Showing posts with label Mahakamani. Show all posts
Showing posts with label Mahakamani. Show all posts

Sunday, December 06, 2015

Kesi ya Rufaa ya Talaka ya Thadei Mtembei Imeahirishwa

wooden gavel and books on wooden table,on brown background

Na Mwandishi wetu

KESI ya rufaa ya madai ya talaka dhidi ya mfanyabiashara na Mkurugenzi wa shule ya sekondari ya St Mathew, Thadei Mtembei imeahirishwa baada ya wakili wa Mtembei, Mussa Kyoboya kudai mrufaniwa yuko India kwa matibabu.

Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Temeke, Tarimo.

Katika kesi hiyo, mpeleka rufaa, Magreth Mwangu anawakilishwa na wakili Chacha Mrungu. Kesi hiyo ilikuja mahakamani juzi ambapo mrufaniwa alitakiwa kupeleka majibu ya rufaa.

Hata hivyo, wakili wake alisema majibu hayako tayari kwani kuna vipengele ambavyo alitakiwa kusaini, lakini ilishindikana kutokana na kuwa nchini India kwa matibabu. Kesi hiyo imepangwa kuendelea Desemba 16 mwaka huu.

Awali, kesi hiyo ilisikilizwa katika Mahakama ya Mwanzo Kizuiani mbele ya hakimu Rajab Tamaambele, ambapo Mwangu na watoto wake walionekana hawana haki, kwa madai sio mke halali na watoto hao ni wa zinaa kutokana na kuzaliwa nje ya ndoa.

Katika madai ya msingi, Mwangu anataka talaka, mgawanyo wa mali na matunzo ya watoto.

Katika sababu za rufaa, mrufani alieleza kusikitishwa na maamuzi yaliyotolewa na Mahakama ya Mwanzo Kizuiani Septemba Mosi mwaka huu, kwa hakimu kukosea kisheria kwa kutosaini nakala ya hukumu ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa saini za wazee wa baraza.

Sababu nyingine ni Mahakama kukosea kisheria kwa kunyang’anya haki ya watoto kwa kutotoa matunzo ya watoto kwa mama, ambaye anaishi na mrufaniwa kwa miaka 20 na kuvunja Sheria ya Mtoto Namba 21 ya mwaka 2009. Maamuzi ya Mahakama ya Kizuiani yalishindwa kufuata sheria kwa wazee wa baraza kushindwa kutoa maoni yao.

Thursday, January 01, 2015

Mhabusu Auwawa Mahakama ya Kisutu

MAHABUSU AUWAWA KWA  RISASI MAHAKAMA YA KISUTU AKIJARIBU KUTOROKA

Na Happiness Katabazi

JESHI la Magereza limefanikiwa kumdhibiti Mahabusu  wa Kesi ya dawa za kulevya ambaye ni Raia wa Sieralioni,  Abdul Koroma (33) asitoroke chini ya Ulinzi wa Askari Magereza ndani  Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkazi Kisutu Dar es Salaam, asitoroke chini ya Ulinzi  baada ya kumtwanga risasi na kumuua papo hapo.

Wakizungumza na mwandishi wa Habari hizi baadhi ya wanausalama waliopangwa kulinda Usalama Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa Masharti ya kutotajwa Majina Yao kwa Madai wao siyo wasemaji wa majeshi Yao wakisema mtuhumiwa ambaye anashitakiwa kwa makosa ya kuingiza nchini dawa za kulevya aina ya Heroin Zenye uzito wa Gramu 1229 na zenye thamani ya Zaidi ya Sh.Milioni 61 iliyopo mbele ya Hakimu Mkazi Waliarwande Lema alistahili kufanyiwa hicho alichofanyiwa.

Walisema Asubuhi marehemu Huyo ambaye ni mahabusu aliletwa na mahabusu wenzake na Askari Magereza na Kisha kufikishwa Katika mahabusu ya Mahakama hiyo mtuhumiwa aliomba apelekwe chooni kujisadia lakini ghafla mtuhumiwa akaanza jaribio la kuparamia ukuta akimbie ndiyo Askari waliokuwa akimsikindikiza chooni wakafyatua risasi hewani ili kumtaka aache ili jaribio lake lakini Inadaiwa Koroma aliendelea na jaribio lake.

