Showing posts with label Tanga. Show all posts
Showing posts with label Tanga. Show all posts

Monday, December 26, 2016

Taarab Zilipendwa- Nahodha Kukaa Nyuma

Huu wimbo ulifana sana enzi zile!!! Ni Taarab ya kweli. The Real Deal!


Saturday, November 05, 2016

Shamba la Miti Lunguza Wazipiga Jeki Shule ya Msingi Muheza Wakabidhi Madawati 200

SHAMBA LA MITI LUNGUZA WAZIPIGA JEKI SHULE ZA MSINGI MUHEZA WAKABIDHI MADAWATI 200.

Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akipokea madawati 200 kutoka kwa Meneja wa Shamba la Miti Lunguza, yaliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Abdallah Mchomvu katika halfa iliyofanyika leo

 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akikagua madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
 Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kulia mwenye hijabu akitazama baadhi ya madawati hayo kabla ya kuyapokea anayefuata ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza,Kahoza Joseph ambaye ni Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri hiyo
 Meneja wa Shamba la Miti Lunguza,Abdallah Mchomvu akizungumza katika halfa hiyo ya kukabidhi madawati kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa kwanza kushoto aliyekaa ambayo yaliyotolewa na wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS)
 Kaimu Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza ambaye ni Afisa Tarafa ya Muheza Khatibu Omari wakati wa halfa hiyo wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo
 Baadhi ya wafanyakazi wa shamba la miti la Lunguza ambalo ni la serikali linalojishughulisha na uhifadhi wa misitu ya asili na ustawishaji wa miti ya misaji (Teak)
Baadhi ya madawati yaliyokabidhiwa leo kwa Mkuu wa wilaya ya MuhezaHajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo ikiwa ni mkakati wa kukabiliana na upungufu wa madawati kwenye shule za msingi wilayani humo. Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

Wednesday, March 06, 2013

Sifa Za Mikoa ya Tanzania

Nimepokea kwa email:



HIZI NDIO SIFA ZA KILA MKOA TANZANIA:

1. DAR - Utapeli

2. ARUSHA - Ustaarabu

3. MBEYA - Matukio

4. MWANZA - Fujo

5. TANGA - Mapenzi

6. MOROGORO - Starehe

7. DODOMA - Bahati

8. IRINGA - Elimu bora

9. RUVUMA - Pombe

10. RUKWA - Uchawi

11. TABORA - Mikosi

12. SHINYANGA - Njaa

13. SINGIDA - Upole

14. KAGERA - Misifa

15. LINDI - Waoga

16. KIGOMA - Ubishi

17. PWANI - Uvivu

18. MTWARA - Hasara

19. KILIMANJARO - Ubahili

20. MARA - Hasira

21. MANYARA - Utajiri

22. GEITA - Presha

23. SIMIYU - Maradhi

24. NJOMBE - Haraka

24. KATAVI - Aibu

25. Visiwani kote- uchezaji wa karata na bao

Haya mwenzangu watokea mkoa gani?

WaHadzabe wakicheza Ngoma

Thursday, April 29, 2010

Ajali Mbaya Tanga - Wanafunzi 18 Wafariki Dunia

Habari hizi kwa hisani ya Da Subi. Mola alaze roho zao mahala pema peponi. Amina.

Jamani, hizi ajali za kizembe Tanzania zitaisha lini?!


BOFYA HAPA KWENDA KWA DA SUBI:


Tuesday, January 13, 2009

Watu 27 Wafa katika Ajali Tanga!

Watu 27 wamekufa katika ajali ya Basi karibu na Hale, Tanga. Nadhani wakati umefika wa serikali kurudisha ule utaribu wa mabasi kutosafiri baada ya saa mbili jioni ili kuokoa maisha ya watu. Huo utaratibu ulikuwepo miaka ya 80 mwishoni baada ya ajali nyingi za mabasi ya mikoani. Mamia ya watu walipoteza maisha na ajali nyingi zilikuwa zinatokea usiku.

*****************************************************************************

Kutoka ippmedia.com

http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2009/01/12/129530.html

Another road accident in week kills 27

2009-01-12

By Lulu George, Tanga

Twenty seven people died on the spot on Saturday night at Hale, near Tanga, hardly a week after 11 family members perished in another grisly road carnage.

As usual police have attributed the accident to speeding but avoided to speak about the much publicised speed governors which bus owners were ordered to install in their buses in the late 1990s.

The Saturday accident occurred at 8.30 pm after a Tanga bound bus christened Tashreef rammed into a stationary lorry, killing 27 on the spot and injuring 23, two of them seriously. The bus was travelling from Dar es salaam to Tanga.

The Chief of Traffic Police James Kombe, on his way to the accident scene, said yesterday that they were in the process of re-introducing new speed governors, more than ten years after the earlier ones were discarded.

He, however, did not say when exactly the gadgets would be installed in the passenger buses.

Tanga Regional Police Commander Simon Sirro said the driver of the fateful bus escaped immediately after the accident and was being sought by police.

He said the conductor and the turn boy of the bus were among the dead.

Tanga Regional Commissioner Mohammed Abdulaziz who arrived at the scene few minutes after the accident, broke into tears after he saw the mangled bodies.

One of the injured Omar Khalfan said the driver of the bus was speeding when the accident occurred.

``Probably he was rushing to reach Tanga before midnight, the deadline for passenger buses to travel,`` he said.

The injured have been admitted to the Muheza designated hospital and Bombo hospital respectively.

Eighteen bodies out of the 27 had been identified as of yesterday.

Sirro named them as; Idirisa Bakari, Hamidu Titu, Salama Ramadhan, Mbaruku Salum, Mussa Hussein, Msahamu Alli, Rahabu Jamal, Shaban Bakari, Hamad Alli and Omar Salehe.

Others are; Amir Sanyo, Salim Musa, Omar Al jabri, Napendaeli Msangi, Said Abdallah, police officer WP Corporal Mariam and two members of the Tanzania People\'s Defence Forces Corporal Mbaraka Mafoni and Corporal Deo Zakaria.

One of the injured Hamid Swahib said soon after the accident, a group of villagers arrived at the scene and started looting from the victims.

``They took my mobile phone and my handbag,`` Swahib said.

This is the second bad accident to occur this year, after last week a mini bus full of family members rammed into a stationary lorry killing 11 of them at Himo in Kilimanjaro Region.

SOURCE: Guardian

Wednesday, October 08, 2008

Magofu Yanabomolewa Tanga



Picha na maelezo kutoka Jiachie Blog:

Sio Dar tu majumba makuu kuu yanakula nyundo kupisha majengo mengine mapya na ya kisasa,la hasha hata kwa wagosi wa kaya nako kazi ni moja tu,kusafisha majumba yalijichokea na kuleta mapya yatakayoleta sura iliochangamka na ya kuvutia katika mji wa Tanga.Tatizo katika ubomojai wamajumba haya ni kwamba wameyabomoa kidogo sijui kuwatisha wenye nyumba/wapangaji waondoke halafu wameyaacha hivyo hivyo,kutokana na hali ya hayo majengo baadhi ya wakazi wa tanga wameanza kulalama kwamba kama wahusika wameamua kuyabomoa majumba hayo basi wayabomoe na si kuyaacha kama yanavyoonekana pichan kwani yanatishia usalama wa wapita njia.
********************************************************
Hivi wadau, kuna Historial Preservation society huko Tanga? Wasiwe wanabomoa majengo ya kihistoria. Sawa ni 2008, lazima twende na wakati lakini pia history ya mji usifutwe kabisa!

Monday, July 28, 2008

Neema Mushi Afufuka!

Wadau, hivi huyo binti ni huyo huyo Neema Mushi au ni mwingine? Shangazi yake anadai kuwa alimfia mikononi mwake. Neema mwenyewe anasema hakufa ila alikuwa anakaa Tanga.

***********************************************************
Kutoka ippmedia.com

Mtu adaiwa kufufuka

2008-07-28

Na Patrick Chambo, PST Hai

Mamia ya wananchi katika Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wameshikwa na butwaa baada ya kumuona msichana aliyedaiwa kufariki dunia takriban miaka mitatu iliyopita akiranda randa mitaani.

Tukio hilo la aina yake, lilitokea katika kijiji cha Machame Mkuu, mkoani Kilimanjaro na msichana huyo anayedaiwa kufa na baadaye kukutwa akitembea mitaani ametajwa kuwa ni Neema Mushi, mkazi wa kijiji hicho.

Aidha, habari zilizopatikana kijijini hapo zilisema kuwa, binti huyo alisema kuwa alikuwa akiishi Tanga. Mchungaji Elimfoo Mushi wa Usharika wa Machame Mkuu, alisema ndiye aliyeendesha ibada ya kumuombea Neema ambaye mwili wake ulifikishwa kanisani hapo.

Akizungumza na PST, Neema alisema kuwa kweli hilo ni jina lake, lakini alikanusha kuwa alikufa na kuzikwa na badala yake alikuwa akiishi Tanga. Alisema eneo alilokuwa akiishi ni siri yake na kwamba akiwa huko alisikia kuwa alikufa na kuzikwa mwaka 2005. ``Mimi sijui kitu, najua nilikuwa naishi Tanga ?na wala siwaambii nilikokuwa naishi. Nimeshangaa narudi watu wanakimbia hadi nilipopelekwa polisi, wakaja ndugu zangu wakanitambua kuwa eti mimi nilikuwa marehemu,`` alisema.

Shangazi wa Neema, Bi. Liliani Mushi, alisema ndiye aliyemuuguza Neema hadi umauti unamfika na kusafirisha mwili wake hadi kijijini hapo na kuzikwa kwenye makaburi ya kanisa. ``Kweli mimi nimeokoka na sali Kanisa la Ephata, huyo mtoto alinifia mikononi huko Namanga nilikokuwa naishi naye nimeshangaa kuambiwa eti njoo umuone Neema, amekuja Machame kutoka Tanga, nilichoka, hakika huu ni muujiza wa Mungu watu wanasema kuwa eti ni msukule, mimi siamini, ninachojua alinifia tukamzika. Huyu hapa muulizeni wenyewe katoka wapi,`` alisema shangazi huyo.

Naye Mchungaji Mushi alisema, ``nasema nijuacho mimi ni kuwa huyu ndiye Neema ambaye msukule, mimi sijui,`` alisema. Polisi wilayani Hai, wamekiri kuchukua maelezo ya Neema, mwili wake uliletwa hapa kanisani na tukauzika makaburini, kwamba ni muujiza wa Mungu au wazazi, Mchungaji na ndugu wengine walioshiriki katika mazishi.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa mkoa Bw. Lucas Ng'ohoko, hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hilo. Aidha, ndugu na jamaa wa Neema wako kwenye harakati za kupata kibali cha polisi ili waweze kufukua kaburi hilo.

SOURCE: Nipashe