Tuesday, May 20, 2008

Polisi Msumbiji waambiwa "PUNGUZENI VITAMBI!"

Leo kuna habari kuwa polisi huko Msumbiji wameamuriwa wapunguze vitambi kwa vile wanashindwa kutekeleza kazi yao. Habari inasema hao wenye vitambi wanashindwa kukimbiza wahalifu hivyo inabidi wavipunguze. Wanasema vitambi hivyo vinasababishwa na pombe na sigara.

Serikali ya Msumbiji imetoa amri kuwa lazima polisi wote wafanya mazoezi ili wawe 'fiti'!

Jamani, sasa wakileta amri kama huo Bongo si itakuwa kasheshe. Maana nakumbuka kuona mapolisi wengi kweli na vitambi.

Kusoma habari zaidi nenda:

http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7408199.stm

Vazi la Taifa


Wadau, nimeona hii picha kwenye blogu ya Michuzi. Anasema hii ni vazi la kitaifa la akina mama. Siyo mbaya, na ina lubega. Naona kama kitambaa ni kaniki iliyo pambwa na bendera. Lakini mshono si mbaya kwa kweli.
Mnaoinaje?

Polisi Enzi za Tanganyika


6th February 1963: The Tanganyika Police Guard of Honour line up beneath Mount Kilimanjaro, during the Afro-Asian Solidarity Conference in Moshi, in modern Tanzania. (Photo by Keystone/Getty Images)

Monday, May 19, 2008

Mjue Msanii Miriam Chemmoss



Huko Bongo Celebrity kuna Mahojiano na Msanii/Mrembo Miriam Chemmoss.
Kutoka Bongo Celebrity:


Endapo kuchanganya utaifa,damu na tamaduni mbalimbali ni mojawapo ya chachu za mafanikio fulani hapa duniani, basi ushahidi wa dhana hiyo unaweza kuupata kwa kuangalia maisha ya mrembo Miriam Chemmoss(pichani).

Miriam ni muigizaji,mwimbaji,mtunzi wa nyimbo na pia mwanamitindo (model) ambaye mpaka hivi leo ana haki ya kusimama na kujivunia rekodi yake katika ulimwengu changamani wa sanaa na maonyesho.Mwenyewe anasema safari yake ndio kwanza inaanza kwani bado ana ndoto na malengo chungu mbovu ya kutimiza.Hivi leo kazi zake nyingi anazifanyia kutokea jijini New York nchini Marekani anapoishi.

Kama ilivyo kwa wasanii wengi,safari ya Miriam katika ulimwengu wa sanaa inaanzia tangu akiwa mwanafunzi mdogo.Lakini ni pale alipohamia jijini New York mwaka 2004 na kujiunga na kundi maarufu lililojulikana kama The Marvallettes Revue lililokuwa chini ya Pam Darden, ndipo nyota yake ilipoanza kung’ara ipasavyo. Baadaye alijiunga na kundi lingine maarufu la Soukouss Stars kama mwimbaji pekee wa kike na mnenguaji kabla ya kuamua kuimba peke yake(solo artist) mwaka 2006.

Kwa upande wa uigizaji,Miriam ameshaigiza katika show mbalimbali maarufu ikiwemo ile ya “District” katika kituo maarufu cha televisheni cha CBS.Pia ameshiriki katika “Bedford Diaries” ya Warner Bros.Sauti yake imetumika katika matangazo mbalimbali ya biashara kama vile Western Union(USA-African Market) nk.Kwa upande wa mavazi Miriam amewahi kuwa model wa jeans za Levi’s,Getty Images/Brazilian Salsa Club(Print),Bebe Noir Clothing Line,New York nk.Mwaka 2007 mtandao wa Jamati.com ulimtaja Miriam katika orodha yao ya Top 10 Sexiest African Women akiwa ni miongoni mwa wasichana wawili kutoka eneo la Afrika Mashariki.

BOFYA HAPA KUSOMA MAHOJIANO NA MIRIAM CHEMMOSS



http://bongocelebrity.com/2008/05/18/one-on-one-with-miriam-chemmoss/#more-1417

Wananchi Afrika Kusini waua Wageni Nchini Mwao!

MMalawi akiokolewa na Polisi!