" Ndipo itabidi mmoja wa Askari Magereza 'ameshone risasi' yaani amefyatulie risasi Koroma ambayo ilimpata na kumsababishia mauti papo hapo ....na baada ya Koroma kupekuliwa wanausalama Hao walipokuwa soski walikuta ndani ya soksi alilovaa kuna kikaratasi kilichochorwa ramani na namba za simu za watu wa kumpokea haoa Dar es Salaam" kilisema chanzo changu.

Tayari mwili wa Koroma ambaye alikuwa akikabiliwa na Kesi yake P121/2013 umeishaondolewa Katika eneo la Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu umepelekwa kuinadi wa Katika Hospitali ya Taifa ya Mhimbili.

Chanzo: Facebook: Happy Katabazi
Disemba 31 Mwaka 2014.


Kisutu Court Dar es Salaam


Saturday, December 06, 2014

Kifo cha Eric Garner - Aluyeuawa na Polisi Mjini New York

Wadau, nina uchungu sana na kifo cha Mmarekani mwesui, Eric Garner (42). Aliuwawa na polisi wabaguzi. Walisema alikuwa anauza sigara kwa senti 50 kila moja, bila kulipa kodi.  Yaani hiyo ni kosa ya wao kuu mtu! Na siku hiyo walivyomwua hakuwa anauza sigara! Basi tu, walikuwa wanawinda weusi!


Wadau, marehemu nilikuwa namfahamu. Nilimwona mara kadhaa huko Staten Island, New York.  Pale alipouwawa kuna duka la vipodozi na mahitaji mengine. Mara nyingi ilikuwa nikimwona anatabasamu, alikuwa na umbo kama marehemu mume wangu ila mrefu zaidi.  Bora alikuwa anauza hizo sigara kuliko kuwaibia watu au kuwa jambazi. Mara la mwisho kumwona Eric akiwa hai ni hiyo hiyo Julai, alikuwa na mke wake na watoto.

Wiki hii polisi aliyemwua, mzungu, yule aliyemkaba kaachiwa bila hatia.  Yule polisi mshenzi anaitwa Daniel Pantaleo. Ukiona video unaona kabisa jinsi Panataleo anavyomwua, na utalia ukimsika ukisikia anasema, "I Can't Breathe!" (Siwezi kupumua).  Na ni wazi kuwa Pantaleo alikuwa na chuki ya siku nyingi na marehemu.  Yule kijana aliyepiga video ya mauaji ya Eric kafungwa!  Jamani!

Watu wanaandama kwa  wingi sasa karibu kila mji mkuu hapa Marekani! Watu weusi wameuawa na polisi waliowaua wanaachiwa. Ni kama vile maisha ya mtu mweusi haina thamani!  Ni maajabu, weusi na wazungu wanaandana pamoja kudai haki kwa watu weusi! Wana hasira maana wengi wameuawa na hakuna anayedhibitiwa. Tusiwasahau, Michael Brown, Sean Bell, Trayvon Martin, Amadou Diallo, Tamir Rice, na wengine wengi!

Mwenyezi Mungu atulinde hapa Marekani!

Mauaji ya Eric Garner, Staten Island, New York
Kwa habari zaidi na Video ya Mauaji ! BOFYA HAPA:

Saturday, February 02, 2013

Letter to Uncle - Part I

Nimepata kwa email:



Hallo Uncle, 

Guess you are fine, so are we. Bongo iko poa tu na MSWAHILI is still at the helm though wengi wetu tusingependa hivyo!!! anatuharibia PROJECT yetu tuliyoianza miaka mingi huko nyuma, "KUWAFUKARISHA WATANGANYIKA". Analeta mpango wa kilimo cha matrekta wakati hili tulilisimamisha, watu wakiwa na uwezo wa maisha ni vigumu kuwafanya WARITADI. So the best option was to make them poorer and poorer.

Unakumbuka, japo ulikuwa mtoto mdogo, kauli mbiu inayosema "NCHI YETU MASIKINI" basi ni nchi ile ile ambayo sasa wanaharakati hawataki ichimbwe gesi, mafuta na urani, eti hatutaweza kuingia mikataba vizuri kama nchi!! Botswana wamewezaje? Na hawa ndiyo wasomi wa nchi hii!!!Kwa mtu asiefuatilia matukio ya kidunia, kikanda na ki-nchi, anaweza akadhani hawa jamaa wazalendo kweli kweli. 

Sasa wanaogopa mabadiliko ya katiba, wanachotaka wao ni kubadili vipengele vinavyowasumbua kuleta serikali nyingine, lakin STATUS QUO yao ibaki pale pale. Ndiyo maana nakwambia tumerithishwa unafiki kuwa ni sehemu ya maisha yetu ya kila siku. MSWAHILI kaanzisha kampeni ya shule za sekondari za kata, imekuwa nongwa, watoto wengi masikini watapata fursa ya kuwa na upeo wa kujua mambo, anawaharibia PROJECT ile kuu. 

Wanaharakati na wachambuzi wa masuala kadha wa kadha wa Bongo ni wa ajabu sana, akiuawa mtu ambae kwa hana maslahi yoyote hukaa kimya kama vile hakujatokea kitu, sasa ngoja auwawe mwenzao, kelele ni nyingi, maandamano kwa kwenda mbele, huu ni usomi wa aina gani uncle? Sheria ya ugaidi iliyopitishwa Bongo ilipigiwa kelele nyingi na wadau wenye luona mbali, lakini kwa vilke ilikuwa inawalenga watu fulani ambao kwa hakika watajijua wenyewe, ikapitishwa, Kenya ambako kuna wakristo wengi kuliko Bongo walisita baada ya kuona itawagawa kama nchi, hiyo ndiyo COMMON SENSE tuisemayo. 

Nimeku-forwardia mail za siku nyingi kidogo kukukumbusha ya kwamba, "Many world events do not just happen, they are made to happen" kwa hiyo sio ajabu kuona kuwa Somalia kuna rabsha licha ya kuwa vita vilikuwa vimekwisha tayari lakini kwa kutumia jina la MAHAKAMA YA KIISLAM, wasomali walipoteza sifa ya kuwa na amani nchini mwao, ndivyo vivyo hivyo itawakumba wamisri na Muslim Brotherhood, halikadhalika Mali, Zanzibar, Tunisia na kwingineko dunia ya Kiislam. Kwa wanaojua, CRUSADE is with us now though it still finds pockets of resistance on a few Islamic individuals, when the Islamic Nation as a whole wakes up to this fact, things will never be the same again, albeit, the cat is out of the bag already!!

Huku Bongo Waislamu sio wanalalamika, wanawaambia wenzao wakristo kwamba mchezo wao ni mauti kwa wenzao, lakini mazoea yana taabu, wanadhana kuwa waislamu hawana akili, wamezaliwa hali wakiwa wapumbavu. Ustaarabu wa dunia ya Magharibi una deni kubwa sana kwa uislamu ( hii inategemea na historia gani Mbongo kasoma maana Bongo inaongoza Afrika kwa kutengeneza HALF-BAKED Intellectuals!!!) Sasa inaingia kichwani kuwa wale waliostaarabisha dunia leo hii tena ndiyo waje kuwa hawajui kitu!! 

Hicho kisemwacho kuwa ni New World Order kinasumbuliwa na uislamu tu hadi sasa, jamaa wa itikadi hii wako busy kubomoa family values, mainstream society morals and ethics, traditions and God Worship etc., stumbling block ni Muslims and Islam, maana kama ni ushoga umeishakubalika, riba poa tu, kusagana poa, tena kwa baraka za makanisa, na watendaji wakuu wa makanisa ndiyo vinara wa kuonesha njia kwa vitendo!! elimu ya Evolution ndiyo hivyo tena, watu ni ma-Profesa wa fani hii, wanaharakati na wachambuzi wako busy wakijikaanga kwa mafuta yao wenyewe, eti tunasema zama za giza zimepita, mbona kwa sasa ndiyo GIZA TOTOLOOO!! 

