September 25, 2013

Al Shaabab ni Nani?



Al Shaabab Ni Nani? ( Makala Raia Mwema)

Na Maggid Mjengwa,

ULIMWENGU umepatwa na mshtuko mkubwa kwa kuona picha za tukio kubwa la kigaidi kwenye moja ya maduka makubwa jijini Nairobi. Hili ni shambulio kubwa la kigaidi kupata kutokea Afrika Mashariki tangu lile la mwaka 1998. Na ajabu ya kihitoria ni kuwa matukio mengi ya kigaidi yametokea katika mwezi wa Septemba.

La Nairobi ni shambulizi la kigaidi la kulaaniwa vikali na wapenda amani wote ulimwenguni. Hata hivyo, moja ya tafsiri ya vitendo vya kigaidi tunavyovishuhudia Nairobi ni kuwepo kwa hali ya vita vya kigaidi vyenye kuendeshwa kwenye maeneo ya mijini (Urban terrorism).

Ni shambulizi lenye athari mbaya kiuchumi si tu kwa nchi ya Kenya, bali hata majirani zake ikiwemo Tanzania. Ni shambulizi lililowaogopesha wageni wengi wakiwamo wawekezaji pia. Kwamba Al Shabaab inalenga pia nchi za Magharibi. Hivyo basi, hata raia wake. Kunahitajika jitihada za pamoja kuwaondoa hofu watu wa mataifa ya nje, kuwa kilichotokea Nairobi kitadhibitiwa kwa njia zote, kisitokee tena.
Na hakika, aina hii ya ugaidi ni ngumu sana kudhibitika hatakama nchi ina jeshi kubwa na lenye vifaa vya kisasa. Inahitaji ushiriki wa raia wema katika kutoa taarifa za wahalifu hata kabla hawajafanya matendo yao maovu. Inahitaji pia maandalizi makini, ya kuwa na vikosi vilivyo tayari wakati wote kukabiliana na matukio kama haya.

Ni dhahiri, kuwa mbinu inazotumika kikundi cha kigaidi cha Al Shaabab ambacho maana hasa ya jina hilo ni ' Vijana', ni moja ya changamoto kubwa katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Al Shabaab iliundwa mwaka 2006. Kinasemekana kuwa na wapiganaji wenye silaha wapatao 10,000. Al Shabaab katika miaka ya karibuni wamepoteza maeneo mengi ya mijini waliyokuwa wakiyadhibiti, ikiwamo mji wa Kismayu ambao majeshi ya Kenya yaliudhibiti baada ya kuwasambaratisha Al Shabaab. Kwa sasa Al Shabaab bado wana nguvu maeneo ya vijijini katika Somalia.

Kufuatia Kenya kujiingisha kijeshi kupanbana na Al Shaabab, kikundi hicho kimeifanya Kenya kuwa adui na kutangaza wazi azma yake ya kuishambulia Kenya. Mwezi Aprili mwaka huu watu watano walipoteza maisha nchini Kenya baada ya wapiganaji wa Al Shabaab kuingia kwa nguvu wakiwa na silaha kwenye mgahawa mmoja kwenye mji wa Garissa nchini Kenya.

Mwaka 2012 ndipo Al Shabaab walipojiunga rasmi na mtandao wa kigaidi wa Al qaida chini ya kiongozi wa Al qiada, Ayman al- Zawahiri.
Hakika, hapa duniani matukio ya kigaidi yameongezeka.
Kwa faida ya wasomaji, nitaanza kwa kuangalia chimbuko la ugaidi kihistoria. Ni rahisi kusema kwamba ulimwengu umebadilika baada ya ugaidi wa Septemba 11 mwaka 2001 kule Marekani. Kwamba ugaidi umesogea karibu zaidi katika fikra zetu. Watanzania bado tunakumbuka tukio la shambulizi la kigaidi dhidi ya jengo la Ubalozi wa Marekani jijini Dar Es Salaam Agosti 7, 1998.

Sura ya ugaidi imeonekana vema zaidi miongoni mwa walimwengu. Bila shaka, picha ya filamu ya televisheni yenye kuonesha majengo mawili ya World Trade Centre kule Marekani yakitunguliwa na kuanguka, zimeonwa na takribani asilimia 75 ya watu wa ulimwengu huu. Katika hili la kuchambua ugaidi, hebu
basi tuanze na kujiuliza; Ugaidi ni nini?

Itakumbukwa wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano walipokutana Dodoma mwaka 2002 walipitisha Muswaada wa Ugaidi. Wabunge wetu walitumia muda mwingi sana kujadili tafsiri ya neno "ugaidi".
Kwa kifupi, ugaidi ukitafsiri kutoka neno la Kiingereza "Terrorism" tunapata maana ya "hofu". Neno la Kiingereza "Terror" lina maana ya hali ya "kutisha".

Vitendo vya kigaidi hutumiwa na mtu au makundi ya watu ili kuwaingizia watu hofu ndani ya mioyo yao na pengine hata kuchukua madaraka ya kisiasa. Ugaidi ni njia ya mnyonge na hata mwenye nguvu kutimiza malengo yake. Hili litafafanulika zaidi kadri utakapofuatilia maandiko haya.

Kihistoria tunaona kuwa, vitendo vingi vya kigaidi humu duniani vimefanywa pia na dola zilizo madarakani kwa minajili ya kuendelea kushika hatamu za dola. Mathalan, msemo wa " Utawala dhalimu" kwa tafsiri ya Kiingereza "Terror regime" hutumika tunapoielezea dola yenye kutumia mabavu na nguvu nyingi kupita kiasi. Dola au mtawala asiyezingatia sheria wala haki za kibinadamu.

Msamiati huu wa utawala dhalimu unatokana na lugha ya Kifaransa na una chimbuko la Mapinduzi ya Wananchi kule Ufaransa kati ya mwaka 1789 hadi 1799. Utawala dhalimu wenye kutisha" la terreur" ulikuwepo kule Ufaransa kunako miaka ya kati ya 1792 hadi 1794. Katika kipindi hicho watu takribani 40,000, wengi wao wakiwa wakulima na wahunzi waliuawa.

Mifano ya tawala dhalimu na za kutisha katika sehemu nyingine za dunia ni kama Urusi ya zamani chini ya dikteta Stalin, utawala wa Kinazi wa Ujerumani kati ya 1933-1945 chini ya Fashisti Hittler.
Katika Afrika, tuna pia mifano kadhaa ya tawala dhalimu na za kutisha ambazo kimsingi ni tawala za kigaidi. Uganda ya Idd Amin, Afrika ya Kati ya Bokassa, Zaire ya Mobutu, na nchi nyingine nyingi. Hizi zilikuwa tawala dhalimu.

Ugaidi kimsingi ni ile hali ya mtu, kikundi au dola, kwa maana ya taifa,kutumia nguvu nje ya wigo wa sheria ili kufikia malengo yao. Mwenye kuendesha vitendo vya kigaidi huchagua watu wake watakaoathirika na vitendo hivyo. Si lazima mtu au watu hao watakaoathirika wawe ni wahusika wa moja kwa moja wa mgogoro husika, isipokuwa, waathirika mara nyingi huchaguliwa na huonekana kama wawakilishi wa malengo ambayo magaidi wanataka kuyafikia.

Malengo au sababu za ugaidi zaweza kuwa ni za kidini, kijamii na kisiasa.
Ugaidi huwa wa kimataifa pale tukio la kigaidi linapofanywa nje ya mipakaya yule anayatenda tendo la kigaidi, au raia wa nchi moja wanapokuwawalengwa na kauthirika na tendo la kigaidi katika nchi ya tatu, mathalan,magaidi kutoka Colombia wanapofanya tendo la kigaidi dhidi ya raia waUingereza katika nchi ya Zambia.

0754 678 252, http://mjengwablog.com

Sunday, March 17, 2013

Mjengwa asitisha mahusiano na Ludovick Joseph kwa Tuhuma za "Kuhusika na matukio ya kigaidi'

TAARIFA RASMI KUTOKA Mtandao Wa Kijamii Wa MJENGWA BLOG

Sunday, 17 March 2013 | Written by Mjengwa Blog

Ndugu zangu,
Kutokana na kuwepo kwa taarifa rasmi za kipolisi zenye kumtuhumu Ludovic Joseph kuhusika na matukio ya kigaidi.

Uongozi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog unasitisha rasmi, kuanzia leo Jumapili, Machi, 17,2013, kuwa na Ludovick Joseph kama msaidizi wa Mtandao wa Kijamii wa Mjengwablog na website ya Kwanza Jamii.

Maggid Mjengwa,
Mmiliki wa Mjengwablog /Kwanzajamii

Wednesday, April 11, 2012

Maggid Mjengwa Aomba Jamii Imsamehe Lulu - Kifo cha Steven Kanumba



Lulu, alivyokuwa na maskendo (scandals) sijui kama itakuwa rahisi kwa jamii kumsamehe katika jambo la kifo cha Steven Kanumba!

**************************************************************


KUTOKA MAGGID MJENGWA BLOG:
Neno La Leo: Jamii Ya Walo Wema Imsamehe Elizabeth ' Lulu' Michael

Ndugu zangu,

Jana amezikwa Steven Kanumba , kipenzi cha wengi.

Mauti ya Steven Kanumba yanatukumbusha wanadamu ukweli huu; kuwa maisha yetu hapa duniani ni mafupi sana. Hivyo, lililo jema kwetu wanadamu ni kuishi kwa kutenda yalo mema. Kuwatendea mema hata tunaodhani wametukosea, maana, tutawasaidia kujifunza kutenda mema. Na ni mwanadamu gani asiyekosea?

