Wednesday, July 24, 2013

Pesa Ina Majina Mengi



PESA INA MAJINA MENGI. Ona;

Kwenye ibada inaitwa Sadaka au Zaka,

Msibani inaitwa Rambirambi,

Shuleni inaitwa Ada au Karo,

Kwenye Vyombo Vya Usafiri inaitwa Nauli,

Ukinunulia Haki inaitwa Rushwa,

Kumdhaminia Mtu Mahakamani inaitwa Dhamana,

Pesa ya uchumba inaitwa POSA,

Pesa ya itolewayo mtu akabidhiwe mke inaitwa MAHARI.

Je PESA inayohongwa kwa mpenzi inaitwaje?

 Jibu tafadhali.

Tuesday, July 23, 2013

Cheki Hiyo Shepu!


Mwanamke mweusi hasa ana hips!  Naomba maoni yenu.

Nedra Phillips

Mh. Tony Blair Atembelea Ikulu Leo






Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Mhe Tony Blair na mkewe Cherrie Blair alipokutana nao Ikulu jijini Dar es salaam leo Julai 23, 2013

PICHA NA IKULU

Monday, July 22, 2013

Mama Bishanga Ampongeza Natasha!



Mimi mama Bishanga na mwanangu Kilian Kamota tunakupa hongera kwa kazi nzuri uliotimiza
ya kufunga ndoa nasi huku tulikuwa tunasherekea ndoa pia ya wa tz wenzetu siku hiyo.

Uliniahidi mwaka 2011nilipokuja TZ kufunga ndoa kuwa nawe utafanya hivyo. Umetimiza ahadi
ya Mungu ya kuungana mume na mke kuwa kitu kimoja halali. Mmependeza sana mdogo wangu
tunza mzee wako, mapenzi ya uzeeni matamu sana. Mpe raha mumeo.

Christina Innocent / Mama Bishanga

OHIO

USA

Tiba ya UKIMWI Upo - Bei US $200,000!

Wadau, wanadai kuwa Tiba ya Kansa unatiba UKIMWI!!!!  Ila tiba hii ni ghali sana dola $200,00 kwa kila mgonjwa. Lakini ukiangalia bei ya dawa labda ni bora kulipa hiyo $200,000! Hata hivyo hii tiba ina mateso fulani kwa mgonjwa ni kubalisha ile Bone morrow kwenye mifupa!

*********************************************

Kutoka: http://www.fool.com/investing/general/2013/07/21/did-someone-just-cure-aids-for-200000.aspx

Did Someone Just Cure AIDS for $200,000?


By Rich Smith

July 21, 2013


Is this the AIDS cure we've been waiting for?

According to multiple reports, Harvard researchers Timothy Henrich and Daniel Kuritzkes have recently noted a surprising side-effect to cancer treatments performed on two separate patients who also happen to be HIV-positive.

After undergoing bone marrow transplants to treat cancers of the blood, both men were later discovered to have no trace of HIV left in their system.

Encouraged by the results, the patients have since stopped taking anti-HIV drug treatments. Seven weeks later (for one patient), and 15 weeks later (for the other), the virus has not returned. And while the researchers are hesitant to pronounce the men "cured" -- warning that there's still a risk the virus can resurface even months after initially disappearing -- they do cautiously concede that the patients are "doing very well."

First, do no harm

The doctors' caution is understandable for many reasons -- first and foremost is the fear of raising hopes that a cure may have been found for one of the world's most intractable diseases, only to have to dash that hope later.

Experts also warn that bone marrow transplant is a truly unpleasant experience -- and in many cases not a practical solution to AIDS because of the cost and complexity of the procedure.

All that being said, the hope for a cure to AIDS springs eternal, and in this case at least, even the fantastic cost of a bone marrow transplant operation may turn out to be a bargain relative to the cost of treating the disease over a lifetime.

