Tuesday, January 13, 2009

Anauza Ubikira Wake!



Natalie Dylan (22) (pichani) wa California anauza ubikira wake kwa atakayemlipa hela nyingi. Kwa sasa anafanya mnada na bei imefika dola $3.7 milioni! Anasema kuwa atatumia pesa hizo kwa ajiliya kulipia masoma yake Chuo Kikuu.

Hivi kweli huyo ni bikira au? Dada yake ni malaya huko Nevada kwenye bunny ranch. Na siku hizi unaweza kwenda kwa Plastic surgeon akarudisha ubikira. Na kuna tofauti gani na anavyofanya na umalaya?

Monday, January 12, 2009

Ushauri Blog

Habari Wakuu;

Nimeanzisha blog yenye nia ya kusaidia kiushauri, mawazo, au zaidi (kadri ya uwezo) kwa wenye kuhitaji msaada wa kisaikolojia/kimawazo. Lugha ya Kiswahili na Kiingereza hutumika. Natoa mchango wangu mdogo kwa wananchi kwani hatuna professional counselors wa kutosha Tanzania.

In turn, napata experience ya field ninayosomea katika mazingira ya watu wangu, na kupata uhalisi na utofauti wa matatizo kati ya watu wa west na wa nyumbani ili niweze kuwatumikia kiufasaha baada ya masomo mwakani.

Natumai majibu na maoni ya maswali kutoka kwangu, na watoa maoni tofauti yatasaidia wengi zaidi ya wanaohusika moja kwa moja. Natumai pia awareness ya mental health nchini tanzania, na interest na recognition ya field ya saikolojia itakua miongoni mwa wananchi na viongozi wa nchi. We do have enough Educational psychologists in our colleges, but it is a wide spectrum field, my focus is on counseling people of all walks of life...not just students.

Asanteni.

Dr.Wannabe

Your questions to:-wannabe.dr@gmail.comweb at http://www.dr12b.blogspot.com/

Kitabu Kipya cha Da Sandra Mushi


Hivi karibuni, mtunzi maarufu Da Sandra Mushi, alizindua kitabu chake kipya, The Rhyme of my Rhyme, huko Dar es Salaam. Ni kitabu cha mashairi.

Hongera sana kwa kitabu chako kipya!
Da Sandra pia amewahi kuandika vitabu na mashairi kuhusu haki za akina mama na mila za WaChagga.






Saturday, January 10, 2009

Msiba Daily News - Cassian Malima

Kutoka Lukwangule Blog:


ALIYEKUWA Mhariri wa 'HabariLeo', Cassian Kigeso Malima (44),pichani, amefariki dunia.
Taarifa iliyotolewa jana na Mhariri Mtendaji wa TSN Media Group, Issac Mruma, ilisema Malima alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa tangu Jumamosi iliyopita.
Ilisema Malima ambaye hivi karibuni alipandishwa cheo kuwa Mhariri Msaidizi wa Magazeti ya Mwisho wa Wiki ya Kampuni ya TSN Media Group, alijiunga na kampuni hiyo Oktoba 10, 2004 akiwa Mwandishi Mkuu Daraja la Pili.


Baadaye alipanda cheo na kuwa Mhariri wa Habari wa Daily News na kuwa mmoja wa waanzilishi wa 'HabariLeo' baada ya kuteuliwa Agosti mosi 2006 kuongoza timu iliyoanzisha gazeti hili la Kiswahili linalomilikiwa na Serikali.


“Alitegemewa sana katika utendaji kazi, lakini pia alikuwa mcheshi na rafiki wa kila mtu … aliheshimu kila mtu,” ilisema sehemu ya taarifa hiyo.
Mruma katika taarifa yake alisema kampuni imepoteza si tu mfanyakazi, bali rafiki aliyekuwa tayari kubeba jukumu lolote alilopewa na alikuwa mtiifu kupindukia.

Mkewe Malima, Hellen Maro, ambaye walizaa binti, Elizabeth, alifariki dunia Mei 19, 2006.
Malima alizaliwa Mwanza Julai 14, 1965, alipata elimu yake ya msingi katika shule mbalimbali nchini, kati ya mwaka 1972 na 1979; elimu ya sekondari katika Sekondari ya Mwanza kati ya 1980 na 1983.
Alipata elimu ya sekondari ya juu katika Shule ya Sekondari ya Lake Mwanza kati ya 1984 na 1986 kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Rostav State cha Urusi kati ya mwaka 1988 na 1994 na kuhitimu Shahada ya Uzamili katika Uandishi wa Habari.
Katika uhai wake, Malima alifanya kazi katika Mamlaka ya Bandari Tanzania (THA) kati ya 1987 na 1988; Mwandishi wa Habari Uhuru/Mzalendo tangu Mei 1988 hadi 1996 alipokuwa Mhariri.

Machi 1998 hadi Septemba 1999 alikuwa Mhariri wa Habari wa Gazeti la Mtanzania na kuwa Mhariri wa Mtanzania na Mtanzania Jumapili kati ya Septemba 1999 hadi Julai 2003 na kisha Mhariri wa Habari wa The African tangu Julai 2003 hadi Oktoba 2004 alipojiunga na TSN.
Aliwahi pia kuwa kiongozi katika vyama mbalimbali kitaaluma ndani na nje ya nchi ikiwa ni pamoja na kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Bunge Tanzania, mbali na kuhudhuria semina, makongamano, warsha na kampeni mbalimbali nje na ndani ya nchi. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi.

Mruma alisema mipango ya mazishi inafanywa na taarifa kamili itatolewa baadaye.

Friday, January 09, 2009

Kwa Nini Tunakubali Kuibiwa!!!!

Kutoka Ippmedia.com

Revealed: Tanzania`s shocking vast wealth

2008-08-31 09:07:51
By Staff Writer

As massive poverty continues to rock the majority of Tanzanians, the latest data reveal that Tanzania`s wealth in terms of the top five metals out of eleven provable mineral deposits amounting to millions of tonnes.

It is hard to believe it, but that is the reality in a country where 38million plus population lives in abject poverty, below a dollar per day, while 89percent of the total population survive on a single meal per day.

According to a geological survey conducted last year by the ministry of energy and minerals, Tanzania has huge reserves in eleven key minerals which include gold, Nickel, Tanzanite, Diamonds, copper, Iron ore, coal, Limestone, soda ash, gypsum and phosphate.

The five key minerals and their provable amounts in brackets is Gold (2,222tones), Nickel (209million tones), Diamonds (Carat 50.9million), Copper (13.65million tones), and Iron ore (103million tones).

However since this was just a geological survey undertaken by experts last year, its actual result is approximated to be accurate by up to 70 percent.

So far, only three types of minerals - gold, diamonds, Tanzanite - are being fully mined by multinational companies which at the end of the day take 97percent, leaving only peanut to the original Tanzanian owners.

If well managed through sound, people-centered mining policies, the mining sector can catapult Tanzanians to the proverbial promised land in decades and generations to come.

Comparing these huge deposits and the actual situation of poverty in the country, the message that comes across one`s mind is that Tanzania is in what experts describe as `resource curse`.

The term `resource curse` refers to the observation that nations with rich endowments of natural resources (oil, metals, timber) often dramatically under-perform economically relative to what one would expect.

Common sense and simple economics suggest that countries blessed with an abundance of natural resources should live long and prosper.

Yet over many years, it has been observed that nations rich in oil, gas, or mineral resources have been disadvantaged in the drive for economic progress.

Why are we poor?

Perhaps the biggest question that begs an urgent answer is; why are we so poor despite having all these huge minerals deposits?

It is a question that policy makers and politicians have been avoiding to seek answers for.

Tanzania like many other African countries is highly blessed with rich natural resources, but its people are swimming in the deep sea of massive poverty.

But the appalling truth is that instead of financing people`s development, Africa's huge mineral resources were used to fund the brutal civil wars that ravaged millions of people during the past four decades.

Today in Africa only a few countries like Botswana, Ghana and South Africa have managed to use their natural resources, especially minerals, to facilitate development and welfare to their people.

This example is vividly manifested in the Democratic Republic of Congo, Sierra Leone, Ivory Coast, Nigeria, Sudan and Angola whereby masters of the wars used natural resources to finance their deadly power struggle.

However in Tanzania, there wasn`t any civil war apart from the role played by the founding President, (the late) Dr Julius Nyerere, in liberating Southern African countries during the nationalist struggle.

While it is an undeniable truth that the move to allow the private sector to participate in the mining industry was brilliant one, the truth is that due to poor policies introduced by the third phase government, the whole idea has become a disaster to Tanzanians.

This is well echoed in the lucrative mining industry which has been mainly benefiting multinational companies, while paying the government a small slice of the cake.

Last year, for instance, the Minister for Energy and Minerals, William Ngeleja, told the parliament that during the period between 2001 and 2006, Tanzania produced gold worth $2.6 billion (Tshs3.38 trillion), but the government earned only $78 million.
In simple arithmetic, this is just 3 percent of the total revenues generated from thousands of tonnes of gold produced in the Lake Victoria gold belt. It also shows that the government earned an average of $13 million annually during that period from the multibillion industry whose real investments currently is valued at $2.5 billion.

According to the available statistics from the mining industry, from June 2000 to December 2006, the two biggest gold mines in the country produced a total of 5,686,710 ounces of gold, which at the current gold price of $600 per ounce is valued at Tshs 4.3 trillion ($ 3.3 billion), but what the nation earned is frightening and a shame.

While mineral production has increased in Tanzania in the past few years with export per year estimated to be nearly $900 million (Tshs1.17 trillion), the contribution of the mining sector to the Gross Domestic Product (GDP) remains very minimal, accounting to 3 percent.