Na moja ya adhabu kubwa mwanadamu unaweza kuipata humu duniani kutoka kwa wanadamu wenzako ni adhabu ya kutengwa na wanadamu wenzako.

Msichana Lulu ameshapata na anaendelea kuipata sasa, adhabu kubwa sana kutoka kwa wanajamii. Adhabu ya kupewa hukumu ya mauaji na kutengwa na wengine. Lulu , ambaye ni mmoja wa waliokuwa karibu na marehemu Kanumba hata katika dakika zake za mwisho maishani, na ambaye alikuwa mpenzi wa Kanumba, hakuweza kushiriki mazishi ya mpenzi wake. Hiyo nayo ni adhabu kubwa kwa Lulu kupewa na wanadamu wenzake.

Yumkini Lulu ana mapungufu yake kama mwanadamu, lakini, kwa sasa hastahili adhabu kali hiyo kutoka kwa wanajamii. Kwa kosa ambalo hakuna aliye na hakika leo kuwa amelitenda. Ndio, Lulu aweza kuwa mwanadamu mwenye mapungufu yake mengine, lakini , hayo yasitufanye wanadamu tuwe na haraka ya kumpa hukumu isiyo ya haki. Na kwenye mienendo ya maisha, ni mwanadamu gani asiye na mapungufu?

Maana, tangu mara ile ilipofahamika, kuwa msichana Elizabeth ‘ Lulu' Michael alikuwepo kwenye mazingira ya kutokea kwa kifo cha Kanumba, basi, jamii, huku ikisaidiwa na vyombo vya habari, haraka ikapata wa kumnyoshea kidole. Na hukumu ya Lulu kutoka kwa wanajamii walo wengi ikawa imetolewa hapo. Kwamba Lulu ndiye muuaji. Kwa sasa, hukumu hiyo haiwezi ikawa ya haki mpaka pale wenye mamlaka ya kututhibitishia hilo watakapofanya hivyo.

Na hata kama ugomvi, uliotokana na wivu wa kimapenzi , wa Lulu na mpenzi wake ulipelekea mauti ya Kanumba, bado maelezo tuliyoyasikia hayamwonyeshi Lulu kuwa na dhamira ya kutaka kutenda maovu anayohukumiwa na wanajamii kuwa kayatenda. Hivyo, naye, kama mwanadamu, anastahili msamaha kutoka kwa wanajamii wengi walo wema.

Katika wakati huu mgumu sana kwa msichana Lulu, vyombo vya habari viwe mbele katika kumsaidia Lulu kama mwanadamu mwenzetu, badala ya kutumia balaa lililomkuta kama mtaji wa kuandika na kutangaza udaku wa kuuzia magazeti na kuvutia watazamaji wa runinga na wasikilizaji wa redio.

Maana, kwa adhamiriae kutumia magumu yanayomkabili msichana Lulu kuvuna, basi, hana atakachokivuna zaidi ya kuvuna dhambi.

Badala yake, media isaidie katika kutufanya wanajamii tujitafakari. Kwa vile, habari za matukio ya mahusiano yasiyo na staha na matendo ya kiuhuni yanayofanywa na baadhi ya wanajamii wakiwemo wasanii, huwa yanashabikiwa na vyombo vya habari badala ya vyombo hivyo kushiriki kukemea na kuelimisha jamii. inasikitisha, kuwa katika wakati huu, vyombo hivyo vya habari vyaweza kabisa kuwa kwenye harakati za kuandaa stori zaidi za ‘ kumning’iniza’ zaidi Lulu ambaye tayari ameshaning’inizwa hadharani.

Ndugu zangu,

Kama wanajamii, na wengine kama wazazi. Lulu anabaki kuwa ni msichana mdogo anayehitaji kusaidiwa katika wakati huu mgumu kwa maisha yake. Yumkini vyombo vya dola vinaweza vimtie au visimtie hatiani. Hivyo, kumwachia huru Lulu.

Lakini, bado hukumu ya jamii ikabaki pale pale. Hukumu ya Lulu kutengwa na jamii. Hiyo ni hukumu mbaya zaidi inayoweza kuchangia hata kuyafupisha maisha ya msichana huyu mdogo. Jamii haina faida na hukumu kama hiyo. Ni heri ikamwacha huru aende akapambane na yanayomkabili mbele yake. Ndio, akapambane na maisha haya magumu ya dunia hii bila kujisikia kutengwa na wanajamii wenzake.

Na naamini, leo kuna wengi kama mimi, wenye kufikiri hili, kuwa jamii ya walo wema imsamehe Elizabeth ‘ Lulu’ Michael.

Na hilo ni Neno La Leo.

http://www.mjengwablog.com/

Maggid Mjengwa
Dar es Salaam.

Tuesday, April 10, 2012

Mliozika Ndugu Kinondoni Mkacheki Hali ya Kaburi Zao!!!

Wadau, nilijua itatokea!  Makaburi mengi huko katika makaburi ya Kinondoni yameharibiwa leo na umati walioenda kuhudhuria mazishi ya marehemu Bongo Superstar Steven Kanumba.  Kweli watu hawana heshima kwa wafu! 



Pole sana Profesa Msuya!




KUONA PICHA ZAIDI ZA UHARIBIFU KATIKA MAKABURI YA KINONDONI  NA MAZISHI YA STEVEN KANUMBA BOFYA HAPA:

Tuesday, January 03, 2012

Babu Wa Loliondo Janga La Kitaifa 2011 - Maggid Mjengwa


Mh. Lukuvi na Binti yake Mwalimu Nyerere wakipata 'kikombe' kutoka kwa Babu
Imeandikwa na Maggid Mjengwa

Babu Wa Loliondo Janga La Kitaifa 2011

 “Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote”,ni wimbo unaovutia ni wimbo; unaelezea wasifu wetu wasifu wa nchi yetu Tanzania kweli jina lako ni tamu tulalapo tunakuota wewe, Ndoto wakati mwingine uashiria kitu kijacho !

Naam ndugu zangu Watanzania, tukiwa tunakaribia kumaliza mwaka nchi yetu imekumbwa na majanga kadhaa likiwepo hili la mafuriko napenda kuchukua nafasi hii kuwapa pole wote  waliofikwa na mafuriko najua Mungu atasimama upande wao, janga hili ni  muendelezo wa majanga mengi yaliyoikuta Tanzania yetu tunayoiota utalalapo, Ambikile Mwaisapile maarufu kama babu wa loliondo ni moja ya majanga hayo .

Inayodaiwa kuwa tiba ya Babu wa Loliondo, badala ya kuwa msaada kwa taifa, imeonyesha madhara zaidi ya kiafya, kijamii na kiuchumi. Tuliandika kutahadharisha na kushauri. Tumepuuzwa; maana, kwa wengine, tiba ya Babu ilikuwa ni mradi, na kwa kweli kugeuzwa kuwa mradi wa kitaifa.

Na kilichojikita katika kuwaacha watu wetu wakitaabika ni unafiki wetu. Tuna maradhi mabaya, na ni sugu. Ndio, miongoni mwetu kuna wenye kusumbuliwa na maradhi ya unafiki. Nitatoa mfano nilipata kukaa na wasomi wawili, tena wana digrii zao. Tukazungumzia ya Babu wa Loliondo.

Mimi na wasomi wale tulikuwa na misimamo ya kufanana, tulipinga upotoshaji unaoendelea katika jamii kuwa Babu wa Loliondo, Ambilikile Mwasapile, anatibu ukimwi, kansa, kisukari na mengineyo. Na kwa vile wote tumekwenda shule, hoja kuu ilikuwa hii; kuwa hadi sasa hakuna hata wagonjwa watatu wa ukimwi waliothibitishwa kitaalamu kuwa wamepona ukimwi kwa dawa ya Babu.

Badala yake, kuna wengi wamekufa baada ya kuacha kutumia madawa waliyoelekezwa na madaktari watalaamu waliosomea tiba.

Wakati tukiendelea kuzungumza, mara akatokea mheshimiwa fulani, naye akaingia moja kwa moja kwenye mjadala. Alimtetea Babu na kusisitiza kuwa. Babu ni lulu ya taifa, lazima aenziwe. Wasomi wale afadhali wangekaa kimya, hapana, walianza kumuunga mkono mheshimiwa kwa hoja nyepesi.

Hawakuwa wapumbavu, walijifanya tu wapumbavu wakiniacha mimi nikipambana peke yangu kuziponda hoja za mheshimiwa yule. Kwa kiasi fulani, niliogopa kuona hulka hii ya wasomi wetu. Wasomi ambao, kwa unafiki, wanashindwa kutetea na kusimamia katika hoja zao za msingi. Na hii, bila shaka, ni moja ya majibu ya swali la kwa nini Tanzania ni masikini?

Hakika, ya Babu wa Loliondo ni aibu yetu kitaifa. Katika karne hii ya 21 nchi yetu inatumia raslimali zake kufanya promosheni ya ndoto ya Mtanzania mmoja kati ya Watanzania milioni 42! Ndio, tunafanya promosheni ya jambo lisilo na uthibitisho wa kisayansi. Si tuliona, haikupita siku bila kusikia  habari za Babu wa Loliondo?

Kwa sasa, tunaweza kabisa kusema, kuwa habari za huduma za Babu wa Loliondo zilitangazwa na kuufikia umma kuliko habari za Wizara yeyote ile katika  Serikali ya Awamu ya Nne. Babu wa Loliondo si mchezo bwana, alikuwa na ‘maafisa habari wake’ wanaowafunika hata maafisa habari wa Wizara za Serikali.