When the treatment is worse than the cure

Consider: According to the National Institutes of Health, what this translates into for a patient living out the projected life expectancy of 24.2 years post-infection is a lifetime cost of up to $618,900 per adult.

That's the "good" news. The bad news is that other sources put the cost of treating an HIV infection at as much as $5,000 a month, with the bulk of the charges going to pay for drugs.

Should a patient beat the odds, and survive to live out a 50-year lifespan post-infection, that could add up to as much as $3 million in treatment costs. But what if we could cut that figure down by a factor of 15?

That's the far-off potential suggested by the Harvard transplant results. According to the American Cancer Society, an allogeneic bone marrow transplant from a donor can cost as much as $200,000. That's hardly cheap, but it's much cheaper than $3 million.

What does it mean to investors?

One industry for which "cheaper" does not necessarily mean "better," however, is Big Pharma, which makes big money under the current system of "treating" AIDS until death.

This is money -- revenue streams -- that could be put at risk if an actual cure for the disease is (or has already been) discovered.

Security Alert - Dar es Salaam - Majambazi

SECURITY ALERT! Dar NOT SAFE at NIGHT !! ARMED ROBBERS robbing / hijacking cars, robbing people, restaurants, supermarkets open at night. They come in with Land Cruiser & Sub Machine Gun. Their hair style look like cops / marines. In red T-shirts & white shirt. They robbed off at Unique Restaurant in West Upanga opp. Jamat Khana an hour ago. Please be careful & do not move around town unnecessarily at nights even in cars! Please pass this message to all your near & dear ones.

Wednesday, July 17, 2013

Picha za Kijana wa KiChina Aliyeponyeshwa na Askofu Kakobe

Haya wadau, picha hizi hapa za kijana wa kijana aliyekuwa hawezi kutembea anatumia wheelchair,  aliyeponyeshwa na Askofu Kakobe mwezi uliyopita kwenye Mkutano Toronto, Canada.











Tuesday, July 16, 2013

Rais Kikwete Afuturu na Watoto Yatima Ikulu leo Jioni

Picha na Maelezo Kwa hisani ya Ikulu




Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasabahi baadhi ya watoto yatima walioshiriki katika futari aliyoiandaa ikulu jijini Dar es Salaam leo.Watoto yatima wanaolelewa katika vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam walihudhuria futari hiyo.








Baadhi ya watoto yatima wakishiriki katika futari iliyoandaliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo jioni.

 PICHA NA IKULU

Daladala laparamia na kugonga ukuta wa Kanisa la St. Joseph mjini Dar!



Kutoka Wavuti.com


Walemavu wa miguu walijikuta wakiangalia mabaki ya baiskeli zao zilizoharibiwa baada ya kunusurika kugongwa na daladala namba T 989 BCN linalofanya safari zake kati ya Mabibo na Kivukoni lililoacha njia na kuparamia ukuta wa mlango wa kuingilia Kanisa la Mtakatifu Yosefu (St. Joseph) jijini Dar es Salaam leo.

Daladala hilo lilipata ajali wakati likijaribu kukwepa gari jingine dogo lililokata kona bila ya kuchukua tahadhari wakati likiingia katika Kanisa hilo.

Gari lingine dogo lenye namba za usajili T 674 BRL lililokuwa limeegeshwa nje ya Kanisa hilo liliharibiwa baada ya kuangukiwa na ukuta.

Picha, Maelezo: Dotto Mwaibale

KWA HABARI NA PICHA ZAIDI TEMBELEA DA SUBI
Source: http://www.wavuti.com/#ixzz2ZE38gx6S

Thursday, July 11, 2013

Mama Mzazi wa Profesa J Afariki Dunia! Aligongwa na Gari!