Bye Uncle, nisiseme mengi, jamaa hawakawii kutumia sindano kunyamazisha ukweli. Regard

Letter to Uncle - Part 2



Hallo Uncle,

Happy new year. MJOMBA has been of late making headlines by opening up roads, bridges and a whole lot of new projects that you would expect the wananchi in all their divergence to come up with nice words of encouragement, but alas me, we keep hearing the same old crap of SERIKALI DHAIFU!!!

 In actual fact uncle, TANZANIANS were not supposed to live a life of luxury, this you can see thru common sense and by actions taken by NYERERE and his cohorts. Look at this: " Ein Volk, Ein Reich, Ein Fuhrer!" This literally means, "One People, One Empire, One Leader!" The German people were subjected to continual propaganda, under the control of Josef Goebbels. It was the Cult of personality - everything was organised to make Germans permanently grateful to Adolf Hitler.

So we come with our own "ZIDUMU FIKRA ZA MWENYEKITI" And we are able to see and hear how a multitude of Tanzanian politicians of every colour (party) sing the same song of praising someone whose decisions have to a large extent brought us to this quagmire we are now in. Take the case of Gas and Mtwara residents uprising, it is nothing but Nyerere's marginalisation of the people of Mtwara and other areas mostly populated by muslims.

But since this is a Nation of Hypocrites, the local media houses will not permit this to be the case, but to be free one has to face the truth, and truth is there for everyone to see. Kigoma region is flexing it's muscle with oil, and I dont know which other part of Tanzania with a large population of muslims will take to the streets, even though they will soon go for the Diocese of NECTA and Dr Ndalichako!! As I told you before, the cat is out of the bag, things will never be the same again.

The funniest thing of all is, ili kuendelee kuwepo na amani eti ni kwa Waislamu waendelee kukubali kudhulumiwa, day in, day out, that's hogwash at it's best. Inahitaji wazalendo wa kweli kurekebisha hali ya mambo ili Taifa lisonge mbele, lakini kwa mtindo huu wa kubadili maneno na kuwapa watu majina ya ndivyo sivyo, hamkani mambo si shwari. Thes are just my thoughts though, you can always correct me as am a human being like the rest.

BYE FOR NOW.

Thursday, September 13, 2012

Polisi Anayedaiwa Kumwua Daudi Mwangosi Afikishwa Kizimbani

Huyo polisi mwenye miaka 23 inawezekana ni ' trigger happy'.  Yaani alikuwa na hamu sana ya kuonyesha upolisi wake na kutumia silaha yake.  Ndo tatizo la kuwapa watu wasiokomaa kiakili silaha. Rest in Peace Daudi Mwangosi.

*****************************************************
Kutoka Ippmedia.com

Mwangosi Killing: Policeman Charged


By The Guardian Reporter

13th September 2012
Police Constable Pacificus Cleophace Simoni (23) appeared before Iringa District Court yesterday charged with the murder of Channel Ten journalist Daudi Mwangosi.


The accused with a white hood draped over a good part of his face, and in a black jacket was escorted into the court by more than seven police officers.

The Public Prosecutor Michael Luena told Senior Magistrate Dyness Lyimo that Constable Simoni with number G2573 residing at FFU quarters in Iringa municipality killed Daudi Mwangosi on September 2 this year at Nyololo village in Mufindi District in Iringa region.

The accused was not allowed to enter any plea because the court has no jurisdiction over murder cases.

The case was adjourned to September 26 this year and he was remanded in custody since the charges facing him are not bailable.

Meanwhile, Home Affairs Minister Dr Emmanuel Nchimbi has said that the probe committee he formed to investigate the murder will continue with its work.

In a statement released in Dar es Salaam yesterday Minister Nchimbi said that the probe committee will continue with its work with a view to get a lasting solution to the misunderstandings between police and journalists and police with political parties.

He said the move also will help to improve the relations between police and civilians, calling on all stakeholders to allow the law to take its course.

Mwangosi who was a Channel Ten Representative in Iringa was killed on September 2 this year at Nyololo village in the region following skirmishes between police and Chadema supporters.

On Tuesday journalists countrywide staged a demonstration to condemn the brutal killing of their colleague vowing to continue pressing the government to take action against all people involved in the killing.

The journalists called on police to respect their work just as journalists recognise and respect members of the force.

Mwangosi who was born in 1972 was buried at Msoka village in Mbeya region on September 4 this year. He is survived by a wife and four children.

SOURCE: THE GUARDIAN

Wednesday, June 06, 2012

Hivi Lulu Ana Miaka Mingapi?

Wadau,  jumatatu ijayo mahakama itasikiliza kesi kujadili umri wa Lulu Michael Kimemeta.  Lulu anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumwua Bongo Superstar, Steven Kanumba.

Hayo ndio matokeo ya kutaka kukua haraka. Mwaka jana Lulu alifanyiwa Birthday Party kubwa ya kusherekea Birthday yake ya 18. Mwenyewe Lulu katika mahojiano na waandihi wa habari kasema ana miaka 18. Kakbiliwa na shitaka la kuua na sasa ana miaka  16 mara 17! Duh!  Msipende kukua haraka wadau!

********************************************


Elizabeth 'Lulu' Michael Kimemeta
 Court ruling on Lulu’s age set for early June


Monday, 28 May 2012

By Rosina John

The Citizen Correspondent

Dar es Salaam. The High Court will on June 11 rule on an application by lawyers of actress Elizabeth Michael alias Lulu seeking a court order to determine her age.

Judge Faud Twaib will give the ruling after both parties concluded their submissions yesterday whereby the prosecution asked the court to dismiss the application because it was filed contrary to the law.

Lulu is charged at Kisutu Resident Magistrate’s Court with murdering local movie star Steven Kanumba on April 7, this year, at Sinza Vatican.

Advocate Peter Kibatara filed the application at the High Court seeking an order to the lower court to determine the age of the accused.Mr Kibatara is requesting for the court to transfer the murder case to juvenile court because the suspect is underage.

According to the lawyers, the accused has not attained the age of 18 years to merit prosecution in the adult court.

However, the lower court said it has no jurisdiction to entertain any application because the charge before it involves murder.

In the application, advocate Kibatala said the lower court has power to investigate the age of the accused according to section 113 of the Child Act.

“But the High Court, seeing that the lower court cannot make an investigation, should do so to satisfy itself that the accused is a child,” said Kibatala.

For their part, prosecution led by State Attorney Shadrack Kimaro asked the court to dismiss the application for lack of merit.Kimaro said that the law cited by the defence counsel in the application does not give authority to High Court to give the order.

According to Kimaro, the defence is required to appeal or seek review on the lower court’s decision instead of filing the application.But if they decided to file the application they should cite a section of the law that gives the High Court authority to give the order.

Monday, April 23, 2012

Lulu Mahakamani Kisutu Leo

 Mcheza sinema Elizabeth 'Lulu' Michael alifikishwa katika mahakama leo kuhusiana na kesi yake kuhusiana na mauji ya Bongo Star Steven Kanumba.  Kesi leo ilikuwa ni kutajwa tu yaani Mention.
Mcheza Sinema, Elizbeth 'Lulu' Michael, katika Mahakama ya Kisutu leo hii 23/4/12 (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)  Kuona picha zaidi Mtembelee Kaka Michuzi


Katika hii picha ya Global Publishers Lulu anaonekana kuwa na kakitambi!   (picha kwa hisani ya Global Publishers)

MAELEZO KUTOKA GLOBAL PUBLISHERS

Mwigizaji Maarufu wa filamu za Kibongo Elizabeth Michael ‘Lulu’ leo majira ya saa nne asubuhi amepandishwa kizimbani kwa mara ya pili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam na kusomewa shitaka la kumuua Steven Kanumba. Baada ya kusomewa shitaka hilo na Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Mahakama hiyo Elizabeth Kaganda mbele ya Hakimu Rita Tarimo hakutakiwa kujibu lolote. Mwendesha Mashitaka huyo alisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamailika hivyo kesi hiyo iliahirishwa mpaka Mei 7 mwaka huu.


Wednesday, April 11, 2012

Lulu Mahakamani Kisutu Leo!

Lulu Akijiandaa kuacti Sinema
Hayati Steve Kanumba ni miongoni mwa wasanii maarufu wa Tanzania wenye nyota za umaarufu (Tanzania Walk of Fame) ndani ya ukumbi wa Dar Live jijini Dar Es salaam ambapo mara baada ya kifo chake wafanyakazi wa ukumbi huo na mashabiki wake wameweka mashada ya maua,kadi na kuwasha mishumaa kama ishara ya kuomboleza kifo chake.
 (Picha kw Hisani ya Abdallah Mrisho Blog)
MAELEZO KUTOKA MICHUZI BLOG:

Muigizaji wa Filamu nchini anaehusishwa na kifo cha Muigizaji Mwenzie, Marehemu Steven Kanumba,Elizabeth Michael a.k.a Lulu amepandishwa kizimbani mapema leo asubuhi kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam kwa kusomewa mashtaka yake kuhusiana na kuhusika kwa kifo cha Muigizaji huyo nguli hapa nchini.


Elizabeth Michael amesomewa mashtaka hayo mbele ya hakimu Agustino Mmbando na wakili Elizabeth Kaganda ya mauaji ya Muigizaji wa Filamu nchini,Marehemu Steven Kanumba yaliyotokea huko sinza vatcan jijini Dar es Salaam april 7 mwaka huu.

Elizabeth Hakutakiwa kujibu chochote Mahakamani hapo kwani mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Kesi hiyo imeahirishwa na kupangwa kusikilizwa tena april 23 mwaka huu.

Muigizaji huyo aliletwa mahakamani hapo kwa mwendo wa kasi kama mshale na kwa ulinzi mkali na pia ndivyo alivyoondolewa Mahakamani hapo kiasi kwamba hakuna hata mwandishi alieweza kupata picha ya Muigizaji huyo mwenye tuhuma za mauaji Na kupandishwa katika gari ndogo nyeupe aina ya suzuki grand vitara yenye nambari za usajiri T 848 BNV huku kwenye kioo nambari zake zikisomeka PT 2565.

********************************************************************

Lulu kortini kwa kumuua Kanumba

Polisi wamficha, wakwepa waandishi
Ajifunika ushungi, avaa kandambili

Msanii wa uigizaji wa filamu nchini, Elizabeth Michael Kimemeta (18), maarufu kama Lulu, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, akikabiliwa na mashtaka ya mauaji ya msanii mwenzake, Steven Kanumba (28).

Tukio la msanii huyo kufikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashtaka lilikuwa kama mchezo wa filamu baada ya polisi kufanya siri na hata kugombana na baadhi ya waandishi wa habari waliotaka kuingia katika chumba cha mahakama kufuatilia kesi hiyo.

Kesi hiyo ilisomwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo, Augustina Mmbando.

Kabla ya kusomewa mashtaka hayo, hakimu alimtaka Lulu kutojibu chochote kuhusu tuhuma zinazomkabili.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda, alidai kuwa Aprili 7, mwaka huu katika eneo la Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alimuua Kanumba.

Kwa mujibu wa Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), Lulu hakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji.

Hata hivyo, mara upelelezi utakapokamilika, kesi hiyo itahamishiwa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kusikilizwa.

Kaganda alidai upelelezi bado haujakamilika, hivyo akaiomba mahakama kupanga tarehe ya kuitajwa kwa kesi hiyo.

Hakimu Mmbando alisema mshtakiwa atakaa mahabusu hadi Aprili 23, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa.

Wakati mshtakiwa huyo akisomewa hati ya mashtaka alidai mahakamani hapo kwamba, umri wake sio miaka (18) kama ilivyoandikwa kwenye hati ya mashtaka bali ana miaka (17).

Pia wakati mashtaka yanasomwa hali mahakamani hapo ilikuwa shwari, huku watu wengine wakinong’ona bila kuwa na uhakika kuhusu msanii huyo kufikishwa mahakamani kutokana na kutoonekana kwa wanafamilia wake na watu wa karibu.

Mazingira ya Lulu kufikishwa mahakamani hapo yalikuwa kama mchezo wa kuigiza kutokana na jeshi la polisi kufanya kuwa siri kubwa.

Gari aina ya Suzuki Vitara liliingia katika viunga vya mahakama hiyo muda ambao haukufahamika likiwa na makachero wa Jeshi la Polisi wanne, wanawake wawili na wanaume wawili na mshtakiwa.

Lilifuatiwa na gari lingine aina ya Toyota Land Cruiser lililokuwa na askari polisi saba waliovaa sare za jeshi hilo wakiwa na silaha.

Hata hivyo, baada ya muda NIPASHE kupitia chanzo chake ilipata taarifa ya msanii huyo kufikishwa katika viunga vya mahakama hiyo na kwamba jalada la kesi yake lilikuwa limeshapangiwa hakimu.

Hatua hiyo ilisababisha waandishi wa habari za mahakama kujipanga na kuweka lindo katika kila kona ya jengo la mahakama hiyo huku wengine wakiwa kwenye mlango wa kutokea mahabusu, kwenye korido za milango ya kuingia katika ofisi za mahakimu.

Hata hivyo, kundi la waandishi waliokaa katika korido ya ghorofa ya kwanza kuelekea kwenye ofisi za mahakimu, ghafla saa 5:20 asubuhi walifanikiwa kumuona mshtakiwa huyo akiwa katikati ya makachero wanawake wawili na nyuma wanaume wawili akiwa amejifunika ushungi wa rangi ya udhurungi, gauni kubwa maarufu kama ‘dira’ la rangi ya njano na kandambili za rangi nyekundu.

Waandishi hao walikimbilia msafara huo uliokuwa na askari wanne pamoja na mshtakiwa, lakini kabla ya kuingia chumba cha hakimu, askari aliyekuwa ameshika simu ya upepo mkononi aliwazuia waandishi kuingia.

Hali hiyo ilisababisha majibishano ya muda na mwishowe alibadili nia ya kuzuia wanahabari hao kufanya kazi yao.

Mshtakiwa alisomewa mashtaka yake na baadaye alipitishwa njia ya mlango wa nyuma hadi kwenye gari aina ya Suzuki Vitara yenye namba za usajili T848 BNV yenye vioo visivyoonyesha ndani (tinted).

Ingawa gari hilo lilikuwa na namba za kirais, kwenye vioo liliandikwa namba PT 2565, na iliondoka mahakamani hapo kwa kasi kumpeleka mshtakiwa mahabusu ya Segerea kusubiri upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Mapema jana saa 3:35 asubuhi, NIPASHE ilizungumza kwa njia ya simu na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Charles Kenyela kuhusu hatima ya kufikishwa mahakamani kwa msanii huyo, mazungumzo yalikuwa kama ifuatavyo:

NIPASHE: Shikamoo afande.

Kamanda Kenyela: Marahaba. Nipigie baadaye niko kwenye kikao.

NIPASHE: Sawa afande. Lakini nilitaka kujua kama Lulu atapelekwa mahakamani leo (jana) na itakuwa mahakama gani Kinondoni au Kisutu?

Kamanda Kenyela: Mmmh! Kwa kweli bado uchunguzi unaendelea. Hivyo, jalada liko kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP).

NIPASHE: Ahsante afande. Shida yangu ilikuwa hiyo tu endelea na ujenzi wa Taifa.

Kamanda Kenyela: Nashukuru sana mwandishi.

Kanumba alifariki dunia usiku wa kuamkia Jumamosi Aprili 7, mwaka huu, baada ya kudaiwa kutokea ugomvi kati yake na Lulu.

Maelfu ya watu, wakiwamo mawaziri, wabunge, viongozi wa siasa, vyama vya kiraia, wasanii wenzake na wananchi wa kawaida, walijitokeza katika msiba huo nyumbani kwake, Sinza Vatican, jijini Dar es Salaam na kwenye shughuli za kumuaga viwanja wa Leaders Club na kuuzika mwili wake katika makaburi ya Kinondoni.

Mazishi hayo yaliongozwa na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal.


CHANZO: NIPASHE