Na katika mzaha huu wa mambo ya msingi kitaifa, tuna maelfu kwa maelfu ya Watanzania wanaotaabika na hata baadhi kufa kwa kuamini kuwa Loliondo kuna tiba, na iko Loliondo tu! , kuna Watanzania walioweka rehani mavuno yao ya  mwaka mzima ili wapate nauli ya kwenda kwa Babu. Si wameambiwa, kuwa hata mawaziri wanapanga foleni ya kwenda kupata kikombe cha Babu!

Na wakishapata kikombe wanapiga picha ya ukumbusho, au labda ya kisiasa.  Asubuhi yake ’maafisa habari’ wa Babu wameshatundika picha ya waziri ukurasa wa kwanza gazetini! Jimboni kwa mheshimiwa wapiga kura wake watamwona au  kusikia kuwa Mheshimiwa naye anaumwa kama sisi, na amepata kikombe cha Babu!

Kikombe cha Babu ni abrakadabra, nilipata kuandika hilo. Na Watanzania, baadhi, kwa hiyari yetu, tumekubali kujifanya, wajinga na hivyo kuwapumbaza wengi wengine. Kwanini? Tulitafute jibu kwa kufikiri kwa bidii.

Hebu jiulize; wakati Shirika la Afya Duniani (WHO), Juni mwaka huu, liliadhimisha miaka 30 ya mapambano dhidi ya ukimwi, je, Tanzania, kama nchi, tulikuwa na banda la maonyesho likielezea ugunduzi wa tiba ya ukimwi  iliyotokana na ndoto ya Babu?!

Labda ndio maana, magazeti yetu ya lugha ya Kiingereza hayakufanya sana promosheni ya tiba ya Babu. Maana, kama habari za Babu zingepewa uzito kama  ilivyo kwenye magazeti yetu ya lugha ya Kiswahili, basi, wana jumuiya ya  Kimataifa, wakiwamo wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, huenda  wangeshindwa kuamini wanachokisoma.

Maana, wawakilishi wa mashirika kama PSI na FHI yenye miradi ya kupambana na ukimwi nchini na mengineyo wangejiuliza; nini hasa wanachokifanya katika  nchi yetu. Na pengine wameshatafsiriwa tunachooandika juu ya Babu kwa Kiswahili chetu!

Si ajabu basi, Ubalozi wa Marekani ulikuja na tamko lake Mei 5 mwaka huu.  Wamarekani hawa, kwa kuwaonea huruma Watanzania, wameshauri watu wanaotumia  tiba mbadala wasiache kutumia dawa walizopewa na madakatri na vile vile  waendelee kujikinga na maambukizi.

Na wakaweka msisitizo kuwa, kuacha kutumia dawa hizo za madaktari watalaamu kunafanya dawa hizo zinapotumiwa tena kushindwa kufanya kazi ipasavyo (drug resistance). Na ajabu ya habari ya tamko lile la Wamarekani ilichapishwa katika gazeti moja tu kwa lugha ya Kiingereza - The Citizen, jina la gazeti  hilo lina maana ya Mwananchi; ingawa wananchi wengi hawakupata habari hiyo kwa lugha yao!

Kwa hakika, hatuhitaji kuambiwa na Wamarekani juu ya ukweli huu na wajibu wetu. Huu ni wakati kwa wizara inayohusika kufanya jitihada za dhati kutoa tamko litakaloweka bayana kuwa tiba inayodaiwa kutolewa na Babu bado haijathibitika kitalaamu kama inaponya maradhi sugu kama vile ukimwi, kansa; na kisukari.

Wakati utafiti huo ukiendelea, umma ukumbushwe kuwa, dawa zinazotambulika kitalaamu kwa sasa ni zile zinazotolewa na madaktari wetu watalaamu. Kwamba  wanaokwenda kwa Babu wana ruhusa ya kufanya hivyo, lakini, kikombe cha Babu  kinaweza kunywewa pamoja na dawa za hospitalini.

Tufanye hivyo sasa, na ujumbe huo usambazwe kwa nguvu zote na maafisa wa  habari wa wizara husika. Ndio, maofisa habari wa Wizara ya Afya nao  washindane na ‘maafisa habari’ wa kujitolea wa Babu wa Loliondo!

Watanzania tunapita kwenye kipindi kigumu sana. Na huu ni wakati wa  kutafakari kwa kina. Na nimepata kumwuliza jamaa yangu swali hili; mwanadamu ; unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Naye akanijibu; ” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!”

 Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani angetamka kuwa, angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.

Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndio njia  mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando  kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri?

Haya ya kwa ‘Babu wa Loliondo’ ni kielelezo cha Watanzania kuamua kuacha kufikiri. Kuna umma uliojifunika vilemba vya ujinga. Umma uko gizani, ; unahitaji mwanga.

Yumkini wakatokea Watanzania wenzetu wakaoteshwa na Mungu juu ya  dawa za tiba kwa mwanadamu. Na hapo wakaingiza suala la imani. Lakini, jambo hilo halituzuii wanadamu kuhoji na kudadisi. Ndio, kuuliza maswali. Na kwa Serikali, jambo hilo haliizuii kufuata taratibu zake za kawaida ikiwamo kufanyia utafiti jambo hilo na kutoa msimamo wa kiserikali.

Hata kama Watanzania watakuwa na uhuru wa kwenda kwenye tiba za imani, lakini msimamo wa Serikali uwepo. Na kwa wengi utabaki kuwa ndio mwongozo;  maana, watakuwa wameufanyia utafiti. Nahitimisha.

Niwatakieni Heri ya Mwaka Mpya.

Maggid Mjengwa.

http://mjengwablog.com/

*************************

 SOMA HABARI ZAIDI ZA VIFO LOLIONDO GLOBAL PUBLISHERS:

http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/loliondo-1

Tuesday, July 26, 2011

Maoni - Umeme: Mahojiano Ya BBC Na JK

(pichani: Makao Makuu yaTANESCO HQ Ubungo)


Hii imeandikwa na Kaka Maggid Mjengwa. Hivi sasa yuko Sweden.



*****************************************************************

Umeme: Mahojiano Ya BBC Na JK; Tafsiri Yangu

Ndugu zangu,

Kuna mengine yamenipita hapa kati. Leo nimesikiliza mahojiano ya mwandishi wa BBC na Rais Jakaya Kikwete kuhusu tatizo la upatikanaji wa umeme Tanzania.

Nimefuatilia pia maoni ya Watanzania mtandaoni juu ya majibu ya Kikwete. Tafsiri yangu; uongozi wa nchi ni kitu kigumu sana. Wengi wamemshambulia Kikwete kwa majibu yake kiasi wengine wamediriki kuandika; kuwa hatuna Rais.

Tunafanya makosa sana kutoa hukumu zenye kusukumwa na hisia hasi. Nimesikiliza mara mbili majibu ya Rais. Sikuona mahala pa kumshutumu Rais isipokuwa nimesikitishwa na maswali ya mwandishi wa BBC ambayo kwa Kikwete ilikuwa kama penalti alizokuwa akipigiwa mikononi na yeye kuzidaka huku akitabasamu.

Tusisahau, kuwa Kikwete ni mwanasiasa mahiri. Mwandishi anayekutana na Kikwete ni vema akajiandaa vilivyo juu ya namna ya kumbana Kikwete ndani ya majibu yake. Afanye hivyo ili kupata maswali mapya na hivyo basi habari mpya kutokana na majibu ya Rais.

Niseme tu, mahojiano yale ya Kikwete na BBC hayakutoa maswali mapya wala kuja na habari mpya. Na huo si udhaifu wa Kikwete bali mwandishi wa BBC aliyemhoji Kikwete.

Si tumemwona? Kikwete aliweza kucheza anavyotaka kwenye mahojiano yale. Na umahiri wake ulijidhihirisha pale alipogeuza sura ya mahojiano yale na Kikwete kuchukua nafasi ya mwandishi kwa kumbana mwandishi na husuan juu ya maarifa ya mwandishi katika eneo husika;

Wakati mwingine na nyinyi mjifunze hayo mambo ya kitaalamu kulikoni kuuliza tu hivi hivi. Unajua ungekuwa na wewe unauliza kwa hoja - unajua kwamba hiki kitu hiki ingekuwa umeme wa jua miezi miwili tu upo - tungeweza kufanya hivyo. Kikwete anamwambia mwandishi wa BBC.

Katika mahojiano yale Kikwete alikwenda na takwimu zake mfukoni. Kama moja ya mbinu katika sanaa ya mawasiliano ili kufikisha ujumbe, mara tatu ndani ya mahojiano yale Kikwete alizungumzia MW 600 zilizozalishwa tangu uhuru na MW 145 zilizozalishwa tangu 2009, na MW 160 zitakazozalishwa ifikapo Desemba mwaka huu. Jumla zitakuwa MW 305 tangu 2009. Na hapo ndipo kwenye hoja ya msingi ya Kikwete. Ana haki kuwashangaa wasioona jitihada zake.

Na Kikwete hakosi majibu ukimwuliza juu ya umeme wa jua, upepo na mvuke. Ana hoja anaposema kuwa umeme huo pia unahitaji mipango na kuwa huwezi kupata umeme wa jua kesho kwa vile jua linawaka.

Kama msikilizaji ningependa mwandishi ambane Kikwete kwenye maeneo ya ufisadi kwenye mikataba ikiwamo yenye kuhusiana na nishati ya umeme. Hakika, kama tungedhibiti ufisadi kwenye mikataba, basi, ni imani ya wengi kuwa tungejenga uwezo wa kuzalisha MW nyingi zaidi za umeme na kwa kasi kabisa, kulifanya tatizo la umeme kuwa ni historia. Tungeweza pia kupunguza gharama za mtumiaji wa umeme.