PictureBlack Rhyno aliandika haya maneno kupitia ukurasa wake wa facebook

HABARI ZILIZOPOKEWA USIKU HUU NI KWAMBA MAMA YAKE MZAZI MSANII MAARUFU WA MUZIKI NCHINI, JOSEPH HAULE A.KA. 'PROFESA J' AMEFARIKI DUNIA USIKU HUU BAADA YA KUGONGWA NA GARI  MAENEO YA MBEZI JUU, JIJINI DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA ANAISHI NA MWANAE.

HABARI ZINASEMA MAREHEMU, BI. ROSEMARY MAJANJARA HAULE, ALIGONGWA NA GARI AKIWA ANAVUKA BARABARA KUELEKEA DUKANI KIASI CHA SAA MBILI USIKU, NA KWAMBA BAADA YA KUGONGWA WASAMARIA WEMA WALIMKIBIZA HOSPITALINI TUMBI KWA KUTUMIA BAJAJI AMBAKO ALIFARIKI DUNIA. TAARIFA ZA AWALI HAZIJATAJA AINA YA GARI NA KAMA BAADA YA AJALI HIYO LILISIMAMA AU LA.

PROFESA J AMETHIBITISHA  HILO MUDA MFUPI ULIOPITA, NA KUSEMA INAMUIA VIGUMU KUAMINI IMETOKEA KWANI ANASEMA MAREHEMU MNAMO SAA MBILI HIVI ALIMPIGIA SIMU NA KUMWELEZA KUWA AMEPATA AJALI NA KWAMBA WAKATI HUO YUKO KITUO CHA POLISI, BILA SHAKA KUPATA FOMU YA PF 3 YA KUMUWEZESHA KWENDA KUTIBIWA HOSPITALI.

"MAMA ALINIAMBIA MWANANGU NIMEGONGWA NA GARI....NJOO NIKO POLISI NAANDIKISHA....MWANANGU NAKUFA....ALINIAMBIA MAMA NA MARA SIMU IKAKATIKA. KILA NILIPOJARIBU KUPIGA IKAWA HAIPATIKANI..." ALISEMA PROFESA J KWA UCHUNGU.

ANASEMA WAKATI ANAPIGIWA SIMU NA MAMA YAKE YEYE ALIKUWA KATIKA MGAHAWA WA NYUMBANI LOUNGE, NAMANGA, DAR ES SALAAM, ALIKOKUWA KATIKA KIKAO NA LADY JAY DEE NA MUMEWE GADNA G. HABASH, AMBAO BAADA YA TAARIFA HIYO WALIMSINDIKIZA HADI HOSPITALI YA TUMBI.

"TULIPOFIKA HOSPITALI SIKUAMINI KUONA BADALA YA KUPELEKWA WODINI AMBAKO NILIDHANI MAMA ATAKUWA AMELAZWA NIKAPELEKWA CHUMBA CHA MAITI AMBAKO NILIMKUTA MAMA AKIWA MAREHEMU", ALISEMA PROFESA J KWA MAJONZI.

GLOBU YA JAMII INATOA MKONO WA POLE KWA PROFESA J KWA MSIBA HUU MZITO NA WA KUSIKITISHA. TUNAMWOMBA MOLA AMPE NGUVU YEYE NA FAMILIA YAKE KATIKA WAKATI HUU MGUMU. 

TUTAENDELEA KUWAPASHA KINACHOJIRI KADRI HABARI  ZAIDI ZITAPOPATIKANA. KWA SASA PROFESA J NA WADAU WENGINE WAKO NYUMBANI KWAKE MBEZI JUU.
source-tzdailyeye 
 
Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake.  Picha hii ilipigwa April 4, 2008 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam  wakati wa sherehe ya uzinduzi wa albamu mpya ya Profesa J ya 'Aluta Continua'
 

Wednesday, July 10, 2013

Trayvon Martin Speaks


Changia Sinema Cultural Wars

 Mchangie sinema anayetengeneza mdau, Deogratius Mhella kuhusu maisha ya Wabongo Marekani.

http://www.kickstarter.com/projects/2088181052/cultural-wars

 Cultural Wars by Deogratius Mhella. As an African young man prepares to marry his African-American fiancée, their families meet and learn a different culture and traditions. How easy or difficult is it to learn and embrace a culture that is different from yours? This movie showcases African and African American cultures/traditions and how they differ or relate.