According to the National Economic Survey report released in 2006, the growth rate of mining and quarrying sector increased from 15.4 percent in 2004 to 15.7 percent in 2005, whereby the increment was attributed to new investments in Tulawaka gold mines in Biharamulo District, Kagera Region.

The report further states that, the contribution of the sector to GDP, which is the total value of goods and services produced in a country during a year, increased from 3.2 percent in 2004 to 3.5 percent in 2007.

We would like to hear from you about this story; what you think the problem is, and what needs to be done. Send your comments through sundayguardian@guardian.co.tz

Siku ya Kuapishwa Rais Obama Inakaribia

Wadau, wangapi mmepanga kwenye huko Washington D.C. kwenye Inauguration (Sherehe za Kuapishwa) ya Barack Obama? Nasikia itakuwa balaa huko kwa jinsi watu watakavyojazana. Vyumba vya hoteli hakuna.

Pia watu wa usalama hapa wame weka masharti mengi kwa wanaoenda. Hakuna kwenda na kiti, mwavuli, backpack, na mambo mengi. Simu za mkononi hazitafanya kazi maana signals ziatkuwa jammed.

Pia wana usalama wanasema katika historia hakuna rais aliyetishiwa maisha kama Barack Obama. Na wanasema kuwa hii ni kwa sababu ni mweusi. Wabaguzi nchi hii bado wanachukia kushinda kwa rais Obama.

Wakati huo huo watu wanaanza kushangilia kuondoka kwa Rais Bush! Wanasema jamaa kaharibu nchi na kutesa watu!

Kwa habari zaidi someni:

http://www.cnn.com/2009/POLITICS/01/08/inauguration.security/index.html?iref=mpstoryview

Kipanya Asema...

Translation:

Man: Stop listening to those street rumours. I don't have AIDS, I only have HIV...

Woman: Oh what a relief! Some people wanted to cheat me out of my luck! They said oh Fataki is sick! Loh! Some people are really bad!!

*******************************************************************
Jamani, kwa kweli kuna haja ya watu kuelimishwa kuhusu huo ugonjwa hatari! Hivi kuna watu ambao wanadhani kuwa unaweza kuambukizwa UKIMWI lakini siyo V.V.U? Tumieni kondomu na mjikinge. Na hebu cheki huyo dada, amesikia maneno lakini bado tu anakubali kwenda kitandani na jamaa! Halafu anasema watu wanatakia mabaya! Khaa!

Thursday, January 08, 2009

Sophia Simba Mwenyekiti Mpya wa UWT

Sofia Simba (Picha kwa hisani ya Michuzi Blog)

Kutoka Lukwangule Blog:

WAZIRI wa nchi ofisi ya rais Utawala bora, Sophia Mnyambi Simba ameibuka kidedea na kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa CCM na kuwabwaga wagombea wenzake Janeth Kahama na Joyce Masunga.

Katika uchaguzi uliofanyika jana usiku na matokeo kutangazwa leo katika ukumbi wa kilimani na msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Seif Khatibu, Sophia Simba aliibuka kidedea baada ya kupata jumla ya kura 470 sawa na asilimia 54.4 ya kura halali 862 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa uchaguzi.

Janeth kahama alipata jumla ya kura 383 sawa na asilimia 48.4 huku Joyce Masunga akiambulia jumla ya kura 10 kati ya kura 862 zilizopigwa sawa na asilimia 1.1.

Kwa upande wa nafasi ya Makamu mwenyekiti wa UWT taifa alikwenda kwa Asha Bakari Makame ambaye alikuwa mgombea pekee na hivyo kupigiwa kura za ndiyo na hapana ambapo alishinda kwa jumla ya kura za ndiyo 736 kati ya kura halali 815 sawa na asilimia 90.3 huku kura za ndiyo zikiwa ni 79 sawa na asilimia 9.7.

Naye Ofisa uhusiano wa Benki ya NMB, Shy Rose Bhanji aliibuka mshindi na kuukwaa uwakilishi wa jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM), toka UWT baada ya kuwabwaga wenzake watano kwa kupata jumla ya kura 499 kati ya kura 807 zilizopigwa huku Mbunge wa Viti maalum Martha Mlata aliibuka kidedea na kupata nafasi ya uwakilishi wa jumuiya ya wazzai toka umoja wa wanawake.

Kwa upande wa nafasi za wawakilishi wa baraza kuu la umoja huo upande wa bara waliochaguliwa katika nafasi hizo ni pamoja na Magreth Mkanga, Betty Malanga, Ellen Magoha, Amina Msenza na Sifa Swai.

Wawakailishi wa baraza kuu la UWT upande wa Zanzibar waliochaguliwa ni pamoja na Zulekha Yunus Haji, Lilian Grace Limo, Catherine Peter Nao, Subira Mohamed Ali na Latifa Nassor Ahmed.

Akiongea baada ya matokeo hayo kutangazwa aliyekuwa mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa UWT taifa, Janeth Kahama alisema kuwa uchaguzi huo ulikuwa mgumu sana na kwamba ulikuwa na rafu nyingi na matusi yalitawala.

“Mimi sina ugomvi na mtu ila ninamuomba radhi sana mume wangu kwa matusi ambayo nilikuwa natukanwa kupitia simu nisamehe sana mzee mwenzangu “ Alisema.

Aliwaomba wanachama wa umoja huo kumpa sapoti mwenyekiti mpya kwa kuwa bila wanachama hakutakuwa na uwt imara na kuongeza kuwa yeye atakuwa tayari muda wowote ambapo mwenyekiti mpya atamuhitaji.

Wednesday, January 07, 2009

Urais Unazeesha


Kuwa rais wa Marekani ni kazi ngumu. Wataalamu wanasema kuwa ukiwa rais unazeeka haraka, mara mbili kuliko mtu wa kawaida. Kazi ipo.

Kusoma habari zaidi na kuona picha za jinsi marais wa Marekani walivyozeeka wakiwa madarakani, BOFYA HAPA:


******************************

Mkutano wa UWT Dodoma

Anna Abadallah akihutubia wajumbe
Baadhi ya wajumbe kwenye mkutano wakiwemo Mama Maria Nyerere



JK akihutubia wakati akifungua mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake katika ukumbi wa Kilimani huko Dodoma leo. Picha nyingine ni Mwenyekiti anayeng'atuka Anna Abdallah akihutubia na picha nyingine wajumbe na waalikwa wakiwa katika mkutano.Mpaka sasa mambo bila bila hasa tukitambua wanachuana ni Mh. Janeth Kahama na Mh. Sofia Simba ambapo mmoja wao atamrithi Mh. Anna Abdallah katika kiti hicho. Matokeo yanatarajiwa baadaye usiku huu!

M-Net 2009 Screenwriters Workshop

Hii ni nafasi nzuri sana kwa WaBongo wenye interest na mambo ya screenwriting, utunzi wa filamu...hasa kuandika script. Script ni ramani ya sinema na ni muhimu kwa sinema nzuri. Nimeona sinema/video nyingi za Bongo na kwa kweli ingekuwa vizuri watunzi wakapata training zaidi. Kazi kwenu!

********************************************************************
M-NET ANNOUNCES PLANS FOR 2009 SCREENWRITERS WORKSHOP

With its brand-new local talk show The Patricia Show on air, its hot new drama The Agency about to hit DStv screens across East Africa and its second Kenyan drama Changes heading into production, African entertainment pioneers M-Net are already focusing on 2009. Today the company announced plans for a special 6-day Screen-Writers Workshop to be held in Nairobi in March.

Now calling for interested writers, producers and industry professionals from Kenya, Tanzania and Uganda to apply for entrance into the fully sponsored event, M-Net is aiming to promote the continued growth of the region’s burgeoning television industry.

By investing in local skills development and by further partnering with the Kenyan Film Commission, M-Net has expanded its ongoing efforts to nurture and foster local talent.

According to recently appointed M-Net Africa Channel Director Biola Adekanbi, the decision to host a Screen-Writers Workshop is a direct result of the enthusiasm and commitment M-Net has found in its partnerships with the local East African film and television community.

"In the last two years M-Net has deeply intensified its efforts across this region and this outreach has been warmly welcomed with positive support across the board. Increasingly the need to tell local stories, promote local stars and holistically involve local crew is becoming paramount to ensuring that good quality, relevant productions are created to meet the demand from millions of DStv viewers for engaging and entertaining content."

She goes on to say, "M-Net is confident that this Screen-Writing Workshop is another step in the right direction, another brick in building on our strong foundations for marketable and relevant programming."

To apply for entrance into the workshop, script-writers from any of the three participating countries must submit a copy of their original script-work completed within the last two years, which is not currently and has never been in production for any commercial television company. The script submitted should be a minimum of 20 pages and a maximum of 30 pages.

In addition, script-writers will also be requested to submit a one-page synopsis, character bible, an updated resume or biography, and a proposal of not more than 1500 words explaining why they would like to attend the workshop.

Thereafter an evaluating committee will shortlist the entrants who will be invited to a one-on-one meeting with M-Net and other stakeholders at which each will be required to write a 10-minute narrative in the format of drama, short story and/or sitcom. Finally, 25 writers will be invited to attend the workshop.

M-Net Program Manager for East Africa Wangeci Murage acknowledges that gaining entrance to the workshop requires entrants to complete a rigorous selection process.

"We’re investing heavily in this initiative and want to ensure we’re able to provide 25 truly determined writers with an innovative and unique opportunity to hone their skills and enhance their talents. For this reason, we want to select candidates who’ll be able to fully maximize on their learnings from this event.

Ultimately, we’d also like to be able identify key partnerships for the future from this process as well as promote greater regional commercial television success."