Tuna tatizo pia la baadhi ya wanasiasa kujiingiza katika kuwekeza kwenye eneo la nishati ya umeme. Wachague kati ya uongozi na uwekezaji. Kiongozi huwezi kuwa na hisa kwenye kampuni binafsi ya kuzalisha umeme na wakati huo huo ukalinda maslahi ya umma badala ya kampuni yako.

Vinginevyo, kwa waliokuwa na utayari wa kuelewa, mahojiano yale ya BBC na Kikwete yamempa nafasi Kikwete ya kujenga hoja ya msingi juu ya nini alichofanikiwa kufanya tangu aingie madarakani katika jitihada za kutatua tatizo la umeme nchini.

Nawasilisha.

Maggid,
Sweden, Jumanne, Julai 26,2011
http://mjengwa.blogspot.com/

Friday, July 01, 2011

Ziara Mbili za Ughaibuni Zolizovunja Urafiki wa Nyerere na Kambona

Ziara mbili za ughaibuni zilizovunja urafiki wa Nyerere na Kambona

Na Maggid Mjengwa

KUNA wakati nilimsikia Ahmad Rashid akitoa hoja bungeni. Wakati huo mbunge huyo wa CUF alikuwa kiongozi wa upinzani bungeni. Ahmad Rashid aliomba kambi ya upinzani bungeni ibadilishwe jina na badala yake iitwe kambi ya ushindani bungeni. Ni kwa vile neno ‘upinzani’ linatafsiriwa vibaya na wananchi. Spika Samwel Sitta alisimama na kutamka; “ Mtaendelea kuitwa hivyo hivyo kambi ya upinzani, kwa vile nyinyi ni watu wa kupingapinga tu!”


Na maneno haya ya Samwel Sitta yanatokana na historia yetu. Maana, haya ni makosa ya kihistoria yaliyofanywa na waliojenga msingi wa taifa letu. Na ndio tunayoyaona hata katika mfarakano wa miaka hamsini iliyopita kati ya Julius Nyerere na Oscar Kambona.

Na mara ile, mwaka 1965, TANU ilipoaachana na mfumo wa vyama vingi na kuasisi mfumo wa Chama kimoja Kambona alipata kutamka; ” Kwanini tupige marufuku ya vyama vingine vya siasa wakati tunajua wananchi walio wengi wanaipigia kura TANU?” Kambona akaongeza kusema; ” Bila shaka, umaarufu wa TANU utabaki kwa muda mrefu, lakini, je, pale umaarufu wa TANU utakapopungua, ina maana tuwe madikteta?” Alihoji Kambona.

Nimepata kukumbushia mara kadhaa, kuwa historia ni mwalimu mzuri. Na wanadamu hatupaswi kuwa vipofu wa historia yetu wenyewe. Kuifumbia macho historia yako ni kujiandalia njia ya kutumbukia korongoni, kwa kujitakia. Tunapoadhimisha miaka hamsini ya uhuru wa Tanganyika tuna lazima ya kuipitia na kuitafakari historia yetu. Kwa macho makavu na maangavu, tuangalie nyuma tulikotoka. Tuangalie tulipo sasa. Ndio, tufanye hivyo ili tuutafute mwelekeo mwema wa nchi yetu hata kwa miaka mingine hamsini ijayo.


Tuna maswali mengi ya kujiuliza, moja kuu ni hili; Je, ni nchi ya namna gani tutayotaka kuijenga na hata kuvirithisha vizazi vijavyo? Kwa maneno mengine; ni jamii gani tunayotaka kuijenga? Sisi wa ’ Kizazi Cha Azimio’ tulikuwa wadogo sana katika miaka kumi ya mwanzo ya uhuru na hata utekelezaji wa Azimio la Arusha. Nimezaliwa Ilala, Dar es Salaam, Machi 11, 1966.


Ndio, kuna mema mengi tuliyoyaona, lakini, tukitafakari sasa, kuna mabaya mengi pia tuliyoyashuhudia. Tuna wajibu wa kusimulia mema na mabaya hayo kwa manufaa ya Watanzania wa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.

Kati ya kumbukumbu zangu mbaya za wakati huo ni jinsi tulivyowaona wazazi wetu wakiishi kwa hofu. Waliogopa kushutumu mamlaka hadharani na kwa sauti. Waliishutumu Serikali na hata kiongozi mkuu wa nchi kwa kunong’ona. Wazazi wetu walimwogopa hata mjumbe wa nyumba kumi.

Ni ukweli, kuwa kwa wakati ule, Serikali na chama tawala havikuwa na uvumilivu wa sauti za upinzani.

Na siku zote, mamlaka bila upinzani huzaa kiburi na majigambo. Huzaa hali ya kutokujali na kukosa usikivu. Taratibu, huzaa hali ya kujisikia u-bwana mkubwa. Hali hii ikiachwa ikaendelea, basi, husababisha madhara makubwa kwa nchi. Huleta hasara kubwa kwa nchi, kiuchumi na kijamii.

Juma la jana nilimalizia kwa kuandika, kuwa makala haya ni jaribio la kuvunja ukimya wa juu ya nini kilitokea takribani miaka hamsini iliyopita. Ni mmoja tu wa mfano , wa jinsi umma ulivyofichwa ukweli wa juu ya nini hasa kilitokea kikasababisha mfarakano wa waliopata kuwa viongozi wa mstari wa mbele kwenye harakati za kuanzishwa kwa TANU na kudai uhuru wa Tanganyika; Julius Kambarage Nyerere na Oscar Salathiel Kambona.


Kuna aliyesoma makala yangu ya juma la jana na kuniuliza; ” Maggid, hivi wewe huogopi?” Ni kweli, kama ningeandika haya mwaka 1976 nilipokuwa mtoto wa umri wa miaka kumi tu, basi, vyombo vya dola vingenishukia mithili ya mwewe anayekishukia kifaranga cha kuku. Sio tu mimi ningeswekwa rumande ya watoto, bali hata mama na baba yangu wangetikiswa na dola kwa ’ dhambi’ ya kumzaa mtoto mwenye fikra za ’ kipinzanipinzani ’ na ’ kihainihaini’. Mtoto ’ anayepingapinga’ tu!


Na hapa ndipo kwenye moja ya mapungufu makubwa ya waliojenga msingi wa taifa letu; kuchukia wenye kufikiri tofauti na watawala. Na zaidi kuwachukia wenye ’ akili’ ya kufikiri na kuutumia vema welewa wao- hostility towards execelency. Si tunajua, kuwa utotoni tulisikia kuna maadui wa nchi wa aina mbili; maadui wa nje na wa ndani. Wapinzani ama wenye kufikiri tofauti ndimo walimowekwa wanaoitwa ’maadui wa ndani!’


Niseme tu, mfulilizo wa makala haya ni moja ya makala zangu muhimu tangu nianze kushika kalamu na kuandika makala magazetini. Na naandika nikiwa sina hata chembe ya hofu. Ni kwa sababu moja kuu; kuwa yanahusu historia yetu na mustakabali wa nchi yetu. Sote tuna wajibu wa kuandika historia yetu.


Hii ni nchi yetu. Hatuna sababu za kuionea aibu historia yetu, badala yake, tujivunie, kuwa tuna historia. Na ni unyonge na utumwa kusubiri wasomi kutoka Marekani na Ulaya waje kutafiti na kutuandikia historia yetu. Historia yako isimulie mwenyewe. Hivyo basi, tuna wajibu wa kuifanya kazi hiyo. historia itusaidie kutukumbusha machungu na furaha ya tuliyoyapitia kama taifa. Si kwa kuandika tu, hata kwa kusimulia machache tuliyoyashuhudia.


Niliahidi kuchambua zaidi juu ya marafiki hawa watatu; Kambona, Nyerere na Kawawa. Nitafanya hivyo sasa.

Naam. Julius na Oscar walikuwa viongozi vijana sana katika Tanganyika huru ya wakati huo. Ikumbukwe, wakati tukipata uhuru, Nyerere alikuwa na miaka 39 na Oscar alikuwa na miaka 36. Hawa walikuwa ni vijana waliokabidhiwa dhamana kubwa ya kuingoza nchi kubwa ya Tanganyika. Naamini, walikuwa ni wenye dhamira njema kwa taifa hili; Julius, Oscar, Rashid na wenzao wengine katika TANU.
Ukweli unabaki, kuwa Oscar Kambona hakuikimbia nchi yake kwa kashfa ya kuiba fedha ya Serikali au ufisadi mwingine. Na kwa utafiti mdogo tu niliofanya, nilichobaini, ni ukweli kuwa marafiki hawa wawili; Oscar na Julius walikuwa na mgongano wa tofauti ya kimaono ya kisiasa yaliyoathiri hata urafiki wao.

Maana, haiyumkini Kambona aliyeaminiwa na Nyerere akaja kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa TANU, akawa Waziri wa kwanza wa Elimu wa Tanganyika huru, akaja kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na hata kwa wakati mmoja kushika wizara mbili; Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya Nje. Kwamba, aje tena baadae kutuhumiwa uhaini na hata kushukiwa uraia wake.


Ndio, kwangu mimi, ya Kambona na Nyerere ilihusu zaidi mgongano wa tofauti za kimaono ya kisiasa . Na ukiingia kwa undani kwenye maandiko na simulizi utaupata ushahidi wa haya. Na kwa hakika, ili siasa ya nchi istawi, basi, inahitaji uwepo wa migongano ya kifikra. Hivyo basi, siasa ni migongano ya kifikra yenye kuhitaji majadiliano endelevu.