Tuesday, July 09, 2013

Ramadhan Karim


RAMADHAN‬ KARIM
Uzuri wa Ramadhani si tambi kwa iliki
     bali ni kusoma Qur-an kwa wingi.
Wala si uji kwa ndizi
bali ni kumuomba MOLA atuhifadhi.
Tena si chapati kwa mchuzi
bali ni kuacha yote ya kipuuzi.
Na wala si juisi kwa sambusa za nyama
bali ni kuomba istighfar kwa Maulana.
Pia wala si daku la wali wa nazi kwa jodari
bali ni tahajudi kwa wingi.

"MOLA ATUWAFIKISHE KUUDIRIKI MWEZI WA
RAMADHANI NA KUPATA FADHILA ZAKE".

Rais Kagame wa Rwanda Amtishia Rais Kikwete

Kutoka: www.afroamerica.net./AfricaGL

I will Just Wait For You At the Right Place And I will Hit You, Rwandan General Paul Kagame Threatens Tanzanian Jakaya Kikwete 

by AfroAmerica Network on July 3, 2013
 
President Kikwete of Tanzania (L) and President Paul Kagame of Rwanda (R)
 
“Those people [Tanzanian President Jakaya Kikwete] you just heard siding with Interahamwe and FDLR  and urging negotiations… negotiations?  Me, I do not even discuss this topic, because I will just wait for you [Tanzanian President Jakaya Kikwete] at the right place and I will hit you! He[Tanzanian President Jakaya Kikwete]  did not deserve my answer. I did not waste my time answering him…It is well known. There is a line you cannot cross, there is a line, a line that you should never cross. It is impossible…”

It is in these ominous terms that the Rwandan dictator General Paul Kagame threatened to get even with Tanzanian President Jakaya Kikwete, while addressing Rwandan Youth on June 30, 2013 during a summit called “Youth Konnect”“, sponsored by his wife, Janet Kagame.
 
Relations between Tanzanian President Jakaya Kikwete and Rwandan leaders have soured in the last weeks. On several occasions Rwandan leaders called the Tanzanian President “a genocide and terrorist sympathizer”, “ignorant”, “arrogant”, and “mediocre leader”. The relations have deteriorated following the recommendation by President Jakaya Kikwete of open negotiations between Rwandan, Ugandan and Congolese leaders and their respective armed opposition in order to bring durable peace and security  in the African Great Lakes region.
 
 
Then, General Paul Kagame, while addressing a closed door meeting with his close aides, called the Tanzanian President “4Bs”, which in Rwandan language means “an opportunist, attention seeker, arrogant and contemptible person.”
 
 
The latest public threats by  General Paul Kagame against the physical person of the Tanzanian President are arguably the most serious sign of how worse the relations among the two countries and the their leaders have become. According to sources in Kigali, General Kagame has also been frustrated by the attention Tanzanian President has been receiving from World powers. Until a few years ago, Rwanda and its dictator was the darling of the West. The attention from the West has since dwindled.
 
 
The upcoming days and months promise to be full of anticipation and sursprises in the Great Lakes Region of Africa.
 
2013 AfroAmerica Network. All Rights Reserved.

Ofisi ya Ardhi Kahama Kuna Nini?

Nimepokea kwa Email: OFISI YA ARDHI KAHAMA KUNA NINI? Ndugu zangu,ninaomba mnisaidie kupata majibu sahihi kwa wanaohusika na suala hili. Mimi ni mwanchi wa Wilaya ya Kahama mtaka mabadiliko na maendeleo binafsi pamoja na Taifa zima.Mwezi wa tisa mwaka jana nilipeleka maombi yangu ya kuomba Hati milki ya kiwanja changu katika ofisi ya wilaya ya kahama.Wahusika wa ofisi hiyo walishughulikia suala hilo hadi kufikia mwisho wa upatikanaji wa Hati Milki.Baada tu ya kufikia mwisho wa hatua hiyo,kikajitokeza kizingiti cha mtu mmoja kuhitajika kuweka sahihi ya nyaraka hiyo ili baada ya hapo ipelekwe kwa Kamishna wa Kanda ili asaini na kuwa tayari Kabla haijasainiwa na Kamishna wa Kanda kuna mtu mmoja anaitwa Afisa Ardhi Mteule.Afisa mteule wilayani Kahama alishasimamishwa toka mwaka jana kwa matatizo yake yeye na waajiri wake na sikumbuki ni mwezi gani.Lakini cha Kusikitisha toka mwaka jana ofisi hiyo iko wazi hakuna mtu aliyewekwa hapo ili aweze kusaini nyaraka za wananchi wa Kahama.Kwa masikitiko makubwa ofisi hiyo haina hata kibali cha kuweka kaimu wa kukaimu kiti chake.Na kwa masikitiko zaidi mtu huyo mdogo hawezi kuteuliwa na mtu yeyote isipokuwa ngazi za juu sana. Huku chin yuko mwananchi ambaye alishafanya hatua zote za nyaraka zake pamoja na malipo ambayo tayari serikali ilishapokea na hata kutumia hela hizo kwa shughuli za serikali mimi mwananchi na mvuja jasho nyaraka zangu bado zimo ofisini kwa kisa cha kwamba Afisa Mteule hajateuliwa na wakubwa.Yanapofanyika haya,wapo tu watu mhimu kama vile Afisa Ardhi wilaya,Mkurugenzi,Mkuu wa Wilaya na hata kamishna wa Kanda kwa nini wasiteue mtu wa kuhudumia wananchi?Mimi ninajua yuko hapo kwa kusudi moja tu ni kuhudumia wananchi. Ukipata nafasi ya kuuliza jibu ni moja tu kuwa mtu huyo hajateuliwa,Je leo ni mwaka,atateuliwa lini ili huyo mwananchi naye apate nafasi ya kufanya maendeleo yake?jibu utapata kuwa hatujui,tunasubiri.Wakati huohuo serikali inahimiza maendeleo,bado serikali hiyo hiyo inazuia watu wasifanye maendeleo kwa kitendo cha dakika 10 tu mtu anakaa kwenye ofisi hiyo na anasaini kila kitu kwa siku moja lakini cha ajabu sahihi moja kwenye nyaraka unaingoja mwaka.Ndugu zangu wanamabadiliko hii ni kweli na sahihi kweli?Kwa picha hii inaonyesha wakubwa wana maslahi yao binafsi katika suala hili,maana kusingekuwa na maslahi,wakubwa wasingenyamaza katika suala hili kwa mwaka mzima huku mwananchi anaendelea kuumizwa.Au katika suala hili serikali iko wapi hapa?Kwa nini serikali inyamaze wakati mwananchi ametoa hela yake?Je sisi wananchi wa chini tukamuulize nani? Je nini kifanyike ili huyyo Afisa Ardhi Mteule Kahama ateuliwe ili wananchi waeze kupewa haki zao?Kama mimi nimmoja je wangapi wananchi wanaolia nyaraka zao hazijasainiwa kwa mwaka mzima? Je wakubwa hawalijui hili?na kama wanalijua kwa nini wako kimya kama kweli hawana maslahi katika hili? Ninaomba nipelekewe malalamiko na nipatiwe majibu toka kwa watu wafuatao; Mbunge wa Kahama mjini Waziri wa Ardhi na makazi. Naibu waziri wa Ardhi Kamishna wa Ardhi makao makuu Dar. Niwakilisha.

Sunday, July 07, 2013

Anaomba Ushauri - Ndugu Yake Ameingizwa Kwenye Uzinzi!

 Nimepokea kwa E-Mail:

Na Mdau A.R.

Jamaa yangu mmoja ameajiri na kampuni inayomilikiwa na mme na mke.
mke immediate bosi wa kijana huyu ambaye hata hajaoa
Siku moja akapewa pesa laki moja akimwambia atafute usafiri na maekezo kwa wakutane hoteli fulani kuna kazi anataka wafanye mahali tulivu.
Kijana alijua mambo ya kiofisi, kachukua usafiri hadi kaenda kule hotelini; kufika kamkuta mama akimsubiri mapokezi, akampokea na kumeleka chumbani, kijana na laptop yake hajui hili na lile.
Mama kakaa, kitandani kijana kwenye kochi, mama yule bosi akaanza kusimulia matatizo ya mumewe, kwamba yupo busy na mambo ya biashara ampi tunda.  Kijana pamoja na kwamba hajaoa, akaanza kumpa shule jinsi ya kumfanya mmewe ampe atakacho, kabla ya kijana kumaliza maelezo yake yule mama akamwambia hata hamwelewi anamwambia nini maana anajisikia hamu sana ya kufanya ni muda mrefu.
Yule kijana kwa hofu akasema ngoja nikimbie pale famasi labda kuna dawa za kutuliza hamu nikuchukulie umeze; mama akasema hataki dawa, mara akaingia chooni maana chumba alichokua kilikuwa na choo ndani.
Alipotoka huko alikuja mtu nguo zote kaacha huko chooni, kijana akataka kutoka nduki, mama akamdaka na kumrusha kitandani huku huku akimpa ishara ya kutokupiga kelele, kammkwangua sruali na ile kitu ya Ludoviki, kijana naye akapa hamu, wakacheza. Walipomaliza mama akampa yule kijana miloni moja na kumwambia asante sana kwa kazi nzuri
Asubuhi ofisini kijana anaona aibu hata kumwangalia lakini mama hajari hata kidogo, siku tatu baada ya ile kapewa laki tena na maelekezo ya kwenda kule hotelini, kijana katii amri ya bosi na kwenda hotelini kutoa dozi
SASA yamekua mazoea lakini si mapenzi maana anapewa aamri. sasa anahisi bosi mkubwa (mme) kajua sasa anataka kuacha kazi maana mkubwa anamuogopa sana. sasa aniomba ushauri nami sina, mwenye uzoefu katika haya anisaidie nimuokoe maana kuacha kazi na kuja kupata nyingine kasheshe