Comprising lectures and writing exercises, the M-Net Screen-Writers Workshop follows an initiative by M-Net last year in which a contingent of Kenyan filmmakers were sponsored on an all-expenses paid trip to Lagos to share ideas and knowledge with Nigeria’s prolific Nollywood film making community.

This time round, selected participants will workshop on the grammar of film, story development, narrative point of view plus character analysis and scene structure. In addition, it will allow industry professionals from the three countries to network and construct multi-national relationships that they are able to use to their benefit.

Interested persons who wish to apply for the M-Net Screen-Writers Workshop can deliver their proposals to Wangeci Murage (M-Net Kenya, Rahimtulla Tower, 18th Floor, Nairobi);

Ronald Shelukindo (MultiChoice Tanzania, Dar es Salaam)

or

Leonah Mbonimpa (MultiChoice Uganda, Kampala).

The deadline for entries is Friday January 16, 2009.

For further information, please contact M-Net Kenya on email: wangeci.murage@mnet.co.za.

Tuesday, January 06, 2009

Ngoma ya Weusi Marekani 1903

Hii Ngoma inaitwa 'Cake Walk'. Hii sinema fupi ilipigwa mwaka 1903 yaani miaka 106 iliyopita.

Msiba Italy - Mohamed Abdul Shakur


Marehemu Mohamed Abddul Shakur aka Captain PAMA (pichani)

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Italy unasikitika kutangaza kifo cha Ndugu MOHAMED ABDUL SHAKUR (PAMA) kilichotokea jana asubuhi katika hospitali ya SAN GIOVANNI DI DIO E RUGGI D'ARAGONA" SALERNO.

Kutakuwa na Mkutano wa Watanzania wote leo jioni saa kumi na moja 17:00 pm.
Sehemu: LAGO PATRIA MABEMBEANI.

TAFADHALI TUZINGATIE WAKATI NA KUFIKA BILA KUKOSA.
Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy,kwa niaba ya uongozi na watanzania wote hapa Italy,anapenda kutoa salam za rambirambi kwa wazazi na ndugu wa marehemu nyumbani na popote walipo, kuwa tumepokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa na tunaungana nanyi katika wakati huu mgumu wa maombolezo.
Mungu ailaze roho yake mahala pema .
Amin.
Abdulrahaman A.Alli.
Mwenyekit

i*****************************************************************
WA WALE WOTE WALIO NJE YA ITALY KWA MAWASILIANO TUPIGIE SIMU NAMBA:
+39 3271753565(Mwenyekiti)
AU
+39 3453118431 (DULLAH)
au
+39 331 8360509 (Katibu mkuu)
au
+081 3340635 (ofisi ya jumuiya)
e-mail: tnzncommunity@yahoo.com
HABARI ZAIDI: http://www.tnzncommunity.blogspot.com/

Monday, January 05, 2009

Mwimbaji wa Injili, Fanuel Sedekia, Afariki Dunia







MWIMBAJI WA INJILI FANUEL SEDEKIA KATUTOKA. HABARI ZA KUSIKITISHA ZIMEINGIA SASA HIVI KWAMBA MWIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI, FANUEL SEDEKIA, AMEFARIKI DUNIA JANA KATIKA HOSPITALI YA PORIYA TIBERIA, HUKO ISRAEL.

HABARI ZINASEMA MAREHEMU ALIKUWA AMELAZWA KWA WIKI TATU HOSPITALI HAPO AKISUMBULIWA NA KISUKARI PAMOJA NA NIMONIA. ALIKUWA HUKO KATIKA MSAFARA WA MAHUBIRI NA MCHUNGAJI MWAKASEGE.

MIPANGO YA KUULETA MWILI WAKE NYUMBANI KWA MAZISHI UNAFANYWA NA TUTAENDELEA KUWAFAHAMISHA HABARI ZINAPOTUJIA. KWA SASA KINACHOFAHAMIKA NI KWAMBA MSIBA UTAKUWA NYUMBANI KWAKE ARUSHA NA ATAKAPOZIKIWA BADO HAIJAJULIKANA KWANI YEYE KWAO NI KIGOMA.
MOLA AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI - AMINA
*******************************************************
REST IN PEACE KAKA FANUEL!

Mtu Mzee Kuliko Wote duniani sasa ni Mmarekani Mweusi

Mwezi November mwaka jana, mtu mzee kuliko wote, Bibi Edna Parker, alifariki huko Indiana, USA akiwa na miaka 115!

Leo wataalam wametangaza kuwa Bibi Gertude Baines (pichani), mwenye miaka 114 ni mtu mzee kuliko wote duniani. Bibi Baines, ni mtoto wa watumwa. Alizaliwa mwaka 1894 huko Atlanta, Georgia.

Kwa sasa anakaa Los Angeles,California kwenye nyumba ya wazee.

Ni baraka kuweza kuishi muda wote huo tena katika karne tatu! 1800's, 1900's, 2000's. Ila wakati mwingine nafikiria kuna wakati utakuwa mpweke hasa ukifikiria watu wote uliokuwa unawafahamu wamekwisha kufa.

Hivi huko Afrika hakuna watu wenye umri mkubwa hivyo? Maana naona hao wataalam wanachunguza nchi zilizoendelea na hata siku moja sijasikia walienda Afrika kuchunguza.

Namtakia Bibi Baines, maisha marefu zaidi. Mungu amlinde.

Na kitu kingine, hapa Marekani kuna usemi "Black Don't Crack!" yaani ngozi nyeusi haivunjiki. Wana maana kuwa watu weusi hawazeeki kama wazungu ambao ngozi yao inasinyaa vibaya.

Wadau, kama mnafahamu watu wenye umri mkubwa zaidi ya miaka 100 hebu tutoe ripoti kwa hao wanaojiita watalaam wa umri waingie kwenye record books.

Najua watu wanatania, au kuna mzee fulani asubuhi tunamtoa na kumanika juani. Je, ana miaka mingapi?

GOD BLESS YOU MS. BAINES!

************************************************************************

LOS ANGELES, California (CNN) -- Gertrude Baines, ma 114-year-old California resident, will likely be crowned the world's oldest woman, according to the organization that keeps track of such honors.

Gertrude Baines told CNN two years ago that she has taken good care of herself, "the way (God) wanted me to."

The previous oldest woman was Maria de Jesus, who died this week in Portugal at age 115, Guinness World Records said.

Baines -- born to former slaves in a small town south of Atlanta, Georgia, in 1894 -- now lives in a Los Angeles nursing home.

Baines appeared cheerful and talkative when the Los Angeles Times interviewed her in November as she cast her vote for Barack Obama for president, whom she said she supported because "he's for the colored people."

"I'm glad we're getting a colored man in there," she said.

Baines apparently prefers using the older term for her race. She was well into her 70s when "African-American" became the common reference in the United States. Watch Baines speak to CNN
She told the Times she spends most of her time "doing nothing but eating and sleeping."
When CNN interviewed Baines two years ago, she was asked to explain why she thought she has lived so long.

"God. Ask him. I took good care of myself, the way he wanted me to," Baines said.
Her only child, a daughter, died of typhoid fever at age 18.

Much of her long life was lived in Ohio, where she worked as a "house mom" at a state university. She eventually divorced and traveled to Los Angeles, where she retired.
Baines will not officially be given the title until after Guinness World Records completes an investigation, the organization said.

"Maria was crowned the world's Oldest Living Woman by Guinness World Records on 28 December upon the death of Edna Parker," the group said.
Parker -- an American -- was 115 years, 220 days old when she died November 26, 2008, in an Indiana nursing home, it said.

********************************************

KAMA MNA HABARI ZA WAZEE WENYE UMRI MKUBWA TAFADHALI WASILIANA NA GUINESS BOOK OF RECORDS:

http://www.guinnessworldrecords.com/member/how_to_become_a_record_breaker.aspx

Saturday, January 03, 2009

Rais Mpya wa Ghana ni John Atta Mills


Aliyekuwa makamu rais wa Ghana chini ya rais Jerry Rawlings, Prof. John Atta Mills (64), amechaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo. Habari zinasema kuwa katika uchaguzi wa jumapili iliyopita Prof. Mills ameshinda kwa asimilia 50.23 ya kura.

***************************************************

Ghana's newly elected president says it's time for the country to "work together to build a better Ghana."

Opposition leader John Atta Mills has been declared the winner of Ghana's presidency. Election officials are calling it the closest race in the West African nation's history.

It's the third time the 64-year-old tax expert and Fulbright scholar had tried to become president of Ghana. Atta Mills had been vice president under former coup leader Jerry Rawlings, who stepped down in 2001.

He won last Sunday's ballot with 50.23 percent of the vote. Election officials say the Ruling party candidate got 49.77 percent of the vote. A special revote in a single district yesterday secured Atta Mills' victory.
Kwa habari zaidi someni:

Friday, January 02, 2009

Salamu za Mwaka Mpya kutoka kwa Rais Kikwete

Kutoka Lukwangule Blog:

Rais kula sahani moja na mafisadi 2009!

RAIS Jakaya Kikwete ameagiza mtumishi yeyote wa Serikali ambaye atahusika na wizi au ubadhirifu wa fedha za umma kufikishwa katika vyombo vya sheria .

Katika salamu zake za mwaka mpya kwa taifa, Rais alisema bado hali si ya kuridhisha katika matumizi ya fedha za umma kumfanya afurahi na akaahidi kuwa mwaka huu utakuwa wa kubanana katika jambo hilo ili ufanisi uweze kufikiwa.

“Kuanzia mwaka ujao nitawaomba wakaguzi wa mahesabu ya Serikali kumkabidhi kwenye vyombo vya sheria mtumishi wa Serikali aliyehusika na wizi au ubadhirifu mara watakapougundua,” alisema Rais.

Aliongeza kuwa kwa sasa utaratibu hauko hivyo lakini akataka ofisi ya CAG itazame upya utaratibu wa sasa ili isaidie kujenga nidhamu hata kama ni ya woga wa kufungwa. “Itasaidia kunusuru fedha nyingi za umma zinazotumiwa isivyo.”

Ifuatayo ni hotuba yake kamili:

Salamu za Mwaka Mpya za Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa Wananchi, 31 Disemba 2008
Ndugu Wananchi;
Hatimaye imewadia ile siku ya kuuaga mwaka mmoja na kuukaribisha mwingine. Leo tunauaga mwaka 2008 na kuukaribisha mwaka 2009.
Kwanza kabisa, naomba sote tumshukuru Mwenyezi Mungu aliyetujaalia uhai na kutuwezesha kuiona siku hii adhimu salama. Ni wajibu wetu kumshukuru Muumba wetu kwani wapo wenzetu wengi hawakujaaliwa kuiona siku ya leo kwa vile wametangulia mbele ya haki. Wakati tukikumbushana wajibu wetu wa kumuomba Mwenyezi Mungu awape marehemu wetu hao mapumziko mema, tumuombe pia awape nafuu na kuwaponya wenzetu wote wanaougua maradhi mbalimbali ili wajumuike nasi katika shughuli za ujenzi wa taifa letu.
Ndugu Wananchi;
Mwaka wa 2008 tunaoumaliza leo ulikuwa mwaka wa aina yake kwa taifa letu na katika historia ya uongozi wangu. Ulikuwa ni mwaka ambao tumepata mafanikio mengi mazuri na mengine ya kihistoria katika nyanja mbalimbali za maisha ya wananchi wa Tanzania na taifa letu. Lakini, pia kulikuwepo na changamoto au matukio machache ambayo yalisababisha baadhi ya watu ndani na nje ya nchi yetu wapate shaka juu ya hatima ya umoja, amani na utulivu wa nchi yetu. Umoja, amani na utulivu ndiyo nguzo kuu na sifa kubwa inayoitofautisha na kutambulisha Tanzania miongoni mwa mataifa barani Afrika.
Ndugu Wananchi;
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwamba tumeumaliza mwaka huu kwa usalama, amani na utulivu. Tuzidi kumuomba baraka na rehema zake, katika mwaka 2009, ili nchi yetu iendelee kuwa na amani, utulivu na watu wake waishi kwa upendo, umoja, masikilizano, mshikamano na ushirikiano kama ndugu wa taifa moja.
Pamoja na kumuomba Mwenyezi Mungu, hatuna budi kutambua kuwa dhamana ya kuhakikisha kuwa nchi yetu inaendelea kuwa tulivu na yenye amani na upendo miongoni mwa watu wake ni yetu wenyewe. Ni ukweli ulio wazi kuwa katika mwaka huu tunaoumaliza sasa baadhi yetu tumekuwa tunafanya vitendo au kutoa kauli ambazo zilikuwa zinalielekeza taifa kubaya. Tena tulikuwa tunafanya hivyo kwa ajili ya kuendeleza manufaa binafsi ya kisiasa. Ni matumaini yangu kuwa tutajiepusha na mambo hayo katika mwaka 2009. Nawasihi viongozi wenzangu wa kisiasa na wa kijamii tubadilike, tuweke mbele maslahi ya taifa ili tuiepushe nchi yetu na mabalaa ambayo baadhi ya wenzetu yaliwakuta.
Hali ya Uchumi wa Nchi na Dunia
Ndugu Wananchi;
Kwa jumla hali ya uchumi wa nchi yetu kwa mwaka 2008 ilikuwa ya kiwango cha kuridhisha. Lakini, hali ingekuwa bora zaidi kama uchumi wa dunia usingepata misukosuko iliyoupitia sasa. Kwa sababu ya matatizo makubwa yanayoukabili uchumi wa dunia, baadhi ya malengo tuliyojiwekea kuhusu ukuaji na mwenendo wa uchumi wetu yameathiriwa.
Mfumuko wa Bei
Ndugu Wananchi;
Bei kubwa za mafuta zilizokuwepo kwa karibu miaka miwili mfululizo na hasa katika miezi kumi ya mwanzo ya mwaka huu zilipokuwa juu sana, imekuwa kichocheo kikubwa cha kupanda sana kwa mfumuko wa bei na ukali wa maisha hapa nchini. Aidha, kupanda sana kwa bei za vyakula tunavyoagiza kutoka nje kama vile ngano, mchele na vinginevyo viliifanya hali ya mfumuko wa bei kuwa mbaya zaidi.
Tulikuwa tumejiwekea lengo, kwa mfano, katika bajeti iliyopita kuwa tutateremsha mfumuko wa bei hadi kuwa asilimia 4.5 mwezi Juni, 2008 kutoka asilimia 5.9 ya mwezi Juni, 2007. Badala yake mfumuko wa bei ukawa asilimia 9.3 mwezi Juni, 2008 na kupanda hadi asilimia 12.3 ilipofika mwezi Novemba, 2008. Hivi sasa bei za mafuta zimeshuka kuanzia Oktoba, 2008 na hivi leo zimefikia dola za Kimarekani 38.4. Hali kadhalika, bei za baadhi ya vyakula nazo zimeshuka. Lakini, itachukua muda mpaka manufaa ya hali hiyo kuonekana kwa uchumi wa nchi yetu na wananchi wake.
Ndugu Wananchi;
Wakati mwingine hali huwa hivyo kwa sababu ya ukaidi na tamaa ya wafanyabiashara. Nimekwishawaagiza Mawaziri wahusika kuzibana mamlaka husika kutimiza ipasavyo wajibu wao kwa mujibu wa mamlaka waliyopewa kisheria kuwalinda wananchi dhidi ya wafanyabiashara wa aina hiyo. Wakati huo huo narudia kuwataka wafanyabiashara watoe ushirikiano unaostahili kwa maslahi ya wateja wao na taifa kwa jumla. Aidha, nazitaka mamlaka husika kutokuchelewa wala kuchelea kuchukua hatua zipasazo kwa wafanyabiashara wakaidi.
Ndugu Wananchi;
Kutetereka kwa mfumo wa fedha wa kimataifa na kuanguka kwa masoko ya hisa katika mataifa yaliyoendelea kumesababisha uchumi wa nchi hizo kudhoofika. Hali hiyo imekuwa na athari za namna na viwango mbalimbali kwa uchumi wa nchi zinazoendelea kama Tanzania.
Nilikwishalieleza siku za nyuma na napenda kurudia kusema kuwa sekta ya fedha hapa nchini bado ni tulivu. Haijaathiriwa na misukusuko inayoikumba sekta ya fedha ya kimataifa. Zipo sababu kuu mbili.
Kwanza, kwamba, sekta yetu ya fedha na soko la mitaji havijaunganishwa na mfumo wa fedha wa kimataifa na masoko ya hisa ya kimataifa. Hivyo basi, hakuna athari za moja kwa moja zinazotukuta hapa nchini kwa sasa.
Pili, kuna usimamizi mzuri wa soko na sekta ya fedha unaofanywa na Benki Kuu. Mpaka sasa, juhudi hizo za Benki Kuu zimesaidia. Hata hivyo, tunatambua haja na hoja ya kuendelea kuwa makini. Inaelekea matatizo ya mfumo wa fedha na uchumi katika nchi zilizoendelea yatachukua muda mrefu kutengemaa. Hatujui siku za usoni mambo ya yatakuwaje.
Serikali itaendelea kushirikiana na Benki Kuu kuzuia athari za soko la fedha duniani zisitufikie au kama zitatufikia, basi makali yake yawe nafuu. Kwa sasa mfumo wa ufuatiliaji (surveilance) na ule wa kutoa tahadhari ya mapema (early warning system) vinafanya kazi ipasavyo. Tuko tayari kuchukua hatua zaidi kama hapana budi.
Ndugu Wananchi;
Athari za hiyo Tsunami ya uchumi wa dunia, kama ilivyoitwa na baadhi ya watu, kwa uchumi wetu tumeanza kuziona kwa baadhi ya sekta. Tuchukue kwa mfano, sekta ya utalii. Katika mapumziko yangu ya mwisho wa mwaka huu nilitembelea mbuga zetu za hifadhi ya wanyama za Tarangire, Ziwa Manyara, Ngorongoro na Serengeti ya Kusini. Katika mazungumzo yangu na viongozi wa hoteli, hifadhi hizo na wale wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) nimeelezwa jinsi idadi ya watalii ilivyopungua na mapato yao kushuka kwa kati ya asilimia 7 na 18.
Aidha, nimezungumza na baadhi ya wamiliki wa viwanda vya kuchambua pamba na viongozi wa Bodi ya Pamba. Wote wamenieleza tabu wanayoipata ya kuuza pamba yao nje. Pia wanaelezea jinsi bei ya pamba ilivyoshuka katika soko la dunia. Katika kipindi cha mwezi Machi hadi Julai, 2008 bei ya pamba ilikuwa senti 82 za dola za Kimarekani kwa paundi na kushuka hadi senti 45 kwa paundi kwa sasa.
Hali kwa zao la kahawa nayo siyo nzuri. Nimeambiwa kuwa kati ya mwezi Agosti, msimu wa kahawa ulipoanza, na tarehe 18 Disemba 2008, bei ya kahawa ya Arabica kwenye soko la dunia, imeshuka kutoka dola za Kimarekani 158 hadi 104 kwa gunia la kilo 50. Hii ni sawa na anguko la asilimia 34. Katika kipindi hicho hicho, bei ya kahawa ya robusta imeshuka kutoka wastani wa dola za Kimarekani 93.6 hadi dola 65.46 kwa gunia la kilo 50. Hii ni sawa na anguko la asilimia 30.
Ndugu Wananchi;
Hata kwa mazao mengine nayo kwa jumla, hali ni hiyo hiyo ya kupungua kwa mauzo nje na kushuka kwa bei. Matatizo tunayoyapata sisi kwa mazao yetu ndiyo yaliyoikuta bidhaa ya mafuta. Kwa sababu ya uchumi kutetereka katika nchi za Marekani, Ulaya Magharibi, Japan, China na India mahitaji ya mafuta yamepungua na bei ya mafuta imeanguka kupita kiasi.

Ndugu Wananchi;
Kupungua kwa mauzo nje na bei ya bidhaa zetu pamoja na kupungua kwa watalii kuna athari kwa uchumi wa nchi yetu. Mapato yetu ya fedha za kigeni yatapungua jambo ambalo litapunguza akiba yetu ya fedha za kigeni, hivyo kuathiri uwezo wetu wa kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje. Aidha, mapato ya Serikali kwa kodi zitokanazo na mauzo hayo yatapungua, hivyo kuathiri uwezo wa Serikali wa kutimiza majukumu yake ya kiutawala na kiuchumi. Isitoshe ajira chache zilizopo katika sekta husika zitapungua na kusababisha watu hao kuwa na hali mbaya kiuchumi.

Ndugu Wananchi;
Hali mbaya ya uchumi wa dunia inasababisha uwekezaji wa kutoka nje nao kuathirika. Baadhi ya wawekezaji walioonyesha nia ya kuwekeza nchini wameahirisha nia yao. Ukiacha hofu inayotokana na hali mbaya ya uchumi wa dunia, wengine wamekuwa wanapata ugumu wa kupata mikopo kutoka katika mabenki. Mabenki yamekuwa yanasita kukopesha na pale yanapokopesha masharti yake huwa magumu kiasi cha kuwakatisha tamaa wakopaji.

Ndugu Wananchi;
Nimezitaja baadhi tu ya athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa uchumi wa nchi yetu ili tutambue kuwa tupo kwenye mazingira magumu na hali ya baadae ni ya mashaka. Tunaweza kunusurika kwenye eneo moja lakini tukaathirika kwenye maeneo mengine kwa sababu uchumi wetu ni uchumi wa dunia ya utandawazi. Kutokana na athari hizo inakadiriwa kuwa hatutafikia malengo yetu ya kukua kwa uchumi mwaka huu 2008 na hata mwaka ujao wa 2009. Inakadiriwa kuwa uchumi utakua kwa asilimia 7.7 badala ya 7.8 mwaka huu na mwakani utakua kwa asilimia 7.3 badala ya asilimia 8 iliyokadiriwa.
Ndugu zangu;
Watanzania wenzangu;
Napenda sote tutambue kuwa kuna kila dalili kuwa mwaka 2009 huenda tutatumia muda mwingi na nguvu nyingi kukabili athari za machafuko ya uchumi wa dunia. Kwa ajili hiyo, hatuna budi kutambua hivyo mapema na kuwa tayari kusimama kidete kukabiliana na athari zake. Sisi katika Serikali tunafuatilia kwa karibu hali inavyoendelea duniani na hapa nchini na kuamua hatua za kuchukua. Tutaendelea kupashana habari. Maombi yangu kwenu wananchi wenzangu ni uelewa wenu na ushirikiano wenu. Umoja, mshikamano na ushirikiano wetu wakati huu ndivyo vitakavyotukinga na kutuvusha katika tatizo hili kubwa.
Ndugu Wananchi;
Yapo mambo kadhaa ambayo hatuna budi kufanya katika kukabiliana na hali hii tete hapa nchini. Miongoni mwa hayo lipo suala la kujenga uwezo wa ndani wa kujitegemea kwa mambo fulani fulani kama vile chakula na bidhaa muhimu kwa matumizi ya watu. Pili, linalolingana na hilo, ni suala la kukuza utalii wa ndani na kutafuta vyanzo vipya vya watalii kama vile Mashariki ya Kati na Asia. Tatu, kukuza masoko ya ndani kwa bidhaa zetu na masoko ya kanda kama vile SADC na EAC. Wakati mwigine tunahangaikia masoko ya mbali wakati soko lipo h apa ndani au nchi jirani.
Ndugu Wananchi;
Kwangu mimi kauli mbiu muafaka kwa mwaka 2009 ni “Mwaka wa Kuhami na Kukuza Uchumi wa Taifa”. Bahati nzuri kauli mbiu hii inawiana na mpango wangu wa kazi nilipoingia madarakani. Nilikuwa nimepanga kuwa, katika nusu ya kwanza ya kipindi changu cha uongozi tuelekeze nguvu zetu katika upatikanaji wa huduma za kiuchumi na kijamii, na nusu ya pili tushughulikie kukuza uchumi. Nafurahi kwamba, tumefanikiwa kuweka misingi madhubuti ya kisera na mipango ya uhakika ya utekelezaji kuhusu elimu, afya, barabara, maji na umeme vijijini. Utekelezaji wake unaendelea na changamoto yetu kubwa ni upatikanaji wa fedha za kutosha kutekeleza malengo tuliyojiwekea.
Nashukuru kwamba ufanisi mkubwa tulioupata katika ukusanyaji wa mapato ya ndani na misaada ya washirika wetu wa maendeleo tumeweza kupata mafanikio tuliyoyapata mpaka sasa. Hata hivyo mahitaji ya rasilimali bado ni makubwa. Ni wajibu wetu kuendelea kutafuta.
Ndugu Wananchi;
Kuanzia mwaka 2009 Serikali itaelekeza nguvu katika kukuza uchumi wa nchi kwa lengo la kuongeza mapato ya nchi na wananchi wake. Bahati mbaya au nzuri yanayotokea sasa duniani yanasisitiza haja na hoja ya kufanya hivyo. Pia, yameongeza jambo jipya la kufanya, nalo ni la kuhami uchumi usitetereke.
Kilimo Kipaumbele cha Kwanza
Ndugu Wananchi;
Katika agenda yetu ya kukuza uchumi, kilimo kimepewa kipaumbele cha kwanza. Tunafanya hivyo kwa sababu nzuri na za msingi kabisa. Kwanza, tunataka kuhakikisha kuwa tunajitosheleza kwa chakula na tunakuwa na ziada ya kutosha. Katika mazingira ya sasa ambapo bei za vyakula duniani ziko juu, kuwa na upungufu wa chakula na kulazimika kuagiza kutoka nje kutazua matatizo makubwa nchini. Mfumuko wa bei utatushinda kuudhibiti.
Pili, kilimo kitatupatia malighafi ya viwanda vya kusindika mazao ya kilimo na kuzalisha bidhaa kamili zinazotokana na mazao ya kilimo. Kuendeleza viwanda vya aina hii ni kipaumbele chetu cha pili katika agenda yetu ya kukuza uchumi wa taifa. Lazima tuanze safari ya kuuza nje mazao ya kilimo yakiwa yameongezewa thamani kuliko kuyauza yakiwa ghafi kama tufanyavyo sasa. Tutafanya kila liwezekanalo kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ili kufanikisha azma yetu hiyo.
Tatu, kilimo ni chanzo kikubwa cha mapato ya fedha za kigeni kwa nchi, mapato ya serikali kupitia kodi na ni tegemeo la watu wengi nchini kwa uhai wao. Asilimia 8.5 ya fedha za kigeni hutokana na mazao ya kilimo na asilimia 80 ya Watanzania wanaishi vijijini ambapo kilimo ndiyo shughuli yao kuu ya kuwapatia mapato na maisha yao.
Hali ya Chakula
Ndugu Wananchi;
Hali ya upatikanaji wa chakula nchini ni nzuri kwa miaka miwili mfululizo sasa, yaani 2007 na 2008, na tumekuwa tunapata ziada ingawaje ni kidogo. Napenda kuwahakikishia kuwa hakuna tishio la njaa nchini. Hata yale maeneo ambayo yamekuwa yanapata upungufu wa chakula tumeweza kuyahudumia kwa kutumia ziada hiyo na akiba kutoka katika Hifadhi ya Taifa ya Chakula (SGR). Kwa mfano, tathmini iliyofanywa mwezi Septemba, 2008 inaonyesha kuwa watu 240,544 katika Wilaya 20 nchini watakabiliwa na upungufu wa chakula kati ya Desemba, 2008 na Januari, 2009. Watu hao watahitaji tani 7,182 za chakula ambacho tayari kimekwishatengwa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Chakula. Hifadhi hiyo sasa ina akiba ya tani 127,420.
Ndugu Wananchi;
Mvua za vuli hazikuwa nzuri kwa mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Lakini, zimekuwa nzuri kwa mikoa ya Kagera, Mwanza na Mara. Hivyo basi mavuno ya vuli hayatakuwa mazuri katika mikoa iliyoathirika. Hali hiyo inaweza kuongeza iadi ya watu watakaohitaji msaada wa chakula. Hata hivyo, hakuna shaka yoyote tutaweza kuwahudumia. Matumaini yetu na sala zetu kwa mikoa hiyo ni kuwa mvua za masika zitakuwa nzuri. Ikiwa hivyo mzigo utapungua. Bahati nzuri mikoa mingine inayopata mvua moja hali ya mvua ni nzuri, hivyo inatutoa hofu ya upungufu mkubwa wa chakula nchini. Tuzidi kumuomba Mungu mvua zinyeshe kama kawaida katika mikoa hiyo nayo.
Ndugu Wananchi;
Dhamira yetu katika kuelekeza nguvu zetu katika kuendeleza kilimo ni kuongeza tija. Bahati mbaya kwa sasa tija iko chini sana jambo linaloelezea hofu za upungufu wa chakula, mazao ya biashara na hali duni ya maisha kwa wakulima wengi. Kwa ajili hiyo Serikali imekusudia mwaka 2009 kutilia mkazo mambo matano:
a. Upatikanaji na matumizi ya mbegu bora;
b. Upatikanaji na matumizi ya mbolea;
c. Upatikanaji wa maafisa ugani;
d. Uendelezaji wa kilimo cha umwagiliaji pale inapowezekana; na
e. Upatikanaji na uimarishaji wa masoko ya mazao ya wakulima.
Ndugu Wananchi;
Mambo yote hayo na mengine ambayo sikuyataja si mapya. Tumekuwa tunayatekeleza katika miradi na programu mbalimbali za kuendeleza kilimo nchini kama vile DADP’s, PADEP na ASDP. Tunachokusudia kufanya mwaka ujao ni kutoa msukumo maalum wa kuendeleza kilimo kama tulivyofanya kwenye elimu na tunavyokusudia kufanya kwa upande wa afya.
Kuhusu upatikanaji wa mbegu, tumepanga kuimarisha vituo vyetu vya utafiti wa mbegu na kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha mbegu hapa nchini. Kwa ajili hiyo nimewaagiza Jeshi la Kujenga Taifa na Jeshi la Magereza watumie sehemu ya mashamba yao kuzalisha mbegu. Nafuraji kwamba viongozi wa idara zetu hizo tayari wameshaelewana na wenzao wa Wakala wa Mbegu nchini kufanikisha mpango huo muhimu. Kwa upande wa mbolea nafurahi kusema kuwa kauli yangu niliyotoa Bungeni tarehe 21 Agosti, 2008 kuhusu pesa za EPA imeshaanza kutekelezwa. Shilingi bilioni 30 zimetengwa kwa ajili ya mbolea ya ruzuku na bilioni 10 kwa ajili ya madawa ya mimea. Madawa ya mifugo yametengewa shilingi bilioni 10 na mikopo ya kilimo TIB shilingi bilioni 10.
Ndugu Wananchi;
Nafurahi pia kuwa dhamira yetu ya kuzalisha mbolea hapa nchini inatekelezwa vizuri. Kiwanda cha kuzalisha mbolea ya phosphate pale Minjingu, mkoani Manyara kimekamilika na kimeshaanza kazi. Wakati huo huo mchakato wa ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea ya NPK hapo Minjingu umeshaanza. Aidha, uamuzi wetu wa kujenga kiwanda cha mbolea ya urea na ammonia kule Mtwara umefikia hatua nzuri. Kampuni ya kuwekeza imekwishapatikana na shughuli za mchakato wa ujenzi wa kiwanda hicho ziko mbioni.
Hatua hizi zote zitakapokamilika, ndani ya miaka miwili ijayo, zitaiwezesha nchi yetu kuwa moja ya wazalishaji wakubwa wa mbolea katika kanda yetu ya SADC na Jumuiya ya Afrika Mashariki. Tutatosheleza mahitaji yetu na kuwa na ziada ya kuuza kwa wengine nchi za nje na kujipatia fedha za kigeni.
Mifugo
Ndugu Wananchi;
Juhudi za kuongeza tija katika kilimo zitaelekezwa pia kwenye mifugo. Nia yetu ni kuboresha ufugaji wetu ili tupate mifugo inayotoa nyama nyingi, maziwa mengi na ngozi zilizo bora. Juhudi hizo zitajumuisha kuboresha aina ya mifugo yetu kwa kutumia madume bora na uhamilishaji. Pia itahusisha upatikanaji wa huduma za kinga na tiba ya mifugo, majosho, malisho, maji, masoko ya mifugo na mazao ya mifugo. Suala la kuwa na viwanda vya kusindika mazao ya mifugo nalo tutalipa uzito unaostahili.
Uwekezaji
Ndugu Wananchi,
Katika mwaka 2009, tutaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuvutia wawekezaji wengi zaidi wa ndani na nje kuja kuwekeza nchini. Sifurahishwi na taarifa nizipatazo kuwa mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara nchini bado hayajaboreka vya kutosha. Na, linalonisumbua zaidi ni kule kuanza kujengeka dhana kuwa Tanzania inaanza kupoteza sifa ya mahali rafiki kwa wawekezaji. Hii si dalili nzuri, lazima tuibadili haraka iwezekanavyo.
Ndugu Zangu;
Dunia nzima hata mataifa tajiri yanavutia wawekezaji seuze siye maskini? Uwekezaji ndiyo chachu ya kukua kwa uchumi. Bila ya uwekezaji uchumi haukui. Wote tunaowasifia kufanikiwa kiuchumi ni kutokana na uwekezaji. Hata China imeendelezwa na uwekezaji tena kutoka mataifa ya kibepari.
Tutayaainisha mambo yanayotufikisha hapo na kuyatafutia majawabu. Natambua kuwepo malalamiko kuhusu usumbufu na urasimu mkubwa katika kuwahudumia wawekezaji. Mlolongo na muda wa uamuzi ni mrefu, kuna usumbufu upande wa kodi na tuhuma za vitendo vya rushwa zinasikika. Wakati mwingine kauli za wanasiasa wetu zimekuwa zinawaogopesha wawekezaji. Yote haya na mengineyo ni mambo ambayo yapo kwenye uwezo wetu kuyarekebisha.
Tumedhamiria kuyakabili kwa dhati matatizo hayo ili tuifanye Tanzania kuwa nchi nzuri kuwekeza. Pamoja na kusimamia kwa karibu mradi wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Tanzania (BEST), nakusudia kuanzisha kitengo maalum cha kusikiliza malalamiko ya wawekezaji na kuyatafutia ufumbuzi (Investors Complaints Bureau). Kitengo hicho kitakuwa chini ya Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi na kazi yake itakuwa ni kutatua kwa haraka malalamiko ya wawekezaji.
Mikopo ya Wajasiriamali Wadogo na SACCOS
Ndugu Wananchi,
Miaka miwili iliyopita tulianzisha mpango wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo wadogo ambao hawana sifa za kukopesheka katika mabenki kwa utaratibu wa kawaida. Tumefanya hivyo ili wanyonge nao wapate fursa ya kujiendeleza na kujikwamua. Kama tujuavyo, tulitenga shilingi bilioni moja kwa kila mkoa wa Tanzania Bara na shilingi milioni 100 kwa kila mkoa kwa mikoa minne ya Zanzibar na milioni 200 kwa mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Tulikubaliana kuwa mikopo hiyo itatolewa na Benki za CRDB na NMB na asasi ndogo za fedha kama vile Benki ya Posta, PRIDE, SELF n.k.
Taarifa zinaonyesha kuwa hadi Novemba 30, 2008 jumla ya shilingi bilioni 39 zimekopeshwa na NMB (16.1bn/=) na CRDB (22.9bn/=) na watu 48,339 wamenufaika pamoja na SACCOS 192 na vikundi 137. Benki na asasi nyingine 12 zimeshakopesha SACCOS 236 na shilingi 4.6 bilioni zimetumika katika wilaya 46 za Tanzania Bara.
Katika ziara zangu katika mikoa ya Bara nimepokea malalamiko ya watu kuhusu upatikanaji wa mikopo hiyo. Moja ya jambo nililojifunza ni kuwa, mahitaji ya mikopo ni makubwa na fedha zilizotolewa ni kidogo. Jawabu lake ni kuongeza fedha, jambo ambalo tuko tayari kufanya. Jambo la pili nililojifunza ni kuwa fedha zilizolipwa na wakopaji wa awali hazijazungushwa. Jawabu lake ni kuzizungusha ili wengine nao wakope. Tunazungumza na mabenki juu ya jambo hilo. Ni dhamira yangu mwaka ujao wa 2009 tufanye tathmini ya kina ya mpango huu ili tubaini mapungufu yake na mbinu za kuyarekebisha ili tuongeze fedha na kunufaisha watu wengi zaidi wa kipato cha chini wainue hali zao za maisha.
Kwa nia ile ile ya kuwasaidia watu wasiokuwa na sifa za kukopesheka moja kwa moja na mabenki wapate mitaji ya kufanyia shughuli zao za kujipatia kipato, tuliwahimiza wananchi waanzishe Vyama vya Kuweka na Kukopa. Tulipoingia madarakani kulikuwa na SACCOS 1,875 na sasa zipo 4,780 kutokana na msukumo maalum tulioutoa kwa uanzishwaji wake. Fedha nyingi za akiba zimewekwa na wanachama wa SACCOS hizo na mikopo mingi imetolewa kwa wanachama hao. Aidha, SACCOS kadhaa zimeweza kupata mikopo ya kawaida ya mabenki na kupitia mikopo ya wajasiriamali wadogo wadogo.
Pamoja na kujenga utamaduni mzuri wa watu kuweka akiba, SACCOS zimekuwa nyenzo muhimu ya kukuza uchumi na vyombo vya kutumainiwa na wananchi wa kawaida katika harakati zao dhidi ya umaskini. Napenda kuahidi kuwa ni makusudio yetu kuendeleza juhudi za kuimarisha na kuanzisha SACCOS nchini.
Huduma za Kiuchumi na Kijamii
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka ujao tutaendeleza jitihada za kuongeza na kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu za kiuchumi na kijamii hususan elimu, afya, maji, umeme na barabara. Kazi kubwa imefanyika na watu wengi sasa wanapata huduma hizo, lakini bado hazijatosheleza mahitaji na viwango vya ubora.
Tunatambua wajibu wa Serikali wa kuongeza fedha katika bajeti za sekta hizo ili miradi mingi zaidi itekelezwe na kukidhi mahitaji ya wananchi. Hiyo ndiyo dhamira yetu kufanya katika mwaka 2009 na miaka ijayo. Sekta ya maji na umeme vijijini tutazipa kipaumbele stahiki.
Ndugu Wananchi;
Kwa upande wa elimu ya sekondari napenda kwa mara nyingine tena kuwashukuru na kuwapongeza sana wananchi kwa moyo wao wa kujitolea na kujituma. Moyo wao huo na ushirikiano wao na Serikali ndiyo siri iliyotufanya tuendelee kupata mafanikio makubwa katika upanuzi wa elimu ya sekondari nchini. Hivi sasa, nchini tunazo sekondari za Serikali 3,039 kutoka 1,202 mwaka 2005 na idadi ya wanafunzi imeongezeka kutoka 524,325 mwaka 2005 hadi 1,222,403 mwaka huu. Haya si mafanikio madogo katika kipindi kifupi hivi.
Naomba moyo huo wa kujitolea na ushirikiano viendelee kwa manufaa ya watoto wetu na wajukuu wetu waliopo sasa na wajao. Sisi katika Serikali tunaahidi kuendelea kutimiza wajibu wetu katika ushirikiano wetu huo. Tutaendelea kukabili changamoto za upatikanaji wa walimu, vitabu, vifaa vya kufundishia, maabara na nyumba za walimu. Tunatambua kuwa ni mzigo mkubwa lakini hatuna budi kuubeba kwa maslahi ya taifa letu.
Matokeo ya Darasa la Saba
Ndugu Wananchi;
Kwa miaka miwili mfululizo matokeo ya mitihani ya darasa la saba yamekuwa si mazuri. Mwaka wa jana kiwango cha kufaulu kilikuwa asilimia 54.2 na mwaka huu ni asilimia 51.2. Hali hii si nzuri na hatuwezi kuacha iendelee. Hatuna budi kujiuliza kulikoni na kutafuta majawabu muafaka. Nimeiagiza Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini kasoro zilizopo na kupendekeza hatua za kuchukua. Aidha, nimemuagiza Waziri Mkuu kulisimamia suala hili kwa ukamilifu.

Barabara
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka huu tunaoumaliza leo, tuliendelea kutoa kipaumbele cha juu kwa sekta ya miundombinu. Tumeongeza bajeti ya miundombinu na sasa ni ya pili kwa ukubwa baada ya elimu. Kiasi cha shilingi bilioni 973.3 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu nchini katika mwaka wa fedha 2008/09. Tumeendelea kujenga barabara mpya za lami, za changarawe na za udongo. Pia tumekarabati na kuimarisha barabara zilizopo.
Lengo letu la kuunganisha Makao Makuu ya Mikoa yote kwa barabara za lami sasa lina muelekeo mzuri. Mipango kwa kuunganisha mikoa ya Lindi, Mtwara, Rukwa na Ruvuma imefikia mahali pazuri. Hivi sasa nguvu zetu tunazielekeza kwa mikoa ya Kigoma na Tabora ambapo naamini mpaka katikati ya mwaka 2009 sura kamili inaweza kuwa imejitokeza. Nafurahi hata hivyo kwamba, taratibu za ujenzi wa daraja la Mto Malagarasi zimefikia hatua za mwisho.
Tunasikitika kwamba misukosuko ya mfumo wa fedha wa kimataifa umetulazimisha kuahirisha kutekeleza mpango wetu wa kupata fedha kwa kutumia hati fungani (soverign bounds) kwa ajili ya kujenga kwa kiwango cha lami barabara zetu kuu nyingi hapa nchini. Ni matumaini yetu kuwa hali ikitengemaa tutautazama upya mpango huo.
Bandari, Reli na ATCL
Ndugu Wananchi;
Katika mwaka 2009 tutaendelea kufuatilia na kusimamia kwa karibu hali katika mashirika ya reli, bandari na shirika la ndege. Hali ya huduma hizo muhimu hairidhishi hata kidogo. Yapo matatizo ya uendeshaji ambayo yamesababisha huduma zitolewazo kuwa za kiwango kisichoridhisha. Tutafanya kila tuwezavyo kurekebisha mambo ili huduma hizo ziboreke na kuwafanya watumiaji kufurahi.

Mapato ya Serikali
Ndugu Wananchi;
Kama ilivyo ada mwaka ujao tutaendeleza juhudi za kuhakikisha kuwa mapato ya Serikali yanaendelea kuongezeka. Tutaendelea kuimarisha Mamlaka ya Mapato na kuziba mianya inayopoteza mapato ya Serikali.
Napenda kutumia nafasi hii, kuwapongeza sana viongozi na watumishi wa TRA kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kukusanya mapato ya Serikali. Pamoja na matatizo ya hapa na pale hali ya mapato ya Serikali imeimarika. Mara mbili katika mwaka huu wamevunja rekodi ya ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Mara ya kwanza ilikuwa mwezi wa Juni walipokusanya shilingi 346.7 bilioni na mara ya pili ilikuwa mwezi wa Septemba walipokusanya shilingi 420.8 bilioni. Tunatambua na kuthamini juhudi zao na nakusudia kuwatunza kwa mafanikio hayo mwishoni mwa mwaka huu wa fedha.
Nidhamu ya Matumizi
Ndugu Wananchi;
Sambamba na juhudi za kuongeza na kuimarisha mapato ya Serikali hatuna budi kuhakikisha kuwa kunakuwepo na nidhamu na uaminifu katika matumizi ya fedha na rasilimali za Serikali. Nimelisisitiza sana jambo hili na kuwataka viongozi wenzangu na watumishi wa Serikali kusoma na kuzingatia maoni na mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali yaliyomo katika taarifa zake za kila mwaka. Nimeagiza Viongozi na Watendaji Wakuu wa Wizara, Idara, Mikoa, Wilaya na Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kusimamia kwa karibu utekelezaji wa Sheria ya Fedha na mali za Serikali na Kanuni zake. Kuna dalili za mabadiliko chanya, lakini hali bado si ya kiwango cha kutufanya tufurahi sana. Mwaka ujao tutaendelea kubanana katika jambo hili ili tufikie ufanisi unaotakiwa.
Ndugu Wananchi;
Kuanzia mwaka ujao nitawaomba wakaguzi wa mahesabu ya Serikali kumkabidhi kwenye vyombo vya sheria mtumishi wa Serikali aliyehusika na wizi au ubadhirifu mara watakapougundua. Najua utaratibu wa sasa hauko hivyo. Nataka tuutazame upya utaratibu wetu wa sasa ili isaidie kujenga nidhamu hata kama ni ya woga wa kufungwa. Itasaidia kunusuru fedha nyingi za umma zinazotumiwa isivyo.
Ni matumaini yangu pia kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ataendeleza kwa kasi na nguvu zaidi kazi waliyoianza ya ukaguzi wa thamani ya fedha zilizotumiwa na kulinganisha na kazi iliyofanyika (value for money audit). Ukaguzi wa asili umekuwa unahusu uandishi wa vitabu kwa mujibu wa kanuni za fedha. Lakini, inawezekana kabisa vitabu vya hesabu vikaandikwa vizuri lakini pesa zikatumika vibaya au hata kuibiwa. Tunataka ulinganifu sawia wa fedha zilizotumika na kazi iliyofanywa.
Ndugu Wananchi;
Nimewaelekeza wenzetu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kufanya kazi kwa karibu na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kusaidia kupambana na wasiozingatia nidhamu ya matumizi ya fedha na mali za umma hususan wezi na wabadhirifu wa fedha za umma. Bahati nzuri Sheria ya Mwaka 2007 iliyounda PCCB mpya imetoa mamlaka ya kufanya hivyo. Nimewataka wawe wakali kwa wala rushwa kama wafanyavyo sasa, lakini pia wawe wakali kwa wale wote wanaokiuka kanuni za fedha za Serikali. Vitendo hivyo siyo tu vinaitia hasara Serikali bali pia vinapunguza uwezo wa Serikali kuwahudumia wananchi walioiweka madarakani. Nimewataka waitumie vyema sheria mpya na fursa waliyonayo ya kuwaongezea uwezo wa rasilimali tuliyowapa kwa kutumiza ipasavyo wajibu wao. Nimewasihi pia kwamba katika kufanya hivyo wasionee wala kupendelea watu bali watende haki.
Ulinzi na Usalama
Ndugu Wananchi,
Tunaumaliza mwaka wa 2008 hali ya ulinzi na usalama wa nchi ikiwa ya kuridhisha. Mipaka ya nchi yetu ni salama na nchi ni tulivu. Hatuna budi kutoa pongeza maalum kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri waliyoifanya na wanayoendelea kuifanya. Uhalifu wa makosa makubwa ya jinai kama vile mauaji, unyang’anyi wa kutumia silaha na unyang’anyi wa kutumia nguvu umepungua. Taarifa za Januari hadi Novemba, 2008 zinaonyesha kuwa kulikuwa na matukio ya aina hiyo 8,330 ukilinganisha na matukio 10,381 katika kipindi kama hicho mwaka 2007. Huu ni ushahidi kuwa Polisi wanafanikiwa kudhibiti uhalifu, hata hivyo bado juhudi ziongezwe ili matukio ya uhalifu yapungue zaidi. Nafurahi pia kwamba hata ajali za barabarani zimepungua mwaka huu ukilinganisha na mwaka wa jana. Mwaka wa jana kulitokea ajali 16,196 kati ya Januari na Novemba, wakati mwaka huu zimetokea ajali 5,500. Hata idadi ya watu waliopoteza maisha imepungua kutoka 2,757 mwaka 2007 hadi 1,270 mwaka huu.
Ndugu Wananchi;
Wakati tunawapongeza wadau na Jeshi la Polisi kwa maendeleo hayo bado naamini kuwa ajali za barabarani pamoja na idadi ya watu wanaopoteza maisha au kujeruhiwa na mali kuharibiwa vinaweza kupungua zaidi. Ajali nyingi za barabarani husababishwa na makosa ya madereva kutokuheshimu sheria ya usalama barabarani. Lakini, pia kuna mchango wa Jeshi la Polisi hasa wale wa usalama barabarani kutodhibiti ipasavyo madereva wazembe. Tatizo hili lipo kwenye uwezo wa Polisi na wadau kulidhibiti.
Madereva wakubali kuzingatia na kuheshimu sheria ya usalama barabarani. Wenye magari wahakikishe wanaajiri madereva wenye sifa nzuri. Aidha, madereva wa mabasi ya abiria watambue kuwa wanabeba binadamu wenzao ambao kwa kipindi chote cha safari usalama wao uko mikononi mwao. Makosa madogo ya dereva yanaweza kuwapotezea watu uhai au kuwapa vilema vya maisha. Lazima watambue umuhimu wa wao kuwa waangalifu. Polisi nao lazima watimize ipasavyo wajibu wao. Polisi lazima wawe wakali kuhakikisha sheria za usalama barabarani zinafuatwa. Naamini Polisi wakiwa wakali tofauti itaonekana.

Mauaji ya Albino
Ndugu Wananchi;
Suala la mauaji ya ndugu zetu wenye ulemavu wa ngozi, yaani albino nimekwishalisemea mara mbili tatu mwaka huu, na mara ya mwisho wakati wa Baraza la Idd tarehe 8 Desemba, 2008. Ni mauaji na mateso ambayo hayana sababu ya kutokea kwa sababu chanzo chake ni cha kipuuzi. Imani kwamba kiungo cha albino kinampa mtu utajiri ni jambo la kijinga. Nirudie kuwasihi wenzetu hawa wanaotafuta utajiri wa haraka haraka kuwa juhudi na maarifa yao ndiyo siri ya kufanikiwa kwao na si vinginevyo. Lakini, kwa vile wapo watu wanaoamini kuwa wakipata viungo vya albino watatajirika na wapo waganga na wauwaji, Serikali haina budi kuchukua hatua za kuwabana watu wote hao na kulitokomeza kabisa tatizo hili.
Tumeunda kikosi-kazi kinachojumuisha Polisi na Idara ya Usalama wa Taifa cha kuendesha mapambano haya. Hivi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kina nchi nzima kuwatambua wahalifu na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria. Mpaka sasa watu 91 wamekamatwa na kufikishwa mahakamani na mapambano yanaendelea.
Kwa nia ya kuongeza kasi na nguvu ya mapambano haya, mapema mwaka ujao tutaendesha zoezi la kura ya maoni nchi nzima. Tutawataka wananchi wawataje watu wanaowajua kuwa wanajihusisha na mauaji au kukata viungo vya albino. Wawataje waganga wanaohusika, wauawaji wa albino, wauzaji wa viungo vya albino na wafanyabiashara wanaotumia viungo hivyo. Taarifa hizo zitasaidia kuwafuatilia na kuwakamata watu hawa waovu. Utaratibu kama huu ulitusaidia katika mapambano dhidi ya ujambazi nchini. Naamini utasaidia kwa hili. Tunafanya matayarisho ya zoezi hilo. Wakati utakapowadia watu wataarifiwa namna ya kushiriki. Naomba ushirikiano wa hali ya juu wa wananchi wakati huo. Jitokezeni kuwataja ili isaidie kukomesha aibu hii kwa taifa letu.
Hitimisho
Ndugu Wananchi,
Tunaumaliza mwaka nchi ikiwa na sifa kubwa katika medani ya kimataifa. Uhusiano wetu na mataifa yote duniani ni mzuri. Hatuna adui. Hali kadhalika uhusiano wetu na mashirika ya kimataifa ya kisiasa na kiuchumi ni mzuri. Nchi yetu inaheshimika na kutumainiwa katika diplomasia ya kimataifa. Tumepokea wageni wengi mashuhuri na wengine ni wa kihistoria kama ziara ya siku nne ya Rais wa Marekani, Mheshimiwa George W. Bush. Tumekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kwa mwaka huu. Pamoja na ugumu wake lakini tumeifanya kazi hiyo vizuri na yapo mambo kadhaa mazuri ambayo nchi yetu itakumbukwa nayo. Miongoni mwa hayo ni amani ya Kenya, kurejesha umoja wa taifa la Comoro, kuongoza vyema mijadala kuhusu masuala magumu kama yale ya uundaji wa Serikali ya Umoja wa Afrika na kuyafikisha mahali pazuri.
Mwaka 2009 nchi yetu itakabidhi uongozi wa Umoja wa Afrika kwa heshima na upendo mkubwa kutoka kwa wanachama wenzetu na mataifa mengine duniani.
Ndugu Wananchi;
Tunaumaliza mwaka nchi ikiwa tulivu. Hii inathibitisha kuwa nchi inaweza kuwa tulivu isipokuwa pale ambapo baadhi yetu tutakapokuwa tumeamua kuwa isiwe hivyo. Naomba mwaka 2009 uwe tofauti. Tuache vitendo vya kuchochea ghasia kwa kisingizio chochote kile. Vitendo hivyo havitavumiliwa hata kidogo. Ni vizuri tukaambiana mapema tusije tukalaumiana. Naomba Watanzania wenzangu wote na hasa wanasiasa wenzangu tuyatambue hayo na tujiepushe nayo. Naomba makundi ya kijamii yatambue ukweli huo na waache kuwaendekeza wanasiasa hasidi.
Ndugu Wananchi;
Naomba nimalize kwa kuwakushukuru kwa mara nyingine tena Watanzania wenzangu wote kwa ushirikiano wenu na uelewa wenu na msaada wenu kwangu na kwa wenzangu wote serikalini katika kipindi chote cha mwaka huu tunaouaga leo. Tumepita vipindi vya raha na vigumu kwa pamoja na tunaumaliza mwaka tukiwa wamoja na watu wenye mshikamano. Naomba tuingie mwaka mpya na moyo huo na tuendelee hivyo.
Nitakuwa mtovu wa fadhila kama sitamshukuru Mwenyezi Mungu kwa wema na upendo wake na kutuvusha salama mwaka 2008. Tuzidi kumuomba atuongoze na kutuvusha salama mwaka ujao na miaka ijayo. Mimi si Sheikh na wala si mwanazuoni, mimi na mfuasi tu. Lipo wazo nimekuwa napewa mara kadhaa kuwa pengine si vibaya kila mwishoni au mwanzoni mwa mwaka tungekuwa na siku ya maombi ya pamoja watu wote wote wa dini tukiongozwa na viongozi wa dini zetu kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa mwaka tulioumaliza na kuliombea taifa mema kwa mwaka unaofuata. Ni wazo linalovutia wengi lakini sidhani kuwa ni ni jambo la kufanywa kwa amri ya Serikali. Nawaachia viongozi wa dini zetu watuongoze.
Naomba tutakiane heri na fanaka tele katika mwaka mpya, 2009.
Mungu Ibariki Afrika
Mungu Ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisiliza.

Queen Latifah Aiibiwa Hotelini Tobago


Mwimbaji maarufu na mcheza sinema, Queen Latifah, ameibiwa pete, bangili na vitu vingine vyenye thamani ya dola $10,000 huko Tobago! Yuko huko kwenye likizo. Hoteli aliyofika ni ya ghali chumba huko ni dola $1,000 kwa siku!

Habari zinasema kuwa Queen Latifah alitoka kwenye kula brunch, alivyorudi alikuta ameibiwa.

Wenye hoteli na polisi wa Tobago wanasema wanafanya juu chini ili wamrudishie Queen Latifah mali yake.

**************************************************************************

Latifah's Jewelery Stolen In $10,000 Holiday Heist

2 January 2009

Queen Latifah has become the victim of thieves, who stole more than $10,000 (GBP6,990) in jewellery from her luxury villa in Tobago.

The actress/singer, real name Dana Owens, was holidaying at the $1,000 (GBP700)-per-night Stone Haven Villas in Black Rock, Tobago with a female friend when burglars struck on Monday.

Latifah, who checked in under the name Cynthia Hadden, reportedly returned from a barbecue brunch held in her honour by the establishment's management to discover a bracelet, two gold rings, a gold chain and a silver ring were missing.

Police were called to the resort after staff security conducted a search of the estate.

Police Commissioner James Philbert tells Trinidad and Tobago's Newsday, "Several searches are being carried out and the police are trying to have the jewellery returned to Queen Latifah. Investigators said the larceny seems to be an inside job and efforts are being made round the clock to make a breakthrough."
Kwa habari zaidi someni:

Thursday, January 01, 2009

Heri ya Mwaka Mpya - 2009




Nawatakia wadau wote heri ya mwaka mpya! Ninaomba 2009 iwe mwaka mzuri kwa wote. Pia ninaomba mungu apumzishe kwa amani roho za wasioweza kuona mwaka 2009. AMEN.
Hapa Boston tumeanza mwaka mpya na baridi kali na theluji mwingi. Baridi kama Alaska. Upepo umekuwa -15 degrees!

Tuesday, December 23, 2008

Heri ya Krismasi!



Wadau,

Ninawatakia sikukuu ya Kirismasi Njema! Pamoja na shamrashamra, mapochopocho na zawadi tukumbuke kuwa ni siku ambayo tunasherekea kuzaliwa kwa bwana Yesu Kristo. Na hapa Boston kama mmesikia kwenye taarifa ya hbari tumepigwa na Snow/Theluji kibao! Watu wanaomba summer ije haraka!

Heri ya Krismasi! Merry Christmas!