Tunaona, kuwa migongano ya kifikra kati ya Oscar na Julius ilianza kuonekana dhahiri katika ziara mbili walizozifanya kwa pamoja katika mataifa mawili tofauti. Ziara ya Marekani mwaka 1963 na ziara ya Uchina mwaka 1965. Na hapo katikati kuna jambo lililoopelekea uwepo wa mahusiano ya mashaka kati ya Julius na Oscar. Ni uasi wa jeshi wa Janauri 20, 1964.


Uasi ule ulipelekea Nyerere na Kawawa waende mafichoni, inasimuliwa walijihifadhi eneo la Kigamboni. Mjini alibaki Oscar Kambona aliyeshiriki kikamilifu kuwatuliza wanajeshi wale. Kimsingi, katika kipindi kile cha maasi, Kambona, kama angetaka, alikuwa na fursa ya kutwaa mamlaka ya nchi akisaidiwa na jeshi. Inasemwa, kuwa akiwa Waziri wa Ulinzi, Kambona alikubalika sana jeshini.


Baada ya ziara ya Marekani akiwa na Oscar Kambona mwaka 1963 ambako Rais John Kennedy alimsifia sana Nyerere kwa kuonyesha uwezo wa kiungozi , miaka miwili baadae, mwaka 1965, Nyerere na msafara wake akiwamo Oscar Kambona walikwenda China kwa mara ya kwanza na kulakiwa na Mwenyekiti Mao Tse Tung. Nyerere akiwa kwenye gari la wazi na mwenyeji wake Mao , alishangiliwa na Wachina wapatao milioni moja waliojipanga barabarani.

Pale Ilala tulikoishi, nakumbuka nikiwa na umri wa miaka sita tu, usiku mmoja pale viwanja vya shule ya msingi Boma tuliangalia sinema ya ziara ya Julius Nyerere Uchina . Nyerere aliiona China na alivutiwa sana. ” What we have seen in China is relevant to us”. Nimemsikia Nyerere akiongea hayo kwenye kipande cha filamu ya zamani kilichopo mtandaoni . ” Ana maana, walichokiona China kinaweza kikafanyika kwetu. Na Julius alianza kwa kubadilisha hata staili yake ya mavazi, yakafanana na ya Mwenyekiti Mao, na wengine katika TANU wakamwiga.

Ni nini kilitokea kwenye Mkutano wa TANU wa Januari, mwaka 1967 na kabla ya hapo. Mkutano uliopelekea kumalizika kabisa kwa urafiki wa Nyerere na Kambona. Fuatilia toleo lijalo.
http://mjengwa.blogspot.com

Wednesday, April 06, 2011

Kikombe cha Babu - Mjadala


pichani- Wagonjwa wakisuburi kupata 'Kikombe' huko Loliondo

Wadau, Maggid Mjengwa na John Mashaka wana moani makali kuhusu 'KIKOMBE' cha babu wa Loliodo. Lazima nami niseme nina ndugu yangu ambaye alienda huko Loliondo kupata kikombe ili apone Kisukari. Alipoipata alijisikia freshi kwa siku kadhaa sasa analalamika maumivu. Nadhani hicho kikombe haimtimbu kila mtu, lakini wako waliopona. Je, hao ambao hawakupona baada ya kunywa hawakuwa na imani, au haikuwa na dawa ya kutosha? Na ni kweli kuwa watu nje ya nje wanatucheka kuwa tuna imani kali na uchawi.

Sioni ubaya kuwa na imani ya kikombe. Ila sasa wengine copycats wanaomwiga babu wanajitokeza kila kona na vikombe. Na watu wanakimbilia kunywa! Ni fesheni nini? Pia msishangee siku moja mkisikia kuna mtu kajitokeza na kikombe' watu wakanywa kwa wingi halafu walikufa kwa wingi kwa vile ilikuwa na sumu!

Someni maoni ya Kaka Maggid na Kaka John Mashaka halafu karibuni mjadili.


Loliondo na Umma Ulio Gizani

Maggid Mjengwa Machi 23, 2011

TUNAWAPITISHA watu wetu kwenye njia yenye giza. Kwenye njia yenye matope. Kwanini?
Socrates, mwanafalsafa wa Uyunani alipata kuonekana akimulika kurunzi mchana wa jua kali. Inaandikwa, kuwa Socrates yule alizunguka sokoni na kurunzi yenye kumulika. Watu walimwuliza, kulikoni? Socrates akawajibu; ”Kwenye nuru hii , kuna walio gizani.”

Kwa Socrates lilikuwa ni tendo la kifalsafa lenye kuelezea hali halisi. Hata katika dunia hii ya kisasa, bado tuna miongoni mwetu, walio gizani mchana wa jua kali. Angalia ya kwa ’ Babu’ wa Loliondo. Ndiyo, kuna wanaohitaji kumulikiwa mwanga.
Na kuna tofauti ya ujinga na upumbavu. Marehemu Mzee Jongo alipata kutamka; ” Kusoma si kuufuta ujinga, bali ni kuupunguza”. Kila mwanadamu ana ujinga wa jambo moja au mia moja. Kuwa na ujinga wa jambo si kosa, hata profesa anaweza asijue namna ya kuchochea kuni za kuchomea mhindi mbichi ukachomeka. Kijana wa darasa la saba anaweza kuwa hodari wa jambo hilo kumshinda profesa.

Lakini upumbavu ni ile hali ya mwanadamu kufanya jambo isivyotakiwa huku akiwa na uelewa wa namna ya kufanya inavyotakiwa. Huo ndio upumbavu. Na ndiyo maana binadamu kuitwa mpumbavu ni tusi. Kuitwa mjinga si tusi, kila mmoja ana ujinga wake. Kuwa na ujinga wa jambo fulani ni kutoelewa jambo hilo. Ni nani anayeelewa kila jambo?
Na mwanadamu unafanyaje unapoamka na kukuta dunia unayoishi ardhi yake imeanza kumegeka na kuchotwa na bahari? Kuna niliyemwuliza swali hilo. Naye akanijibu; ” Huo ndio utakuwa mwisho wa dunia!” Aliyenijibu alikuwa amechoka kufikiri. Nilidhani amgetamka, kuwa angeanza kujifunza kuogelea. Maana, kwa kuogelea majini angeweza kukutana na kisiwa, au nchi kavu.

Wanadamu tumejaliwa akili ili tuweze kufikiri. Na kufikiri ndiyo njia mojawapo ya kuiteka kweli. Kufikiri kunahamisha milima na hata kuiweka kando kuruhusu mwanga upite. Inakuwaje basi mwanadamu anapoacha kufikiri? Haya ya kwa ’ Babu’ wa Loliondo ni kielelezo cha Watanzania kuamua kuacha kufikiri. Kuna umma uliojifunika vilemba vya ujinga. Umma uko gizani, unahitaji mwanga.

Yumkini wakatokea Watanzania wenzetu, wakaoteshwa na Mungu juu ya dawa za tiba kwa mwanadamu. Na hapo wakaingiza suala la imani. Lakini, jambo hilo halituzuii wanadamu kuhoji na kudadisi. Ndiyo, kuuliza maswali. Na kwa Serikali, jambo hilo haliizuii kufuata taratibu zake za kawaida ikiwamo kufanyia utafiti jambo hilo na kutoa msimamo wa Kiserikali. Hata kama Watanzania watakuwa na uhuru wa kwenda kwenye tiba za imani, lakini msimamo wa Serikali uwepo. Na kwa wengi utabaki kuwa ndio mwongozo, maana, watakuwa wameufanyia utafiti.

Si tumemsikia yule nabii mwingine wa Tarakea, naye ni kijana wa miaka 28. Ikasemwa, kuwa naye kaoteshwa na Mungu dawa ya kutibu wagonjwa. Mpaka Serikali ilimpomzuia ili ifanye uchunguzi, tayari alikuwa na wagonjwa 100. Ndiyo, Watanzania tu wagonjwa tunaogombewa. Na viongozi wetu pia ni wagonjwa. Si tumewaona wakipanga foleni ya kikombe kwa Babu?

Katika dunia hii Serikali hupendwa na watu, lakini, si vema na busara, kwa serikali za dunia kutaka kujipendekeza kwa watu. Kuna mambo yenye kupendwa na watu, na watu wakawa na haraka ya kutaka kuyafanya. Lakini, kama serikali itahitaji kufuata taratibu ili kinachopendwa na watu kifanyike, basi, serikali haina namna nyingine, bali kufuata taratibu.

Si tuliona yale ya DECI. Waziri Mkuu Mizengo Pinda alisimamia taratibu, akasimamisha wimbi lile la DECI. Kuna wengi walishutumu, lakini , hao hao, leo wanaishukuru Serikali. Maana, DECI nayo ilikuwa ni Abrakadabra.

Na si juzi hapa tumemsikia Paroko wa Kigango cha Mt. Yohane wa Msalaba Parokoia ya Mbezi Luis Padri Vivian. Niweke wazi, Paroko yule amesema kile ambacho kuna wengi hawataki kukisikia. Ameusema ukweli wake. Ameifanya kwa dhati, kazi ya utumishi wa Mungu wake.

Paroko yule wa Mbezi Luis alitamka; "Sina chuki wala tatizo lolote na tiba ya Loliondo, lakini kama unataka kwenda lazima ujiulize maswali manne yafuatayo;
Kwanza, tiba inayotokana na miujiza ya Mungu lazima iwe endelevu isiwepo kwa kipindi kifupi tu.

Pili, watu wajiulize kama miujiza kutoka kwa Mungu huwa na masharti?
Tatu, wajiulize kama tiba hiyo inafanya kazi ndani ya Loliondo, kwanini isifanye kazi Dar es Salaam na kwingineko?

Nne, wajiulize kuhusu tiba hiyo ya magonjwa sugu ukiwemo ukimwi ni je, Mungu aliwaumba wanadamu na kisha kuamua kuwaangamiza? Au wanadamu wanaangamia kutokana na vitendo vyao vya ujanja ujanja?

Mwisho Paroko yule akasema; "Ukiishajiuliza maswali hayo na kujiridhisha kwa majibu utakayopata, basi, unaweza kufanya maamuzi ya kwenda Loliondo.

Ndiyo, tujiulize; katika mataizo yetu haya, tumechoka kufikiri? Tumechoka kuuliza maswali? Hapana. Tusichoke kuutafuta ukweli, hata kama umegubikwa na ukungu. Hivi ni Watanzania wangapi wamesikia au kusoma maelezo ya Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Arusha, Mount Meru Dk. Toure?

Nahofia si wengi, maana, maelezo yake yaliyopaswa kuwa habari kubwa ya ukurasa wa mbele yalipewa nafasi ndogo sana kwenye moja ya magazeti ya kila siku. Tena yaliwekwa katika ukurasa wa pili ndani ya habari nyingine. Si tunafahamu, kuwa baadhi ya wanahabari nao wanachagiza ’ Abrakadabra’ za ’ Babu’ wa Loliondo. Zinauza magazeti, na msimu ndio huu!

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Hospitali ya Mount Meru alisema, kuwa tangu tiba ya ’ Babu’ ianze, hajapata hata mgonjwa mmoja wa ukimwi aliyepata kikombe cha ’ Babu’ na kurudi hospitalini hapo kupimwa tena. Hivyo, mpaka hii leo hatuna ushuhuda wa kimaabara kwa maana ya hospitalini. Ushuhuda tunaousikia ni wa mitaani.

Ndiyo maana tiba ya ’ Babu’ itabaki kuwa ’ Abrakadabra’ mpaka hapo itakapothibitishwa vinginevyo kimaabara hospitalini na si kwenye vijiwe vya barabarani.

Halafu tunaambiwa, kuwa tiba ya ’ Babu’ inatibu kansa pia. Hivi Kliniki ya Kansa ya pale Ocean Road mpaka hii leo imeshindwa kuwapeleka kwa ’ Babu’ wagonjwa watano tu walio kwenye matibabu ya kansa. Waende huko wakapate kikombe halafu wachukuliwe vipimo tena tuone nguvu ya tiba ya ’ Babu’ katika kuwasaidia wagonjwa wa kansa.

Ndugu zangu, Mfalme Suleiman alimwambia Mola wake; ” Watu wangu wanaangamia kwa kukosa hekima”. NdiYo, Mfalme Suleiman alipoambiwa na Mola kitu cha kuchagua, basi, alichagua hekima ili aweze kuwaongoza watu wake.

Angalia leo, walio wagonjwa na kwenye hali ngumu za kiuchumi wanazidi kuwa wagonjwa na hali zao za kiuchumi zinazidi kuwa duni. Ndiyo, kuna wanaofunga safari zenye gharama kubwa kwenda Loliondo. Wanakwangua akiba zao. Kuna hata wanaokopa fedha ili waende Loliondo.

Ndiyo, wanakwenda kupata tiba isiyo na hakika katika wakati huu tunaozungumza. Kuna wagonjwa walioacha kutumia dawa zao. Wamerudi na kuanza upya. Kuna waliopoteza maisha. Inasikitisha sana. Ni nani wa kuwasaidia kuwamulikia mwanga? Naam. Kwenye nuru hii kuna walio gizani. Tuwasaidie.

===========================================================


John Mashaka anaandika....

I read with lot of interest Mr. Maggid Mujengwa’s article entitled “Ya Loliondo Na Umma Ulio gizani”, a philosophical description of a confused society. Mr. Mujengwa depicted Tanzania as a nation that is using a flashlight in a broad day light with a notion that, perhaps, it could aid her see better. Figuratively or philosophically speaking, Socrates the philosopher used this metaphor to describe a hopeless and a confused society. One question Mr. Mujengwa failed to address was the root cause of this confusion. How could Tanzanians be convinced that, flashlight is brighter than the sun? Is it because of ignorance, confusion or desperation?

Plato, one of the greatest philosophers to have ever lived, strongly advocated in favor of an examined life; An examination of one's life addresses fundamental questions such as: who am I, what do I want to do with my life, how will I know whether I have achieved my goals, what matters to me; wisdom; a feeling of accomplishment; wealth, power; social change or pleasure and how will I balance them. If you haven't asked yourself these questions, then life becomes meaningless. You become more like a boat in turbulent high seas without compass direction, going along with the tides and currents of the ocean. A boat that is destined for a clear tragic end of capsizing, Tanzania that is.

Tanzanians are not in control of their lives. Instead, they are controlled by the events of the day, and ignorantly perceiving flashlight to be more powerful than the sun, based on Socrates account on ignorance. As a nation, Tanzania has not asked itself these basic questions, because social-economic, hopelessness and despair amongst her people speak for itself. A sea of humanity flooding Loliondo, is a confirmation of the broken system. Her sick hopping from their hospital beds, carried in stretchers, just to have a sip of the wonder concoction is very troubling. This signifies the dying or non-existing healthcare system in Tanzania. Tanzania does not know where it is headed; it is a lost vessel sailing in the turbulent high seas without a direction, and only waiting to capsize

I must slightly differ with Mr. Mujengwa, based on my strong conviction, that, Babu Mwasapile’s patients are not uninformed, but rather hopeless, desperate, CONFUSED and poverty burdened men and women from all walks of life. Loliondo list of visitors is made up of the mighty and the powerful, the rich, the poor, scientists and herdsmen; famous and the little known peasants. Babu has received people who have made their way by selling their few worldly possessions, as well as the flamboyant tycoons arriving in style; in their private aircrafts, all with one goal; drinking the magical mixture, with hope ridding themselves of their excruciating illnesses. This is a national embarrassment, and depiction of Tanzania as a primitive and backward country in the eyes of the world

We are not talking about dumb, stupid, or simple-minded people; we are talking of brilliant and well educated individuals serving in the government, International, private and public agencies. We are talking of people who have been humbled by illnesses, and like anybody else, must heed the need to find treatment by standing in a long queue in the middle of nowhere; away from their posh homes, and comfort of their beds to find cure from the miraculous drink. We are talking of a hopeless and a desperate society on edge.

Desperation has no class, it has no social status or identity, it has no color or creed. It affects PhD holders and the illiterate alike. We must remember that, desperate and hopeless men do not value life; they have no shame or fear. Tell a man, who has exhausted all options to get rid of cancer, that his urine is the only cure to his excruciating illness. Even a King who desperately wants to live will heed the advice. These are the people flanking Babu of Loliondo’s compound trying to get rid themselves of terminal illnesses, endless pain, and misery.

Babu of Loliondo could not have emerged at a perfect time for the hopeless, when divine intervention is direly needed to save their souls. Babu has exposed our desperation, vulnerability and weakness as a society. He has exposed how useless education can be in the face of human despair. He has exposed how far we are lost in the turbulent high seas, and only going with the tide and flow. We are lost. Just like DECI which was a product of greed, ignorance and despair, Babu Liliondo’s purported magic cup is nothing but a tragic health and social a time bomb yet to explode!

MUNGU IBARIKI TANZANIA

John Mashaka
mashaka.john@yahoo.com

Sunday, March 27, 2011

Maoni ya Mdau Kuhusu Mjengwa Blog na Dawa za Babu

ndugu mjengwa...

habari za kazi.

kwanza nakupongeza kwa kutumia muda wako mwingi kuelimisha umma wa watanzania ambao kwa bahati mbaya wengi wamo katika giza nene.

nimeshawishika kukuandikia mail hii baada ya kusoma makala zako kadhaa kuhusu dawa ya babu wa loliondo. niliona matusi, kubezwa na kudharauliwa unakokupata kufuatia kuwaambia watanzania ukweli, jamii ambayo kwa miaka kadhaa imezoea kuambiwa uongo, blah blah na kupumbazwa.

kimsingi nakubaliana nawe kuwa dawa ya babu ni abra kadabra. ni pumbazo ambalo limeingia katika jamii yetu kwa wakati huu na kwa bahati mbaya wasomi, wanasiasa na watu mashuhuri wamekuwa ni baadhi ya watu wanaofurika huko loliondo kupata kitu kinachoitwa kikombe.

hivi karibuni televisheni ya kenya ya ntv imetoa documentary kwa lugha ya kiswahili na lugha ya kiingereza kuelezea kile kinachoitwa maajabu ya loliondo. watu wamehojiwa wakiwemo wagonjwa, madaktari na baadhi ya wananchi wa kawaida hasa wa arusha. kuna maoni mchanganyiko kuhusu suala hili lakini ni wazi kuwa watu wamepumbazwa na maelezo kuwa mtaalamu wa dawa hiyo ni mchungaji mstaafu. kwa kuwa ni mchungaji mstaafu basi bila shaka dawa yake ni ya kweli!!!!

suala hili linaendeshwa kidini zaidi badala ya kijamii. wengi wa watu wanaodai kuponywa hisia zao wameziegemeza zaidi katika cheo au hadhi ya uchungaji wa babu. hii ni psychological treatment ambayo kwa vyovyote itaonekana kwa siku kadhaa kama sio miezi lakini baadae itaondoka na ndipo watu watakapojiona kuwa ni wapumbavu na hawakupata nafuu yoyote kutokana na kikombe cha babu.

ingekuwa mtaalamu huyu wa loliondo hakuwa mchungaji mstaafu hwenda hali ingekuwa tofauti kwa wanasiasa wetu na viongozi wa kijamii lkn hili la uchungaji ndilo linalowapumbaza watu na kujiona kuwa kumpinga babu na dawa yake ni sawa na kupinga imani jambo ambalo kwa mtazamo wangu si sahihi na ni kujipotosha wenyewe. dawa ya babu na imani ya dini hapa ni vitu viwili tofauti ambavyo vimewekwa pamoja.