Rais Kikwete Afungua Tamasha la Matumaini Uwanja wa Taifa Leo

 Muziki wa Injili ulitawala. Hapa Solomon Mukubwa akitumbuiza
 MC wa Tamasha la Matumaini Godwin Gondwe a.k.a Double G akiwa kazini
 Bango lajieleza
 Uzalendo kwanza
 Nnape Nnauye akiwa na wadau
 JK akitete jambo na Eric Shigongo, mwandaaji wa Tamasha la Matumaini
 Wagunge wapenzi wa Simba wakipiga jalamba
 Profesa Maji Marefu akiongoza wabunge wapenzi wa Simba
 Wabunge wapenzi wa Simba
 Mwigulu Mchemba na skafu yake akiwa na  wabunge wapenzi wa Yanga
 Halima Mdee (kati mbele, bukta nyeusi) akiongoza kikosi cha wabunge wapenzi wa Yanga
 Kikosi kazi cha wabunge wapenzi wa Yanga
 Da' Asha Baraka akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT) Dionis Malinzi
 Mwandaaji wa Tamasha la Matumaini akisema machache
 Millard Ayo wa Clouds FM akirusha vitu live
 Wapiganaji wakila mzigo
 Wapiganaji kazini
 Wapiganaji wakishuhudia
 Wapiganaji wakirekodi matukio
 JK akifungua rasmi Tamasha la Matumaini
 JK akiwaasa Watanzania wasidanganyike na watu wanaotaka kuwatenganisha
 Hatudanganyiki....
 JK akilisifia Tamasha la Matumaini kuwa ni moja ya majibu ya wanaotaka kutenganisha Watanzania kwa misingi ya kikabila ama kidini
 JK akijiandaa kupiga filimbi kuanzisha mechi ya wabunge wpenzi wa Yanga na Simba
 JK akiwa refarii akihesabu wachezaji kabla ya kuanzisha mechi
 JK akiaga baada ya kuanzisha mpambano huo 
 JK akikaribishwa na mwandaaji Eric Shigongo. Kati ni Waziri wa Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara
 JK akiingia uwanja wa Taifa akiongozana na Waziri wa Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara na Eric Shigongo
 JK akiwa meza kuu
 Meza kuu
 Mwandaaji wa tamasha Eric Shigongo akiongea machache
 JK akimpongeza Eric Shigongo kwa hotuba nzuri
 Waziri wa Habari,  Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt Fenella Mukangara akimkaribisha JK kutoa hotuba yake
 Tamasha la Matumani Oye!
 JK akiongea na kadamnasi kwenye tamasha hilo katika hotuba iliyorushwa moja kwa moja na TBC
 TUSIDANGANYIKE...
 JK akiongea na kadamnasi
 "Tamasha hili ni majibu kwa wanaotutakia mabaya Tanzania...."
 JK akiongea na kadamnasi
 JK akisalimiana na wachezaji wa Bongo Movie
 JK akipeana mikono na kipa wa zamani  Yanga na Taifa Stars Peter Manyika ambaye sasa ni msanii wa Bongo Fleva na Bongo Movie
 Jk akisalimiana na Bongo Movie Stars
 JK akisalimiana na Katibu Mkuu wa FAT mstaafu Mwina Kaduguda
 JK akisalimiana na kipa (wa kweli)  wa Yanga Barthez
 JK akiingia uwanjani
 Kikosi cha wabunge wapenzi wa Simba
 Waamuzi na wabunge wapenzi wa Yanga
 JK akilakiwa na refa Othman Kazi
 JK akiweka saini katika mpira utaochezewa
JK akiweka saini 
 JK akitambulishwa waamuzi
 JK akikagua wabunge wapenzi wa Yanga
 JK akisalimiana na straika mkali wa Yanga kutoka DRC
 Hiki kifriji vipi.....
 JK akisalimiana na wabunge wa Yanga. Huyu ni Esther Bulaya
 JK akisalimiana na mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa Yanga
JK akisalimiana na kiongozi-mchezaji wa Yanga
 JK akisalimiana na mshambuliaji hatari wa yanga Halima Mdee

 JK akisalimiana na nahodha wa Simba Amos Makala
 JK akisalimiana na Simba
 JK akisalimiana na mchezaji wa kulipwa wa wabunge toka Nzega, Dkt Hamisi Kigwangalla
 JK akisalimiana na Profesa Maji Marefu
 JK akisalimiana na wachezaji wabunge wa Simba
 JK akisalimiana na mshambukliaji hatari wa Simba William Ngeleja
 JK akiendelea kusalimia wabunge wana Simba
 JK akisalimiana na beki tatu wa wabunge wa Simba Joshua Nassari
 Haya waheshimiwa... mchezo mwema...
 Nyimbo ya Taifa ikipigwa, kila mtu mguu sawa
 Wimbo wa Taifa 
 JK akipungia umati unaomshangilia kwa nguvu
 JK akipena mkono na mashabiki
 JK akiteta jambo na JB huku Dkt Cheni akiwa pembeni
 Mashabiki wakiwa nje ya uwanja
 Nyomi ya nje inapita ya ndani
Mshabiki wa Yanga akielekea uwanjani