Waafrika Kusini wakisherekea kupigwa na kuuliwa kwa wageni nchini mwao!

Leo kuna habari ya fujo zilizotokea huko Afrika Kusini. Wanasema kuwa wananchi wenye hasira wanaua wageni/wahamiaji kutoka nchi zingine amboa wako kwao. Mpaka sasa watu 22 wameuliwa. Kisa eti ni chanzo cha wao kukosa kazi! Wengi ya waliouliwa wanatoka nchi za kiafrika kama Zimbabwe, Mozambique na Malawi.
Wageni huko wanakimbilia vituo vya polisi na makanisani kuomba hifadhi kusudi wasiuliwe.

Hivi Afrika Kusini imelaaniwa nini? Watu ni wepesi kusahau. Miaka mingapi Tanzania na nchi nyingi za dunia ziliwasaidia waAfrika Kusini mpaka walivyopata Uhuru wao. Mnakumbuka Mwalimu Nyerere alivyozuia timu ya Olympiki ya Tanzania kushiriki katika michezo kwa vile Wazungu kutoka Afrika Kusini walikuwa wanashiriki wakati weusi huko wananyanyaswa na Apartheid? Mnakumbuka Dakawa na Mzimbo huko Morogoro? Na tusisahau hao WaSouth Africa walioacha mbegu Bongo!

Hebu tukumbuke ni MSouth Africa aliyesababisha ajali iliyotoa roho mpendwa Waziri Mkuu wetu, Edward Moringe Sokoine! Na yule jamaa yuko wapi? Je, ni moja wa hao wanaotaka kuona waBongo huko wanauliwa!

Askofu Desmond Tutu amewaomba waache kuua watoto wa watu waliowasaidia kutoka kwenye mikono ya Apartheid. Ni aibu!

Kwa habari zaidi someni:

Mzungu achomwa kisu moyoni kwenye Mchezo wa Ngono!

Wazungu wamebuni michezo ya ajabu ya ngono. Wengine wanaenda kwa DOMINATRIX, kusudi watendewe.

Sasa kuna mchezo wa kuchukua kisu na kuitumia kuchora kwenye mwili wa mpenzi wako. Wakati huo mko kazini yaani 'juu/chini'!

Huko Ottawa, Canada kuna mzungu alimwomba mpenzi wake achore moyo kwenye kifua chake juu ya moyo wake. Sijui yule dada alikuwa amenogewa na utamu wa tendo mpaka kajisahau, kaishia kumtoboa kifua mpenzi wake na ilichoma moyo! Madaktari walidhani jamaa hatapona lakini ilikuwa si wakati wake na hajambo sasa.

Jamaa anasema bado anapenda mpenzi wake ingawa alimchoma kisu moyoni. Walikuwa mchezoni katika mapenzi! Pia walikuwa wamelewa!

Polisi walimfungulia mashitaka yule dada, na kapewa miaka mitatu 'Probation'Yaani hataenda jela kama hatatenda kosa lingine kwa miaka mitatu.

*****************************************************************************

Canadian pierces lover's heart in botched sex game

Fri May 16, 2008

OTTAWA (Reuters) - A Canadian man who asked his lover to carve a heart-shaped symbol on his chest during a rough sex game almost died when she accidentally pressed too hard and punctured his heart, a newspaper said on Thursday.

The Winnipeg Free Press said the 25-year-old woman had been sentenced to three years' probation after she pleaded guilty to assaulting the man in February 2007.

The 24-year-old man was initially given little chance of survival but made a full recovery and is backing the woman. Both had been drinking heavily and engaging in rough sex when he asked the woman to carve the symbol, the paper said.

Kwa habari zaidi soma:

http://thechronicleherald.ca/Canada/1055957.html

Saturday, May 17, 2008

Zimamoto Kazini Cambridge Leo I

Nyumba ikiungua moto kwenye kona ya River St. na William St., Cambridge MA leo.

Zimamoto Kazini Cambridge Leo II

Zimamoto Kazini Cambridge Leo III

Karibu na napokaa kuna nyumba ulianza kuunga moto. Bahati wameiwahi. Tunasikia harufu ya moshi. Zimamoto na polisi wamefanya evacuation ya nyumba karibu na pale. Nyumba iliyoungua iko karibu na sehemu ya kufua nguo (laundromat) mtaani River St.


