Saturday, October 01, 2022

Mnaifahamu Tanzania Life Project ?




Tanzania Life Project ni NGO inayaosaidia wananchi wanaoishi kwenye vijiji vilivyo n ukosefu wa maji kupata maji.   Wanachimba visima ili kusaidia kupata maji na kuepuka kutembea misafa mirefu kutafuta maji

Nilipotoka Tanzania nilikutana na baadhi ya watu waliojitolea (Volunteers) walioenda  Dodoma, Tanzania kusaidia wanavijiji.

Kwa kweli niliguswa sana na moyo wao wa kusaidia watu kupata maji.  Ninakumbuka enzi zile...Tabora maji yalikuwa ya shida sana. Ukiyapata yana rangi ya maziwa. 

Zaidi ya kuchimba visima, wanatoa ruzuku kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, na wantaoa elimu kwa wanawake na wanaume kwa ajili ya kuimarisha maisha yao.


tKwa habari zaidi BOFYA HAPA: