Showing posts with label Soccer. Show all posts
Showing posts with label Soccer. Show all posts

Saturday, June 24, 2017

Shujaaz Wawafunda Waandaaji wa Mashindano ya East Africa Cup 2017

Mkuu wa utafiti wa Kampuni ya Well Told Story,Dkt Anastasia Mirzoyants akitoa maelezo kwa washiriki wa Warsha iliyoandaliwa na  Mradi wa Shujaaz  iliyofanyika Hotel ya Uhuru mjini Moshi.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha iliyoandaliwa na watayarishaji wa Mradi wa Shujaaz kwa ajili ya kutoa eimu juu ya maswala mbalimbali ikiwemo Ujasiliamali pamoja na Kilimo,Warsha ambayo inafanyika sambamba na Mashindano ya Kimataifa ya Vijana kwa vijana wa nchi za Afrika Mashariki.
Mkuu wa utafiti wa Kampuni ya Well Told Story,Dkt Anastasia Mirzoyants akitoa maelezo kwa washiriki wa Warsha iliyoandaliwa na  Mradi wa Shujaaz  iliyofanyika Hotel ya Uhuru mjini Moshi
Washiriki katika Warsha hiyo.
Mkuu wa utafiti wa Kampuni ya Well Told Story,Dkt Anastasia Mirzoyants akizungumza na Wanahabari mara baada ya kumalizika kwa Warsha iliyoandaliwa na  Mradi wa Shujaaz  iliyofanyika Hotel ya Uhuru mjini Moshi
Baadhi ya Vijana waliofanikiwa kuingia katika Kijiji cha Shujaaz wakionesha umahiri wao katika uimbaji ambapo pia walipata zawadi kutoka Shujaaz.
Timu za watoto chini ya miaka 13 za Msimamo na Right to Play kutoka Dar es Salaam zikichuana katika mashindano ya East Africa Cup 2017 yanayofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari ya Moshi Ufundi.
Vijana chini ya miaka 13 wakioneshana umahiri  katika kusakata soka katika mashindano ya East Africa Cup 2017 yanayofanyika katika viwanja vya Moshi Technical.
Baadhi ya vijana wakifuatilia mchezo huo.
Katika Kijiji cha Shujaaz wakishiriki michezo mbalimbali ikiwemo ya kukimbia huku wakiwa ndani ya magunia.
Kijiji cha Shujaaz kimekuwa kivutio kikubwa kwa vijana wanaoshiriki mashindano ya East Africa Cup 2017.

Na D ixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

Tuesday, July 08, 2014

Brazil Wapondwa Vibaya na Ujerumani Katika Mashindano ya World Cup!

Katika Mashindano ya Kombe la Dunia huko Brazil, Brazili ilipondwa vibaya sana na Ujerumani!  Brazil wameanguka  1-7.  Duh! Hata Pele ana aibu!

Kwa habari za Ushindi wa Ujerumani BOFYA HAPA:

Shabiki wa Brazil akilia machozi baada ya Brazil Kutolewa katika mashindao ya World Cup. Unaweza kuona picha zaidi kwa  KUBOFYA HAPA:

Saturday, August 25, 2012

Mpira London


MASHABIKI ARSENAL WAMTEMEA MOTO ROBIN VAN PERSIE

Urban Pulse na Freddy Macha waweletea habari moto moto siku moja baada ya kutangazwa kuhama kwa mshambuliaji na nahodha wa Arsenal, Robin Van Persie kwenda Manchester United  adui  wake mkubwa. Mahojiano yalifanywa kando kando ya uwanja maarufu wa Emirates ambapo washabiki walikuwa wakielekea kufurahia mechi ya kwanza ya ligi (2012-2013) baina ya Arsenal na Sunderland.


Monday, March 12, 2012

Tanzia - David Mwakipunda


TANZIA

 

Marehemu David Mwakipunda

 FAMILIA YA  MZEE NSUBISI SAMUEL MWAKIPUNDA INASIKITIKA   KUTANGAZA KIFO  CHA BWANA DAVID SAMUEL MWAKIPUNDA(MCHEZAJI WA ZAMANI TIMU YA MPIRA WA KIKAPU-PAZI)  KILICHOTOKEA SIKU YA JUMAPILI TAREHE 11/03/2012.MAZISHI YATAFANYIKA MAKABURI YA KINONDONI DAR ES SALAAM  SIKU YA JUMATANO TAREHE 14/03/2012. HABARI ZIWAFIKIE NDUGU JAMAA NA MARAFIKI POPOTE PALE WALIPO.

“BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE” .

Monday, July 12, 2010

Mabomu Yaua Watu 74 Uganda

Watu walioenda klabuni kutazama Mashindano ya Kombe la Dunia huko Kampala, Uganda wameuaua katika shambulizi la mabomu.

Kwa sasa kundi fulani la magaidi kutoka Somalia wanasema kuwa wao ndo walitenda huo unyama. Wamediriki kufungua hata website ya kupokea pongezi!

Jamani, mnaua waafrika wenzenu, binadamu kwa ujumla halafu mnataka kupongezwa? Kweli mwisho wa dunia iko karibu!

Mungu alaze roho za waliokufa mahala pema mbinguni. AMEN. Mungu wape nguvu familia ya marahemu katika kipindi hiki kigumu.

Kwa habari zaidi someni:

http://news.bbc.co.uk/2/hi/world/africa/10605457.stm

http://edition.cnn.com/2010/WORLD/africa/07/12/uganda.bombings/index.html?hpt=P1&fbid=4CVcBwhbh2z

Wednesday, June 09, 2010

Waandishi wa Habari Waibiwa Afrika Kusini!!!

Duh! Hii kali. Waandishi wa habari walioenda kwenye mashindano ya World Cup, huko Afrika Kusini wameibiwa hotelini kwao! Kazi ipo. Picha waliokuwa wanajenga kuwa Afrika Kusini ni salama, hakuna wezi wala vibaka, watu wanapendana inadoa kubwa kweli sasa.

******************************************************************************

World Cup Journalists Robbed

By Richard Allen Greene, CNN

(CNN) -- Three journalists covering the World Cup in South Africa were robbed of money, passports, cameras and computers early Wednesday, police said.
Armed suspects entered three hotel rooms where the journalists were staying near the town of Magaliesburg, police Col. Charmaine Muller told CNN.
Two of the victims "slept through the whole thing", but a Portuguese photographer woke up as it was taking place at about 4 a.m. local time (10 p.m. Tuesday ET), she said.
A suspect pointed a gun at him and told him to keep quiet, she said.
Police were called after the suspects left and are still investigating, she added. No one has been caught yet.
Hundreds of thousands of sports fans and journalists are descending on South Africa for the World Cup soccer tournament, the biggest sporting event in the world this year. It begins Friday.

Tuesday, April 22, 2008

Tazama Mechi Hapa!

Dada Subi ameniletea linki hii:

*********************************************

Samahani kwa kuchelewa kuleta tangazo (nilikuwa najihudhurisha mbele ya liwali asinisahau kwenye ujira)ni hivi, nimebandika link hapa: http://nukta77.com/soccer.aspx mtu kuweza kuchagua pa kutizamia mechi za michezo mbalimbali ikiwemo huu wa soka/futiboli la leo (Liverpool vs Chelsea)

Kwa wale washamba wa vijiji vya USAgara/USA river na vitongoji vyake, huu ndiyo wakati mzuri wa kwenda sambamba na walioko Tz
Subi

Monday, September 10, 2007

Poleni Taifa Stars, lakini Mmejitahidi!


MAMBAS (Msumbiji) 1- TAIFA STARS - 0

Hiyo mechi ilikuwa kali na mlijitahidi sana. Mjipongeze kuwa mliweza kufika mbali safari hii!

WaTanzania na wapenzi wa Kandanda tusikate tamaa. Ni kweli moyo unauma, lakini Taifa Stars wameonyesha kuwa na sisi tumo katika ngazi na kimataifa kwa mchezo wa kandanda.

******************************************************************************
From ippmedia.com

Lawama sasa zamwandama Maximo

2007-09-10

By Mwandishi Wetu,

Baada ya timu ya taifa, JK Boys, kuchapwa bao 1-0 na timu ya taifa ya Msumbiji `Mambas` (nyoka wakali), baadhi ya wapenzi wa soka wameanza kumuangushia lawama nzito kocha mkuu, Marcio Maximo.

Hata hivyo, kabla ya lawama hizo kuanza kutolewa, Maximo tayari aliwataka Watanzania kuyapokea matokeo yoyote ya mechi hiyo pasipo kumlaumu yeyote. Wakizungumza mara baada ya mechi hiyo iliyochezwa juzi usiku, wapenzi hao akiwemo Shaaban Alexander `Chama`, amesema kitendo cha Maximo kuwakumbatia wachezaji anaowapenda na kuwapanga uwanjani bila msaada, ndicho kimechangia timu kufungwa.

``Kuna wachezaji ambao Maximo huwezi kumweleza kitu, atawapanga tu ingawa hawana msaada wowote...angalia Joseph Kaniki aliyeingizwa dakika chache alivyochangamsha,`` amedai Chama.

Aidha, amesema haungi mkono kitendo cha kocha Maximo kumuacha mshambuliaji Kudra Omari ambaye amekuwa kinara wa ufungaji mabao katika michuano ya ligi ndogo na ile ya Tusker. ``Sijui ni kigezo gani anachotumia huyu kocha kuchagua washambuliaji, inawezekana anashikwa masikio na watu, afanye kazi aliyoijia nchini bila kuelekezwa,`` amesema.

Naye shabiki mwingine, John Edward `Edu`, amelalamikia kitendo cha kocha huyo kushinikiza timu hiyo kwenda `kutalii` Ulaya wakati kulikuwa na timu nyingi za kiafrika zakuweza kupimana ubavu na JK Boys.

``Hakuwa na sababu ya kupeleka timu Ulaya, au timu za Afrika anaziogopa iwapo zingetufunga...hizo timu walizocheza na Stars Ulaya si lolote hazifahamiki kabisa,`` amehoji shabiki huyo. Tanzania imekosa nafasi ya kuingizwa katika `kapu` baada ya kipigo hicho, huku Senegal wakipanda ndege mwakani kuelekea moja kwa moja Ghana baada ya kushika nafasi ya kwanza kwa kuibugiza Burkina faso mabao 5-1.

Saturday, September 08, 2007

Taifa Stars Billboard in Dar

Taifa Stars wakishinda mechi yao itakuwa mara ya kwanza tangu 1980 kwenda fainaili ya Nations Cup! Mechi leo ni dhidi ya timu Mambas wa Msumbiji.
TUNAWATAKIA KILA LA HERI !