Gari ya Polisi ikizuia magari kupita mtaa wa Pleasant St. kwenda River St.
Gari ya Polisi ikiuia magari kupita River St. Hiyo basi No. 70 ilikwama hapo hapo! Abiria walishuka na kutembea kwenda Central Square. Zimamoto juu ya nyumba inayoungua River. St.

Mzimamoto akivaa nguo zake haraka kwenda kuwasaidia wenzake
Gari ya Zimamoto, Chifu wa Zimamoto wa Cambridge ni yuke aliyevaa koti ya njano
Fire Hydrant (Bomba la maji) ambayo walitumia kupata maji kuzima moto. Wadau Mareknai mnajua ni mwiko kuegesha magari mbele au karibu sana na hydrant maana utapata faini kali! Iko kwenye kona ya River na Pleasant St.



Yalikuja zimamoto kutoka vikosi vyote vya Cambridge






Zimamoto walipanda kwenye fire escape ya hiyo nyumba Pleasant St. na kucheki kama kuliwa na watu ndani. Waliamuru watu wanaokaa block yote ile ya Pleasant na River watoke kwenye fleti zao kwa usalama wao.

Friday, May 16, 2008

Staili Mpya ya Viatu vya Akina Dada

VIATU VYA KARNE YA 21!
Naona Akina Dada wanaovunjika miguu watakuwa wengi huko Emergency Room. Hivi unatembeaje na hivi viatu? Eti hivi viatu vimekuwa fesheni Japani.











Ellen DeGeneres anaoa!


Yule shoga ambaye anajulikana kuliko wote hapa Marekani, Ellen Degereneres (50) ametangaza leo kuna anaoa! Ndiyo, anaoa na siyo kuolewa! Anamwoa mpenzi wake, mrembo Portia DeRossi.

Jana, mahakama huko California waliamua kuwa ni ruksa kwa wasenge na mashoga (wapenda jinsia moja) kufunga ndoa kama wanavyofanya hapa kwetu Massachusetts. Bila kuchelewa Ellen katangaza habari yake 'njema'.
Kama mnakumbuka zamani shoga wa Ellen alikuwa mcheza sinema, Anne Heche. Walikorofishana halafu Anne alienda kuolewa na mwanaume!
Hivi kwenye honeymoon wanafanya nini hao?

*************************************************

LOS ANGELES, California (AP) -- Ellen DeGeneres is putting the California Supreme Court ruling in favor of gay marriage into action -- she and Portia de Rossi plan to wed, DeGeneres announced during a taping of her talk show.

During a taping of her TV show, Ellen DeGeneres says she plans to marry her girlfriend, Portia de Rossi.

DeGeneres was taping the episode of "The Ellen DeGeneres Show" on Thursday, the day the state's high court struck down California laws against gay marriage, and it was to air Friday, a person close to the production said.

The person, who was not authorized to discuss the matter publicly, spoke to The Associated Press on the condition of anonymity.

Citing the court's ruling, DeGeneres said she and girlfriend de Rossi ("Ally McBeal," "Nip/Tuck") would be getting married.

De Rossi, 35, who was in the studio, and DeGeneres, 50, were applauded by audience members, the person close to the production said.

CCM Bangalore, India



KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!

CCM JUU,JUU, JUU ZAIDI!
CHAMA CHETU CHA MAPINDUZI YAJENGA NCHI!

Wednesday, May 14, 2008

Kitoweo Barabarani



Hapa kwetu Cambridge/Boston kuna bata kibao. Zamani wazungu walikuwa wanawawinda kwa ajili ya chakula. Siku hizi na supermarket hawana haja nao. Kwanza wamesahau utaalamu wa kuwinda, hata kuisafisha baada ya kuchinja hawawezi. Bahati yao hao bata wamekuwa kama pets tu. Wanabakia kuwaangalia tu.

Hii picha nilipiga leo maeneo ya Alewife, Cambridge.

Black President!

">

Cheki hao waJamaica wa Kizungu wanavyomshabikia Obama!