kuna wengi duniani wanaotumia kivuli cha dini kwa maslahi yao na watu kupumbazika kwa kuona kuwa kinachosemwa na mtu husika hakipaswi kupingwa maana ukipinga utakuwa umepinga dini na dini inaogopwa. mtu huogopa kuwa akipinga ataonekana ameasi au atalaaniwa na dini au mungu.

maslahi ya dawa hiyo tunaambiwa yanagaiwa kwa kanisa husika, wasaidizi wake na kiasi kidogo huchukuwa yeye babu. katika hali kama hiyo iwapo kanisa linapata share fulani jee unategemea kuna kiongozi wa kanisa lake atakaemkataza? hilo haliwezekani maana kanisa litakosa mapato ambayo halikutegemea kuwa yangetokea.

mnakumbuka kufukuzwa kwa father NKWERA na waumini wake na kutengwa na kanisa lake? sababu kuu ilikuwa ni kufanya maombi na kuponyesha wagonjwa jambo ambalo lilisemwa kuwa si katika mafundisho ya kanisa. inawezekana kanisa la babu na la father NKWERA ni tofauti lakini hoja ipo pale pale. father NKWERA hakuwa ananufaisha kanisa kwa wakati ule lakini babu analiingizia kanisa fedha za kutosha hivyo watu wanafumba macho.

kwa bahati mbaya wanasiasa nao wamekumbwa na uozo huu. wakati waziri wa afya alitoa tamko awali kabisa la kupiga marufuku dawa hiyo hadi uchunguzi ufanyike, waliibuka wanasiasa uchwara ambao kwa kutaka sifa waliona tamko lile la waziri halina maana. kina SHIRIMA NA LUKUVI wakalivalia njuga jambo hilo na kudai kuwa serikali ipo pamoja na babu. waziri wa afya kwa kuepusha shari ya udini aliamua kukaa pembeni na kujinyamazia kimya.

hawa kina SHIRIMA na LUKUVI wanadai kuwa ni suala la kiimani hivyo serikali isiingilie imani za watu. wamesahau siku chache tu kabla ya uchaguzi mkuu mwaka jana mtu mmoja aliyejipa cheo cha mtabiri maafuru afrika mashariki na kati alitangaza kuwa mgombea mmoja wa uchaguzi angefariki dunia kabla ya uchaguzi mkuu na kupelekea uchaguzi kuahirishwa.

serikali hiyo hiyo wanayoisema kina LUKUVI na SHIRIMA ilitoa tamko kali la kupinga kauli hiyo na kumtaka mtabiri huyo anyamaze kimya au atachukuliwa hatua. serikali haikusema kuwa mambo yake ya utabiri ni maswala ya kiimani anayetaka aamini na asietaka aachane nae. lakini sasa tunaambiwa kuwa masuala ya imani serikali haiwezi kuingilia. hatua ile ya serikali kwa mtabiri yule ilikuwa sahihi kabisa lakini kwa sasa tunaona serikali ikiwa na kigugumizi kuhusu babu huyu.

hivi sasa kina babu wanaongezeka, wengine wakitokea mbeya. si hasha baada ya siku chache tukasikia mwengine ameibuka dar es salaam au mtwara au mwanza au hata pemba akidai nae ameoteshwa kuwa awahudumie watanzania kwa dawa ambayo formula yake haijulikani.

kwa ufupi dawa ya babu ni kanyaboya kwa hoja zifuatazo:

1. maradhi anayosema inatibu ni maradhi yanayosababishwa na vitu tofauti. baadhi husababishwa na virusi, mengine bakteria na mengine ni matatizo ya kutokuwa na uwezo wa homoni fulani mwilini. kwa vyovyote vile dawa ya matatizo haya haiwezi kuwa ni moja kwa sababu hata chanzo chake si kimoja. kwa mfano huwezi kupeleka gari gereji kwa matatizo tofauti kisha ufumbuzi wake kuwa ni huo huo mmoja. tatizo la gear box, chasis au tyre haviwezi kuondoshwa kwa aina moja ya ufumbuzi.

2. kauli za babu anapohojiwa na vyombo mbali mbali vya habari zinatofautiana. kuna sehemu anasema kuwa dawa yake inatibu maradhi matano kama alivyoambiwa na mungu. kuna sehemu anasema kinachotibu sio huo mti bali ni maombi yake na kuna sehemu anadai kuwa kinachotibu ni kikombe hivyo dawa husika isipotekwa kwa kikombe chake (kikitumika cha mtu mwengine) haitamsaidia mgonjwa. hizi ni kauli zenye mgongano. kwa mtu mwenye kutumia akili, hapa babu anajaribu kutumia ujanja wa kuzuia watu wengine wasiweze nao kujitengenezea dawa hiyo na kugawa kwa watu. anajaribu kutengeneza dominancy au monopoly katika jamii. kutakapokuwa na babu wawili au watatu bila shaka idadi ya wagonjwa wanaokuja kwake itapungua na hatimae maslahi kupungua pia.

3. kuna wakati babu hueleza kuwa dawa husika haiwezi kufanya kazi kwa mtu aliyefanya ujanja kwenye foleni kwa kuwapiku wenzake aliowakuta. hii ni njia nyengine ya ajabu kwa kuwa hakuna uhusiano wowote wa kitiba na suala la mtu kupanga foleni au kutokaa foleni.

4. kuhusu malipo ndo ujanja wa wazi kabisa. babu anadai ameambiwa na mungu kuwa atoze shs 500 tu kwa watz na dola 1 kwa wageni. hata hivyo hakusema iwapo kutakuwa na mabadiliko ya kupanda au kushuka thamani ya pesa itakuwaje? jee shs 500 au dola 1 itabakia hivyo milele? na jee binaadamu wanaotoka nchi ambazo hazitumii dola wala shs? au mungu hatambui fedha za nchi nyengine katika dunia yake zaidi ya dola na shilingi?

5. dawa husika anadai ni lazima itolewe loliondo tu. hii pia ni ujanja wa kuhakikisha kuwa hakuna babu wengine wanaoweza kufanya kazi hiyo katika mikoa mengine. ukitaka usitake ni lazima uende loliondo tu. ni kucheza na akili za watu na kwa bahati mbaya watu wamepumbazika.

6. kuhusu kulipia hapa napo pana jambo. kazi ya mungu huwa ya kujitolea lakini hakuna pahala babu anaweka utaratibu kwa watu wasio na uwezo wa hiyo shs500. jee anataka kutwambia kuwa mungu hajali watu mafukara ambao hata hiyo shs500 kwao ni kiwango kikubwa? vitabu vyote vya dini vinataja haja ya kuwahurumia mafukara na wasio na uwezo. lkn kwa hili babu yupo kimya sana. labda baada ya mfuko kujaa ndipo atakapotoa ofa kwa wasio na uwezo.

7. mwisho dawa ya babu haina dozi. hiki ni kituko chengine. kwa aliye mahututi aliye na nafuu nk wote ni kikombe kimoja tu. hili ni la kuchekesha kama sio kusikitisha. hata hao waganga wengine wa kienyeji hutoa dawa kwa mujibu wa hali ya mgonjwa. lakini pia kabla ya mgonjwa kupewa dawa huchunguzwa kama ana aleji au tatizo lolote kama vidonda vya tumbo nk. lkn hilo halipo kwa babu. kikombe hicho hakijali uzito wa ugonjwa wala afya yake. hakijali presha ya mgonjwa wala lishe yake. iwe ameshakula au ananjaa kikombe ni kimoja tu. hii ni hatari kwa jamii. hata katika mambo ya kawaida ya binaadamu hali haipo hivyo. gari la tani 3 litabeba mzigo wa tani 3 na la tani 10 litabeba mzigo wa tani 10. huwezi kusemwa magari yote yabebe tani 10 wakati yana uwezo tofauti.

sikutaka kutumia hoja za kisayansi kuwa dawa hii haijathibitishwa kwa kuwa watu wengi wanajidanganya kuwa dini ni zaidi ya sayansi. kwa maoni yangu dini na sayansi havipingani hata siku moja. ukiona hivyo kuna tatizo pahala.

mbali na hali niliyotaja hapo juu, kuna madaktari na wataalamu wa afya huko arusha ambao walishuhudia wagonjwa wakitolewa hospitali na kupelekwa kwa babu wamethibitisha kuwa baadhi yao pamoja na kupata kikombe hicho na kujidanganya kwa siku chache kuwa wamepona wamejikuta wapo hoi na kurudi tena hospitali. huu ndio ukweli ambao utajulikana siku si nyingi kwa kuwa maji hayo yaliyochemshwa hayana dawa yoyote na hayasaidii kuondoa ugonjwa.

kwa bahati mbaya pamoja na ukweli huu baadhi ya watu hudai kuwa wagonjwa hao waliojiona kuwa hawajapona eti walikwepa foleni au kutofuata utaratibu wa babu!!! huu sasa ni ujinga mwengine. wengine wanadai kuwa madaktari hao wanamuonea wivu babu eti kwa sababu kawanyanganya wateja wao!!! wakati watu wanawatahadharisha wao kuepuka kanyaboya wao bado wamo katika usingizi mzito wa kulewa kikombe cha babu...

kwa ufupi wafuasi wa babu wanataka kusema kuwa ni lazima watu wote waliopata kikombe hicho kumsifu babu na anayekwenda kinyume kwa kudai kuwa hajapona huonekana ndio mkorofi. kuna haja ya watanzania kutafakari na kuchukua hatua. tukumbuke kauli ya mhe rais KIKWETE kuwa AKILI YA KUAMBIWA CHANGANYA NA YA KWAKO....

Wakatabahuuu,

mdau
ughaibuni...

Saturday, March 26, 2011

Tiba ya Loliondo - Msimamo wa Mjengwa Blog

(Pichani) Baadhi ya waliofanikiwa kupata kikombe cha 'Dawa ya Babu' huko Sumange Village Loliondo

Nimesikia habari za watu kupona magonjwa yao baada ya kunywa dawa, pia nimesikia habari za watu amabo walizidiwa baada ya kunywa hiyo dawa na kuacha kutumia madawa waliopewa mahospitalini. Pia nimesikia habari za watu kufariki wakiwa wanasubiri kupata dawa ya ya babu.
Ningependa kusikia kutoka kwa watu waliokunywa daw ya babu kabla ya kuaamua kama inafanya kazi au la. Mungu yu Mwema na kweli kama ametupa dawa ya kuponyesha magonjwa yasiyo na dawa basi ingekuwa vizuri dunia nzima wajue habari hiyo.

******************************************************************************
Hii ni tamko rasmi kutoka Mjengwa Blog:

Ndugu Zangu,

Hii ni nchi yetu. Tunayaandika haya kwa mapenzi ya nchi yetu. Yanayotokea Loliondo yanaanza kubeba sura ya kashfa. Taratibu, Loliondo inaonekana kuwa ni aibu ya kitaifa kwenye masuala ya kimsingi ya afya ya watu wake.

Si kawaida, na yawezekana ni mara ya kwanza kutokea, kwa blogu ya jamii kutoa msimamo juu ya jambo la kitaifa. Tunauona umuhimu huo, tunafanya hivyo. Ndio, Hali ni mbaya Loliondo. Kuna Watanzania wenzetu wanakufa kila siku. Wanakufa wakiwa kwenye foleni ya kupata kikombe cha Babu au baada ya kunywa kikombe hicho na kuacha kutumia dawa zao walizokuwa wakitumia kabla.

Asubuhi hii nimepokea simu kutoka Dodoma. Kuna mganga aliyenielezea hali mbaya zinazowapata wagonjwa wake wa kisukari mara baada ya kupata tiba ya Babu na kuacha kutumia dawa zao. Anasema ni mbaya zaidi kwa wagonjwa wa kisukari, maana, kisukari kinapanda haraka. Anasema kuna wagonjwa waliokufa baada ya kuacha kutumia dawa zao.

Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele katika kupigia debe tiba ya Babu bila kufanya uchunguzi yakinifu. Ndio, duniani kuna fikra dhanifu na fikra yakinifu. Ya ‘ Babu’ wa Loliondo ni dhania iliyopaswa kuhojiwa kabla ya kupigiwa debe.

Hivi, wanahabari wetu wanashindwaje mpaka hii leo, kuwahoji madaktari bingwa kwenye maradhi kama UKIMWI, kisukari, na mengineyo. Madaktari hawa wako Agha Khan, wako Bugando, Mount Meru na kwengineko. Hivi, Watanzania wenzetu hawa, katika kazi zao, mpaka hii leo hawana cha kusema, cha kitaalam juu ya Tiba ya Babu? Au media imechagua kuficha ukweli?

Tunajua, kuwa habari za ‘ Babu wa Loliondo’ zinauza magazeti kwa sasa. Lakini, ni dhambi na kutoitendea haki nchi yetu kama tutaamua kufanya biashara na afya za watu wetu. Ni laana kubwa.

Ona sasa, Watanzania kwa maelfu wanakwenda gizani bila kuhoji, au kusaidiwa kuhoji. Katika dunia ya sasa ya Sayansi na Teknolojia hatuwezi kwenda mbele kwa kuendekeza ‘ Abrakadabra’ kama hizi za Loliondo.

Huu ni wakati, kwa Wizara na waziri mwenye dhamana, kutoa tamko rasmi juu ya ukweli kuhusu tiba hiyo ya Babu. Na kama ‘ Babu’ ataruhusiwa aendelee na tiba yake kwa wenye imani, basi, Babu huyu asaidiwe kuhamishia shughuli zake Arusha mjini. Lifanyike hilo ili tunusuru maisha ya Watanzania wenzetu walio katika hatari ya kupata maradhi mapya katika mazingira ya sasa ya Loliondo.

Tunayasema haya kwa mapenzi ya nchi yetu, basi.

Maggid,
Iringa,
Ijumaa, Machi, 25,2011
http://mjengwa.blogspot.com

Thursday, January 27, 2011

Mapinduzi Misri?

UPDATE : SATURDAY, JANUARY 29, 2011

CAIRO (AP) - Egyptian security officials say at least 25 protesters and 10 policemen have died in this week's anti-government protests.

They say the death toll was likely to significantly rise as more reports come in from hospitals and morgues around the country. They also say that at least 750 policemen and 1,500 protesters have been wounded in clashes.
The officials were speaking Saturday on condition of anonymity because they were not authorized to share the information with the media.

The protests are the most serious challenge to President Hosni Mubarak's 30-year authoritarian rule. Mubarak, in an attempt to contain the unrest, said on Friday he was firing his Cabinet and sent army troops out to the streets to restore order, but protests and a wave of looting are continuing.

********************************************************************

Bila shaka mmesikia kwenye taarifa ya habari kuwa dunia ya waarabu unawaka moto. Vijana wamechachamaa wakitaka mapinduzi. Tuone mambo yatakavyokuwa lakini mimi nawaombea amani.


********************************************************
Ndugu Zangu,

Kuna Mapinduzi yanayoongozwa na vijana kwenye Dunia ya Waarabu. ( The Arab World). Tumeona Tunisia. Kule Yemen moto bado unawaka. Na sasa Egypt. Hali si shwari. Vijana wako mstari wa mbele; wanataka mabadiliko. Wamengia mitaani kwenye mji wa Suez. Kesho ni Ijumaa. Uarabuni, kama ni shughuli, basi huanza baada ya swala ya Ijumaa. Kuna dalili, kuwa Cairo yaweza kuwaka moto kesho. Mohammed ElBaradei katua Cairo, naye anasema ametua ili nae aingie mitaani kuandamana na vijana kushinikiza mabadiliko.Kama kivumbi kitatimka kesho Ijumaa, basi, Polisi wa Misri wanatazamiwa kutumia nguvu kupita kiasi. Je, nguvu hizo zitatosha kuzunia nguvu ya umma unaotaka mabadiliko? Tusubiri tuone.

Angalia picha za matukio: http://mjengwa.blogspot.com

Maggid
Dar es Salaam

Saturday, April 04, 2009

(pichani Maria Sarungi)

Sinema, 'Elfu Huanza Moja' imepata tuzo kwenye tamasha la filamu FESPACO.

Mnaweza kusoma mahojiano na mtengeneza sinema Maria Sinema kwa KuBOFYA HAPA:


Tuesday, December 09, 2008

Uhuru 9-12-61

Bendera ya Tanganyika


Uhuru wa Tanganyika ulikuwa Disemba 9, 1961. Ni miaka 47 iliyopita. Pichani ni mezi kadhaa kabla ya uhuru mwaka 1961, Mwalimu akiwa na Mama Barbro Johansson nyumbani kwake Kahororo, Bukoba. ( Picha kwa hisani ya Maggid Mjengwa Blog)

Tuesday, November 04, 2008

WaTanzania Wamshabikia Obama - CNN

Hongereni kaka Maggid Mjengwa na Alex Mayunga kwa kuonesha ujasiriamali kwa vitendo katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa raisi Marekani. Mmeweza kutumia nafasi na wasaa ipasavyo!

Waweza kutizama CNN Video hapa: http://nukta77.com/matangazo.aspx

Subi

Tuesday, July 29, 2008

Bagamoyo Beach



Picha kutoka Maggid Mjengwa blog

Nimeona hii picha hii kwa kaka Mjengwa. Aliipiga Bagamoyo beach hivi karibuni. Kweli TV na sinema zinasababisha mabadiliko katika jamii. Miaka ya nyuma usingeweza kukuta wapenzi wakiongea hivyo hadharani. Au siyo? Lakini ni jambo la kawaida kuonyesha mapenzi hadharani katika video na sinema. Watu wameiga. Kwenye giza ni mambo mengine lakini.

Hivi mnakumbuka enzi za censorship Bongo? Enzi za Mwalimu na kabla ya TV kuingia 1993. Yaani kabla ya kuona sinema, Tanzania film company wanafuta busu, na mambo mengine ya mapenzi. Scene ya mapenzi inakatwa! Kweli walikuwa tuchunga kweli. Hata magezeti na vitabu vya mapenzi yalikuwa marufuku. Mmewahi kusoma kitabu cha After 4:30? Labda ganda ilitolewa na kuwekwa brown paper!

Lakini watu walikuwa wanapendana na kufanya mapenzi!

Wednesday, February 06, 2008

Fesheni Mpya Bongo!



Hii Fesheni ya suruali nimeona kwa Maggid Mjengwa. Mnaionaje? Karibu ifanane na sketi. Sijui wametumia mita ngapi kuishona. Halafu tai karibu inafika kwenye magoti!

Issac Mizrahi atasemaje hapo, tutaiona kwenye runway Paris?




Tuesday, October 02, 2007

Mazishi (Funeral) ya Mzee Godwin Kaduma Iringa









Msanii mkongwe, Mzee Godwin Kaduma, aliyefariki dunia wiki iliyopita amezikwa kwao, Itamba, Iringa.

Mungu amlaze mahali pema mbinguni. AMEN

REST IN ETERNAL PEACE.