Showing posts with label Pikipiki. Show all posts
Showing posts with label Pikipiki. Show all posts

Saturday, October 22, 2016

Pikipiki Mzimu Jijini Dar Yazua Hofu!

 Mwananchi akipita kwa kuikwepa pikipiki yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika Kituo cha waendesha bodaboda cha Maganga Veterinary Dar es Salaam.
 Mwonekano wa pikipiki hiyo kwa nyuma.
Pikipiki hiyo ikiwa katika kijiwe hicho cha  Veterinary Maganga Temeke jijini Dar es Salaam.

Na Dotto Mwaibale

PIKIPIKI yenye namba za usajili T 684 CJZ aina ya Fokon iliyotelekezwa kwa zaidi ya mwaka mmoja katika kituo cha waendesha bodaboda cha Maganga Veterinary Temeke jijini Dar es Salaam inazua hofu kwa wananchi na hata kwa askari polisi ambao wameshindwa kuipeleka kituoni.

Imeelezwa kwamba pikipiki hiyo iliegeshwa katika eneo hilo na mtu mmoja ambaye alifika nayo akiwa akiiendesha mwishoni mwa mwaka jana.

Akizungumza jana na mtandao wa www. habari za jamii.com mmoja wa waendesha bodaboda wa kituo hicho ambaye hakupenda kujitambulisha jina lake alisema pikipiki hiyo inawapa hofu wananchi wa eneo hilo na hata waendesha bodaboda.

"Hata sisi wenyewe tuna hofu na pikipiki hii ndio maana tunaegesha mbalimbali na pikipiki zetu na ndio maana sitaki kutaja jina langu" alisema mwendesha bodaboda huyo.

Aliongeza kuwa awali baada ya pikipiki hiyo kutelekezwa katika kituo hicho mtu yeyote alipokuwa akiisogelea au kuigusa ilikuwa ikijiwasha yenyewe lakini baada ya kupita mwezi mmoja iliacha kujiwasha jambo ambalo limeongeza hofu kwa wananchi.

Mkazi mwingine wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina moja la Ismail alisema hata walipotoa taarifa kituo cha polisi cha Maganga walishindwa kuichukua pikipiki hiyo kutokana na tabia ya kujiwasha.

Alisema aaskari wa kituo hicho ambacho kipo mita 10 na eneo ambalo ipo pikipiki hiyo walitoa taarifa kwa wenzao wa kituo cha Chang'ombe ambao nao wameshindwa kuichukua na kwenda nayo kituoni kwa ajili ya kumtambua mmiliki wa pikipiki hiyo kupitia namba zake za usajili.

Ismail alisema inawezekana pikipiki hiyo ilifungwa kifaa maalumu cha utambuzi iwapo kama imeibiwa na ndio maana ilipokuwa ikiguswa au kusogelewa inajiwasha yenyewe licha ya baadhi ya watu wanahusisha kujiwasha kwake na imani za ushirikina.

Imeelezwa kuwa pikipiki hiyo wakati inatelekezwa ilikuwa katika hali ya upya lakini hivi sasa imeanza kupoteza upya wake kwa kukosa huduma ya matunzo.

Jitihada za mtandao huu kumpata Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa huo wa Maganga ili kuzungumzia suala hilo zimeshindika baada ya kuelekezwa alikuwa Manispaa ya Temeke kwenye mkutano.


Wednesday, May 02, 2012

Mbuzi Mwenye Maarifa!

Cheki Mbuzi wa Pakistan alivyo na maarifa kutafuta dishi!  Kanona kweli!

Wednesday, August 20, 2008

Ajali ya Pikipiki huko Oklahoma

Hivi karibuni, kwenye saa saba za usiku (1:00am) jamaa alikuwa anaendesha lori karibu na Tulsa, Oklahoma. Alitokea jamaa aliyekuwa anaendesha pikipiki kwa kasi 120mph (240kilometres) kwa saa. Dereva alisikia kitu kikigonga lori lakini aliendelea kuendesha kidogo. Alivyosimama na kushuka kwenye gari ona alichoona......








Ingawa Brandon Lee White (26) alikuwa anavaa helmet haikumsaidia alifariki papo hapo.
Msiendeshe pikipiki kwa kasi.

Friday, April 18, 2008

Arusi ya Ajabu Afrika Kusini

Huko Afrika Kusini wanapenda sana mambo ya uzungu. Sasa wameingia na Biker Culture, yaani maklabu ya pikipiki. Moja wa bikers alikuwa anaoa, waliamua kufanya arusi ya kiBiker. Sijui na vows walisemea wakiwa kwenye pikipiki. (Asante Da Subi kwa kuniletea picha)

Bibi Arusi akipelekwa sehemu ya sherehe

Wapambe wa Bibi Arusi

Huyo anayeendesha pikipiki anaonekana kama shoga

Huyo anaonyeshwa mavuzi ya kwapa yalichanwa na kuwekewa relaxer



Karibu wanafika kwenye sehemu
Mitaa ya SOWETO

Wanawasili
Wageni waalikwa

Bwana Arusi