Tuesday, May 13, 2008

Binti wa miaka 12 afundishwa kuwa Dominatrix

Dunia hii! Leo kuna habari kuwa dada fulani huko Missouri aalifundishwa kuwa Dominatrix tangu ana miaka 12. Alilazimishwa kufanya kazi hiyo na wazazi wake.

Kwa wasiojuo Dominatrix ni wale akina mama wanaolipwa kutesa wanaume kingono. Hao wanaume wanjipeleka wenyewe huko. Tena wengine watu wa makamu na wazee! Dume anaweza kuchapwa viboko pia. Kwa yale matendo ya ajabu kabisa inabidi mwanaume avae nepi maana anaweza kujikojolea au kujinyea. Wazungu wanapenda sana hiyo shuguli.

Dominatrix analipwa kumpiga mwanaume, kufanya naye ngono, kumfunga pingu na makufuli na madubwasha mengine kusudi asiweze kukimbia. Hapa Boston kuna dume alikufa huko kwa dominatrix.

Hao madomintarix hawana haya hata kidogo. Wanatangaza biashara zao wazi.

Police wanasema huyo dada aliyekamatwa leo kwa sasa ana miaka 2o. Wanasema kuwa alilazimishwa kufanya ngono na wanaume na baba yake wa kambo tangu ana miaka 12. Alilazimishwa kuangalia sinema za pono pia. Mama yake mzazi alitoa baraka zote.

Duniani kuna mambo!

*************************************************************

KANSAS CITY, Missouri (AP) -- Federal prosecutors have unsealed an indictment accusing a man and woman of training the woman's child to be a dominatrix, selling her sexual services and photographing some of the acts.

U.S. Attorney John Wood said the case is unusual in that a parent has been charged with the commercial sex trafficking of his or her own minor child.

Todd B. Barkau, 35, of New York state, and the 44-year-old mother were charged in the seven-count indictment. They once lived together in Blue Springs, Missouri, where the sex business was allegedly run.

"Barkau obtained control of a 12-year-old girl and he groomed, trained and forced her to become a sexual dominatrix," Wood said at a news conference in Kansas City on Monday.

Kwa habari zadi BOFYA HAPA:

Mafisadi watajwa Bongo

Hivi kweli ni hao tu?

*********************************************************
Kutoka ippmedia.com

Mafisadi: Majina yatua ikulu

2008-05-13

Na Mwandishi wetu, Jijini

Hatimaye ile orodha ya watumishi wa Serikali wanaotuhumiwa kushiriki dili lililoiwezesha kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond kuweza kuingia mkataba wa kifisadi ulioiingiza nchi katika hasara ya mabilioni ya pesa imetua ikulu kwa ajili ya kusubiri hatua za kiutawala kuchukuliwa dhidi yao.

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda amesema tayari Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Philemon Luhanjo ameshakabidhiwa orodha ya wahusika na na kupewa maelekezo ya kuchukua hatua za kiutawala.

Amesema Bw. Luhanjo anatakiwa kuchunguza na kuwachukulia hatua watumishi wote wa Serikali wanaotuhumiwa na sakata hilo la mkataba `bomu` wa Richmond, lililozua gumzo kubwa nchini.

Akasema Katibu Mkuu Kingozi ataanza kwa kuwachukulia hatua watuhumiwa wote waliotajwa kwenye ripoti ya Kamati Teule ya Bunge, iliyochunguza mkataba wa Richmond.

Miongoni mwa watuhumiwa waliohusishwa na sakata hilo na kutakiwa kujiuzulu kutokana na kuzembea ama vinginevyo, kutokana na ripoti ya Kamati hiyo ya Bunge ni pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Johnson Mwanyika, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, Bw. Edward Hosea na Mkurugenzi wa Nishati na Madini katika Wizara ya Nishati na Madini Bw. Bashir Mlindoko.

Kwa mujibu wa mapendekezo ya kamati hiyo teule ya Bunge iliyokuwa chini ya Mwenyekiti wake Dk. Harrison Mwakyembe, kigogo mwingine anayepaswa kuchukuliwa hatua za kinidhamu ni Katibu Mkuu wa makosa yao au vinginevyo, kadiri sheria zitakavyoruhusu. ``Maelekezo yote amepewa Katibu Mkuu, suala hili sasa linafikia mwisho kwa kuwa anaandaa hatua za kuwachukulia, kama ni Wizara ya Nishati na Madini Bw. Arthur Mwakapugi.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Pinda, watuhumiwa hao wanaweza kutimuliwa kazini au kupunguziwa madaraka, kutokana na uzito wakuwafukuza kazi au kuwateremsha vyeo, well and good,`` akasema Bw. Pinda. Waziri Mkuu amesema hivi sasa Serikali haikubali kuchafuliwa na hivyo kila anayebainika kujihusisha na vitendo vya rushwa na ufisadi anawajibishwa.

SOURCE: Alasiri

Monday, May 12, 2008

Mh. Maua Daftari afiwa na Mumewe!

Hii habari ya kusikitisha sana. Pole sana Mh. Dk. Dada Maua Daftari. Mola akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu. Mola ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi. AMIN.

***************************************************************
Kutoka Michuzi Blog:

Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein akimfariji Naibu Waziri wa Mawasiliani Sayansi na Teknoloji Mh. Mauwa Daftari aliyefiliwa na Mumewe huko Nyumbani kwake Oysterbay Dar
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi akiongoza sala ya Maiti ya kumsalia Marehemu Mzee Juma Omar Juma Mume wa Naibu waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Mh. Mauwa Daftari aliyefariki dunia usiku kuamkia leo nyumbani kwake Mtaa wa Bongoyo Oysterbay jijini Dar. wa kwanza shoto ni Makamu mwa Rais Dk. Ali Mohamed Shein.

Morogoro Hotel




Hapo Morogoro Hotel pazuri kweli. Asubuhi unaamka na unapata hali ya hewa safi kutoka mlimani. Morogoro mji kasoro bahari!
Kujua zaidi kuhusu Morogoro Hotel Bofya Hapa:

Walim - 'Louima' au nini?

Hapa Marekani miaka ya tisini kuna mHaiti, Abner Louima, ambaye alitiwa plunger (kizubulio cha choo) kwenye sehemu ya kutolea haja kubwa na polisi wa kizungu wa New York. Louima alipona na kulipwa mamilioni ya dola kama fidia.

Leo nilivyokuwa napitia Ippmedia.com nikaona hii habari ya ajabu ya Mjerumani aliyefariki Dar es Salaam jana. Wanasema kuwa eti alikuwa anatoka damu nyingi sehemu ya kutoa haja kubwa.

Imetokea nini tena? Ni ugonjwa au mambo mengine? Tungojee autopsy itasemaje.

*******************************************************

Mjerumani akutwa amekufa sakafuni chumbani kwake

2008-05-12

Na Gabriela John

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Italy Wood Tiles Ltd ya jijini Dar es Salaam, Fransisos Johanes (45) ambaye ni raia wa Ujerumani, amekutwa sakafuni chumbani kwake amekufa huku akitokwa na damu nyingi sehemu ya haja kubwa.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Bw. Jamal Rwambow alisema tukio hilo lilitokea juzi asubuhi eneo la Mbezi Tanki Bovu, jijini Dar es Salaam. Alisema mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

Sunday, May 11, 2008

Happy Mother's Day





Wadau,

Nawatakia akina mama wote sikukuu njema ya Siku ya Mama (Mother's Day). Wote tuna mama, hebu tazama kitovu chako hiyo ndo linki ya daima kati ya wewe na mama yako.

Nani kama Mama? Hakuna. Kumbuka ulivyokuwa unaumwa, ulivyoanguka na kuanza kulia, aliposota kukupatia mahitaji yako. Alivyokuwa anakulinda usiumie.

Na kitu kingine, akina mama wengine wanaumwaga wakiwa na mimba. Mimi moja wao. Halafu uchungu wa kuzaa (labor pains) ndo usiombe. Wanasayansi wanasema kuwa mwanaume hawezi kusika maumivu makali kama sisi wanawake tunavyosika kwenye uzazi. Ajabu tukimwona mtoto, tunasahau!

Leo umkumbuke Mama yako, kama uko mbali umpigie simu. Umnunulie zawadi ya shukurani kama unaweza, kamtembelee. Kama ametangulia kwenye mahala pema mbinguni umwombee.
Happy Mother's Day!

AKINA MAMA OYEEEEE!